Showing posts with label FAIDA ZA MAJANI. Show all posts
Showing posts with label FAIDA ZA MAJANI. Show all posts

Wednesday, 28 June 2017

ULAJI WA MARA KWA MARA WA MBEGU ZA MABOGA HUKUKINGA NA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 1O MWILINI MWAKO...


ULAJI wa maboga ni muhimu lakini ni Watanzania wachache wanaojua faida ya boga na mbegu zake. Mbegu za maboga zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa, maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu
bora na muhimu kutafuna kila wakati baada ya kuzikaanga au zikiwa mbichi au kama zimepikwa na boga lenyewe kwani imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10.
KIBOFU CHA MKOJO
Mbegu za maboga zimekuwa zikitumika kuimarisha afya ya wanaume kutokana na kuwa na kiasi kingi sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni muhimu sana kwa afya ya kibofu cha mkojo Urinery Bladder. Mbegu za maboga pamoja na mafuta yake, yote kwa pamoja hutoa kinga kwenye kibofu kupatwa na matatizo ya kiafya, yakiwemo yale ya saratani ya kibofu.

KINGA YA MWILI
Mbegu za maboga zenye kiasi kingi cha madini ya Zinc yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha kwenye damu sukari na huboresha nguvu

za kiume pia huongeza uwezo wa kufikiri. Upungufu wa madini ya Zinc mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, mwanamke au mwanaume kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo wa kuelewa wanachofundishwa darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.
Mbegu za Maboga


MAFUTA YA OMEGA -3
Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu sana mwilini. Jamii ya karanga pamoja na mbegu za maboga ni miongoni mwa mbegu zenye kiasi kingi cha mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa mbegu za maboga utakuwezesha kupata kirutubisho hiki muhimu katika mwili wako na kukupa faida za mafuta haya ambazo ni nyingi.


UGONJWA WA MOYO
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini aina ya maginizia Magnesium ambayo huboresha utendaji kazi wa viungo vya mwili. Huimarisha usukumaji wa damu kwenye moyo, huimarisha ukuaji wa mifupa na meno, huifanya mishipa ya damu kupitisha damu kwa urahisi na hufanya upatikanaji wa haja kubwa kuwa laini.

KINGA DHIDI YA SARATANI
Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za maboga wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za tumbo, matiti, mapafu na kibofu, hivyo unapokula mbegu hizi husaidia mambo hayo na mengine mengi.


UGONJWA WA KISUKARI
Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama mbegu za maboga, umeonesha kuwa ulaji wa mbegu za maboga, husaidia kurekebisha kiwango cha Insulin mwilini na hivyo kumuepusha mtu kupatwa na ugonjwa hatari wa kisukari.


MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI
Mara nyingi akina mama watu wazima ambao wamefikia ukomo wa hedhi, hupatwa na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na hali hiyo. Hata hivyo, wataalamu wamegundua kwamba ulaji wa mbegu umeonesha kuwa mbegu za maboga zina uwezo wa kurekebisha hali hiyo na kuondoa kabisa matatizo ya kiafya yatokanayo na ukomo wa hedhi.

AFYA YA MOYO NA MAINI
Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi cha mafuta mazuri, kamba lishe Fibre na virutubisho vinavyoimarisha
kinga ya mwili Antioxidants, zimeonekana kuwa bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza kumpatia mlaji kinga dhidi ya matatizo ya kiafya katika moyo na ini.

DAWA YA USINGIZI
Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi. Ulaji wa mbegu za maboga saa chache kabla ya kupanda kitandani, hasa ukila pamoja na tunda lolote, kunasaidia kupata usingizi mzuri mwororo.
Mbegu za Maboga

DAWA YA UVIMBE
Wataalamu wamethibitisha kwamba mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe Inflamatory Diseases sawa na dawa aina ya Indomethacin lakini mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo dawa, ndiyo maana tunahimiza kutumia mbegu za maboga ambazo huwa ni dawa asili.

JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGA
Ili kupata faida zake zote, zikiwemo zile za mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo zikiwa kavu, bila kuzikaanga japokuwa zilizokaangwa bila kuunguzwa nazo siyo mbaya. USHAURI Hakikisha pia unapata mbegu zilizohifadhiwa vizuri ambazo
hazijaoza wala kuwa na fangasi. Iwapo utapenda kuzikaanga, basi hakikisha unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15, unaweza pia kuongeza chumvi kidogo kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa hazina mafuta mengi kama zile kavu.

Thursday, 31 December 2015

FAIDA ZA MCHAICHAI KWA AFYA YAKO



UJUE MCHAICHAI
Ni wengi wanaoutumia na
kuufahamu mchaichai kama
kiungo cha chakula jikoni na
wengine hutumia kama dawa ya
mbu.
Lakini, je unafahamu kuwa
majani haya yana faida kubwa
kiafya . Mafuta ya mchachai
hutumika katika viwanda
vinavyotengeneza pafyumu na
sabuni.
Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa
mchaichai una vichocheo
muhimu vinavyoweza
kupambana na athari kadha wa
kadha tumboni, kwenye mkojo
na hata kwenye vidonda. Watu
wengine huamini kuwa
mchaichai unaweza kutibu
baadhi ya maradhi kama vile
homa ya matumbo, matatizo ya
ngozi, madhara yanayotokana
na ulaji wa chakula chenye
uchafu na pia hutibu maradhi
ya kichwa na hata misuli.
Mchaichai pia unatajwa kuwa
kinywaji kinachoweza
kupunguza joto. Chai ya
mchaichai inasaidia kupunguza
joto kwa mgonjwa wa homa.
Faida nyingine za mchaichai
kiafya ni pamoja na:
KINGA DHIDI YA SARATANI
Tafiti mbalimbali zimeonyesha
kuwa kwenye kila gram 100 ya
mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa
kuukinda mwili dhidi ya
ugonjwa wa saratani. Mwaka
2006, timu ya watafiti kutoka
Chuo kikuu cha Gurion, Israel
waligundua mchaichai una
uwezo wa kuua seli zinaweza
kusababisha saratani.
MMENG'ENYO WA CHAKULA
-Husaidia umeng’enyaji wa
chakula
Chai ya mchaichai hurahisisha
utaratibu wa mmeng’enyo wa
chakula na pia hutibu
magonjwa ya kuhara na
maumivu ya tumbo ikiwamo
kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa
kuondoa uchafu mwilini
Katika matibabu,
unatibu magonjwa
mengi ikiwemo
kushusha joto, hasa kwa
wagonjwa wanaosumbuliwa na
malaria kali.
KUSAFISHA FIGO NA MKOJO
Mchaichai pia una kazi ya
kusafisha figo ambayo kazi yake
kubwa ni kusafisha damu
mwilini, kuondoa mafuta
mabaya mwilini ambayo mengi
yanatengenezwa na kemikali
kiwandani na hivyo mwili
kushindwa kuziondoa na
baadaye kusasababisha
magonjwa mbalimbali ikiwemo
saratani.
Figo inapokuwa safi na imara,
hata kazi nyingine kama
kusafisha mkojo zinafanyika
kirahisi kwani mkojo unapozidi
kuwa mchafu mtu hujikuta
akivimba mwili na wakati
mwingine kufikia hata hatua ya
kupoteza maisha.
MAUMIVU WAKATI WA HEDHI
Mchaichai pia huwasaidia kina
mama ambao wanaumwa na
tumbo kipindi cha hedhi, ambao
wengi wao huchukulia kama
chango.
“Unapokunywa mchaichai,
unawezesha kusafisha mirija ya
uzazi na hivyo kuwezesha damu
kupita kwa urahisi,”
MAJIPU NA MCHAFUKO WA DAMU
vilevile mchaichai una
kazi ya kusafisha damu, hasa
kwa watu ambao wamekuwa na
tabia ya kupata magonjwa ya
ngozi kama mapele na kutoka
majipu
KUZUIA KUHARISHA
Mchaichai pia unaelezwa kuwa
ni dawa ya kuzuia kuharisha
ambapo una uwezo wa
kupambana na mdudu aina ya
protozoa anayesababisha
ugonjwa huo.
MAMA WAJAWAZITO
Endapo mjamzito atatumia
majani ya mmea huu kwa muda
mrefu, ataweza kujiepusha
kujifungua kwa njia ya upasuaji
kwani husaidia katika kulegeza
nyonga ambazo hubana katika
kipindi cha ujauzito na kufanya
njia kuwa ndogo kuwezesha
mtoto kupita,
WENYE VIDONDA VYA TUMBO
Hata hivyo kwa wagonjwa
wanaosumbuliwa hasa na
vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia
kuondoa gesi ambazo huwapata
mara kwa mara.
HUONGEZA CD4
Kwa wagonjwa wa ukimwi,
mchaichai unaelezwa kuwa
huongeza CD4 na inashauriwa
kuwa ni vyema mgonjwa wa
aina hiyo akapendelea kutumia
zaidi mchaichai kuliko majani
ya chai.

Wednesday, 3 December 2014

FAIDA ZA KUTUMIA MAJANI YA TUNDA LA STAFERI



  • Juisi yake hutibu kansa haraka na kwa ufanisi zaidi
  • Ina nguvu mara 10,000 zaidi ya tiba ya mionzi katika kuziua seli za kansa
  • Hutibu maumivu ya nyuma ya mgongo/low back pain
  • Ni tiba ya asili ya maumivu ya mishipa, yasage majani yake mpaka yalainike kabisa kisha paka taratibu eneo la mshipa lililo na maumivu mara 2 kwa siku
  • Hutibu maumivu ya jongo/gout
  • Hurekebisha usawa wa kiasi cha damu sukari mwilini
  • Huongeza kinga ya mwili
  • Hudhibiti ukuwaji wa bacteria, virusi, vijidudu nyemelezi na uvimbe
  • Huongeza stamina ya mwili na kurahisisha kupona haraka unapokuwa mgonjwa
  • Hutibu jipu na vivimbe
  • Hukimbiza chawa.

Friday, 29 August 2014

KIBOKO YA KUSAFISHA FIGO: KUNYWA JUISI YA GILIGILANI


CLEAN YOUR KIDNEYS


Years pass by and our kidneys are filtering the blood by removing salt, poison and any unwanted entering our body. With time, the salt accumulates and this needs to undergo cleaning treatments and how are we going to overcome this?

It is very easy, first take a bunch of parsley or Cilantro ( Coriander Leaves ) and wash it clean
Then cut it in small pieces and put it in a pot and pour clean water and boil it for ten minutes and let it cool down and then filter it and pour in a clean bottle and keep it inside refrigerator to cool.

Drink one glass daily and you will notice all salt and other accumulated poison coming out of your kidney by urination also you will be able to notice the difference which you never felt before.

Parsley (Cilantro) is known as best cleaning treatment for kidneys and it is natural!

Thursday, 1 May 2014

FAIDA ZA ALO VERA MSHUBIRI



Mmea wa aloe
vera ukilimwa kwenye rutuba sahihi,
kutunzwa vizuri na kusindikwa kwa
uangalifu huwa na faida nyingi kwani una
vichocheo vinavyoua vimelea vya
magonjwa kama bakteria, virusi na fangasi.
Mtandao wa Mediclinic unaeleza kuwa
Aloevera, 

huchochea utengenezwaji wa
chembechembe mpya na tishu mpya zenye
afya. Hufanya mfumo wa fahamu kufanya
kazi vizuri na kutuliza matatizo yanayoathiri
mfumo wa fahamu. Huondoa sumu mwilini
na kufanya utendaji kazi wa mwili urudi
katika hali ya kawaida.

Pia, husaidia kujenga seli mpya baada ya
majeraha ya moto, kujikata, michubuko,
vidonda vya tumbo, kung’atwa na wadudu
wakali na wanyama. Husaidia matatizo ya
kutopata haja, pia maumivu wakati wa haja
kubwa na ndogo. Huondoa matatizo ya
ngozi kama pumu ya ngozi (eczema),
chunusi (acne) na fangasi.

Ni msaada kwenye umeng’enyaji wa
chakula, kuongeza kinga ya mwili, kuondoa
maumivu sehemu mbalimbali za mwili,
matatizo ya usingizi, uchovu wa mwili
usioeleweka, ugonjwa wa koo na pumu.

Hutibu matatizo ya kuhara na kutopata haja
kubwa kiurahisi, hutibu sukari, vidonda vya
tumbo. Wanaume wengi wanaosumbuliwa
na matatizo ya kuziba kibofu cha mkojo na
pia kinamama wanao sumbuliwa na
uambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI)
ambayo huwafanya misuli ya kuzuia mkojo
kulegea, mapafu, kusafisha maini na
kuondoa sumu kwenye ngozi, aloe vera ni
tiba.

Ili kupunguza uchungu, unaweza
kutengeneza juisi yake na kuichanganya na
asali ya nyuki wadogo.

Wednesday, 30 April 2014

FAIDA ZA GILIGILIANI KAMA KIUNGO, DAWA NA UREMBO.




Giligiliani  Mboga.

Giligiliani ni kiungo cha kawaida sana,wengi tunakitumia jikoni 

kwenye mapishi mbalimbali,Kinaharufu nzuri na ladha ya uchachu 

kwa mbali.Majani na mbegu za giligiliani vyote hutumika kama 

viungo jikoni.


Giligiliani inawingi wa Vitamini A, B6, C,B12,pia ina wingi wa madini 

chuma(iron),Calcium na Magnesium

Giligiliani inasifika kwakua dawa na kinga ya magonjwa 

mengi.Historia inaonyesha kwamba Kiungo hiki kilitumika kama 

dawa tangu enzi za kale nchini Egypt.Hata hivyo,tafiti za kisayansi 

za karne hii ya 21 zinathibitisha taarifa hizi



Giligiliani  Mbegu


Ni vyema kujua kwamba tunaposema chakula Fulani ni dawa,basi 

maana yake ni kwamba chakula hicho 


kinavirutubisho Fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa 

Fulani au laa kuupa mwili uwezo wa 


kukabiliana na kujikinga na ugonjwa Fulani na si vinginevyo.


Hizi ni baadhi ya faida za giligiliani katika afya :



1.     Inawezesha usagaji mzuri wa chakula mwilini,hutuliza 

tumbo na huondoa gesi kwenye 

 
utumbo mwembamba  ambayo mara nyingi husababishwa na 

vyakula tunavyokula hivyo 

hupunguza 


utoaji  gesi chafu (kunyampa) kwa kiasi kikubwa sana


2.   Inazuia magojwa ya tumbo yasabaishwayo na bacteria 

aina ya Salmonella.moja ya magonjwa haya ni kuumwa 

tumbo na kuhara.


3.  Inazuia Ugonjwa wa (UTI.) Yaani Urinary tract infection


4.  Inazui kutapika na hali ya kuvurugika tumbo


5.  Inaondoa gesi tumboni


6.  Inashusha sukari kwenye damu.(lower blood sugar)


7.  Inapunguza  cholesterol mbaya mwilin



8.   Chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zinazoitajika mwilini ili 

kuwezesha usagaji mzuri wa chakula (Dietary fiber)


9.   Inawafaa sana wanawake ambao hupata hedhi nzito



10.Inaondoa maumivu,muwasho,na uvumbe(antinflammatory)


11. Huondoa chunusi na madoa kwenye ngozi


Unaweza kuandaa giligiliani katika njia mbalimbali ili 

kuitumia kama dawa

 

Kuondoa hedhi nzito.chemsha kijiko 1 cha chai cha mbegu za 

giligiliani na maji vikombe 


viwili.Chuja kisha ongeza sukari kidogo.Kunywa ikiwa 

yamoto au Maji ya vuguvugu

 

Kuondoa maumivu (Inflamation) chemsha kijiko kimoja cha 

chai cha mbegu za giligiliani 


zilizosagwa  na maji kikombe kimoja.Chuja kisha kunywa 

ikiwa vuguvugu



Kushusha sukari na kushusha cholesterol.Kunywa chai ya 

giligiliani (mbegu) mara kwa mara,pia 


tumia mbegu na majani ya giligiliani kwa wingi kwenye 

chakula.


Ili kuondoa chunusi na madoa meusi.Twanga au sigina 

majani ya giligiliani,chuja au kamua ili 


kupata maji yake.Pima vijiko vinne vya maji ya giligiliani 

kisha changanya na kijiko 1 cha chakula 


cha manjano(Binzari manjano).pakaa kwenye ngozi ,acha 

ikauke kisha osha au nawa na maji 


vuguvugu.Onyo:usisugue ngozi


Kutibu kuhara damu (dysentery).Changanya vijiko 2 vya 


chai vya maji ya giligiliani na kikombe 


kimoja cha maziwa fresh ambayo hayajatolewa krim


Chai ya giligiliani (mbegu) husaidia kuondoa au kutuliza 

asidi tumboni 


Matumizi ya mara kwa mara ya vyakula ambavyo ni tiba 

huupa mwili nafasi nzuri ya kuvuna 


virutubisho na kupata tiba ya magonjwa mbalimbali.


Ni vyema kujua kwamba asilimia kubwa ya vyakula na viungo 

tulivyonavyo majumbani ni tiba ya 

magonjwa mbalimbali.Madawa na Tiba nyingi za kisasa pia 

hutokana na mimea,virutubisho 

huvunwa kutoka kwenye mimea na vyakula na kuchanganywa 

na Kemikali ili kutoa vidonge na 

madawa ya magonjwA mbalimbali.



MATUMIZI SABA YA BAKING SODA(MAGADI SODA)

USIOYAJUA-magadi soda si chakula tu.



Leo asubuhi Dada yangu alinichekesha sana,alifanya siku yangu ianze vizuri pale aliponiletea kibao kichafu cha kukatia nyama alichobeba kutoka nyumbani kwake ili nimsaidie kukisafisha.Nilicheka sana kwani kila mara najitaidi kumfundisha mbinu mbalimbali za jikoni lakini hasikilizi.sasa leo yalipomfika,na kufikia hatua ya kutaka kukitupa kibao hicho ndipo alipokumbuka kua niliwai mfundisha namna ya kukisafisha.Akaamua kujibeba yeye na kibao chake  akanifata.Na ndipo hapo nilipomuweka kwenye darasa la vitendo kwa makubaliano kwamba siku nyingine sitamsaidia.
Najua wengi mnaifaham Baking soda au Bicarbonate of soda kwa lugha ya Kiswahili huitwa magadi soda ,kwa wale msioifahamu,Baking soda au bicarbonate of soda ni  hitaji la kawaida kabisa jikoni,hutumika sana katika vyakula vya kuhoka kama keki na mikatepia hutumika katika maandazi,pan cakes,chapatti na vyakula vingine vingi.Hata ivyo Baking soda wakati mwingine hutumika kulainisha vyakula ambavyo ni vigumu kuiva au visivyolainika haraka  vinapopikwa kama mahindi yasiokobolewa,mboga za majani za kienyeji kama mgagani, msusa,majani ya kunde yaliyo komaa na kadhalika.Hapa nchini Baking soda ya jina kubwa  na kufaamika kwa wengi inaitwa SIMBA.
Baking soda hupatikana kwa wingi madukani na hata sokoni.kuna ile ambayo imepita kiwandani na kusindikwa kitaalam na kuna ile ya kienyeji ambayo iko kiasili zaidi.
Siri kubwa ambayo wengi hawajui kuhusu baking soda,Ni ambavyo huweza kutumika kufanya shughuli nyingi za usafi.Uwepo wa alkalini ndani ya baking soda huipa uwezo wa kuondoa uchafu wenye asili ya asidi.
1.Kusafisha kibao cha kukatia nyama au mboga.
Kwa wale mnaotumia kibao cha plastiki au mbao kukata nyama mnajua ambavyo kibao hushika uchafu  na hata kubadilika rangi,hata baada ya kukiosha.Kutatua tatizo hilo na kufanya kibao chako kiwe safi na cheupe tena,Nyunyuzi  baking soda ya kutosha kisha sugua na dodoki adi kibao kiwe safi,kama ni uchafu wa muda mrefu loanisha kibao na maji kisha nyunyuzi baking soda na uache kwa dakika 15 ndipo usugue na dodoki



Kibao cha kukatia nyama kilichobadilika rangi.
2.Kuzibua sinki la jikoni.
Sinki la jikoni mara nyingi huziba na kugoma kupitisha maji machafu kwasababu ya mafuta na uchafu wa chakula.Mwaga kikombe kimoja cha baking soda kwenye tundu la sinki,kisha mwaga vikombe vitatu vya maji ya moto sana.Acha kwa angalao masaa manne kabla hujatumia sinki.Ni  vyema ukafany ivyo usiku unapoenda kulala kwani sinki halitatumika adi asubuhi.




Baking soda ikiwa kwenye tundu la sinki na maji ya moto pembeni tayari kwa kuzibua sinki
3.Kukata harufu ya mkojo chooni.
Kama unasafisha choo lakini bado kuna harufu mbaya ya mkojo.Chukua nusu kikombe cha baking soda changanya na nusu kikombe cha vinegar nyeupe kisha mwaga ndani ya choo  na unyunyuze kwenye sakafu ,na baada ya nusu saa unaweza kudeki sakafu ili pabaki safi.
4.Kusafisha na kung’arisha sinki,bathtab na tiles.
Ingawa wengi hupenda kuweka tiles,masinki na Bathtubs kwenye nyumba zao,utakubaliana na mimi nikisema wengi hawajui namna ya kuzifanyia usafi,unakuta sinki au tiles nyeupe zimegeuka na kua za rangi ya njano kwa uchafu.
Chukua nusu kikombe cha baking soda changanya na nusu kikombe cha sabuni ya majichanganya vizuri ili kupata kama uji mzito.Kisha tumia kusugua sinki,tiles au bathtub.



Baking soda ikitumika kusafisha tiles
5.Kusafisha Oven
Kawaida unapohoka vyakula kama nyama,samaki,mboga za majani na matunda kama nanasi,mchuzi au umajimaji kutoka kwenye vyakula hivi humwagika ndani ya oven.Wakati mwingine unapo rost vyakula ndani  ya mafuta kwenye grill,mafuta huruka na kuchafua oven.Kwa kawaida uchafu wa aina hii Uganda haraka sana ndani ya oven.
Ili kusafisha .weka baking soda yakutosha kwenye sehem ya chini kabisa ya oven,kisha iloanishe na maji,usiweke maji mengi,kiasi tu cha kutosha kuloanisha baking soda.Fanya hivi usiku kabla ya kulala na ifikapo asubui uchafu wote ulioganda utakua umelainika,tumia dodoki kusafisha.
6.Kukata /Kuondoa harufu mbaya ndani ya friji.
Kutokana na uwekaji wa vyakula iana mbalimbali vyenye harufu tofauti tofauti mara nyingi friji huwa na harufu isioeleweka.Kwa sisi yunaoishi Tanzania na kukabiliwa na tatizo la umeme,umeme unapokatika kwa muda mrefu friji hutoa harufu.
Chukua boksi la baking soda,lifungue na kisha fungua mfuko wa plastiki uliobeba baking soda ili ukae wazi,kisha weka baking soda hiyo kwenye sehem ya chini ya friji yako,itanyonya harufu yote  ndani ya friji na kuiacha ikiwa fresh.Ukiweka boksi lenye baking soda kidogo utendaji wake huwa wataratibu sana,hivyo ni vyema ukaweka boksi jipya.



Baking soda ndani ya friji ili kukata/kuondoa harufu mbaya
7.Kukata harufu kwenye nguo mpya
Mara nyingi unaponunua nguo mpya inakua na harufu ya upya na ndio maana watu wengi hufua nguo mpya kabla hawajavaa.Nguo za mtumba nazo hua na harufu kali inayolazimu kufua kabla hujavaa,hizi zote ni harufu za kemikali zilizotumika katika utengenezaji wa nguo,na kwa nguo za mitumba ni harufu ya madawa yenye kemikali zinazotumika kuhifadhi nguo.
Ili kuondoa harufu hizo,pima kikombe kimoja cha baking soda changanya kwenye maji lita tano ,kisha loweka nguo kwenye maji hayo kwa masaa matatu au zaidi,suuza na uanike.
Kwakua baking soda inaweza fanya yote haya,unakila sababu ya kua nayo jikoni kwako,hasa kwa ajili ya kusafishia kibao cha kukatia Nyama na mboga,pamoja na kuzibua sinki lako la jikoni.Ukweli ni kwamba,kibao cha kukatia nyama kikiwa kichafu,au kimebadilika rangi na mabaki ya nyama yamenata au kuganda  kwenye kibao hicho,inatia kinyaa na pia ni hatari kwa afya ya familia yako.Sinki la jikoni nalo likiziba na kuacha kupitisha maji machafu ndio mwanzo wa kurundika viombo vichafu na kua na maji machafu kwenye beseni kila wakati,chanzo kikubwa cha inzi jikoni na magonjwa ya tumbo.
Kama kawaida,naboresha maisha ya familia yako,Kazi yangu ni kukuelimisha tu,utendaji ni juu yako.
Jali afya ya familia yako.