Showing posts with label MARADHI YA BINADAMU. Show all posts
Showing posts with label MARADHI YA BINADAMU. Show all posts

Friday, 18 August 2017

DALILI YA KUZIDI ASIDI MWILINI YOUR BODY IS ACIDIC HERE IS WHAT YOU NEED TO DO (THE REAL TRUTH BEHIND CANCER)

  
DALILI YA KUZIDI ASIDI MWILINI:
Sababu ya Acidity
• Uvutaji wa sigara kwa wingi
• Kunywa pombe kupita kiasi
• Vidonda vya tumbo
• kuzidi kwa asidi ya tumbo
• Kutokula kwa wakati
• Kula kukaanga na viungo vya chakula mara kwa mara
• Matatizo katika utendaji wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula tumboni
• Kukaa na njaa kwa muda mrefu au kuto kula chakula cha Asubuhi
• Kula vyakula vingi vya mafuta, kama chocolates
• kuwa na Mimba kunasababisha asidi pia.
• kuzeeka
• Utokaji yatokanayo na jua na joto
• Muafaka wa chakula tabia
• kuwa hisia mbaya
• Udhaifu wa mishipa ya mwilini
Dalili ya Acidity
• Mchomo au maumivu katika tumbo, 1-4 masaa baada ya mlo
• maumivu ya kifua
• Kiungulia cha Muda mrefu
• Uvimbe katika kifua
• Kuhisi njaa mara kwa mara
• Daima maumivu katika tumbo la juu
• Kucheua
• Kichefuchefu
• Kuona Uchungu ladha katika kinywa
• Kupoteza hamu ya kula
• Kutapika
• Kukohoa
• Sauti ya mabadiliko na malezi ya kidonda katika umio (tube kuunganisha kinywa na tumbo)
• Maumivu ya sehemu za misuli ya mwili
• Maumivu katika masikio
DAWA YA KUONDOSHA HAYAMARADHI MWILINI
Mwili wako unayo Asidi nyingi aka Asidi ndio chanzo kikuu cha Maradhi yote Mwilini Mwako. Toa Asidi iliyozidi Mwilini mwako kwa njia hii hapa chini. Chukuwa Siki ya Tunda la tufaha vijiko 2 changanya na Kijiko 1cha magadi soda chapa ya Simba koroga vizuri mpaka itoke povu kisha tia ndani ya glasi moja ya maji ya kunywa koroga vizuri upate kunywa asubuhi kabla ya kula kitu. Fanya hivyo kwa siku 7 umepona maradhi yoyote yale mwilini mwako.
ONYO: Mwanamke Mwenye mimba asinywe hii dawa Tafadahali sana.

Wednesday, 9 March 2016

AINA ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI (ANAEMIA)



Leo tuangalie tatizo la upungufu wa damu mwilini. Anaemia ni jina la jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini.


Kiwango cha kawaida cha chembe nyekundu za damu (Haemoglobin-Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu na zikiwa pungufu ya hapo mtu huyo anakuwa na tatizo la upungufu wa damu.

Upungufu wa damu mwilini hutokea iwapo mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu zinapopungua kupita kiwango cha kawaida kinachotakiwa kwenye mwili wa binadamu.

Tatizo hili linaweza kumpata mtu yeyote ingawa visababishi vinaweza kutofautiana.
Licha ya utofauti huo mara nyingi tatizo hili husababishwa na mambo makuu matatu ambayo ni kupoteza damu mfano wakati wa hedhi kwa wanawake hasa wanaotokwa na damu nyingi au kuvuja damu kunakosababishwa na vidonda vya tumbo.

Sababu nyingine ni uzalishwaji duni wa chembe nyekundu za damu unaosababishwa na upungufu wa vitamini au lishe duni pamoja na magonjwa sugu. Pia magonjwa ya kurithi.

Iwapo mtu atapungukiwa kiasi cha madini, ulaji wa madini ya chuma katika mlo wa kawaida wa mtu hauwezi kufidia kiwango cha madini kilichopotea na kiasi hicho kinachokuwa kimebaki hutumika mara moja.

Aina za upungufu wa damu mwilini
Zipo aina mbalimbali za upungufu wa damu ikiwemo Haemolytic Anaemia. Hali hii ya upungufu wa damu, chembe nyekundu za damu huharibiwa haraka kuliko mwili unavyoweza kuzalisha chembe nyingine.

Upungufu huu husababishwa na mambo mengi ikiwemo kansa aina ya Lymphoma au utumiaji wa baadhi ya dawa ambazo huweza kuangamiza chembe nyekundu za damu kwa mfano dawa aina ya Methylodopa inayotibu matatizo ya presha ya kupanda.

Mtu mwenye aina hii ya upungufu wa damu anaweza kupatwa na homa, kutetemeka kwa mwili, maumivu ya tumbo na mgongo na mapigo ya moyo kushuka ghafla.
Pernicious Anaemia. Huu ni upungufu wa damu unaotokana na ukosefu wa kutosha wa asidi aina ya Folic (Folate) katika chakula.

Asidi aina ya Folate hupatikana katika mbogamboga za rangi ya kijani, matunda na nyama.Aplastica Anaemia. Huu ni upungufu wa damu unaotokea wakati chembe nyekundu za damu zinaposhindwa kuzalishwa ipasavyo.





Sickle cell Anaemia. Ni aina nyingine ya upungufu wa damu ambao chembe nyekundu za damu huwa na muundo usio wa kawaida unaozuia na kuathiri mishipa midogo ya damu na hivyo kusababisha kuziba kwa mishipa hiyo ya damu.

Dalili za upungufu wa damu mwilini (anaemia)
Mtu mwenye tatizo la upungufu wa damu mara nyingi huwa amepauka mwili na hujisikia kuchoka, udhaifu na huwa na mwendo kasi wa damu (yaani high pulse rate). Mgonjwa kuhisi kiu, kizunguzungu wakati akisimama, moyo kwenda kasi wakati akitumia nguvu kufanya jambo lolote, kuhema mfululizo na kupumua haraka haraka.

Dalili nyingine ni mapigo ya moyo kwenda kwa kasi, kuhisi uchovu sana au hata kuishiwa kabisa na nguvu. Wakati mwingine mgonjwa anaweza kuhisi maumivu ya kifua pamoja na kuchanganyikiwa anaposhughulikia jambo fulani.

Kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake, kupoteza nguvu na macho kukosa nuru ya kuona vizuri ni dalili nyingine za mtu mwenye tatizo hili.
Matibabu yake

Matibabu ya upungufu wa damu aina yoyote yanategemea aina ya upungufu wa damu inayomkabili mgonjwa.

Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya chuma kutokana na visababishi vya tatizo.
Matibabu ya lishe yanaweza kutumika kwa ushauri wa daktari ingawa yanaweza yasitoshe hadi pale mgonjwa atakapoongezewa damu.

Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizo huweza kutumiwa na madaktari hospitalini sambamba na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko mahututi huweza kuongezewa damu. Ushauri, ukiona dalili hizo, muone daktari haraka

AINA ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI -2


Katika makala ya wiki iliyopita tuliangazia tatizo la upungufu wa damu mwilini wengine huita Anaemia ambalo ni jina la jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini.

Tukasema kiwango cha kawaida cha chembe nyekundu za damu (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila milimita ya damu, zikiwa pungufu ya hapo mtu huyo anakuwa na tatizo la upungufu wa damu.
Tulitaja aina za upungufu wa damu kama vile Pernicious Anaemia na Aplastica Anaemia. Sasa endelea…
Sickle Cell Anaemia:
Ni aina nyingine ya upungufu wa damu ambao chembe nyekundu za damu huwa na muundo usio wa kawaida unaozuia na kuathiri mishipa midogo ya damu na hivyo kusababisha kuziba kwa mishipa hiyo ya damu.
DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU
Mtu mwenye tatizo la upungufu wa damu mara nyingi huwa amepauka mwili na viganja na kucha kuwa nyeupe na hujisikia kuchoka, udhaifu na huwa na mwendo kasi wa damu (yaani High Pulse Rate) na macho yake huwa meupe.
Dalili nyingine ni mgonjwa kuhisi kiu, kizunguzungu wakati akisimama, kuwa na mahangaiko ya moyo wakati akitumia nguvu kufanya jambo lolote, kuhema mfululizo na kupumua harakaharaka, mapigo ya moyo kwenda kwa kasi, kuhisi uchovu au hata kuishiwa kabisa na nguvu.
Dalili nyingine ni kusikia maumivu ya kifua pamoja na akili yake kushindwa kufikiri sawasawa, vilevile kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake, kupoteza nguvu na macho kukosa nuru ya kuona vizuri.
VIPIMO NA MATIBABU
Uchunguzi wa wingi wa damu hufanyika kwa kupima kiasi cha mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu kitaalamu huitwa Haemoglobin pamoja na kufanya kipimo kingine cha damu kijulikanacho kama Peripheral Smear.
Vipimo vingine vya maabara ni pamoja na kipimo cha kufahamu uwezo wa kuhifadhi madini ya chuma yaani Total Iron Binding Capacity (TIBC), kiasi cha Feritin katika damu pamoja na kiasi cha Folic Acid.
Aidha, katika mazingira mengine kipimo cha kuchukua sehemu ya supu ya mifupa na kuichunguza maabara yaani (Bone Marrow Biopsy) kinaweza kufanywa, japo si mara kwa mara.
Matibabu ya upungufu wa damu aina yoyote yanategemea aina ya upungufu wa damu unaomkabili mgonjwa.
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya chuma kutokana na visababishi vya tatizo.
Licha ya hiyo, matibabu ya lishe yanaweza kutumika kwa ushauri wa daktari ingawa yanaweza yasitoshe hadi pale mgonjwa atakapoongezewa damu.
Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizo huweza kutumiwa na madaktari hospitalini sambamba na matibabu ya tatizo linalosababisha, iwapo mgonjwa yuko katika hali ya mahututi huweza kuongezewa damu.
Tatizo la upungufu wa damu ni tatizo la hatari sana endapo mwenye tatizo hilo atachelewa kupata matibabu mapema. Ukiona dalili hizo wahi kumuona daktari.

Friday, 6 March 2015

WARTS UGONJWA UNAOATHIRI SEHEMU ZA NYETI ZA WANAUME NA WANAWAKE



Warts inaweza kutokea kwenye mikono. Sehemu zilizoota vinundu ni vinyama vilivyoota na ukiviangalia kwa makini vinamwonekano kama taulo.

Ni ugonjwa ambao pia unaweza ukatokea kwenye kiungo chochote cha mwili kama vile usoni na mikononi.


Zinaa ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanaongezeka kila siku na sababu kubwa ni jamii kutokuwa na utaratibu wa kupima afya mapema na hivyo kuchelewa kupata matibabu sahihi. Matokeo yake ni kusababisha madhara makubwa.


Warts ni miongoni mwa magonjwa hayo. Watu wengi waliopatwa na ugonjwa huo hawaonyeshi dalili zozote.


Daktari bingwa wa Magonjwa ya Uzazi na Ngozi wa Kituo cha Magonjwa ya Maambukizi (IDC), Dk Goodluck Mushi anasema ugonjwa wa Warts unaoambukizwa kwa njia ya kujamiiana.


Dk Mushi anasema Warts kwa jina jingine ni nyama zinazotokea sehemu za siri katika uume au uke au ndani ya uke pia katika haja kubwa sehemu ya pembeni au katika mashavu ya ukeni.


Ugonjwa wa Sunzua ama warts husababishwa na virusi aina ya Human Papilloma (HPV), ambavyo husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni.


Anasema mbali na sehemu hizo pia sunzua hutokea pembeni ya mdomo au katika ulimi.


Anasema kati ya watu 100 wenye magonjwa ya zinaa, 40 wana virusi vinasababisha ugonjwa huo wa warts.


Anasema asilimia kubwa ya watu wanaougua ugonjwa huo ni wanawake kutokana na maumbile yao.


Kwa upande wa mwanaume anapata kutokana na michubuko na hivyo virusi hivyo huingia katika njia ya mkojo na mwanaume anaweza kumwambukiza mwanamke kwa kumwagia mbegu.


Hali ikoje mikoani?


Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto kutoka Hospitali ya Wilaya ya Bariadi, Dk Nicholas Mbasa anasema kati ya wanawake 200 ambao walifika katika hospitali hiyo kutibiwa asilimia 38 waligundulika kuwa na ugonjwa wa Warts katika kipindi cha mwaka 2013 pekee.


Dk Mbasa ambaye pia ni specialist wa Magonjwa ya kifua kikuu na ukoma anasema tatizo la ugonjwa huo linaongezeka kila siku kutokana na uelewa mdogo kwa baadhi ya jamii.


Anasema baadhi ya wanaume walio katika ndoa ambao huomba kufanyiwa tohara katika hospitali hiyo, wengi wao wanakutwa na ugonjwa huo na kuanzishiwa matibabu.


Mikakati kuukabili


Dk Mbasa anasema moja kati ya mikakati inayoendelea kwa nchi nzima ni katika kupambana na ugonjwa huo ni kutoa elimu na kuhamasisha jamii kwenda katika vituo vya kutolea tiba kwa ajili ya uchunguzi na tiba sahihi.


“Vilevile tunaendesha kampeni za tohara kwa wanaume kwani wanaume wanaotahiriwa hupunguza uwezekano wakupata warts kwa asilimia 77 hadi 95, huku upande wa maambukizi ya VVU, mwanamume ambaye amefanyiwa tohara hupunguza uwezekano wa kupata VVU kwa asilimia 60,” anasema.


Kundi hatarini


Daktari bingwa wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kutoka Kliniki ya MediCorps, Francis Makwabe anasema watu walio na umri kuanzia miaka 14 hadi 35 wapo katika hatari ya kupata ungojwa huo hususan wanawake waliovunja ungo na wale walikatika umri wa kuzaa.


Dk Makwabe anasema wenye mimba wapo katika hatari ya kupata sunzua kwa sababu mama mjamzito anakuwa na upungufu wa kinga ya mwili.


Vilevile, anasema wagonjwa wa kisukari wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huo kutokana na kupungua kwa kinga ya mwili pamoja watu wanaotumia dawa kali. Kundi jingine lililopo katika hatari ya kupata warts, analitaja ni la wale wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo, kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja na kufanya ngono kinyume cha maumbile.


Mbali na kundi hilo vilevile watoto wadogo wanaweza kuambukizwa ugonjwa huo kwa kufanyiwa vitendo vya ubakaji.


Dalili zake:


Moja kati ya dalili za ugonjwa huo ni kuwa na vinyama au vinyuzi nyuzi mithili ya taulo laini katika sehemu za siri ambapo mara nyingi huwasha wakati wa joto au unaponyoa nywele sehemu za siri.


Vinaweza kuota pia kwenye ulimi, mashavu ya uke, mapajani, katika lips za mdomo na usoni.


Vinyama hivyo pia vinaweza kutokea usoni, hasa sehemu karibu na kope ama maeneo mengine kama vile vidole vya miguu na mikono.


Madhara


Warts inaweza kubainika kwa vipimo vya maabara. Warts zikitokea katika shingo ya kizazi, inaelezwa kuwa inasababisha saratani ya kizazi kwa wanawake na kwa upande wa wanaume inasababisha kansa kwenye sehemu ya njia ya mkojo.


Anasema mtu wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi yupo katika hatari ya kupata ugonjwa huo kwa sababu nyama hizo huota na kukua kwa haraka kutokana na upungufu wa kinga iliyoshuka.

Matibabu


Dk Mushi anasema licha ya ugonjwa huo kusababisha madhara kwa binadamu, ikiwamo saratani na kukosa mtoto, lakini unatibika ikiwa mgonjwa atawahi matibabu.

Wednesday, 26 November 2014

JINSI YA KUZUIA NA KUTIBU KUHARISHA WAKATI UNAPOKUWA SAFARINI.


Kwa nini uharishe wakati ukiwa safirini?
Kuna maambukizo mengi watu hupata wakati wanaposafiri na ambayo huleta kuharisha. Mengi ya haya maambukizo hayadhuru watu wanaoishi katika sehemu hizo ambazo wewe unasafiri kwani wao huenda walishaugua kabla (na sasa wamejenga kinga). Watu pia huharisha wakati wanaposafiri kutokana na uchovu wa safari na kubadilisha chakula.


Nitajuaje kama kuharisha kwangu ni maambukizo au ni kutokana na sababu nyingine?
Ni vigumu kusema tofauti yake. Kama unaenda choo laini 2-3 kwa kutwa na bila dalili nyingine zozote, kuharisha kwako sana sana huenda haukuambukizwa na vimelea vibaya. Maambukizi haya yatafuatwa na kupata choo cha maji maji mara nyingi. Dalili nyingine ni pamoja na kuharisha damu, homa, maumivu ya tumbo na kichefu chefu.

Nitazuiaje kuharisha?
Kitu cha maana kabisa na rahisi ili kuzuia kuharisha ni kuosha mikono mara kwa mara. Kufanya hivi ni muhimu sana haswa kabla ya kula chakula, pia mara nyingi kuosha mikono mara kwa mara ni vizuri. Kwa kuwa sabuni na maji sio ghali na hupatikana kila mara, kuna vitambaa vilivyolowekwa katika dawa za kuulia wadudu (hufanya kazi vizuri sana) huwa ni rahisi zaidi kutumia wakati ambapo sabuni na maji havikupatikana. Vitambaa hivi hupatikana katika maduka mengi ya dawa, hata ya vyakula au stoo za vitu mchanganyiko huko Umarekani, vichukue vitambaa hivi uendapo safari. Kama hujui jinsi ya kuvipata, mwulize daktari au muuguzi wako.
 
Vyakula vingine ni salama zaidi. Chakula chochote au kinywaji ambacho ni cha moto sana wakati kinapoandaliwa ni salama. Mikate, pipi pia ni salama.

Vyakula ambavyo vina hatari ya kuleta madhara na kukufanya uwe mgonjwa ni kama mboga mboga mbichi, saladi na vinginevyo vibichi au vilivyopikwa na kuiva nusu kama vile samaki na nyama. Kama utaosha mikono yako na kutumia kisu kisafi kumenya na kukata tunda, kwa kawaida ni salama. Epuka matunda ambayo hayana kumenywa kama vile matunda damu. Vyakula vya maziwa kama vile maziwa na jibini si salama labda kama vimesindikwa kwa ufundi (kuchemsha kwa mvuke). Unaweza kutengeneza maziwa salama kwa kuyachemsha mpaka kuchemka na kuyaacha yapoe. Maziwa ya pakiti (irradiated milk) ni salama kwa kunywa.
 
Maji yanaweza kukufanya ukawa mgonjwa pia. Kama maziwa, ukichemsha maji yako yatakuwa safi na salama kwa kunywa. Maji yauzwayo, yaliyohifadhiwa kwenye chupa pia kwa kawaida ni salama kwa kunywa. Vinywaji vilivyosindikwa kwenye chupa (vyenye kutoa vipele vya hewa kama vile soda) pia ni salama kwa kunywa. Hewa ya carbon inayotiwa katika vinywaji vilivyosindikwa pia huua vimelea kwa kipindi cha masaa manne, hata hivyo kutia hewa hii katika bomba la maji haifanyi maji yake kuwa salama kunywa kwani maji yaliyochanganywa hayakuwa yamechemshwa. Ni lazima uepuke kutumia vibonge vya barafu labda viwe vimetengenezwa na maji safi na pia wakati wa kupiga mswaki utumie maji safi na salama.
Itakusaidia zaidi endapo utafanikiwa kuepuka vyakula vya aina fulani kwa kuwa tumbo lako halikuvizoea japo vilizoeleka zamani.
 
Nifanye nini kama nitaharisha?
Kuna aina mbili za dawa za kuzuia kuharisha kwa wasafiri. Ya kwanza ni zile dawa za kupunguza kasi ya kuharisha lakini hazitibu maambukizo yaliyoleta kuharisha. Dawa hizi zinasaidia kupunguza dalili za ugonjwa. Dawa zinazotumika sana zinaitwaloperamide (“Imodium”) na Bismuth subsalicylate (“Pepto-bismol”), ambazo zote zinapatikana maduka yote ya dawa bila ya agizo la daktari.
Dawa hizi zisitumiwe na watoto wadogo.
Pia, kuna (antibiotics) dawa zinazoua vimelea vibaya ndipo hutibu ugonjwa. Kwa kuzitumia dawa hizi huweza kupunguza idadi ya siku za ugonjwa.
 
Wakati unapoharisha maji maji ni lazima utumie (antibiotic) dawa za kuulia vimelea vya ugonjwa ambazo daktari au muuguzi wako atakupa uchukue safarini. Unaweza pia kutumia loperamidend Bismuth subsalicylate kuzia kuharisha mpaka dawa ya kuulia vimelea vibaya ifanye kazi. Kama uko
taabani, una homa au unaona damu katika choo chako, ni lazima utumie dawa ya kuulia vimelea (antibiotic) na SIO ile ya leperamide au Bismuth subsalicylate.

VITU VYA KUKUMBUKA WAKATI WA KUSAFIRI
OSHA MIKONO, Na kama Huwezi kuosha mikono vya kutosha, hasa kabla ya kula  Basi (tumia vile vitambaa vilivyowekwa dawa ya kuulia vimelea vibaya kama Purell au Aavanguard kama ni rahisi zaidi kutumia) wengine huita sanitizer.

EPUKA VYAKULA HIVI.
Vibichi, au nyama, samaki, isiyoiva vizuri, maziwa ambayo hayajachemshwa au jibini, majani ya mboga mboga. Matunda ni lazima yaandaliwe kwa njia ya usafi, mahindi yakuchemsha na vyakula kama hivyo.

MAJI NA MAZIWA
Vinaweza kufanywa kuwa safi na salama kunywa kwa kuchemshwa na kuacha chini vipoe.
 Maji yanayouzwa katika chupa kwa kawaida ni salama.
Kama umeenda choo laini mara moja au mbili kwa siku tumia dawa ya  kukusaidia katika dalili hizi, lakini choo cha maji maji kabisa haswa kuchanganyika na damu, maumivu na homa, tumia dawa ile ya kuulia vimelea vibaya (antibiotic).

DAWA ZA KUZUIA KUHARISHA
Wakati uonapo dalili:
Loperamide (“Imodium”)
Matumizi: Kunywa  vidonge viwili kwa kuanzia, kisha kunywa kidonge kimoja kila  upatapo choo (usinywe zaidi ya 8 katika masaa 24). Usiwape watoto wachanga, wadogo au ukiwa mja mzito.
 
Bismuth subsalicylate (“Pepto-bismol”)
Matumizi; Kama ni vidonge meza vidonge viwili kila baada ya dakika 30 mpaka kuharisha  kupungue. Hata hivyo usinywe vidonge zaidi ya 16 katika masaa 24. Kama unakunywa vitu vya maji maji, kunywa vijiko vya chai 6 (30 mls) kila baada ya dakika 30 mpaka kuharisha kupungue. Usinywe vidonge zaidi ya 8 katika masaa 24. Usiwape watoto wachanga na watoto wadogo.

kutibu Maambukizo
Antibiotic:
Daktari au muuguzi wako atakupa dawa ya antibiotic kusafiri nayo unywe  ukipatwa na kuharisha kubaya. Hakikisha kuwa unaelewa jinsi ya kunywa dawa hizi kabla ya kuondoka katika ofisi ya daktari au muuguzi. Majina ya dawa za antibiotic zinazotumika na kujulikana sana ni kama Azithromycin (Zithromax), Ciproflaxacin, Levofloxacin (Levoquin) na Fifaxaamin Na pia utaandikiwa dawa kwa mujibu wa daktari.

Monday, 3 November 2014

UGONJWA WA CHANGO LA UZAZI - (MKE/MUME)




Tunapozungumzia mgonjwa wa chango tuna maana kuwa ni matatizo yaliyopo katika viungo vya uzazi kwa mke au mume. Huu ni ugonjwa ambao humpata mtu katika umri mdogo utotoni. Kwa mfano :- mume, hupata maumivu ya tumbo mara kueneza anapokuwa mdogo. Kwa upande wa mwanamke hupata maumivu ya tumbo anapoanza kuvunja ungo. Maumivu hayo hupelekea mtu (mume/mwanamke) kupata madhara katika viungo vyake vya uzazi.



DALILI ZAKE



  • Kwa mwanaume atakuwa akishiriki tendo la ndoa, anawahi sana kufika kileleni na kurudia mara nyingine ni vigumu sana.
  • Pia mwanaume hatakuwa na uwezo wa kusimamisha.
  • Ni vigumu kumpa mimba mwanamke.

Mwanamke mwenye chango la uzazi ana dalili zifuatazo:-


  • Kupata maumivu makali wakati anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi
  • Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa
  • Siku zake za hedhi hazitakuwa na ratiba, zitakuwa zinabadilika badilika
  • Hujisikia homa kali anapokaribia siku zake za dhedhi
  • Kupatwa hasirakali/ jazba anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi.
  • Kujisikia uchovu mkubwa anapokaribia siku zake za hedhi.
  • Kupata mchubuko kwenye mapaja na sehemu za uke.
  • Kuchukia kushiriki tendo la ndoa
  • Kupata uvimbe kwenye kizazi
  • Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi

Madhara yake kwa mwanamke

  • Kwa mwanamke ni vigumu kupata mimba
  • Mwanaamke anaweza kuwa tasa kabisa
  • Kuingia na kutoka kwa mimba
  • Kuwa na hamu ya tendo la ndoa lakini hafikii kileleni
  • Kuwa na uke mdogo sana


Madhara kwa Mwanaume


  • Kuwa na mbegu ambazo haziwezi kutunga mimba
  • Kiwango kinachozalishw cha megu ni kidogo mno
  • Kuwa na kiwewe cha kushiriki tendo la ndoa
  • Kusimama na kusinyaa kwa uume


Tiba ya Chango la Uzazi 

  • Ni vizuri sana kumweleza Dr. Dalili zote mtu anapojisikia.
  • Mara nyingi ugonjwa huu hautibiwi kwa dawa za hospitalini, bali ugonjwa wa chango la uzazi hutibiwa na miti shamba.
  • Dawa inayotibu ugonjwa huu ni dawa inayotibu kizazi.
  • Matumizi yake kawaida mtu ataitumia kulingana na ukubwa wa tatizo lake.
  • Huchanganywa na viungo vya uzazi vya wanyama, ambavyo kazi yake ni kuondoa matatizo yaliyopo, kwenye kizazi cha manamke/mwanaume.
  • Wengi wana amini kuwa dawa za miti shamba hazina uwezo wa kutibu haya ni mawazo potofu, miti shamba ndiyo suluhisho la kila tatizo katika afya zetu.Mimi mwenyewe ni shuhuda nimelelewa katika miti shamba, ukipewa dawa ya mitishamba haijakusaidia ufahamu kuwa kiwango cha Dr/Mganga huyo hakijakomaa.

Monday, 27 October 2014

MAUMIVU YA MAGOTI NA VISIGINO

TATIZO hili huwapata watu wote, maumivu ya magoti yanaweza kuwa makali au yakawa kwa mbali, vilevile magoti yanaweza kuvimba.
Maumivu haya yanaweza kuwa mbele ya goti au nyuma ya goti, maumivu yanapotokea mgonjwa hutembea kwa shida na kushindwa kunyanyuka akiwa amekaa.
Maumivu ya visigino huwa katika kisigino chote na hupanda kwa juu, wakati mwingine maumivu huwa kama sindano. Maumivu ya visigino yanaweza kuwa muda wote au yakatokea kwa vipindi, yaani asubuhi unapoamka inakuwa tabu kukanyaga chini lakini ukishakanyaga kwa muda fulani miguu inazoea na mwendo unakuwa wa kawaida na maumivu yanapungua.
CHANZO CHA TATIZO
Maumivu ya magoti hutokana na sababu mbalimbali, inaweza kusababishwa na kusimama au kutembea kwa muda mrefu ingawa siyo sana, ajali yoyote inayoumiza goti iwe barabarani, kuanguka au michezoni, maambukizi ya bakteria katika magoti kutokana na majeraha pia inaweza kuwa ni sababu.
Chanzo kingine ni ugonjwa wa Gauti, umri mkubwa hasa kwa kinamama pia huchangia uwepo wa tatizo hili pale mama anapofikia ukomo wa hedhi ambapo vichocheo vya ‘Estrogen’ vinaanza kupungua mwilini.
Matatizo haya ya magoti yana vyanzo vingi utakapoenda hospitali utapata ufafanuzi.
Maumivu ya visigino pia hutokea tu, huweza kusababishwa na kuumia hasa michezoni au kuvaa viatu vyenye soli ngumu na ukatembea navyo kwa mwendo mrefu.
Maumivu mengine hutokea nyuma ya mguu chini ya goti na kushuka hadi katika kisigino, husababisha misuli ya nyuma ya mguu kuuma au kukamata, wakati mwingine msuli hututumka kama mwanamichezo.
Hii inatokana na kutembea mwendo mrefu kwa kupanda milima, ngazi hasa ghorofani kama ni ghorofa refu sana na wewe kila siku unatumia ngazi.  Pia kuvaa viatu virefu na kutembea navyo mwendo mrefu.
DALILI ZA TATIZO
Maumivu ya magoti na visigino wakati mwingine huwa hayavumiliki. Maumivu huja na kupotea au huwa makali kwa mfululizo, maumivu yanaweza kutokea kwa kupwita kama ndani kuna jipu, goti linaweza kuwa kavu na kuhisi kabisa kama mifupa inagongana au kusuguana, wakati mwingine linakuwa na joto.
Visigino au nyuma ya miguu kunakuwa na maumivu kama kunawaka moto, ukipumzika na kuweka miguu juu utakuta yanapungua taratibu lakini ukikanyaga tu, yanaongezeka kwa kasi.
UCHUNGUZI
Mgonjwa anaweza kufanyiwa vipimo vya damu, x-ray na uchunguzi mwingine ambao daktari ataona unafaa. Uchunguzi hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya.
MATIBABU NA USHAURI
Magonjwa haya huwa yanatibika endapo mgonjwa atazingatia uchunguzi na matibabu kwa kufuatilia kwa kina.
Dawa zipo aina nyingi, kuna za kupaka, vidonge na sindano, hivyo inategemea uchunguzi unasemaje.

Sunday, 26 October 2014

SPINAL DISC (DISC ZA UTI WA MGONGO) ZINAVYOLETA MATATIZO MWILINI











Spinal Disc ni disk zinazokaa kati kati ya pingili “Spinal Vertebrae” za uti wa mgongo. Kuna wakati disk hizo hutoka sehemu yake na kusogea pembeni tatizo ambalo linajulikana kwa majina kadhaa kama vile

DEGENERATIVE DISC DISEASE au HERNIATED DISC au SLIPPED DISC. 

Tatizo hili husababisha maumivu makali ya mguu, mgongo, bega au Mkono. Maumivu haya huwa ni makali mno, katika mazingira mengine huuja na kutoweka, katika mazingira mengine maumivu haya huwa endelevu.

Naamini wengi wetu tumeshawahi kusikia au kuona ndugu, rafiki, jamaa, jirani fulani akiumwa mguu, mkono, bega au mgongo tena kwa maumivu makali sana.

Wengi wamehangaika hospitali nyingi bila mafanikio, wengine wamekimbilia kwenye huduma za maombezi na wengine wamekimbilia kwenye tiba mbadala na wengine wamekimbilia kwa Sangoma.

Kote huko wamekosa ufumbuzi wengine wamepoteza maisha na wengine wamepata kupooza kabisa mguu au miguu wakiwa wameshatuoa fedha nyingi sana na mateso makali.


Nilibahatika kufanya mazungumzo na baadhi ya waliowahi kupatwa na matatizo kama haya. Ndugu Selemani Mkoba alinielezea tatizo hilo lilivyomtesa na baada ya kuhangaika hospitali kwa zaidi ya miezi 3 wakati wote kiteseka kwa maumivu makali na kupoteza hela nyingi bila mafanikio aliamua kwenda kwa waganga wa kienyeji.



Anasema Mganga alimpa matumaini makubwa lakini wiki kadhaa zikawa zinapita bila kupata unafuu wowote. Anasema Mgonga alikuwa akimpa matumaini kwa kumwambia ugonjwa unaingia ghafla lakini kutoka unatoka taratibu sana . Ndugu Mkoba anasema kwa bahati alipomwelezea tatizo hilo mmoja wa rafiki zake ambaye si daktari alimwambia aondoke haraka huko na kuwahi Muhimbili. Rafiki yake huyo alimweleza kuwa analifahamu tatizo hilo.


Ndugu Mkoba amasema alienda Muhimbili kama alivyoshauriwa na rafiki yake, akafanyiwa kipimo cha MRI ambapo waligundua tatizo hilo katika uti wa mgongo na kupangiwa siku ya upasuaji. Alifanyiwa upasuaji na alipozinduka alikuwa na maumivu makali ya wastani yatokanayo na upasuaji tu .. maumivu ya mguu hayakuwepo tena. Maumivu yatokanayo na upasuaji yaliendelea kupungua na sasa ni miezi mitatu amebakiwa na maumivu madogo sana mbayo yanaendelea kupoteza huku akiendelea na mazoezi. Anaweza kuendesha Gari, anaweza kutembea na kufanya shughuli zake ambazo zilisimama. Aidha Ndugu Mkoba anasema angependa watu wajue hili ili wasi mateso aliyoyapata yeye na walio kwenye mateso hayo wapate ufumbuzi haraka maana ni mateso yanayotisha.



MGAWANYIKO WA UTI WA MGONGO NA MATOKEO YA DISCK ZINAPOCHEZA

Uti wa mgongo umegawanyika katika aina kuu zipatazo nne (4) za pingili “Spinal Vertebrae”
Cervical Curve: Hili ni eneo la juu la uti wa mgongo, Eneo hili linaanzia uti wa mgongo unpokutana na kichwa na kuishia eneo la mwisho la Shingo, kwa lugha nyepesi ndilo eneo linalomiliki shingo, pingili zilizopo katika eneo hili zinaitwa “Cervical Vertebrae”.

· Maeneo yanayoathiriwa na Disc kucheza katika eneo hili “Cervical Disc Herniation” ni Mikono au Mabega au kifua, moja wapo ya viungo hivi vitapata maumivu makali sana.


Thoracic Curve: Hili ni eneo la uti wa mgongo linalofuatia kuelekea chini likianzia inapoishia Shingo, Eneo hili linaishia katikati ya mgongo, kwa lugha nyepesi eneo hili ndilo linalomilike mbavu. Pingili zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa “Thoracic Vertebrae”.

· Kucheza kwa disck katika eneo hili kutakusababishia maumivu makali ya Mgongo eneo la juu ya Kiuno.

Lumbar Curve: Eneo hili linaanzia inapoishia Thoracic Curve na kuelekea chini na kukutana na Eneo linaloitwa Sacral Curve au eneo la kiuno linapoanzia. Eneo la Lumba linazungukwa na ma matumbo na mazagazaga mengine yasiyokuwa na mifupa. Pingili za uti wa mgongo zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa “Lumbar Vertebrae”

·
Ikiwa Disc zitacheza katika eneo hili mhusika atapata maumivu makali ya mguu maumivu ambayo yaukumba mguuu wote kuanzia sehemu ya ndani ya ---- na kushuka chini mpaka mwisho wa mguu kwenye kisigino.

Sacral Curve: Eneo hili linaanzia pale Lumbar Curve inapoishia hadi mwisho wa uti wa mgongo kwa chini. Katika lugha nepesi eneo hili ndilo linalomiliki kiuno. Pingili zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa “Sacral Vertebrae”



SABABU ZA MATATIZO HAYA

· Ajali ya Gari
· Kuanguka
· Kupigwa/kupigana
· Michezo
· Ajali katika sehemu za kazi
· Kasoro wakati wa kuzaliwa
· Kubeba vitu vizito
· Ukaaji mbaya wa muda mrefu
· Misukosuku mbali mbali ya mwili kama


MATIBABU

Tatizo hili linatibika ikiwa mgonjwa atawahi kufanyiwa uchunguzi sahihi na tatizo hilo kugundulika. Kuna matibabu ya namna tofauuti ambayo daktari anaweza kukupa lakini hali inapokuwa mbaya Madaktari hulazimika kufanya upasuaji. Mgonjwa anatakiwa kupimwa kwa vipimo sahihi na kipimo kinachoAMINIWA zaidi ni MRI. Aidha kwa bahati Tanzania moja ya nchi chache barani Afrika zenye mitambo hii ya MRI na moja ya nchi chache barani Afrika zenye madaktari bingwa wa matatizo haya.

Wadau badala ya ya kutumia fedha nyingi kwa waganga wa kienyeji tuwahi hospitali hususani Muhimbili kuonana na mabingwa wa NEURAL. Rai yangu kwa serikali pamoja na kuwa sisi tumekuwa moja katika nchi chache zenye huduma hii, mahitaji ya Madaktari hawa ni makubwa sana bado, Serikali ipeleke Madaktari zaidi nje kwa ajili ya kupatiwa ujuzi huu na kuongeza mashine za MRI angalau zifike 10.


NAMNA YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI

Matunzo mazuri ya ujauzito
Kuepuka kipigana au kupigwa, usimpige mwenzako kwasababu unaweza kumsababishia tatizo baadae
Kama unaendesha gari ama piki piki kuepuka mwendo unaoweza kukusababishia ajaili
Uangalifu katika michezo na mazoezi mazito
Kujilinda kiafya ili kujiepusha na maradhi yasiyotambulika
Tujiepusha na ukaaji mbaya wa muda mrefu katika sehemu zetu za kazi, pendelea kutafuta maelekezo jinsi ya kukaa katika sehemu yako ya kazi.
Pendelea kuangalia afya mara kwa mara na kupata ushauri wa madaktari.


MWISHO
Napenda kuwajulisha wasomaji wangu kuwa mimi si daktari, sijawahi kupitia fani hiyo nimeandika makala hii baada ya kupitia uzoefu mbali mbali, kuhoji waliowahi kupatwa na matatizo haya na kufanya utafiti kupitia mitandao mikubwa ya kitabibu Duniani, kwa kusoma kazi za madaktari bingwa katika mitandao hiyo. Kwa namna moja au zaidi inawezekana kuna mahali nimeweka maelezo yasiyo na usahihi kwa asilimia 100, naomba usiitumia taarifa hii kama sehemu ya matibabu, bali itumia taaruifa hii kuchukua hatua sahihi.