Showing posts with label MAGONJWA YA WANAWAKE. Show all posts
Showing posts with label MAGONJWA YA WANAWAKE. Show all posts

Tuesday, 26 January 2016

UPUNGUFU WA DAMU KIPINDI CHA UJAUZITO (ANAEMIA IN PREGNACY)


Upungufu wa damu (anaemia) hutafsiriwa kama kupungua kwa kiwango cha hemoglobin katika damu damu chini ya kiwango kinachokubalika kiafya. Kiwango cha kawaida cha haemoglobin (Hb) katika mwili wa
binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu. Hata hivyo shirika la afya duniani (WHO) linatambua kiwango cha mpaka 11gm/mililita kuwa cha kawaida kwa mama mjamzito. Hivyo basi mjamzito mwenye kiwango chochote cha haemoglobin chini ya 11 gm/mililita
hutafsiriwa kuwa na upungufu wa damu. Hata hivyo nchi nyingi hasa zinazoendelea hutambua kiwango cha mpaka gramu 10 kwa mililita kuwa ni upungufu wa damu kwa mjamzito.Kwa mjamzito anayehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza, upungufu wa damu kipindi cha ujauzito humaanisha kiwango cha hemoglobin chini ya <11.0 g/dL, na mimba inapofikisha wiki 28 upungufu wa damu hutambuliwa iwapo hemoglobin itashuka na kuwa chini ya 10.5 g/dL.
Kwa kuzingatia hilo, mama mjamzito hushauriwa kupima wingi wa damu siku anapohudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na pindi mimba inapofikisha wiki 28.
Viwango vya Anaemia
Upungufu wa damu unaweza kugawanywa katika viwango vikuu vinne, yaani upungufu wa damu wa kawaida (mild anaemia) ambao ni kati ya 9-11 gm/ml, upungufu wa damu wa kati (moderate anaemia) ambao ni kati ya 7-9 gm/ml, upungufu wa damu mkali (severe anaemia) ambao ni kati ya 4-7 gm/ml na upungufu wa damu mkali zaidi (very severe anaemia) ambao ni chini ya 4gm/ml.
Mzunguko wa madini ya chuma mwilini
Kwa kawaida mwili wa mwanamke huifadhi gramu 3.5 mpaka 4.5 za madini ya chuma. Asilimia 75 huifadhiwa kama hemoglobin katika chembe damu nyekundu, asilimia 20 kama ferritin katika mifupa na asilimia 5 inayobaki huifadhiwa katika misuli na vimengenyo vingine vya mwili.
Wanawake wasio wajawazito hupoteza karibu gramu 1 za madini ya chuma kutoka katika seli za mwili zinazokufa kila siku na gramu 1 zaidi kila siku wanayokuwa kwenye hedhi.
Ukubwa wa tatizo
Upungufu wa damu kipindi cha ujauzito ni tatizo linalowakumba kina mama wajawazito wengi sana, siyo tu Tanzania bali nchi nyingi zinazoendelea. Inakisikiwa kuwa karibu theluthi moja ya wajawazito katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito hukumbwa na tatizo hili.
Kwa mujibu wa WHO, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 56 ya wajawazito huko kusini mashariki ya Asia hukumbwa na tatizo hili. Kwa hapa Tanzania, hakuna takwimu sahihi kuhusu tatizo hili. Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mtoto ikiwemo kifo.
Chanzo cha upungufu wa damu wakati wa ujauzito
Kipindi cha ujauzito huambatana na mabadiliko mbalimbali ya mwili. Moja ya mabadiliko hayo ni ongezeko la maji (plasma volume) katika mzunguko wa damu. Katika hali hii, pamoja na kwamba kiasi cha damu huonekana kuongezeka, kiwango cha hemoglobini hupungua mpaka kufikia 11.5mg/dl.
Karibu asilimia 85 ya anaemia wakati wa ujauzito husababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kusababishwa na kula chakula chenye kiasi kidogo cha madini haya au mwili wa mjamzito kushindwa kutunza madini ya chuma ya kutosha kutokana na ama mimba zilizopita au kupoteza kiasi kingi wakati wa hedhi kabla ya kushika mimba.
Vyanzo vingine ni pamoja na
Upungufu wa folic acid
Ugonjwa wa sickle cell
Lishe duni kabla na wakati wa ujauzito
Kupoteza damu kwa sababu ya kuumia au kuwa na minyoo (hookworms)
Ugonjwa wa malaria wakati wa ujauzito
Ugonjwa wa chembe damu nyekundu ujulikanao kama beta thalassaemia. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaoishi Asia ya kusini, Ulaya ya kusini na Afrika.
Upungufu wa vitamin B12
Ugonjwa sugu wa kuvunjika chembe damu nyekundu (chronic haemolysis) kama vile ugonjwa kurithi wa chembe damu nyekundu (hereditary spherocytosis)
Ugonjwa wa kupoteza hemoglobin kupitia mkojo (paroxysmal nocturnal hemoglobinuria)
Saratani ya damu (leukemia)
Matatizo ya kupoteza damu kwenye njia ya chakula (gastrointestinal bleeding)
Matatizo katika utumbo hasa wakati wa ujauzito.
Vihatarishi vya tatizo hili

Masuala ya kijamii kama vile umri wa mjamzito, kiwango chake cha elimu na uelewa kuhusu afya yake, kama ana mwenza wa kumsaidia kiuchumi, makazi anayoishi vinaweza kuchangia mjamzito kupata upungufu wa damu
Vihatarishi vingine ni vile vinavyohusu masuala ya uzazi kama vile idadi ya mimba zilizotanguli (waliowahi kuzaa wana hatari ya kupata anaemia kuliko wanaopata mimba kwa mara ya kwanza), kuwa na mimba ya mapacha na kuwa na historia ya kuzaa mtoto njiti
Vihatarishi vingine vinahusu tabia za mjamzito kama vile uvutaji sigara, unywaji wa pombe na kutohudhuria kliniki wakati wa ujauzito
Pia kuwa na magonjwa kama vile kisukari, magonjwa ya figo, pamoja na shinikizo sugu la damu
Madhara ya upungufu wa damu kwa mama na mtoto

Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mama na mtoto ikiwemo kifo. Madhara haya ni pamoja na
Madhara kwa mama kipindi cha ujauzito: kukonda au kuongezeka uzito kwa kiasi kidogo sana, kuhisi uchungu kabla ya muda, kondo la nyuma kutunga pasipostahili, shinikizo la damu wakati wa ujauzito, na chupa kupasuka kabla ya wakati.
Madhara kwa mama wakati wa kujifungua: kupatwa na uchungu usioeleweka na usio wa kawaida, mtoto kuvuja damu ndani kwa ndani, kupatwa na shock, hatari ya ganzi (anesthesia risk) kwa anayefanyiwa upasuaji, na moyo kushindwa kufanya kazi.
Madhara kwa mama baada ya kujifungua: maambukizi baada ya kujifungua, kizazi kushindwa kurudi katika hali ya kawaida au damu kuganda kwenye mishipa.
Madhara kwa mimba na mtoto atakayezaliwa: Madhara ni pamoja na mtoto kuzaliwa njiti, mtoto kuzaliwa na uzito mdogo, mtoto kuwa na score ndogo (poor Apgar score), mtoto kuzaliwa akiwa amechoka (fetal distress), na upungufu wa damu kwa mtoto
Watoto wanaozaliwa wakiwa na upungufu wa damu hukua kwa tabu, huwa na maendeleo duni ya kiakili na kimatendo (poorer intellectual developmental milestones), uwezekano mkubwa wa kuwa na kasoro mwilini na hata kifo. Kasoro hizo ni pamoja na matatizo ya magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases)
Dalili
Mjamzito mwenye upungufu wa damu wa kawaida mara nyingi anaweza asioneshe dalili zozote. Hata hivyo iwapo upungufu ni mkubwa, dalili za awali ni pamoja na uchovu wa mara kwa mara na kupumua kwa shida, kukosa hamu ya kula, mapigo ya moyo kwenda kasi, na kuchafuka kwa tumbo.

Wakati wa uchunguzi mjamzito anaweza kuonekana mweupe kuliko kawaida hasa sehemu za viganjani, kucha za vidoleni, ulimi, au macho. Anaweza pia kuwa na dalili za kuvimba miguu.
Dalili nyingine ni kama zilivyoelezwa katika makala iliyopita ya upungufu wa damu.
Vipimo na uchunguzi
Uchunguzi wa upungufu wa damu hufanywa kuwa kupima kiasi cha haemoglobin pamoja kufanya kipimo kingine cha damu kijulikanacho kama peripheral smear.

Vipimo vingine vya maabara ni pamoja na kipimo cha kufahamu uwezo wa kuhifadhi madini ya chuma yaani total iron binding capacity (TIBC), kiasi cha feritinkatika damu, kiasi cha folic acid. Katika mazingira mengine kipimo cha kuchukua sehemu ya supu ya mifupa na kuichunguza maabara yaani bone marrow biopsykinaweza kufanywa. Hata hivyo hivi si vipimo vinavyofanywa mara kwa mara.
Matibabu
Mama mjamzito huitaji miligramu 2 mpaka 4.8 za madini ya chuma kila siku. Ili aweze kupata kiasi hiki, inampasa kula kati ya miligramu 20 mpaka 48 za madini ya chuma. Kwa jamii ambayo upatikanaji wa vyakula vyenye madini hayo ni wa shida, suala hili linaweza kuwa gumu sana kutekelezeka, ndiyo maana Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweka mpango maalum wa kuwapa wajawazito wanaohudhuria kliniki madini ya chuma na folic acid ili kufidia pengo hilo.

Vidonge vya madini ya chuma ni salama, nafuu na njia makini ya kuongeza na kurekebisha upungufu wa damu mwilini. Kwa wajawazito ambao hawawezi kunywa, kwa sababu yeyote ile, njia ya sindano inaweza pia kutumika.
Wajawazito wanashauriwa kutumia miligramu 60 za madini ya chuma (ferrous sulphate) na 500mg za folic acid kila siku, ambapo utaratibu huu huendelea kwa miezi mitatu mpaka sita ili kuongeza hifadhi ya madini ya chuma mwilini, hata kama kiwango kinachotakiwa kitakuwa kimefikiwa.
Utumiaji wa vidonge vya madini ya chuma na baadhi ya vyakula: Kuna baadhi ya vyakula kama vile chai ya rangi ambavyo vikiliwa wakati mjamzito amekunywa vidonge vya madini ya chuma vinaweza kupunguza unyonyaji wake katika utumbo. Kwa upande mwingine baadhi ya vyakula vyenye vitamini C kama vile matunda ya jamii ya machungwa huongeza uwezo wa utumbo kunyonya madini ya chuma mwilini.
Vyakula vya kuongeza damu: Pamoja na mkakati huo, wajawazito hushauriwa pia kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kama vile nyama, maini, mayai, samaki, mimea jamii ya kunde, maharage makavu, mboga za majani, matembele, na mikate iliyoongezwa madini ya chuma.
Matibabu ya upungufu wa damu mkali kwa wajawazito walio katika wiki za mwisho (baada ya wiki ya 32): Wagonjwa wa kundi hili hutibiwa hospitali. Wengi wanaweza pia kuwa na dalili za matatizo ya moyo, hivyo wanapaswa kulazwa na kupumzika kitandani, na wakati fulani kuongezewa hewa ya oksijeni. Pamoja na kutibiwa matatizo ya moyo, huongezewa pia damu (packed red cells) kwa vile vidonge vya madini ya chuma havitafaa kurekebisha tatizo hili kwa haraka kabla ya muda wa kujifungua kufika.
Matibabu ya maradhi mengine: kwa mazingira yetu, magonjwa kama malaria na minyoo huchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa upungufu wa damu kwa wajawazito, hivyo basi magonjwa haya hayana budi kutibiwa kikamilifu ili yasilete madhara kwa mjamzito. Wajawazito wanaoishi maeneo yenye malaria kwa wingi hupewa dawa za SP kwa ajili ya kuwalinda wasipatwe na ugonjwa huu. Pia dawa za minyoo za Albendazole au mebendazole hutolewa kwa wajawazito baada ya miezi mitatu ya mwanzo ili kuua minyoo. Ili kuzuia kujiridia kwa minyoo, wajawazito pia hushauriwa kuvaa viatu/kandambili kila wakati, na kuhakikisha miili na mazingira yao yapo safi

Tuesday, 27 January 2015

KUUMWA TUMBO WAKATI WA HEDHI


KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya.Kutokana na simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata akina mama wengi wakati wa hedhi nimeona ni bora niandike makala hii ili iweze kuwasaidia na wengine kujua nini chanzo na mhusika afanye nini pale anapopatwa na tatizo hilo.
Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.
Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu hayo huanza pale yai linapotoka katika mrija (fallopian tube) na kuteremka chini ya mrija huo wakati wa Ovulation.
AINA YA MAUMIVU
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.  Ya kwanza  ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.
Aina ya pili  ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
Nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia kumi mpaka kumi na tano  wanasema kuwa hupata maumivu     makali.
Uchunguzi unaonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.
Sababu hizo ni kama  kuwa na umri wa chini ya miaka 20, kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo, kutoka  damu nyingi wakati wa hedhi, wanawake ambao hawajawahi kuzaa.
Magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:
 Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo
Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaota katika mfuko wa uzazi.
PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.
Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.
baadhi ya magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. niliishia kuelezea ugonjwa wa uvimbe katika nyonga ambao husababishwa na magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya zinaa.
 dalili za ugonjwa huo ni:
Maumivu kuja na kuondoka, kwa kiwango tofauti (spasmodic).
Maumivu zaidi huwa sehemu ya chini ya tumbo na huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo ambayo husambaa mpaka mapajani.
Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.
Kupata choo laini au hata kuharisha na wengine hufunga choo.
TUMBO KUWA KUBWA AU KUWA GUMU.
Kupata maumivu ya kichwa, kujisikia kuchoka.
Kiwango cha maumivu ya tumbo la hedhi na mchanganyiko wa dalili inategemea mtu na mtu, mtu mwingine anaweza akawa anapata karibu dalili zote nilizozitaja hapo juu na mwingine ni baadhi tu au hata dalili moja. Wanawake wengi hujitambua  bila hata msaada wa daktari.
USHAURI
Iwapo mwanamke atapata maumivu makali sana ni bora akamuone daktari ili wafanye vipimo kama vile Ultrasound, CT na CT-Scan, MRI na vinginevyo ili kufahamu nini chanzo cha  maumivu hayo kuwa makali
MATIBABU
Matibabu ya maumivu ya tumbo la hedhi kwa kawaida huweza kutibika kwa urahisi kwa kutumia vidonge vya kupunguza maumivu, kama vile Ibuprofen, naproxen au aina nyinginezo za vidonge visivyokuwa na steroids (NSAIDS). Pia kuna wakati madaktari wanaweza kumshauri mgonjwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba, Vidonge hivyo huzuia mzunguko wa yai au Ovulation na kupunguza ukali wa maumivu ya tumbo la hedhi.
Pia  wanawake wanashauriwa kufanya baadhi ya vitendo ambavyo hupunguza maumivu  hayo, kama kuoga maji moto, kuweka kitambaa chenye joto katika sehemu ya chini ya tumbo, kufanya mazoezi kama yoga, meditation,  kutumia vidonge vya vitamin E, Thiamine na Omega 3 kumetajwa kuwa husaidia katika suala hilo. Wanawake wanaopatwa na matatizo kama 

hayo ni bora wapumzike vyema na kupata usingizi wa kutosha.
Vilevile unaweza kujiepusha na kupatwa na maumivu ya tumbo la mwezi kwa kufanya yafuatayo:
Kujitahidi kula matunda, mbogamboga na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi, pombe, kafeini, sodium na sukari, kufanya mazoezi ya viungo, kujiepusha na wasiwasi na mawazo na kuepuka kuvuta sigara.

ATHARI ZA MAAMBUKIZI KATIKA MIRIJA YA UZAZI



TATIZO hili kitaalamu hutamkwa ‘Salpingitis’, ni maambukizi ndani ya mirija ambayo huathiri na kuleta mabadiliko yasiyotarajiwa katika mirija hiyo.
Tatizo hili huambatana na hali ya maambukizi katika viungo vya uzazi au ‘PID’.
Maambukizi katika mirija ni matokeo ya kusambaa kwa maambukizi haya toka ukeni, katika kuta za kizazi hadi kwenye mirija na vifuko vya mayai.
Maambukizi yakiwa makali na ya muda mrefu husambaa nje ya kizazi na kusababisha tatizo liitwalo ‘Pelvic Perisoneum.
Maambukizi katika mirija ya uzazi yapo katika makundi mawili, kwanza Acute ni yale sugu ‘Chronic Salpingitis’ na pili ni yale makali ‘Chronic Salpingitis’, maambukizi haya hutokea kwa vipindi tofauti kutokana na ukali wa ugonjwa.
Dalili za ugonjwa
Dalili hizi hujitokeza zaidi baada ya kumaliza damu ya hedhi, dalili ni kama vile kutokwa na hali ya uchafu usio wa kawaida ukiwa na harufu mbaya, uchafu huu unaweza kuwa na rangi ya njano au ya damu. Pia maumivu wakati ukiwa kwenye upevushaji mayai ‘Ovulation pain’, maumivu makali wakati wa hedhi ambapo hapo awali hayakuwepo, maumivu chini ya tumbo muda wote yakiambatana na maumivu ya kiuno.
Hali ikiwa mbaya mgonjwa hupata kichefuchefu, hutapika, huhisi homa kila wakati, mwili kutokuwa na hali nzuri huku tumbo likiuma na uchafu ukiendelea kutoka ukeni ukiambatana na harufu mbaya. Mgonjwa pia hulalamika muwasho au maumivu ukeni na wakati mwingine huhisi maumivu anapokojoa.
 Kama tulivyoona, maambukizi haya huanzia ukeni na husambaa hadi katika viungo vingine kwa ndani.
Athari za tatizo
Maambukizi yanaweza kusambaa hadi katika mirija toka ukeni hadi ndani ya kizazi pale mwanamke anapokuwa katika damu ya hedhi na kama damu itarudi kwa juu, hii siyo hali ya kawaida na tutakuja kuiona katika makala zijazo. Matatizo mengine yanayoweza kusababisha hali hii ya maambukizi ni usafishaji wa kizazi mara kwa mara na uharibikaji wa mimba.
Magonjwa yaenezwayo kwa ngono pia ni tatizo kubwa katika uharibifu wa mirija.
Bakteria wanaosababisha tatizo hili la maambukizi na uharibifu wa mirija ni ‘Neisseria Gonorrhea’ ambayo husababisha ugonjwa wa kisonono au gono.
Kwa ujumla ugonjwa huu husababishwa na aina nyingi ya vijidudu vya bakteria.
Ugonjwa huu hushambulia viungo vya uzazi vya mwanamke ambako mimba hutungwa. Huwapata zaidi wanawake walio katika umri wa kuzaa hasa umri wa kuanzia miaka 15-35.
 Wanawake wengi huwa hawapati dalili za awali za ugonjwa, dalili zinapojitokeza tatizo hili huchangia wanawake wengi kutafuta tiba kwa muda mrefu na wengi hukusanyika katika kliniki za magonjwa ya kinamama.
Mirija ya mayai inaposhambuliwa na ugonjwa husababisha kuziba hivyo humfanya mwanamke apoteze uwezo wa kuzaa au ikitokea akapata mimba basi itakuwa nje ya kizazi.
Nini cha kufanya?
Ni vema mwanamke awahi hospitali kufanyiwa uchunguzi pale anapohisi kuna hali isiyo ya kawaida ukeni na chini ya tumbo ambayo inaendelea kwa muda mrefu.
Epuka matatizo au vyanzo mbalimbali vya maambukizi ukeni katika kizazi.
Katika makala zilizopita tumezungumza mengi kuhusu uchunguzi na tiba ya kuziba mirija.
 Ni muhimu wewe kuanza kufuatilia hospitali za mikoa kwa uchunguzi na tiba.

Tuesday, 16 December 2014

UGONJWA WA KWENYE MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE (PELVIC INFLAMATORY DISEASES)



MAAMBUKIZI ugonjwa wa kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke (Pelvic Inflamatory Diseases)  ambao pia hujulikana kama shingo ya uzazi (kitaalamu huitwa cervix) ambayo hujulikana kwa jina la cervicitis hutesa sana wanawake wengi wenye umri mbalimbali.
Maambukizi hayo husambaa hadi kwenye mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia Trachomatis ndivyo vinavyosababisha ugonjwa huu kwa akina mama na wataalamu huuita Pelvic Inflamatory Diseases (PID) yanayotokea kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa ugonjwa huu, njia hizo ni pamoja na kufanya ngono isiyo salama, maambukizi ya njia ya uzazi hasa baada ya kujifungua.
Wanawake wanaotoa mimba kwa njia zisizo salama, wana uwezekano wa kupata maambukizi au wale ambao mimba hutoka (miscarriage) au wakipewa damu iliyo na vimelea vya maambukizi.
Dalili za ugonjwa huu
Dalili za ugonjwa huu wa PID ni nyingi kama vile mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu, kupata maumivu ya mgongo au mwanamke kutokwa na uchafu wenye harufu sehemu za siri.
Kuna dalili nyingine kama vile kuhisi maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa. Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi na mgonjwa kuwa na homa na kuhisi kichefuchefu au kutapika.
Mwanamke aliyeambukizwa maradhi haya ya maambukizi, anaweza kufanya vipimo  kwa kuchunguza mkojo ili kufahamu kama mgonjwa ana mimba.
 Mkojo huchunguzwa na darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa maambukizi.
Kuna kipimo kiitwacho kitaalamu Full Blood Picture hutumika ili kujua aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na maambukizi hayo au kama kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha.
Daktari anaweza kujua kama mgonjwa ana maradhi haya kwa kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki huitwa cervical culture.
Mgonjwa pia anaweza kufanya vipimo vingine ili kujua kama ana maambukizi ya magonjwa yatokanayo na kujamiiana, kama vile virusi vya ukimwi na kisonono. Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia kama kuna athari yoyote katika mfumo wake wa uzazi.
Matibabu
Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ana magonjwa hayo, atatibiwa na dawa za jamii ya antibayotiki ili kuua vimelea vya ugonjwa.
Dawa za maradhi haya zipo nyingi kama vile Cefoxitin pamoja na Doxycycline, Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin nakadhalika. Tunashauri kuwa dawa hizi zinunuliwe kwa kushauriwa na daktari.
Ushauri
Kuna njia kadhaa zinazoshauriwa kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi kama vile kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu au kujizuia kabisa kufanya ngono, kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza na kupimwa vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI).

Saturday, 29 November 2014

JE,UKE WAKO UNATOA HARUFU MBAYA..? JINSI YA KUMALIZA TATIZO LAKO..



Tatizo la uke kutoa harufu mbaya ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi.


Wanaume wengi kila kukicha huwa wanalalamika kuwa inaboa na inakera kupeana Raha na Utamu na Mwanamke ambae sehemu zake za siri zinanuka.Inawatoa out of the mood,mwisho wake wanaconcetrate kudo fasta,wamalize hamu zao kila mtu aondoke.
Wapo baadhi ya wanawake wanajijua wanasumbuliwa na hili tatizo lakini cha kushangaza hawana muda wa kutafuta solutions za kumaliza tatizo lao(wanaishia kuchekwa kuwa vituko vya mtaa bila kujijua bcoz hawajui kuwa matatizo yao ya uke kutoa harufu mbaya,yanasimuliwa na wale wanaume ambao washawahi kulala nao wakiwa wanapiga story na marafiki zao maskani mtaani).

lakini wapo wanawake wachache wenye busara,ambao wanajijua wanasumbuliwa na hili tatizo na wangependa kujua sababu na jinsi ya kulimaliza,na hao ndio wamenifanya mie niandike hii post
Nitaanza kuelezea sababu kisha nitaelezea ni jinsi gani unaweza kumaliza tatizo lako.

Sababu zinazosababisha uke kutoa harufu mbaya ni kama zifuatazo,

1.BACTERIAL VAGINOSIS
Kwa mujibu wa madaktari bingwa,inasemekana kuwa hili ndio tatizo namba moja linalosababisha uke kutoa harufu mbaya.Inawezekana ukawa msafi mpaka mwisho lakini ukisumbuliwa na hili tatizo basi lazima uke wako utatoa harufu mbaya.
Kila uke una bacteria ambao wapo naturally kwa ajili ya afya njema ya uke wako,Lakini kama ikitokea hawa Bacteria wakazidi na kuwa wengi kupita kiasi ambacho uke wako unaweza kuhimili ndio hapo hiki kitendo kinaitwa Bacterial Vaginosis.

Sababu zinazosababisha Bacterial Vaginosis hazijulikani kwa usahihi lakini madaktari wanasema inaweza ikasababishwa na kitendo cha kupeana Raha na Utamu bila condom especially kama vitu vilivyoingia kwenye uke wako wakati wa kupeana Raha na Utamu vilikuwa vichafu(vitu kama vidole au mashine ya mwanaume,or may b dildo etc) au mara nyingine inatokea naturally bila sababu.

Ukitaka Kujua kuwa unasumbuliwa na Bacterial Vaginosis,utajikuta unapata Dalili zifuatazo;

Uke kutoa maji maji mazito au mepesi yenye rangi ya njano(yellow) au Brown yenye harufu mbaya
Maumivu kwenye maeneo ya kiuno au nyonga
Unaweza usipate au ukapata maumivu ya kichwa.
Uke wako unaweza ukawa unawashwa au usiwashwe (ur vagina might itch or not)

2.YEAST INFECTION
Hili Pia ni Tatizo,lipo kama la Bacterial Vaginosis.tofauti yake ni kuwa kwenye Bacterial Vaginosis waliokuwa wamezidi ni bacteria lakini huku wanaozidi ni fungus candida albicans.
Ni wanawake wachache huwa wanapata Bacterial Vaginosis lakini wanawake wengi lazima wapate Yeast Infection japo mara moja katika maisha yao.

Mara nyingi Yeast Infection hutokea Naturally au inaweza kusababishwa na aina ya vyakula au vinywaji unavyokula au kunywa especially kama vimejaa yeast(vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe etc)
Ukitaka kujua kama unasumbuliwa na Yeast Infection,utajikuta unapata Dalili zifuatazo;

Uke wako ukawa unawashwa au usiwashwe (ur vagina might itch or not)
Maumivu kama uke unaungua pale unapokuwa unajisaidia haja ndogo(when u pee)
Uke kutoa maji maji mazito yenye rangi nyeupe kama jibini(cottage cheese)


3.SEXUALLY TRANSMITTED DISEASES (STDs)
Kuna baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na kupeana Raha na Utamu bila Condom,kama vile Chlamydia na Gonorrhea(kaswende na kisonono),kama ukiyapata huwa yanasababisha Uke kutoa Harufu mbaya kwa sababu dalili zake zinahusiana na kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya.

4.VAGINAL OR CERVICAL CANCER
Unapokuwa una kansa ya uke au kansa ya mlango wa kizazi(cervical cancer),kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya ni sehemu ya dalili zake.Unapojiona kuwa una tatizo la uke kutoa harufu mbaya,ni heri na itakuwa busara ukienda hospitali,kama ni kansa ya mlango wa kizazi itakuwa sio ngumu kuitibu kama ukiwahi mapema.

5.POOR HYGIENE
Inawezekana pia tatizo la uke wako kunuka linasababishwa na uchafu. May b unaoga mara moja tu kwa siku au siku nyingine hata hauogi. Hauna mazoea ya kufua nguo zako za ndani(underpants),na ikitokea siku umezifua basi hata hauzisugui zikawa safi.n.k

MAMBO UNAYOTAKIWA KUFANYA UKITAKA UKE WAKO USITOE HARUFU MBAYA

1.OSHA UKE WAKO KWA MAJI SAFI KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA HAJA NDOGO(PEE)

Asilimia kubwa ya wanawake hawana mazoea na utaratibu huu.Ni utaratibu muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanamke. Unapokuwa unajisaidia haja ndogo,most of the tym lazima utakuwa umechuchumaa/umechutama(umesquat),haja ndogo yako inapokuwa inatoka,lazima kutakuwa na mabaki kidogo kidogo yatakurukia na kubakia kwenye lips za nje au za ndani za uke wako(labia majora or minora).

Hayo mabaki baada ya muda yatachanganyika na jasho(sweat) na kutengeneza harufu mbaya,kwa hiyo ili kujiepusha na yote haya,ni heri ukaosha uke wako kwa maji safi kila ukimaliza kujisaidia haja ndogo.

2.UKIWA UNAOSHA SEHEMU ZAKO ZA SIRI,TUMIA MTINDO(STYLE) WA KUPELEKA MKONO KUTOKA MBELE KURUDI NYUMA
Kuna baadhi ya wanawake teyari wameshazoea kusafisha sehemu zao za siri kwa kupeleka mkono kutoka nyuma kuja mbele.Huu mtindo sio mzuri kiafya kwa kuwa huko nyuma kuna Tigo(anus),na kwenye Tigo kumejaa uchafu na bacteria wengi tu.Sasa wakati unajisafisha,unapopeleka mkono nyuma unakuwa kama unazoa bacteria na uchafu kutoka kwenye Tigo,halafu ukauleta mkono mbele unakuwa unawaacha hao bacteria na uchafu kwenye uke wako. Na huo ndio mwanzo wa uke wako kutoa harufu mbaya na kupata infections za ajabu ajabu.

Ukitaka kuwa salama,haijalishi kuwa umemaliza kujisaidia haja kubwa au ndogo,au wakati unaoga,ukitaka kusafisha sehemu zako za siri,tumia mtindo wa kupeleka mkono mbele kurudi nyuma ili usije kuwaleta bacteria na uchafu wa Tigo mbele.

3.VAA NGUO ZA NDANI ZENYE ASILI YA PAMBA(COTTON)
Pamba(cotton) ina uwezo wa kupitisha hewa hata kama ni kidogo sana. Na sehemu za siri za Mwanamke zinahitaji flow ya hewa inayopita,nyingine iwe inaingia na nyingine iwe inatoka.Hii flow ya hewa hata kama ni ndogo itasaidia kufanya sehemu zako za siri kuwa fresh muda wote na utapunguza uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.
Na pia punguza kuvaa nguo za kubana sana muda wote,nguo za kubana zinasababisha majasho sehemu za siri na ukizingatia hamna flow ya hewa kwenye sehemu zako za siri basi lazima hayo majasho yataanza kutoa harufu mbaya.

4.USIVAE NGUO YA NDANI MOJA SIKU NZIMA
Kwa jinsi maumbile ya Mwanamke yalivyo,unatakiwa kubadili nguo ya ndani mara mbili au tatu kwa siku.
May b ulivaa nguo ya ndani asubuhi,ikifika mchana,ingia ladies room(bafuni/chooni),Vua Nguo yako ya Ndani,kisha unaweza ukaoga mwili mzima(which is better) au ukasafisha sehemu zako za siri.Nguo ya ndani uliyovua unaweza ukaifua(which is better) au ukaikunjakunja na kuiweka ndani ya kipande cha khanga au kitenge ndio uweke kwenye handbag yako ili kama ikitokea ukaopen handbag yako in public,watu wataona khanga au kitenge,hawatojua ndani umeweka nini.

5.PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI AU YEAST KWA WINGI
Unaweza ukapunguza uwezekano wa kupata Yeast Infection au Bacteral Vaginosis kwa kuacha au kupunguza kula vyakula vyote vyenye sukari au yeast kwa wingi.
Vyakula hivyo ni kama vile vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe/bia n.k
Ukizidisha Vyakula au vinywaji hivi,ina maana utakuwa unazidisha yeast mwilini,na wakizidi kwenye uke utapata yeast Infection,mwisho wake uke wako utaanza kutoa harufu mbaya.

6.BADILI PADS ZAKO MARA KWA MARA UNAPOKUWA KWENYE SIKU ZAKO
Ili kuzuia uke wako usitoe harufu mbaya kipindi ambacho upo kwenye siku zako,inashauriwa kubadili ur pad mara kwa mara(may b after each 4 or 6 or 8 hours,it will depend how many pads can u afford per day)
Kubadili pads mara kwa mara kunasaidia ujisikie upo comfortable,inazuia bacteria kujikusanya,inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata infection na mwisho inaondoa uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.

7.NYOA(SHAVE) NYWELE ZAKO ZA SEHEMU ZA SIRI MARA KWA MARA
Nywele zako za sehemu za siri zinapokuwa ndefu,unakuwa umetengeneza maficho(hiding place) ya kila aina ya uchafu kuanzia jasho,majimaji yatakayokuwa yanakutoka ukeni ukiget aroused,mabaki ya haja ndogo n.k
Ili kuepusha yote haya ni heri ukawa unazikata nywele zako za sehemu za siri mara kwa mara.

8.NENDA HOSPITALI MAPEMA NA HARAKA TENA SANA
Yaani hata usichelewe,kwani haya matatizo especially Bacteral Vaginosis na Yeast Infection ni matatizo ambayo yanaweza kutibika kwa dawa.Ni heri uwahi mapema ili uongeze uwezekano wa kupona haraka bila matatizo.

Thursday, 27 November 2014

KULEGEA KWA MISULI YA UKE (VAGINAL PROLAPSE)



Tatizi hili huwatokea zaidi wanawake walio kaika umri mkubwa ingawa pia linaweza kutokea katika umri mdogo.Tunapozungumzia kulegea kwa misuli ya uke hapa kuna tofauti kidogo na kutanuka kwa misuli hiyo.Tukizungumzia kulegea ina maana misuli ya ukeni inashindwa kubcana na kuachia njia.Hapa misuli inayoachia njia inapolegea hata ukichuchumaa uhisi nyama zimejaa ukeni.


Chanzo cha tatizo
Kulegea kwa misuli ya uke kutokana na matatizo mbalimbali na hasa uzazi wa karibu karibu,mama anayezaa kwa vipindi viwili vifupi vifupi kwa njia ya kawaida hupatwa na tatizo hili,kulegea kutokana na matatizo ya vichocheo (Hormones) za kike,kulegea kunaweza kusababishwa na magonjwa sugu kama kansa,TB na maambukizi ya HIV,Magonjwa ya zinaa haswa kawende pia huchangia.


Kulegea kwa misuli ya uke kutokana na matatizo mbalimbali na hasa uzazi wa karibu karibu,mama anayezaa kwa vipindi viwili vifupi vifupi kwa njia ya kawaida hupatwa na tatizo hili,kulegea kutokana na matatizo ya vichocheo (Hormones) za kike,kulegea kunaweza kusababishwa na magonjwa sugu kama kansa,TB na maambukizi ya HIV,Magonjwa ya zinaa haswa kawende pia huchangia. 

Mama anayeongezwa njia, baada ya uke kutanuka pia misuli pia inalegea,ingawa uke pia unaweza kutanuka hata bila hata ya misuli kulegea.Tatizo hili la kulegea misuli pia huchangiwa na umri mkubwa kwahiyo kwa wabibi hali hii inapojitokea ni kawaida hasa kuanzia umri wa miaka 70 na kuendelea.

                                                                      
Dalili za tatizo
Mama mwenye tatizo hili wakati wa kujisafisha ukeni atahisi kama tundu limeziba au limejaa nyama na inabodi atumie muda kujisafisha mara kwa mara atakuwa anasumbuliwa na muasho na uchafu wa mara kwa mara wakati wa kufanya tendo la ndoa, maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hutokea pale tu inapotokea michubuko na maumivu wakati wa tendo la ndoa.


Mama mwenye tatizo hili wakati wa kujisafisha ukeni atahisi kama tundu limeziba au limejaa nyama na inabodi atumie muda kujisafisha mara kwa mara atakuwa anasumbuliwa na muasho na uchafu wa mara kwa mara wakati wa kufanya tendo la ndoa, maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hutokea pale tu inapotokea michubuko na maumivu wakati wa tendo la ndoa. 

Tatizo ambalo huambatana na uambukizo wa muda mrefu ukeni,pamoja na mama kutojisikia wakati wa tendo la ndoa,maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hutokea pale tu inapotokea michubuko,uambukizi huweza kupanda hadi kwenye mlango wa uzazi,tumbo la uzazi,mirija na vifuko vyo mayai.

Maambukizo yanapofikia huko mama huumwa na tumbo chini ya kitovu mara kwa mara,mwenendo wa siku za hedhi huvurugika kupata ujauzito.

Hali ya kulegea kwa misuli ya uke pia humuathiri hata mume kwani naye hushindwa kufurahia tendo la ndoa,kulegea na kutnuka kwa uke yote huathiri mahusiano ya kimapenzi kwani mama hafurahii na baba yake hafurahii tendo la ndoa.

Katika kutanuka kwa uke tumeona kuwa uke unatanuka zaidi ya kipenyo chake cha halali ambacho ni sentimeta nne,hivyohivyo kipenyo cha uume ni sentimeta nne.

Utawezaje kujua kama unatatizo? 
Mama mwenye tatizo la kutanuka kwa uke au kulegea kwa misuli ya uke anaweza kujigundua kwa kufuatilia dalili zote.Njia nyingine pitisha vodole viwili ukeni kama vitapwaya ongeza view vitatu vikiweza kuingia vitatu au zaidi bila shida yoyote sambamba na dalili ambazo tumekwisha ziona basi ujue unatatizo hili la kulegea kwa misuli ya uke inapolegea kama tulivyoona hapo awali utahisi kitu kinajaa au kuvimba au nyama zinajitokeza ukeni unapochuchumaa.


Mama mwenye tatizo la kutanuka kwa uke au kulegea kwa misuli ya uke anaweza kujigundua kwa kufuatilia dalili zote.Njia nyingine pitisha vodole viwili ukeni kama vitapwaya ongeza view vitatu vikiweza kuingia vitatu au zaidi bila shida yoyote sambamba na dalili ambazo tumekwisha ziona basi ujue unatatizo hili la kulegea kwa misuli ya uke inapolegea kama tulivyoona hapo awali utahisi kitu kinajaa au kuvimba au nyama zinajitokeza ukeni unapochuchumaa. 

Uchunguzi
Muone daktari wa magonjwa ya akina mama kwa uchunguzi na ushauri wa tiba.Vipimo mbalimbali vitafanyika kubainisha tatizo kama kipimo cha damu,vipimo vya ukeni mfano kipimo cha speculum examination,kuotesha uchafu wa ukeni,kama mama ana maumivu ya tumbo vipimo vya ultrasound pia vitafanyika,mwenendo wa mfumo homoni na historia ya tatizo kwa ujumla itafanyiwa tathimini,vilevile itasaidia kujua kama tatizo ni la kuzaliwa nalo,uzazi wa karibu karibu au ni nini.Uchunguzi huu ufanyika ili kuweza kupanga tiba ambayo huwa zaidi ya umoja ili kuweza kufanikisha.


Muone daktari wa magonjwa ya akina mama kwa uchunguzi na ushauri wa tiba.Vipimo mbalimbali vitafanyika kubainisha tatizo kama kipimo cha damu,vipimo vya ukeni mfano kipimo cha speculum examination,kuotesha uchafu wa ukeni,kama mama ana maumivu ya tumbo vipimo vya ultrasound pia vitafanyika,mwenendo wa mfumo homoni na historia ya tatizo kwa ujumla itafanyiwa tathimini,vilevile itasaidia kujua kama tatizo ni la kuzaliwa nalo,uzazi wa karibu karibu au ni nini.Uchunguzi huu ufanyika ili kuweza kupanga tiba ambayo huwa zaidi ya umoja ili kuweza kufanikisha. 

Matibabu na ushauri
Tiba hutolewa katika Hospitali kubwa au katika cliniki maalum za magonjwa ya akinamama,tiba ni kurekebisha misuli hiyo kwa njia ya upasuaji mdogo na baadhi ya dawa ili kumrudisha mama katika hali ya kawaida.


Mwanamke aepuke vyanzo mbalimbali mojawapo ni uzazi wa karibu karibu hivyo afuate uzazi wa mpango uwe wa kalenda,sindano,vidole au vijiti au kitanzi.

Tiba hutolewa katika Hospitali kubwa au katika cliniki maalum za magonjwa ya akinamama,tiba ni kurekebisha misuli hiyo kwa njia ya upasuaji mdogo na baadhi ya dawa ili kumrudisha mama katika hali ya kawaida.Mwanamke aepuke vyanzo mbalimbali mojawapo ni uzazi wa karibu karibu hivyo afuate uzazi wa mpango uwe wa kalenda,sindano,vidole au vijiti au kitanzi.

Epuka kupata magonjwa au maradhi ya ukeni mara kwa mara kwa kujisafisha vizuri na unapohisi tu unatatizo ukeni haraka muone daktari anayeshugulika na magonjwa ya kinamama kwa msaada mkubwa.

Chakula bora hasa mboga za majani na matunda mara kwa mara kwa kulinda na kuimarisha mwili mojawapo ni kuweka sawa mwenendo wa mfumo wa homoni kuimarisha muonekano wa mwili na viungo vya uzazi na upevushaji wa mayai.Wahi hospitali kwa uchunguzi.




Friday, 7 November 2014

VYAKULA MUHIMU KWA WAJA WAZITO-2

Wiki iliyopita tuliona orodha ya vyakula hatari kwa wajawazito. Orodha hiyo imekatazwa kuliwa na wajawazito kwa sababu ina madhara kwa afya ya mtoto. Darasa hili ni muhimu kama mama anahitaji kuzaa mtoto mwenye afya na akili timamu.

Baada ya kujua orodha ya vyakula visivyofaa kwa wajawazito, wiki hii tujifunze vyakula vinavyofaa kuliwa zaidi na wajawazito. 

Kumbuka kwamba vyakula vyote vinaweza kuwa ni muhimu mwilini lakini huzidiana kulingana na mahitaji na hali ya mtu kwa wakati maalumu.

Mahitaji ya madini na vitamini mwilini wakati wa ujauzito huwa ni makubwa, hususani madini ya kashiamu, chuma na Vitamin B9 (folic acid).

MADINI YA KALISI (Calcium)
Wakati wa ujauzito, madini mengi ya kalisi husafirishwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno. Katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo, mama huhifadhi madini hayo mwilini mwake. Kiumbe kinapokamilisha umbo lake katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho, hifadhi hiyo huanza kutumiwa na kiumbe hicho, hivyo mahitaji yake kuongezeka.

Katika kipindi hiki, mjamzito anatakiwa kula kwa wingi vyakula vinavyoongeza madini ya kalisi kama vile maziwa na vyakula vitokanavyo na maziwa. Kukiwa na upungufu wa madini hayo, meno ya mama na mifupa huathirika pia.

MADINI YA CHUMA (Iron)
Mahitaji ya madini ya chuma nayo huwa makubwa kwa wajawazito. Madini hayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu ambayo huhitajika kwa wingi na mama pamoja na mtoto.

Madini joto hupatikana kwa kula kwa wingi vyakula kama vile nyama, samaki, mayai, vyakula vilivyopikwa kwa nafaka zisizokobolewa (ugali wa dona, mkate mweusi, n.k) na mboga za majani kama vile spinachi na brokoli. Ili kupata madini hayo ya kutosha kutokana na vyakula hivyo, inashauriwa mjamzito kutumia pia vidonge vya Vitamin C (Vitamin C food supplements).

VITAMIN B9 (Folic Acid)
Vitamini hii ni muhimu sana kwa mjamzito, ni kosa kubwa sana la kiafya kwa mjamzito kuwa na upungufu wa vitamin hii. Vitamin B9 ndiyo inayohusika na ukuzaji na uimarishaji wa mfumo wa fahamu wa kiumbe tumboni. 

Aidha, Vitamin hii ndiyo inayotoa kinga ili viungo vya mtoto visiathirike na kuepusha uzaaji wa watoto walemavu au wenye kasoro za viungo kama ‘midomo ya sungura’ na kadhalika.

Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin B9 ni pamoja na mboga za majani, juisi ya machungwa, mapeasi, vyakula vilivyopikwa kwa ngano na mchele (hasa brown rice) na mayai. 

Hata hivyo, kutokana na hali ya vyakula vyetu, mjamzito hawezi kupata kiwango kinachotakiwa cha vitamin hiyo kwa kula vyakula peke yake.

Ili kupata kiwango cha vitamin hiyo kinachotakiwa, mjamzito atatakiwa kutumia pamoja na vidonge vya lishe vya Vitamin B9 ili kuepuka upungufu huo. Inashauriwa kutumia vidonge hivyo miezi michache kabla ya kushika mimba na katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito, kipindi ambacho vitamin hiyo huhitajika kwa wingi.

Kwa ujumla, lishe bora ni muhimu kwa mjamzito katika kipindi chote cha ujauzito wake. Matatizo mengi ya kuzaa watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali, hutokana na upungufu wa madini na vitamin muhimu mwilini katika kipindi cha ujauzito. 

Monday, 3 November 2014

KUTOKWA NA MAJIMAJI SEHEMU ZA SIRI



Tatizo hili huwatokea wanawake na wanaume. Mwanaume hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo, mwanamke hutokwa na majimaji haya katika njia ya mkojo au ukeni.
Majimaji haya yanaweza kuwa mepesi au mazito, pia yanaweza kuwa ni usaha kutegemea na chanzo cha tatizo.
Mwanaume mwenye tatizo hili, majimaji yanaweza kutoka yenyewe na kujikuta amechafua nguo za ndani au asubuhi anapoamka anajikuta amechafuka.
Wakati mwingine unapojisaidia haja kubwa majimaji haya hutoka kama manii yakiwa yanateleza toka katika njia ya mkojo.
Kwa upande wa mwanamke, kutokwa na majimaji haya inategemea ni wakati gani, aidha wakati wa ujauzito au wakati ambao siyo wa ujauzito.
Hali hii ikitokea wakati wa ujauzito siyo dalili nzuri, wakati mwingine huhatarisha hali ya ujauzito. Katika kipindi ambacho siyo cha ujauzito, tatizo hili linapotokea huwa na vyanzo vingi.
Jinsi tatizo linavyotokea
Mwanaume mwenye tatizo hili, kama anatokwa na usaha, utakuwa na historia ya kufanya ngono zembe siku za nyuma na siyo muda mrefu sana. Endapo utakuwa na majimaji mepesi itategemea kama yanawasha au la, kama hayawashi basi aidha utakuwa una tabia ya kujichua au ulishawahi kuumia njia ya mkojo.
Majimaji yanapotoka na kuhisi muwasho katika njia ya mkojo, inaashiria maambukizi sehemu hiyo yanayoweza kusababishwa na Fangasi, Klamidia na Trikomonia.
Hali hii pia inaweza kuwatokea hata wanawake ambao wanaweza kupata matatizo ukeni na katika njia ya mkojo kama inavyojielezea hapo juu.
Mwanamke kutokwa na uchafu mzito ukeni inategemea na chanzo, aidha inaweza kusababishwa na mabadiliko ya mwili au maambukizi. Hali hii inategemea na uchafu au majimaji hayo yapo katika hali gani.
Mwanamke mjamzito na asiye mjamzito endapo atatokwa na uchafu mzito ukeni ambao hauna harufu wala muwasho, hilo siyo tatizo na maambukizi, ni mabadiliko tu ya mwili. Kwa mwanamke ambaye siyo mjamzito, hali hii inaashiria kutopevusha mayai na hawezi kupata ujauzito.
Uchafu wenye rangi aidha njano, rangi ya udongo au damu, au unatoa harufu, basi ni tatizo linalohitaji uchunguzi wa kina.
Dalili za tatizo
Kama nilivyoelezea jinsi tatizo linavyotokea, hali ya kutokwa na uchafu au majimaji ukeni huambatana aidha na muwasho, harufu au la.
Kama hakuna harufu au muwasho hali inapotokea kwa mwanamke tatizo linaweza kuwa katika mfumo wa homoni na hali inapotokea ikaambatana na muwasho harufu tatizo ni maambukizi.
Maambukizi yanaweza kuwa Kisonono au Gono, Kaswende, Klamidia, Trikomonia na Fangasi.
Matatizo haya yanaweza kuambatana na  maumivu katika njia ya mkojo, chini ya tumbo na kiuno kwa wanaume na hata kuathiri uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
Kwa wanawake tatizo linaweza kuambatana na maumivu katika njia ya mkojo, maumivu ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa, maumivu chini ya tumbo na maumivu ya kiuno.
Mwanamke pia hupoteza hamu ya tendo la ndoa, mzunguko wa hedhi huvurugika, kutopata ujauzito na kupoteza hamu ya tendo la ndoa. Matatizo haya humfanya mgonjwa apoteze hamu ya kula na mwili kuwa mchovu na kukosa raha.
Uchunguzi
Hufanyika katika kliniki za magonjwa ya kinamama. Muone daktari bingwa wa kinamama kwa uchunguzi wa kina.
Vipimo vipo vya aina nyingi kama vya damu, kupima shingo na mdomo wa kizazi, kupima uchafu utokao ukeni, kipimo cha Ultrasound na vingine ambavyo daktari ataona vinafaa.