Showing posts with label FAIDA MBALI MBALI. Show all posts
Showing posts with label FAIDA MBALI MBALI. Show all posts

Thursday, 12 December 2024

FAIDA ZA MMEA WA MSEGESEGE KUMTIBU MTU ALIYEROGWA UCHAWI USIOTIBIKA KIRAHISI

 


1. Kama unahitaji kumtibia mtu aliyerogwa uchawi

usiotibika kirahisi au amezunguka sana kutafuta 

matibabu mbalimbali basi utakwenda katika mti huu kwa kufuata adabu za kuchukua mti kitiba kisha 

utachukua majani yake kisha 

utakwenda 

kuyapondaponda majani hayo kisha utachanganya 

katika maji yako ya kuoga na majani mengine utatia 

katika maji ambayo utakuwa unakunywa kiasi cha 

kikombe kimoja asubuhi na jioni,pia utakuwa 

unakoga maji hayo asubuhi na jioni kwa muda wa 

siku saba hadi 14.Kama kupata majani mabichi ya mti 

huo itakuwa ni vigumu basi utachuma majani mengi

kisha utayaanika alafu uyasage upate unga 

wake,kisha unga huo utakuwa unachanganya katika 

maji yako ya kuoga na unga mwingine utakuwa 

unaweka katika maji ya vugu vugu au katika uji wako 

kisha unakunywa.Hakika utakwenda kupona maradhi 

hayo.



KUFUKUZA NA KUONDOA MAJINI WA KICHAWI KATIKA MWILI


2. Kama unahitaji kufukuza majini wachafu katika 

mwili utachemsha majani ya mti huu kisha utatumia 

kumpigia nyungu mgonjwa anayesumbuliwa na 

majini wachafu katika mwili wake,tumia dawa hii 

asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba 

mfululizo.Inshaalla majini hao wataondoka haraka 

sana.



KUTIBU TATIZO LA KIFUA AU UGONJWA WA PUMU


3. Kama unahitaji kujitibu au kumtibu mtu

anayesumbuliwa na tatizo la kifua au pumu 

utakwenda katika mti huu kisha utachimba mizizi 

zake kisha utakwenda kuitwanga mizizi hiyo upate 

unga wake.Unga huo utatumia kiasi cha kijiko kimoja 

cha chai kuchanganya katika juisi ya asali(zile za 

kienyeji na sio za viwandani) au ataweka katika 

kikombe cha uji kisha utatumia kunywa kikombe 

kimoja asubuhi na jioni kwa muda wa siku 7-21.


DAWA YA KUONGEZA NYEGE KWA WANAWAKE

 

Iwapo kama unachangamoto ya kutopata hamu ya 

tendo la ndoa, hali hii husababishwa na matatizo 

ya homoni imbalance (homoni zinazosisimua 

kupata hamu ya tendo la ndoa .kama unahitaji 

kuondokana na changamoto hiyo basi tengeneza 

dawa ifuatayo;

MAHITAJI

1. unga wa kungu manga vijiko vya chakula 

viwili

2. unga wa tangawizi vijiko vya chakula viwili

3. unga wa ubuyu vijiko vya chakula viwili

4. unga wa pilipili mtama vijiko vya chakula viwili

5. unga wa mdalasini vijiko vya chakula viwili

6. Asali mbichi lita moja

MAANDALIZI

Utachanganya unga huo pamoja katika Asali na 

ukoroge vizuri hadi upate ujiuji mzito kabisa.

MATUMIZI

Mgonjwa atachukua vijiko vikubwa vya chakula 

viwili vya dawa hiyo na aweke kwenye maji ya 

vugu vugu kiasi cha glasi moja, kisha ukoroge 

vizuri na unywe.Utakunywa kutwa mara mbili 

glasi moja hadi dawa itakapokwisha.

JINSI YA KUTUMIA BAMIA KUONGEZA UTE UKENI

 


Bamia (okra) inajulikana kwa kiasi kikubwa cha nyuzinyuzi za majimaji, na hivyo inaweza kusaidia kuboresha ute wa uke.

Ifuatayo ni namna ya kutumia bamia kuongeza ute ukeni:

1. Osha Na Kata Bamia.
Anza kwa kununua bamia nzuri na safi. Osha bamia kwa maji baridi na kisha kata sehemu zote zisizohitajika, kama vile mashina na miisho.

Unaweza kukata bamia kwa vipande au kuiacha yote kulingana na jinsi unavyopenda.

2) Chemsha Bamia.
Weka bamia katika sufuria ya maji yanayochemka na chemsha kwa muda wa dakika 5-7 au hadi iwe laini lakini isiyoiva sana.

Usipike bamia kwa muda mrefu sana kwani inaweza kuwa laini sana na kupoteza manufaa yake ya nyuzinyuzi.

3) Kula Bamia.
Baada ya kuandaa na kuchemsha bamia sasa unaweza kula bamia iliyopikwa.

Bamia pia inaweza kuchanganywa na mboga nyingine.

4) Kujaribu Juisi Ya Bamia.
Unaweza pia kutengeneza juisi ya bamia kwa kusaga bamia iliyokatwa vizuri na maji, na kisha kunywa juisi hiyo. 

Juisi ya bamia inaweza kuwa njia rahisi ya kuchukua faida ya nyuzinyuzi za majimaji katika bamia.

HITIMISHO:

Ni muhimu kumbuka kwamba kula bamia mara kwa mara inaweza kusaidia kusawazisha uzalishaji wa ute ukeni, lakini hakuna chakula au nyongeza ya chakula inayoweza kutoa matokeo ya haraka.

Ili kuongeza ute ukeni na kuboresha afya ya uke kwa ujumla, ni muhimu kudumisha lishe bora na afya, kunywa maji ya kutosha, na kuepuka mambo yanayoweza kusababisha ukavu wa uke kama vile msongo wa mawazo, dawa zinazosababisha ukavu, na bidhaa za kuosha uke zenye kemikali nyingi.




Saturday, 15 April 2023

FAIDA YA KULA MAGANDA YA NDIZI MBIVU KIAFYA.

 




Watu Hula Maganda ya Ndizi. 

Wewe Unazijua Faida Zake?

How healthy are bananas? Bananas are rich in Vitamin B6 and a good source of fiber, vitamin c, magnesium and potassium. 

Bila shaka hujawahi kuona mtu akila maganda ya ndizi kutokana na ukweli kwamba kinacholiwa ni kilicho ndani na kutupa ganda. 

Hata hivyo katika nchi za Asia, kama vile India, watu wamekuwa wakila ndizi na maganda yake kwa miaka mingi sasa.

Tofauti na ndizi yenyewe, ganda lake huwa gumu kidogo na lina uchungu ambao si rahisi mtu kupenda kula na ndiyo sababu watu wengi hawawezi kula maganda ya ndizi. 

Lakini pamoja na uchungu wake, kuna virutubisho muhimu sana ndani yake ambavyo tutakupa siri na sababu kwa nini uwe unakula na maganda ya ndizi pia.

Utafiti uliofanyika umebaini kuwa, Maganda ya ndizi mbivu yana kiwango kingi zaidi cha Vitamin B6 na B12 pamoja na madini ya Manganizi (Magnesium) na Potasia (Potassium) kuliko ndizi yenyewe. 

Hivyo unapokula ndizi na kutupa maganda yake unakuwa umetupa virutubisho vingi zaidi kuliko ulivyokula.

Aidha, utafiti unaonesha ndizi ina asilimia 8 ya kiwango cha madini ya Manganizi kinachohitajika kila siku na mwili, madini haya ni muhimu kwa kurekebisha kiwango cha sukari mwilini na shinikizo la damu.

Kiwango cha madini ya potasia kilichomo kwenye ndizi ni asilimia 12 ya mahitaji ya kila siku ya mwili ambayo ni muhimu katika ukuaji wa seli za mwili.

Asilimia 17 ya mahitaji ya mwili ya kila siku kwa upande wa kamba lishe (fiber) utaipata kwa kula ndizi. 

Kirutubisho hiki ni muhimu katika usagaji wa chakula na kupunguza hatari ya mtu kupatwa na kisukari.

Kwa upande wa vitamin B6 na B12, ndizi inatoa kiasi cha asilimia 20 ya mahitaji ya kila siku ya mwili wa binadamu.

 Vitamini hizi ni muhimu katika zoezi la kugeuza chakula tunachokula kuwa nishati inayohitajika mwilini.

Ili kupata faida za kutosha za ndizi mbivu, inashauriwa kula ndizi iliyoiva kama tulivyoona wiki iliyopita na pia ule na maganda yake ambayo huwa laini kutafuna na matamu kadri ndizi inavyoiva zaidi. 

Kama hutaweza kula ganda zima, basi angalau hakikisha unalamba nyama na nyuzi nyuzi zote zinazobaki kwenye ganda baada ya kumenya, kwani hivyo ni virutubisho muhimu sana katika mwili wako

Wednesday, 22 December 2021

MAZIWA NA UNGA WA KARAFUU NI TIBA YA MARADHI MENGI

 

MAZIWA NA UNGA WA KARAFUU NI TIBA YA MARADHI MENGI.
Kijiko kidogo cha Unga wa karafuu ya kusaga changanya na glasi moja ya maziwa Kunywa kwa siku 1X3 kabla ya kula kitu tumboni inatibu Maradhi haya hapo chini👇
1- Ugumba.
2- Udhaifu wa kijinsia.
3- Udhaifu wa moyo, tumbo, ini, wengu na figo.
4- Mishipa ya moyo na viungo.
5- Maumivu ya viungo.
6- Pumu, kohozi, kikohozi na pua iliyojaa.
7- Kwikwi
8- Usagaji chakula duni tumboni
9- Matatizo ya Kumbukumbu mbaya na kutokuelewana.
10- Gesi kwenye tumbo na utumbo.
11- Udhaifu wa misuli ya kibofu, kukojoa bila hiari na kushindwa kujizuia mkojo.
12- Udhaifu na maumivu ya fizi na meno.
13- Udhaifu wa jumla na uchovu.
14- Hedhi mara mbili kwa mwezi
15- Udhaifu wa kuona na macho.
16- Chunusi, magonjwa ya ngozi na kuumwa na wadudu.
17 - Inadhibiti sukari ya damu na kudumisha viwango vyake.
18- Baridi na Maradhi ya kifua..
19- Maumivu ya koo na Mafindofindo.
20 - husaidia kuzuia saratani.
21 - Wasiwasi, unyogovu na hali ya kisaikolojia.
22- Bawasiri na uvimbe kwenye Tundu ya Haja kubwa.
23 - vidonda vya tumbo na maambukizi.
24- Upungufu wa Kinga mwilini na kinga kwa ujumla

Tuesday, 4 May 2021

MIMEA YA KUSAFISHA TUMBO ILI LIWE SAFI. LAXATIVES HERBS


Laxatives: Medicines producing gentle action of the bowels. Laxatives are used for non-persistent constipation. Sometimes it is given with a carminative to prevent griping.


Herbs for laxatives

Pansy Herb
Cascara Bark
Turtle Bloom Leaves
Balmony Leaves
California Barberry Root
Culvers Root
Dandelion Root
Rhubarb Root
Oregon Grape Root
Virginia Poke Root
Cape Aloe
Sacred Bark
Wahoo Bark
Alder Bark (Europ. Black)
Indian Senna Fruit
Senna Leaves
Blackthorn Flowers
Mandrake Root
May Apple Root
Buckthorn Bark
Mountain Grape
Senna Pods
Hart’s Tongue
Fringe Tree
Wormwood 

References

https://italisvital.info/laxatives-herbs/



 

Tuesday, 28 July 2020

FAIDA ZA KUPAKA MAFUTA NYAYONI WAKATI WA KULALA USIKU



KUPAKA MAFUTA NYAYONI

1. Mwanamke mmoja anasema babu yake aliishi miaka 87 bila ya kuumwa na mgongo, viungo, kichwa, meno wala mwili baada ya kufunzwa siri na mzee mmoja wa Kolkata alipokuwa anafanya kazi ya kuweka mawe juu ya reli akamuambia apake mafuta nyayoni kabla kulala.

2. Mwanafunzi mmoja anasema mama yake alikuwa anahakikisha kila siku lazima apake mafuta nyayoni kabla kulala. Na yeye alipodhoofika macho mama yake alimuanzilisha dawa hii na macho yako yakapona.

3. Mfanyabiashara mmoja anaeleza kuwa alipoenda safari mji wa Chitral kwa likizo alishindwa kupata usingizi na akatoka nje kutembea. Askari wa hotel ile akamuuliza shida ni nini, akamuambia hapati usingizi. Yule askari akamuuliza kama anayo mafuta, akasema hana. Askari akamletea mafuta kwenye kichupa akamuambia kusugua nyayoni dakika chache. Baada ya muda mfupi alikuwa anakoroma usingizini.

4. Mimi pia nimeanza kusugua mafuta nyayoni mwangu usiku kabla kulala, sasa nalala vizuri na sina machofu.

5. Nilikuwa na maumivu ya tumbo. Baada ya kusugua mafuta nyayoni siku mbili tu nikapona maumivu.

6. Hii dawa ni kama uchawi. Nilisugua mafuta kwa nyayo yangu kabla kulala usiku na nilipata usingizi mtamu sana.

7. Mimi natumia hii dawa kwa miaka 15 sasa na inanipa usingizi muruwa sana. Nawasugulia wanangu pia nyayoni na wamekuwa na afya njema.

8. Miguu yangu ilikuwa inaniuma sana, nilianza kusugua nyayo yangu kwa mafuta kwa dakika mbili kila usiku kabla ya kulala. Maumivu yangu imepotea yote.

9. Miguu yangu ilikuwa imevimba na nilikuwa nachoka haraka kila napotembea. Nilipoanza kusugua nyayo zangu kwa mafuta, zimerudi kawaida baada ya siku 2 na machofu pia imepotea.

10. Nilianza kusugua mafuta kwenye nyayo yangu kwa dakika mbili kila usiku kabla kulala na nimeanza kupata usingizi mtamu sana.

11. Hii dawa ni ya ajabu sana. Ni bora kuliko vidonge vya usingizi. Sasa nasugua mafuta kwenye nyayo kila usiku kwa ajili ya kupata usingizi murwa.

12. Babu yangu alikuwa anawashwa nyayo na maumivu ya kichwa. Alianza kusugua mafuta ya boga nyayoni na mwasho pamoja na maumivu ya kichwa ilipotea.

13. Nilikuwa na ugonjwa wa thyroid na ilikuwa inasababisha maumivu makali miguuni. Niliambiwa nianze kusugua mafuta kwanyayo kabla kulala. Sijaacha hata siku moja. Sasa sina maumivu.

14. Miguu yangu ilifanya mapele. Nilipoanza kusugua mafuta kwenye nyayo kabla kulala nilikuta tofauti kubwa baada ya siku nne tu.

15. Nilikuwa nina bawasili miaka 13 iliyopia. Sahib wangu mmoja alinipeleka kwa mhenga mmoja mwenye umri wa miaka 90. Alinishauri nianze kusugua mafuta kwa vidole vya mikono, kwenye kucha na pia matone machache kwenye kitovu. Nilianza kutekeleza ushauri wake hakimu na nilipata unafuu mara mmoja mpaka kwenye tatizo la kupata choo. Machofu ya mwili yalipotea na pia kukoroma usingizini, nilijsiikia huru.

16. Dawa ya kusugua mafuta kwenye nyayo ni dawa mujarrab.

17. Kusugua mafuta kwenye nyayo yangu ilinisababishia kupata usingizi haraka.

18. Nilikuwa naumwa na miguu na magoti lakini tangu nimeanza kusugua mafuta kwenye nyayo kila usiku nimepata nafuu na Napata usingizi mtamu.

19. Tangu nimeanza kusugua mafuta kwenye nyayo yangu kila usiku kabla kulala nimepata nafuu kwenye maumivu ya mgongo na Napata usingizi murwa sana.

Siri yenyewe ya kutoka India ni sahali, nyepesi na fupi sana kwa kila mtu popote alipo: Sugua mafuta ya aina yoyote – ikiwa ni ya zaituni au yay a haradali – kwenye nyayo yako kwa muda wa dakika tatu na ukiweza kwenye guu zima kwa muda wa dakika tatu zingine kila guu. Usisahau wala usidharau hata siku moja kusugua mafuta kwenye nyayo na uwasugulie watoto pia hivyo hivyo. Ifanye kuwa desturi kwenye maisha yako kisha usubiri kuona matokeo ya qudra. Kama unavyochana nywele yako kila siku basi uwe unasugua mafuta kwa nyayo kila siku.

Kwa mujibu wa tiba ya asili ya kichina, nyayo za binadamu zina nukta zaidi ya mia zenye kutibu viungo mbalimbali vya mwili zinaposuguliwa. Tumia Mafuta ya Zaituni au Mafuta ya Nazi kujipaka Unyayoni.

Thursday, 24 May 2018

FAIDA ZA SIKI YA TUFAHA .BENEFITS OF APPLE CIDER VINEGAR


FAIDA ZA SIKI YA TUFAHA (APPLE).
(ORGANIC APPLE CIDER VINEGAR)
Huzuia homa ya mafua
Huzuia ugonjwa wa tumbo,
Hutibu bawasiri
Huondosha mawe kwenye figo
Inaweka uzuri katika mwili
Husaidia maradhi ya kansa
Husaidia kupunguza shinikizo maradhi ya pua na maambukizi
Hupunguza Mapigo ya Damu
Kupunguza cholesterol
napunguza kuvimba relives arthritis,
Husaidia kutubu pumu na Uzio wa hali na nguvu nywele,
Husaidia kupunguza Maradhi ya guti,
Hutibu Kuvu, upele, bakteria
Husaidia kushusha chini sukari iliyozidi kwa mgonjwa wa kisukari,
Hupunguza maumivu ya kuumwa na mdudu
Husaidia kupunguza uzito wa mwili kwa kutibu hamu ya kupenda kula na kuondosha kwa chini mafuta kujikwamua
Hupunguza au kuzuia kuwashwa washwa kwa mwili .
Husaidia kupunguza kipanda uso

Monday, 5 September 2016

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.




MBOGA YA MCHICHA HUTIBU MARADHI YAFUATAYO

Kuumwa mgongo

Kusafisha njia ya mkojo

Kusafisha damu

Unatibu tigo

Unatibu minyoo

Unatibu damu

Baridi yabisi

Tezi la shingo

Homa

Kuongeza damu

Unatibu maumivu

Tonic ya nywele

Unasaidia kupata haja ndogo kwa wingi

MATAYARISHO

Chukua mchicha kilo 1 chemsha maji lita 2 na nusu.
Yakichemka loweka mchicha kwa dakika 15. Tumia kikombe. Ni bora utumie yote kwa siku . Dozi ni siku 5

KUTIBU MGONGO

Chukua mchicha ponda. Chua mara 3 kwa siku. Usiku unapasha moto mchicha kisha unufunga mahali panapouma. Lala nao wakati vuguvugu la joto lake lenye maji ndani (dawa) ikiingia ndani fanyahivyo kwa siku 5, ukibadilisha kila siku (fresh)

TIBA YA TEZI LA SHINGO

Chukua mchicha kiasi kidogo, ponda, fungia shingoni pale penye uvimbe wakati unapolala kwa kitambaa, kwa muda wa siku 5.

Friday, 20 May 2016

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KULA MAYAI NA MAMBO MENGINE

MAYAI SIO CHAKULA TU. YANA FAIDA INGINE HII HPA CHINI....
YAI limekuwa na matumizi kama chakula kwa muda mrefu, wapo ambao hutumia chakula hicho kwa kukaanga, kuchemsha, kunywa likiwa bichi na au kuchanganya katika vyakula vingine mbalimbali.Lakini pia kuna matumizi ya Yai zaidi ya chakula, kwani linauwezo mkubwa wa kurutubisha ngozi, nywele na pia kuondoa uchovu.
Jinsi ya kufanya ukitaka kutumia Yai kuboresha muonekano wa ngozi na nywele zako.
Chukua Yai, changanya na asali kijiko kimoja cha chai mafuta ya Olive .Chukua mchanganyiko huo kisha pakaa usoni na shingoni, kaa nao kwa dakika kumi hadi 15. Hii itasaidia kama una mashimo usoni yatokanayo na chunusi kubana.
Pia itasaidia kulainisha ngozi yako na kuwa nyororo, mchanganyiko huu pia utasaidia kukuondolea michubuko au alama za kuungua na jua, mafuta au krimu usoni.Unaweza kutenganisha kiini cha Yai na ule ute mweupe, kisha chukua ute weka kwenye kikombe au bakuli, baada ya hapo pigapiga ule ute hadi uwe na mapovu kisha chukua povu, linawe usoni au paka mwili mzima kisha liache likauke.
Baada ya hapo osha na maji ya uvuguvugu, ukifanya hivyo mara kwa mara itakusaidia kufanya ngozi yako iwe anga’avu.Kama umetoka kazini na unaonekana umechoka na unataka kutoka usiku, chukua ute wa yai na pakaa chini ya jicho na uache kwa dakika 10 hadi 15 kisha safisha, itasaidia kuondoa muonekano wa uchovu katika macho yako.
Iwapo unasumbuliwa na kuwashwa ngozi, matumizi ya Yai pia ni njia sahihi kuepuka tatizo. Maski ya Yai ina utajiri wa ‘Acid’ za Amino ambazo husaidia kupunguza na kuondoa miunguzo au muwasho mwilini kutokana na protini inayopatikana kwenye Yai.
Kama unawashwa mwili mzima, chukua ute wa yai kidogo halafu nyunyiza katika maji utakayoyaoga sambamba na sabuni ya kuogea ndani ya siku chache utaona matokeo.
Kwa upande wa nywele wale ambao, nywele zao hazina afya au ukuaji wao ni hafifu wanaweza kupaka yai kichwani, hakikisha inagusa mizizi inayosaidia kuotesha nywele, kama nilivyoeleza awali protini iliyopo kwenye yai ndio chanzo cha kila kitu.Unaweza kutumia Yai kama ‘Hair Conditioner’, chukua kiini chake changanya na asali, mafuta ya watoto na maji kidogo.
Changanya vizuri kisha paka kichwa kizima acha kwa dakika 20 kisha osha na maji ya baridi chukua ute mweupe changanya na shampoo yako kidogo.

FAIDA 11 ZIPATIKANAZO KWA KUNYWA MAJI YA NDIMU..


Umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini,lakini kunywa maji yenye ndimu na vuguvugu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku. 
Vitamin C nyingi iliyomo katika limao na ndimu ni siri ya faida za tunda hili,ukiachia vitamini C ndimu ina 
vitamini B-complex, madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa(apple) au Zabibu).
Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi huwapa tabu baadhi ya watu,wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na radha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida.
Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao na katika makala hii tunazitaja faida 11 muhimu.

Faida 11 Za Kunywa Maji Yenye Ndimu

Faida #1: Huchochea Mmeng’Enyo Wa Chakula Tumboni
Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.
Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

Faida #2: Huboresha Kinga Za Mwili
Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

Faida #3: Husaidia Unyonywaji Wa Madini Mwilini
Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

Faida #4: Husaidia Kinga Dhidi Ya Saratani
Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicals mwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

Faida #5: Husaidia Kupunguza Hatari Ya Kiharusi
Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic (ischemic stroke) hasa kwa wanawake.
Soma pia: Madhara ya kula chumvi nyingi kwa afya ya binadamu

Faida #6: Usafishaji Wa Mwili Na Damu
Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

Faida #7: Kurekebisha Sukari Katika Mwili
Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.
Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

Faida #8: Dawa Ya Kikohozi Na Mafua
Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

Faida #9: Inasaidia Urekebishaji Wa Ngozi Na Kupona Makovu
Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.
Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

Faida #10: Husaidia Kupungua Uzito
Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

Faida #11: Kuondoa Harufu Ya Mdomo
Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.

Anza Siku Kwa Kunywa Maji Yenye Ndimu Kila Siku
Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.
Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.
Anza leo kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku asubuhi na uone mabadiliko ndani ya mwili wako

Sunday, 15 May 2016

FAIDA ZA KIAFYA ZA KITUNGUU MAJI.


FAIDA ZA KIAFYA ZA KITUNGUU MAJI.....
Zifuatazo ni faida za kiafya za kitunguu maji.
1. Juisi ya Kitunguu Huua vijidudu vya kifua kikuu.
Tafiti mbalimbali za kisayansi zimethibitisha kuwa juisi ya kitunguu ina uwezo wa kuua vijidudu vinavyo sababisha maradhi ya kifua-kikuu (Huua baada tu ya mgonjwa kunusa moshi wake)
2. Kitunguu maji huongeza hamu ya kula.
Kitunguu maji kikifanyiwa kuwa achari, ukali wake hupungua huongeza mno hamu ya kula.
3. Huupa mwili nishati na nguvu
Kitunguu maji kikiliwa kikiwa kimechomwa, huongeza nguvu na nishati mwilini na huimarisha misuli ya mwili.
4. Huufanya uso kunawiri
Kitunguu maji kikichomwa na kasha kuliwa huufanya uso kuwa mweupe, mn’gavu na wenye kunawiri.
5. Kitunguu maji huongeza hamu ya kula
6. Kitunguu husaidia kulainisha tumbo
7. Kitunguu husaidia kutibu tatizo la kukosa haja kubwa
8. Kitunguu maji kikipikwa na kuliwa pamoja na samli , husaidia kuongeza nguvu za kiume pamoja na kuboresha nguvu za kiume.
9. Kitunguu kikitengenezwa supu pamoja na nyama, huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.
10. Kitunguu maji husaidia kutibu homa ya manjano.
11. Kitunguu maji husaidia kuvunja vijiwe tumboni
12. Kitunguu maji hutumika kutibu tatizo la kukosa hedhi kwa wanawake
13. Kitunguu maji kina utajiri wa Vitamini C ambayo husaidia kuzuia kukua kwa bacteria kwenye jeraha na kuongeza nishati kwenye mbegu za kiume.
14. Kitunguu maji kina madini ya salfa,chuma na vitamin ambayo husaidia kutia nguvu kwenye mishipa
15. Kitunguu maji husaidia kuwatibu wagonjwa wa kisukari.
16. Kitunguu maji husaidia kutibu maradhi ya moyo pamoja na kuimarisha mfumo wa mzunguko wa damu mwilini.
17. Kitunguu maji kimethibitika kuwa vijiuasumu vyenye nguvu zaidi kuliko penesilini (penicillin) kwa hivyo hupoza kifua kikuu, kaswende (syphillis) na kisonono (gonorrhea), pamoja na kuua vijidudu vingi vya hatari.
18. Hutibu tatizo la Pumu:
Kitunguu maji kikitumika pamoja na asali, husaidia kutibu tatizo la pumu.
19. Husaidia kutibu tatizo la Uvimbe wa pafu (Pneumonia )
18. Kituu maji husaidia kutibu tatizo la Saratani za aina mbalimbali.(Cancer):
20. Kitunguu maji husaidia kutibu vidonda ndugu.
21. Kitunguu maji husaidia kutibu tatizo la mvilio wa damu
22. Kitunguu maji husaidia kutibu majipu
23. Husaidia kutibu tatizo la Chunusi
24. Husaidia kuondoa tatizo la Ukurutu (Eczema) kwenye ngozi.
25. Husaidia kutibu Saratani ya ngozi.
26. Husaidia kutibu matatizo ya figo.
27. Husaidia kutibu tatizo la Kikohozi kwa wakubwa na wadogo
28. Husaidia kutibu maradhi ya macho na Kikohozi
29. Husaidia kupunguza uzito wa mwili

Thursday, 31 December 2015

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA LIMAU KWA CHAKULA NA MATIBABU





Faida za limau au ndimu zinajumuisha matumizi kama tiba kwa ajili ya vidonda vya kooni, matatizo katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya meno, homa, kuvuja damu ndani ya mwili, baridi yabisi, kutibu malengelenge, uzito kupita kiasi, matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kipindupindu na shinikizo la juu la damu. Pia ni dawa nzuri kwa ajili ya nywele na ngozi.
Tangu karne nyingi limau linajulikana kama dawa, husaidia pia kuongeza kinga ya mwili, kusafisha tumbo na hujulikana pia kwa kazi yake nzuri ya kusafisha damu.
Juisi ya limau ina faida kadhaa nyingi kama vile kuondoa mchanga katika figo, kupunguza kukamaa kwa mishipa (strokes) na kupunguza joto la mwili. Kama kinywaji ambacho huondoa uchovu mwilini, juisi ya limau itakusaidia kubaki mtulivu na mpole.
Faida nyingi za limau zinatokana na virutubishi vyake vingi mhimu kwa mwili kama vile vitamini C, vitamini B6, vitamini A, vitamini E, folate, niacin thiamin, riboflavin, pantothenic acid, shaba, kalsiamu, chuma, magnesium, potassium, zinki, phosphorus na protini.
Limau ni matunda ambayo yana kitu mhimu sana katika kuondoa sumu mwilini kiitwacho kwa kitaalamu kama “flavonoids” ambacho chenyewe ni mhimu sana katika kupigana na kansa mbalimbali mwilini.
Limau husaidia pia kuzuia matatizo ya kisukari, kufunga choo, shinikizo la juu la damu, homa, husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri na matatizo mengine mengi yakiwemo kuimarisha ngozi ya mwili, nywele na meno.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Madaktari wa magonjwa ya mfumo wa mkojo cha Marekani (American Urological Association) unaonyesha kuwa juisi ya limau au ‘lemonade’ inaweza kuondoa au kuzuia kujitokeza kwa mawe kwenye figo.
Watu hutumia limau kutengeneza juisi ya limau maarufu kama “lemonade” kwa kuchanganya pamoja maji maji ya limau, maji na asali au hata sukari ya kawaida. Watu wengi pia hutumia limau katika kusafisha au kuosha vyombo sababu ya uwezo wa kuondoa madoa na uchafu mwingine kirahisi zaidi.
Marashi au harufu ya limau hufukuza mbu, wakati huo huo kuinywa juisi ya limau iliyoongezwa mafuta ya zeituni husaidia kuondoa mchanga katika kibofu cha mkojo. Limau inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi na hutumika kwa namna nyingi tofauti.
Zifuatazo ni faida mbalimbali za limau mwilini:
1. Kufunga choo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula
Juisi ya limau husaidia kutibu matatizo yahusianayo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula na kufunga choo. Ongeza matone machache ya limau kwenye chakula chako (kuwa makini sababu limau huwa haipatani na maziwa), na itakusaidia katika kumeng’enya chakula.
Limau hufanya kazi kama wakala msafisha damu na mwili kwa ujumla. Na hii ni nzuri kama unapata juisi yako ya limau baada ya chakula cha mchana au cha usiku. Juisi ya limau inatengenezwa kwa kuchanganya maji ya limau, maji kidogo, chumvi ya mawe kidogo na asali au hata sukari. Weka na barafu kidogo pembeni.
Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.
2. Hutibu homa
Juisi ya limau inaweza kumtibu mtu anayesumbuliwa na homa, mafua au baridi. Limau husaidia kutibu homa kutokana na sifa yake ya kuongeza kiasi cha jasho mwilini.
3. Huongeza afya ya meno
Juisi ya limau mara nyingi imetumika katika kulinda afya ya meno. Kama juisi fresh ya limau itanyunyizwa juu ya jino linalouma inaweza kusaidia kuondoa maumivu. Kusugua (masaji) juisi ya limau juu ya fizi za meno kunaweza kusaidia watu wenye matatizo ya kutokwa damu kwenye fizi huku ikiondoa harufu mbaya katika fizi na mdomo kwa ujumla.
Unaweza kupata faida hizi kama utakuwa unapiga mswaki ukitumia dawa yenye limau ndani yake (lemon tooth paste).
4. Hutunza nywele
Juisi ya limau imejidhihirisha yenyewe kuwa dawa nzuri kwa upande wa matatizo mbalimbali ya nywele. Juisi ya limau ikipakwa kwenye ngozi ya kichwa inaweza kutibu matatizo kama ya mba, kupotea au kukatika kwa nywele, na matatizo mengine yahusuyo nywele na ngozi ya kichwa.
Kama utakuwa ukisafisha nywele zako kwa kutumia juisi au maji ya limau moja kwa moja basi utazifanya nywele zako zipate mng’aro wake wa asili bila gharama yoyote ya ziada.
5. Hulinda ngozi
Kwakuwa Juisi ya limau ni dawa ya asili dhidi ya bakteria, inaweza pia kutibu matatizo mbalimbali ya ngozi. Juisi ya limau inaweza kutumika kupunguza maumivu kwenye ngozi sababu ya kuungua na jua, pia husaidia kupunguza maumivu kutokana na kung’atwa na nyuki. Juisi ya limau au majimaji ya limau yanaweza kutumika kupakaa juu ya ngozi na kutibu chunusi na ukurutu.
Limau pia hutumika kama dawa ya kukufanya usionekane mzee kwakuwa yenyewe huondoa mikunjo na madoadoa ya ngozi.
Kunywa maji ya limau yaliyochanganywa na asali kunasaidia ngozi kuwa na afya zaidi na hata ukipekuwa huko sokoni utazipata baadhi ya sabuni ambazo zimetengenezwa kutokana na limau.
6. Hutibu majeraha ya moto
Upakaji wa maji ya limau (juisi) kwenye eneo la ngozi lililoungua huweza kusaidia makovu kupotea na hii husaidia pia kwa mtu aliyepatwa na malengelenge au vipele vyenye maji maji yanayouma ndani. Na kwa sababu limau ni wakala wa kupooza au wakala mtulizaji (cooling agent), huweza kupunguza maumivu au kuhisi kuungua kwenye ngozi hasa wakati unakuwa na majeraha yanayounguza ngozi.
7. Huzuia kuvujika kwa damu
Limau inayo sifa ya kudhibiti bakteria mwilini (antiseptic properties) na kugandisha damu, sifa hizi au kazi hizi mbili za limau husaidia kusimamisha kuvuja kwa damu ndani ya mwili. Unaweza kutumia maji ya limau ukiweka kwenye kipande cha pamba na kuiweke puani kuzuia pua kuvuja damu.
8. Hupunguza Uzito
Ikiwa utakunywa juisi ya limau iliyochanganywa na asali na maji ya uvuguuvugu, hasa asubuhi tu unapoamka inaweza kusaidia kupunguza uzito.
9. Hutibu matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji
Juisi ya limau husaidia katika kutuliza matatizo katika mfumo wa upumuwaji kama vile pumu. Kwakuwa limau ina kiasi kingi cha vitamini C, husaidia kutibu na kutuliza matatizo ya muda mrefu kwenye mfumo wa upumuwaji.
10. Kipindupindu
Magonjwa kama kipindupindu na malaria yanaweza kutibika kwa kutumia juisi ya limau tu kwa sababu limau hufanya kazi ya kusafisha damu na mwili kwa ujumla.
11. Hutuliza maumivu ya miguu
Limau huwa na harufu ya kuvutia (aromatic) na pia inayo sifa ya kudhibiti bakteria na hutumika kutuliza maumivu au miguu kuwaka moto. Ongeza juisi (maji ya limau) kwenye dishi lenye maji ya moto kidogo na utumbukize miguu kwa dakika kadhaa kwa kuondoa haraka maumivu ya miguu na utajisikia umepata tulizo fulani (relaxed).
12. Baridi Yabisi
Limau au ndimu pia ni kikojoshi, yaani ni kitu kinachosisimua uzalishwaji wa mkojo na kwa sababu hiyo inaweza kutibu baridi yabisi na maumivu ya kwenye mishipa. Husaidia kutoa nje bakteria wabaya na sumu mbalimbali mwilini.
13. Hutibu malengelenge (Corns)
Juisi ya limau inaweza kusaidia kukausha malengelenge au vipele ambavyo huwa na majimaji ambavyo hujitokeza mara nyingi chini ya unyayo au katikati ya vidole vya mikono. Kunywa juisi ya limau na maji ndani yake husaidia wagonjwa kupunguza mawe kwenye nyongo.
14. Hutibu maambukizi ya kwenye koo
Limau ni tunda bora kabisa ambalo hupigana dhidi ya matatizo yanayohusiana na maambukizi kooni sababu ya sifa yake kubwa ya kudhibiti bakteria mwilini.
15. Hutibu shinikizo la juu la damu
Kunywa juisi ya limau kuna msaada mkubwa kwa watu wenye matatizo ya moyo kwa sababu limau lina kiasi cha kutosha cha potasiamu. Limau hudhibiti shinikizo la juu la damu, kizunguzungu, na uchovu sugu kwa sababu yenyewe limau hutoa hisia za utulivu kwa mwili na roho pia. Mara nyingi limau imetumika kwa watu wenye mfadhaiko wa akili na majonzi.

Wednesday, 3 December 2014

FAIDA 10 ZA KUTUMIA MAFUTA YA NAZI



1. Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo:
Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.
2. Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula:
Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.
3. Mafuta ya nazi hung’arisha ngozi:
Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji.
4. Huongeza nguvu mwilini:
Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ‘medium chain triglycerides – MCT’ ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa ‘ketones’ ambacho ni chakula cha ubongo. Kwahiyo ikiwa unatafuta lift ya kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.
5. Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya:
Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya. Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!
6. Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama:
Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula. Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki kuwa magumu hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.
7. Huzuia maradhi mengi hatari mwilini:
Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric acid. Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini. Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mine na utaona maajabu.
8. Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu:
Hii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
9. Hutumika kulainisha uke mkavu:
Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.
10. Husaidia katika ugonjwa wa mzio/aleji:
Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza, moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.
MHIMU: Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani ile ya asili. Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.