Thursday 1 May 2014

SEHEMU YA PILI; SHINIKIZO LA DAMU LA JUU (HYPERTENSION)




 
MAKALA HII INATOKA SEHEMU YA KWANZA NA HII NI SEHEMU YA PILI
SABABU ZA KUPANDA SHINIKIZO LA DAMU
Shinikizo la damu hupanda wakati damu
nyingi inapopita mshipani au wakati
mshipa unapokuwa mwembamba.
Mtu anaweza kupata ugonjwa huu kwa
mambo yasiweza kuepukika na mambo
yanayoweza kuepukika.


Mambo yasiyoweza kuepukika mfano
kurithi tatizo la kupanda kwa shinikizo la
damu kupitia kuzaliwa pamoja kwenye
familia yenye watu wenye shinikizo la damu
la juu.
Pia inasemekana kwamba uwezekano wa
kupata tatizo hilo huongezeka mtu
anapozidi kuzeeka na kwamba wanaume
wenye asili ya afrika wanakabili uwezekano
mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa huo.
Mambo unayoweza kuepuka ni pamoja na
matumizi ya chumvi (Sodium). Hii inahusu
hasa wagonjwa wa kisukari, watu ambao
shinikizo la damu hupanda sana, wazee na
watu fulani weusi.
Mafuta mengi katika damu yanaweza
kufanyiza utando wa kolesteroli
(Cholesterol) kwenye kuta za ndani za
mishipa. Hivyo, mishipa huwa myembamba
na shinikizo la damu huongezeka.
Watu ambao ni wazito kupita kiasi kwa
asilimia 30 wanaweza kupata tatizo la
kupanda kwa shinikizo la damu.
Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha
utando mgumu wa mafuta kwenye kuta za
mishipa, ugonjwa wa kisukari, mshtuko wa
moyo na kiharusi.
Ijapokuwa uthibitisho unapingana, kafeini
inayopatikana katika kahawa, chai na
vinywaji vya kola yaweza kusababisha
tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu.
Kunywa kileo mara nyingi na kupita kiasi na
kutofanya mazoezi kwaweza kuongeza
shinikizo la damu.


DALILI NA ISHARA (SYMPTOMS & SIGNS) ZA

KUPANDA SHINIKIZO LA DAMU
Mara nyingi watu wenye shinikizo la damu
la juu hawana dalili za moja kwa moja na
huwa inagundulika baada ya kufanya
uchunguzi kwa kawaida au wakati
maangalizi ya afya yanafanywa kwa sababu
nyingine.
Watu wengine wenye shinikizo la damu la
juu huwa wanapata maumivu ya kichwa
(Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi
nyakati za asubuhi), pamoja na
kuchanganyikiwa, kizunguzungu, kelele
sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
kutoweza kuona vizuri au matukio ya
kuzirai.
KUJUA KAMA SHINIKIZO LA DAMU

LIMEPANDA
Pale mtu anapokuwa na dalili za kupanda
kwa shinikizo la damu, hupaswa kufika
kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya
kufanyiwa uchunguzi ili kubaini kama
shinikizo la damu limepanda.
Vipimo vya shinikizo la damu vinapatikana
katika vituo vya afya na wajuzi mbalimbali
wa afya wanaweza kuvitumia.
Kipimo kimoja cha shinikizo la damu
hakimaanishi kupatikana au kuugua
ugonjwa huo, inanidi kupimwa zaidi ya
mara mbili kwa nyakati tofauti.
Kama shinikizo lako la damu liko juu, ni
muhimu kufanyiwa uchunguzi zaidi wa
matatizo mengine ya kiafya.
Vipimo vingine ni pamoja na kuchunguza
damu ili kufahamu wingi wa kolesteroli
(Cholesterol) mwilini, kupimwa BUN na
electrolytes, kuchunguza mkojo (Urinalysis),
ECG, Echocardiography na pia ultrasound ya
figo.


JINSI YA KUISHI NA SHINIKIZO LA DAMU LA

JUU
Mabadiriko ya maisha hupendekezwa ili
kushusha shinikizo la damu lililopanda
kabla ya kuanza matumizi ya dawa za tiba
(Antihypertensives).


1.  Kudumisha uzito wa mwili wa kawaida.
Kwa mfano Mwili Molekuli Index (BMI) ya
20-25 kg/m°2
2.  Kupunguza kiasi cha chumvi (Sodium)
unachotumia.
Kupunguza ulaji wa sodium kwa < 100
mmol/siku (<6g ya kloridi sodium au < 2.4
g ya sodium kwa siku).
3. Kufanya mazoezi kwa ukawaida.
Kushiriki katika shughuli za mara kwa mara
za kimwili kama vile kutembea upesi kwa
dakika 30 au zaidi.
4.  Usinywe sana kileo.
Watafiti fulani wanasema kwamba
wanaume walio na ugonjwa wa kupanda
kwa shinikizo la damu hawapaswi kunywa
zaidi ya mililita 30 za kileo kila siku,
wanawake na vilevile watu ambao si wazito
sana hawapaswi kunywa zaidi ya mililita 15
za kileo.
Kileo cha mililita 30 kinalinganishwa na
mililita 60 za vinywaji aina ya Spirits kama
wiski & vodka, kadhalika mililita 240 za
divai (Wine) au mililita 720 za pombe (Beer).
5.  Kutumia lishe yenye matunda na mboga.
Kwa mfano angalau visehemu vitano kwa
siku.
6.  Kula vyakula vingi vyenye potasiamu,
magnesi na kalisi.
Uchunguzi mbalimbali unaonyesha
kwamba kula vyakula vingi vyenye
potasiamu na kalisi kwaweza kupunguza
shinikizo la damu.
7.  Dhibiti mfadhaiko.
8.  Acha kuvuta sigara.
9.  Dhibiti kiwango cha kolesteroli

(Choresterol).
10.  Dhibiti ugonjwa wa kisukari.


11. Usitumie dawa zinazoweza kuongeza

shinikizo la damu.
MWISHO

0 comments:

Post a Comment