Showing posts with label NJIA YA MKOJO. Show all posts
Showing posts with label NJIA YA MKOJO. Show all posts

Monday, 17 November 2014

MAHUSIANO KATI YA TUMBO KUJAA GESI NA MUUNGURUMO-2



Naendelea kuelezea kati ya uhusiano wa tumbo kujaa gesi na miungurumo
inayotokea tumboni nk.Kuna ile hali ya mtu kutokujisikia kufanya kitu chochote, yaani kulala inakuwa ni ngumu kwake, kukaa anapata tabu sana, akienda kwenye kazi zake anakua mzito.
Wakati huohuo, anaandamwa na kukosa choo kwa muda mrefu nayo ni dalili kubwa sana ya tatizo linaloitwa constipation kitaalamu.
Dalili nyingine kubwa inakuwa ni maumivu chini ya kitovu na hii huwatokea sana wanaume na wanawake pia huandamwa na dalili kama hii.Ikiwa unapatwa na dalili kama hii na wakati huohuo unakuwa hupati choo basi kuna uwezekano mkubwa ukawa na tatizo hilo la constipation.
Dalili nyingine kubwa inayowatokea wanaume ni ile ya kukosa hamu kabisa ya kushiriki tendo la ndoa, hata akishiriki inakuwa ni mara moja na anashindwa kuendelea.Kama unakumbwa na dalili hiyo na wakati huohuo unaandamwa na kutokupata choo kwa muda na tumbo kuunguruma basi ujue unaandamwa na tatizo hili la constipation.
Dalili nyingine kubwa ni kupatwa na kitu kinachoitwa bawasili au mgolo, na hii ni ile hali ya kutokwa na kitu kama kinyama mtu anapokwenda haja kubwa.Wakati mwingine kinakua kinauma sana na kuandamwa na choo kigumu, nayo ni dalili ya constipation.
Kama unapatwa na dalili kama hizi basi ni vizuri kuwasiliana nasi kupitia namba zetu ili kulitatua tatizo hili.
Kwa ushauri, vipimo na tiba dokta wetu anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.

JE, KUNA UHUSIANO WOWOTE KATI YA TUMBO KUJAA GESI NA MIUNGURUMO KWA MWANAUME KATIKA TENDO LA NDOA?


Watu wengi wamekuwa wakiwasiliana nasi wakihusisha haya mambo mawili hasa wanaume pasipo kujua kama yanahusiana kwa ukaribu au laa.
Na kwa maana hiyo, leo watu wengi wataweza kujua uhusiano wa haya mambo mawili yaani miungurumo ya tumbo, tumbo kujaa gesi na miungurumo ya hapa na pale katika kushiriki tendo la ndoa au kupungukiwa na nguvu katika kushiriki tendo la ndoa.
Tatizo hili kitaalamu huitwa constipation, yaani mtu kuwa na tatizo la kupata choo kidogo, au kutokupata kabisa, na hii huwatokea watu mbalimbali pasipo kujua vyanzo ni nini, lakini hapa utaweza kujua vyanzo vyake na jinsi gani utajiepusha. Tutaanza na dalili zake.
DALILI ZA CONSTIPATION
Dalili za constipation ni kama zifuatazo;
Ni ile hali ya mwanamke au mwanaume anapokuwa anakula chakula kila siku lakini anakuwa hapati choo, wataalamu wanasema kila chakula kinapoingia basi kuna chakula kingine kinatakiwa kitoke, lakini mtu unapokula kila siku na haupati choo kwa siku mbili au tatu au wiki moja basi ujue kwamba unaandamwa na tatizo hilo.
Ni pale mtu anapopata choo kigumu sana kupita kiasi, na wakati mwingine choo hicho kinaambatana na maumivu makali sana kupita kiasi na wengine wanakuwa wanachanika katika njia ya haja kubwa na pale wanapopatwa na choo  au kusikia haja wanakuwa wanaona kama muda wa mateso umekaribia au umefika na choo chao mara nyingi kinakuwa kinaambatana na damu.
Kukumbwa na uchovu kupita kiasi, hii hutokea sana kwa baaadhi ya watu ambao hukumbwa sana na tatizo hili la kupata choo kigumu kupita kiasi na kupatwa na maumivu makali pia (constipation), na hivyo kupatwa na uchovu sana na wanakuwa kama wamefanya kazi kubwa sana lakini si hivyo basi hii nayo ni dalili kubwa sana ya constipation.
Pia kuna hali ya mtu kuandamwa na homa za hapa na pale, na mara nyingi mtu anashindwa kufanya kazi zake kama kawaida, hii nayo ni dalili kubwa sana ya constipation.
Pia kuna ile hali ya mtu kutokujisikia kufanya kitu chochote, yaani kulala inakuwa ni ngumu kwake, kukaa anapata tabu sana, akienda kwenye kazi zake anakuwa mzito sana, yaani hata kutoka kwenda kufanya ibada nayo inakuwa ni ngumu,  wakati huohuo anaandamwa na kukosa choo kwa muda mrefu nayo ni dalili kubwa sana ya tatizo hili (constipation).
Dalili nyingine kubwa inakuwa ni maumivu chini ya kitovu, na hii huwatokea sana wanaume na vilevile hata wanawake nao huandamwa sana na dalili kama hii, pia kama unakuwa unapatwa na dalili kama hii na wakati huohuo unakuwa hupati choo basi kuna uwezekano mkubwa sana ukawa na tatizo hili la constipation.
Na dalili nyingine kubwa ambayo huwatokea sana wanaume ni ile kali ya kukosa hamu kabisa ya kushiriki tendo la ndoa na hata akishiriki basi inakuwa ni mara moja tu na anashindwa kuendelea kabisa.

MATATIZO YA UZAZI KWA MWANAUME NA JINSI YA KUYAKABILI


Viungo vya uzazi vya mwanaume vimegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kuna viungo vya uzazi vya nje na vile vya ndani.
Viungo vya uzazi vya nje ni vile tunavyoviona kama uume na mfuko wa korodani.

Viungo vya uzazi vya ndani ni mirija ya mbegu za kiume ambacho ni kifuko cha akiba cha mbegu na tezi dume au tezi ya ‘Prostate’.
Viungo hivi vyote vina umuhimu mkubwa kwa mwanaume katika kumfanikisha kuweza kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi pamoja na uzalishaji wa mbegu za kiume.Matatizo yakitokea katika sehemu yoyote hapo humuathiri mwanaume inategemea wapi athari ipo.
Athari ni kushindwa kufanya tendo la kujamiiana na kuzalisha mbegu au manii. Manii ni majimaji yanayolisha mbegu za kiume na kuzisafisha na huzalishwa na tezi dume.
Chanzo cha tatizo
Hutegemea mahali linapoathirika. Matatizo hutokea popote katika viungo vya uzazi vya mwanaume iwe nje au ndani.
Uume
Matatizo kwenye uume ni kupata maumivu katika njia ya mkojo kutokana na maambukizi au kuumia njia ya mkojo.Mwanaume mwenye tatizo hili hulalamika maumivu wakati wa kukojo, muwasho katika njia ya mkojo na mkojo kutotoka vizuri.
Kuumia kutokana na kuingiziwa mrija wa mkojo mara kwa mara katika njia ya mkojo.
 Maambukizi inaweza kuwa Yutiai za mara kwa mara na magonjwa ya zinaa kama kisonono na mengine.
Ugonjwa wa kaswende huathiri sehemu ya nje ya uume zaidi ambapo vipele na vidonda vyenye muwasho na maumivu  hujitokeza mara kwa mara.Tatizo hili hujitokeza kama tulivyoelezea hapo juu na huchunguzwa katika vituo vya afya.
Ni vema kuwahi hospitali endapo utahisi dalili hizo kwani ukichelewa itasababisha madhara makubwa mojawapo ni kuziba kwa njia ya mkojo, kusambaa kwa maambukizi katika viungo vingine kama kibofu cha mkojo, korodani na tezi dume.Athari nyingine ni ugumba kwa mwanaume.
Tezi dume
Tezi dume ipo kwa ndani jirani na kibofu cha mkojo na mfuko wa haja kubwa. Kazi ya tezi hii ni kutengeneza na kutunza manii.Tezi dume hupatwa na matatizo mbalimbali kama maambukizi na kutanuka hadi kuwa saratani.
Kutanuka huanzia katika umri wa miaka arobaini na tano na huanza taratibu sana.
Maambukizi ya tezi dume hutokana na muendelezo wa maambukizi toka katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu cha mkojo na kufika kwenye tezi dume.
Tezi dume ikitanuka huanza dalili za uhafifu katika utoaji wa mkojo ambapo mkojo hautoki vizuri au unashindwa kabisa kutoka. Tezi hii inapotanuka inabana shingo ya kibofu cha mkojo.
Dalili dhahiri za ugonjwa huu hujitokeza kadiri umri unavyoongezeka, hasa zaidi ya miaka hamsini na sitini.
Endapo utachelewa kupata tiba hadi umri wa zaidi ya miaka sitini, kuna hatari ya tezi hiyo kuwa kansa au saratani.Uchunguzi wa awali wa tezi dume hufanyika kawaida katika  kliniki kubwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya kabla dalili hazijajitokeza rasmi.
Kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi mara kwa mara hasa unapofikia umri wa miaka 45 na zaidi. 
Kadiri umri unavyoongezeka ndipo dalili zinapojitokeza taratibu hadi tatizo linakuwa kubwa.
Endapo utawahi kufanyiwa uchunguzi mapema , basi tezi dume inaweza kutibika au kuzuia isitanuke na ukaepuka upasuaji na saratani.

Tuesday, 11 November 2014

MAAMBUKIZI YA TEZI DUME (PROSTATITIS) SEHEMU YA PILI

Maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria (Chronic non-bacterial prostatitis)

Kama jina lake linavyoeleza, maambukizi ya aina hii kwenye tezi dume husababishwa na msongo wa mawazo, matatizo katika vichocheo vya mwili
 (homoni) na hata matatizo katika mfumo mzima wa neva.Pia kumekuwepo na dhana ya kwamba maambukizi ya aina hii huchangiwa na kuwepo kwa

maumivu ya kibofu cha mkojo yanayotokana na maambukizi katika kibofu hicho 
(Cystitis)au hali ya hewa hususan baridi ambayo huongeza maumivu ya tezi dume na hali ya joto ambayo hupunguza maumivu hayo. Baridi pia huchangia kujirudia kwa dalili na viashria vya maambukizi haya.

Katika utafiti uliofanyika kaskazini mwa nchi ya 
Finland (nchi ambayo ina majira ya baridi kali sana),umeonyesha ya kuwepo kwa maambukizi ya aina hii yanayoambatana na dalili na viashiria vyake kali sana kuliko sehemu yoyote duniani.
Maambukizi haya ya tezi dume bila uwepo wa bakteria hutokea kwa wanaume walio katika umri wa miaka 35-45 na inakisiwa kutokea kwa asilimia 90-95 ya maambukizi yote ya tezi dume .

Kuna aina mbili kuu za maambukizi haya ambazo ni:

1.Maambukizi haya yanayoambatana na mcharuko 
(Inflammatory Chronic Prostatitis/Chronic Pelvic Pain Syndrome)
2.Maambukizi yasiyokuwa na mcharuko 
(Non-infalmmatory chronic prostatitis, CP/Chronic Pelvic Pain Syndrome au CPPS)

Nini hasa hutokea wakati wa maambukizi haya?

Kukosekana kwa udhibiti wa mfumo wa neva mwilini kutokana na kuwepo kumbukumbu za maumivu yoyote 
(past trauma), maambukizi kwenye tezi dume, mrundikano wa kemikali tofauti tofauti na kuwepo kwa hali ya kuvutika kwa neva za kwenye nyonga husababisha mcharuko (inflammation) 

katika tezi dume unaosababishwa na kutolewa kwa wingi kwa kemikali aina ya substance P
(kutoka kwenye msihipa ya neva)ambayo ndio husababishwa kutolewa chembechembe zinazosababisha mcharuko mwili (mast cells) kwa wingi na matokeo yake ni kuathiri tezi dume pamoja na viungo vilivyokaribu yake kama kibofu cha mkojo, mpira wa kupitisha mkojo (urethra),korodani nk.

Dalili na viashiria vya maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria
•Maumivu makali ya kwenye sehemu za siri au kwenye nyonga kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu bila kuwepo kwa maambukizi ya mfumo wa mkojo 
(UTI)
•Maumivu haya makali yanaweza kuenea hadi kwenye mgongo kwa chini, kwenye puru 
(rectum) na kumfanya mgonjwa kushindwa kukaa chini/ kwenye kiti.
•Maumivu wakati wa kukojoa
•Maumivu katika jointi za mifupa
•Maumivu ya misuli 
(myalgia)
•Maumivu ya tumbo
•Uchovu usioelezeka
•Kichomi kwenye uume/dhakari 
(constant burning pain in the penis)
•Maumivu ya mara kwa mara kwenye nyonga, korodani au kwenye puru 
(rectum) bila uwepo wa maambukizi kwenye kibofu cha mkojo
•Maumivu wakati wa kutoa shahawa (wakati wa kujamiana)
•Kukojoa mara kwa mara
•Maumivu baada ya kutoa shahawa (baada ya kujamiana) ni dalili kubwa ya maambukizi haya
•Kupungua hamu ya kufanya mapenzi
•Kushindwa kujamiana vizuri 
(sexual dysfunction)
•Kushindwa kusimika/kudisa (jogoo kushindwa kupanda mtungi)Erectile dysfuction


Vipimo vya uchunguzi
Hakuna kipimo maalum cha kuchunguza maambukizi haya ya tezi dume.

Vipimo vinavyoweza kusaidia katika uchunguzi wa maambukizi haya ni pamoja na 

•kipimo cha kuangalia shahawa 
(semen analysis)
•kipimo cha kuangalia wingi wa cytokines kutoka kwenye majimaji ya tezi dume
•Vipimo vya kuangalia viashiria vya mcharuko
(inflammation) kama cytokines,myeloperoxidases na chemokines
Inflammatory 
CP/CPPS huambatana na kuwepo kwa seli za usaha (pus cells) kwenye mkojo, shahawa na kwenye majimaji ya tezi dume wakati Non inflammatory CP/CPPS haina seli hizi za usaha kwenye mkojo, shahawa na majimaji ya tezi dume.Kielezo hiki si kigezo cha kutumika kama kipimo cha kuchunguza maambukizi haya.
Seli za usaha (pus cells) huwa ni chembechembe za damu nyeupe zilizokufa.

Matibabu ya maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria
Maambukizi haya sio rahisi kutibu kwani hakuna tiba maalum inayokubalika na wataalamu wa afya.
Lengo kuu la matibabu ya maambukizi haya ni kupunguza mvutano unaosababishwa na kuvutika kwa misuli ya nyonga na ya kwenye puru ,

kupunguza msongo wa mawazo na vichangizi vya msongo huu wa mawazo.

Miongoni wa matibabu yanaweza kusaidia ni pamoja na:
•Kujua chanzo cha msongo wa mawazo/wasiwasi
(panic disorder) au taharuki na kumsaidia mgonjwa kuepuka vichagizi hivi
•Ushauri nasaha pamoja na kumhakikishia mgonjwa ya kwamba hali yake itatengemaa
•Kumuona daktari wa magonjwa ya akili
•Kufanya mazoezi ya yoga ili kufanya nyoga pamoja na mishipa ya neva ya nyoga na misuli kuwa katika hali tulivu
(relaxation)
•Massage ya tezi dume 
(Digital prostate massage)
•Mazoezi ya viungo kwa wale ambao bado hawajafikia hatua ya kupata maumivu makali 
(Chronic Fatigue Syndrome)
•Dawa za kupunguza msongo wa mawazo kama antidepressants, benzodiazipines nk.
•Dawa za antibiotiki na alpha blockers hazijatoa matokeo ya kuridhisha katika uponyaji wa maambukizi haya
•Tiba ya acupuncture imeonyesha kuwapa unafuu baadhi ya wagonjwa

Wanaume wenye maambukizi haya ya tezi dume wako kwenye hatari ya kupata tatizo la maumivu makali sana 
(Chronic fatigue syndrome) na ugonjwa wa Irritable Bowel Syndrome( unaoambatana na maumivu ya tumbo, tumbo kuwa kubwa, kuharisha mara kwa mara au kutopata haja kubwa, msongo wa mawazo, wasiwasi, kuharisha damu na nk).

KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE




Tezi Dume (Prostate gland)

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.


Kuvimba Tezi Dume (BPH)



Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.
Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.
Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.

BPH husababishwa na nini?
Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.
Kuna dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na


  1. Uhusiano kati ya BPH na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.
  2. Uhusiano kati ya BPH na Dihydrotestosterone (DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji na uklimbikaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH.
  3. Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli: Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.


Dalili za BPH
Dalili za BPH hutokea kwa sababu ya kubanwa kwa njia ya kutoa mkojo nje ya mwili (urethra) au kibofu kushindwa kuthibiti mkojo. Aidha dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote 


  1. Hukojoa mkojo unaokatika katika
  2. Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  3. Husita kabla ya kuanza kukojoa
  4. Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
  5. Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
  6. Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
  7. hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  8. Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)
  9. Au dalili zinazotokana na madhara ya BPH


Madhara ya BPH
BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na 



  1. Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
  2. Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
  3. Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
  4. Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
  5. Madhara katika figo au kibofu
  6. Shinikizo la damu
  7. Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
  8. Maambukizi mbalimbali
  9. Nimonia (Pneumonia)
  10. Damu kuganda
  11. Uhanithi


Vipimo na Uchunguzi

Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na


  1. Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonja hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
  2. Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.
  3. Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.
  4. Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.
  5. Kipimo cha kuchunguza kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.


Matibabu

Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

Matibabu kwa njia ya dawa
Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake. Dawa hizo ni pamoja na


  • Finasteride na dutasteride ambazo huzuia uzalishajiwa homoni ya DHT. Matumizi ya dawa hizi husaidia kuzuia kukua na kuvimba kwa tezi dume au kulifanya tezi dume kusinyaa kabisa kwa baadhi ya wanaume.
  • Terazosin, doxazosin, tamsulosin na alfuzosin husaidia kulainisha misuli ya tezi dume na hivyo kupunguza mbano wa mrija wa urethra, hali inayosaidia mkojo kutoka vizuri.



Matibabu kwa njia ya Upasuaji
Upasuaji mdogo (minimal Invasive procedures)

Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo ni


  • Tiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume. Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.
  • Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.
  • Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.


Upasuaji mkubwa

Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume (Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).

Vitu vya kufanya baada ya Upasuaji wa Tezi dume
Mara baada ya upasuaji wa tezi dume inashauriwa 



  • Kunywa maji kwa wingi ili kusafisha kibofu cha mkojo
  • Epuka kujikakamua sana unapojihisi kwenda haja kubwa
  • Kula lishe bora ili kuepuka kupata choo kigumu. Iwapo mgonjwa atapatwa na choo kigumu ni vyema amuone daktari ili amshauri jinsi ya kuondoa tatizo.
  • Epuka na acha kunyanyua vitu vizito.
  • Hairuhusiwi kuendesha gari wala kuendesha mtambo wowote ule mpaka utakapopona kabisa.


Matatizo yanayoweza kutokea baada ya upasuaji


  • Shida wakati wa kukojoa: Kawaida huchukua muda wa siku kadhaa mtu kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida ya kukojoa.
  • Shida ya kuthibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.
  • Kutokwa na damu: Katika siku za wali mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo. Hta hivyo hali hii hukoma baada ya wiki kadhaa. Hata hivyo iwapo utokaji damu ni mzito sana, inashauriwa kumuona daktari haraka.



Uwezo wa kufanya ngono baada ya upasuaji

Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH uhofia sana kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ngono mara baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hili.


  • Mdiso au kudindisha (Erections): Madaktari wengi husema kuwa iwapo mgonjwa aliweza kupata mdiso au kudinda muda mfupi baada ya upasuaji, uwezo wake wa kuendelea kupa mdiso ni mkubwa zaidi. Hata hivyo iwapo mgonjwa hakuwa na uwezo wa kudisa tangu awali, upasuaji wa tezi dume hauna uwezo wa kumrejeshea uwezo wake wa kudisa.
  • Kutoa mbegu (Ejaculation): Ingawa wanaume waliofanyiwa upasuaji wa tezi dume bado wanaweza kupata mdiso, mara nyingi upasuaji huu huwafanya wawe wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Hali hii kwa kitaalamu huitwa retrograde ejaculation au kilele (mshindo) kikavu (dry climax). Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.
  • Kufika kilele (Orgasm): Huwa hakuna tofauti kubwa ya kufika kilele (orgasm) kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.


BPH na Saratani ya Tezi Dume: Hakuna Uhusiano wa moja kwa moja
Ingawa baadhi ya dalili za BPH zinafanan na zile za saratani ya tezi dume, kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hata hivyo, mwenye BPH anaweza pia na saratani ya tezi dume bila saratani hiyo kugundulika, ama wakati huo huo au siku za baadaye. Hivyo inashauriwa kuwa, ni vema wanaume wote kuanzia miaka 40 na keundelea kufanya uchunguzi wa tezi dume zao walau mara moja kila mwaka. 

Saturday, 27 September 2014

UTI NI UGONJWA WA HATARI UNAWEZA KUHARIBU FIGO.KIBOFU CHA MKOJO.






Peter Elias, Mwananchi

Maambukizi Katika Njia ya Mkojo (UTI) ni moja kati ya magonjwa ambayo hayapewi msisitizo wa kutosha katika jamii licha ya kuwa wengi huathirika kwa ugonjwa huu bila kujua chanzo, tiba na kinga yake.

Ugonjwa huu huanza kuathiri mirija inayopitisha mkojo, baadaye huenea katika kibofu na figo. Mgonjwa anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo na kupoteza maisha kama ugonjwa huu hautatibiwa mapema.

Wataalamu wa afya wanasema UTI husababishwa na vimelea ambao huingia kupitia mirija inayosafirisha mkojo na kuutoa nje. Vimelea hawa wanashambulia kibofu na baadaye huendelea mpaka kwenye figo. Hii ndiyo hatua kubwa ya ugonjwa ambayo inaweza kusababisha kifo au tatizo la kudumu.

Hawa ni vimelea wa jamii ya bakteria walio wanajulikana kwa jina la escherichia coli (E.coli).

Bakteria hawa wanapatikana katika utumbo mpana lakini husafiri kupitia njia ya haja kubwa kwenda katika njia ya mkojo na kusababisha maambukizi katika kibofu na figo.

UTI inavyoenea

Dk Veronika Kaniki kutoka hospitali ya Sekou Toure, anabainisha tabia na mazingira yanayoweza kusababisha maambukizi katika njia ya mkojo kuwa ni kushiriki ngono mara kwa mara na watu tofauti bila kutumia kinga.

Anasema hii inamfanya mtu kuchukua bakteria wa UTI kutoka kwa mwenzi wake ambaye tayari ana maambukizi hayo.

Dk Kaniki anaongeza kuwa kujitawaza kutoka nyuma kuja mbele baada ya haja kubwa kunapelekea maambukizi hasa kwa wanawake.

Hii ni kwa sababu vimelea hao hupatikana kwa wingi katika utumbo mpana.

Hivyo, kitendo cha kujisafisha kwa njia hiyo, anasema huwasafirisha bakteria hao kutoka sehemu ya haja kubwa kuja katika njia ya haja ndogo. Anasema mazingira haya husababisha UTI kwa wanawake kwa sababu njia ya haja kubwa na ndogo zipo karibu sana.
“Mama wajawazito pia wako hatarini zaidi kwa sababu mimba kukandamiza kibofu na kusababisha kukosekana kwa uwazi katika njia ya mkojo ambayo kitaalamu inajulikana kama incomplete emptying,” anafafanua Dk Kaniki.

Mtaalamu wa magonjwa ya figo kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Fransis Fredrick anasema takwimu zinaonyesha kuwa kwa kila wanawake watano, mmoja amewahi kupata ugonjwa huo.

Hali hiyo anaielezea kuwa huweza kuwa ni ya kujirudia mara kwa mara kwa baadhi ya wanawake, hasa kinamama wajawazito na watu wenye umri mkubwa.

Mbali na wanawake kupata maambukizi zaidi, Dk Fredrick anaeleza kuwa watoto wa jinsi zote pia wako hatarini.

Anasema ni vema mazingira ya chooni na bafuni yawe safi ili kuwalinda watoto dhidi ya maambukizi haya.

Dk Fredrick anabainisha kuwa maambukizi katika njia ya mkojo yanaweza kusababishwa na bacteria, fangasi au virusi. Anasema matibabu yake hutolewa kulingana na aina ya vimelea waliosababisha maambukizi hayo.

Kisukari huathiri zaidi

Maambukizi haya yanaweza pia kuwaathiri watu wenye kisukari kirahisi zaidi kwa sababu ya sukari nyingi iliyopo katika mkojo.

Sukari hiyo huchochea kuzaliana kwa bacteria wanaosababisha maambukizi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyofanywa na Chama cha Kisukari cha Marekani (ADA), asilimia 9.4 ya watu wanaokutwa na kisukari wanaugua pia UTI wakati asilimia 5.7 ni wenye maambukizi lakini hawana kisukari.

Wenye kisukari wanaathirika zaidi kwa sababu pia bakteria kuzaliana kwa wingi na baadhi ya mishipa inaharibika na kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo. Hata hivyo, ripoti hiyo imebainisha kuwa sukari nyingi iliyopo kwenye damu ya mgonjwa wa kisukari inaua seli nyeupe za damu, hivyo mwili unakosa kinga ya kupambana na bakteria hatarishi walioingia mwilini.


Athari, dalili, tiba

Dk Kaniki anafafanua kuwa endapo mtu hatatibiwa mapema au kumaliza dozi, ugonjwa huu unaweza kuwa sugu na kusababisha kuharibika kwa figo na kibofu.

Anasema maambukizi yanayotokea chini ya kibofu huathiri kibofu na mirija inayotoa mkojo nje.

Maambukizi yanayotokea katika figo ni hatua ya juu na athari zake ni kubwa zaidi kuliko athari zitokeazo katika mirija na kibofu.

Alibainisha athari nyingine kuwa mwanamke mjamzito anaweza kuzaa mtoto kabla ya wakati au mtoto kuzaliwa akiwa na uzito pungufu.

Anasema wagonjwa wanashauriwa kupata tiba mapema na kumaliza dozi na kwamba watoto wadogo na wazee pia wanaweza kupata maambukizi hayo kirahisi.

Ripoti ya ADA inabainisha dalili za awali kwa mtu mwenye maambukizi katika njia ya mkojo ni maumivu wakati wa kukojoa, kuhisi kukojoa laini ukienda chooni mkojo unatoka kidogo sana, kukojoa mkojo wenye damu na maumivu ya tumbo na mgongo.

Dalili kwa maambukizi yaliyokomaa, zinaelezwa kuwa ni homa kali, kutetemeka, kutapika, kuharisha na maumivu ya mgongo.

Hata hivyo, kinga ya ugonjwa huu inaelezwa kuwa ni kuzingatia kanuni za usafi hasa baada ya haja kubwa na kujisafisha kuanzia sehemu ya mbele kwenda nyuma ili kutoruhusu vimelea kuingia katika njia ya mkojo kwa urahisi.

Inashauriwa kumwona daktari baada ya kuona dalili hizi na kutumia kikamilifu dawa itakayopendekezwa na daktari.

Ni muhimu kwa mgonjwa kumaliza dawa ili kuzuia kujirudia kwa ugonjwa huo mara kwa mara na kusababisha madhara au usugu.

Sunday, 31 August 2014

FAHAMU UGONJWA WA KIBOFU CHA MKOJO



WIKI iliyopita tulizungumzia ugonjwa wa uvimbe sehemu ya kizazi kwa wanawake, leo tunachambua ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao huwa ni tatizo kubwa kwa wanaume.Wanaume, hasa wenye umri mkubwa wanaweza wakawa na ugonjwa wa saratani hii ya ‘prostate’. Ni tezi iliyo kwenye viungo vya uzazi vya wanaume chini ya kibofu panapopitia mrija wa mkojo.
Saratani zipo za aina nyingi na moja ya saratani hizo ni hiyo ya kibofu cha mkojo. Aina hiyo ya saratani inaweza kusababishwa na mazingira ikiwemo matumizi ya maji yasiyo salama.
Kabla ya kuelezea saratani hii ya kibofu cha mkojo au prostate nieleze kwamba kibofu cha mkojo kinapatikana sehemu ya chini ya maeneo ya tumbo na ni kiungo ambacho kina uwazi ndani ulio kama mfuko na kazi yake kubwa ni kukusanya na kuhifadhi mkojo unaotolewa na figo kabla ya kutolewa nje wakati muhusika anapoamua kukojoa.
Kibofu cha mkojo kina tabaka tatu za tissue ambazo ni mucosa, lamina propia na muscularis.
Tabaka la mucosa – ukuta wa ndani kabisa ambao ndiyo unakutana na mkojo wa binadamu, lina kuta nyingi sana za seli au chembechembe zinazojulikana kama transitional epithelium cells ambazo pia hupatikana kwenye sehemu ya mirija inayojulikana kama ureters, urethra na kwenye figo. Seli hizi zinazuia uvujaji wa mkojo kwenda kwenye sehemu nyingine ya mwili.
Ureter huingiza mkojo kutoka kwenye figo na urethra hutoa mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo wakati wa kukojoa.
Tabaka la lamina propia – ukuta wa katikati ambao ni mwembamba sana kati ya kuta  hizi tatu na  ambao mishipa ya damu na neva inapatikana hapa- ni muhimu sana wakati wa kupanga makundi ya saratani ya kibofu cha mkojo wakati wa tiba.
Tabaka la muscularis -  ukuta wa nje ambao ndani yake kuna misuli maalumu na ndiyo ukuta mnene kati ya hizi tatu. Una kazi kubwa ya kupumzisha kibofu cha mkojo ili uingie ndani na ukishajaa basi hukaza kibofu na kufanya mkojo kutoka nje.Nje ya kuta hizo tatu, kibofu cha mkojo kimezungukwa na  mafuta ambayo hukinga kibofu kutokana na mtikisiko wowote na kukitenganisha na viungo vingine.
Turudi kwenye mada, kazi ya ‘prostate’ ni kudhibiti kibofu na mtiririko wa mkojo lakini pia ni muhimu katika tendo la ndoa kwani humwezesha mwanamume kuwa na nguvu ya kufikia kilele. ‘Prostate’ ya kawaida kwa mwanamume mtu mzima ina ukubwa kama punje ya karanga na ukubwa huu huongezeka kadiri mtu anavyokua. Katika umri wa miaka 40 tezi huanza kutanuka na kadiri inavyotanuka, hubana mrija wa kupitisha mkojo na kufanya mkojo utoke kwa shida na kusababisha tatizo katika tendo la ndoa.
Urothelial carcinoma (transitional cell carcinoma) – Hii ndiyo aina ya saratani inayotokea kwa wingi na hutokea kwenye seli za transitional epitheliumo na asilimia 95 ya saratani zote za kibofu cha mkojo huwa ni aina hii.
Squamous cell carcinoma – aina hii hutokea baada ya maradhi ya kwenye kibofu cha mkojo kwa muda mrefu kama vijiwe vya kibofu cha mkojo .
Adenocarcinoma – hutokea baada ya shambulizi kwenye kibofu cha mkojo kwa muda mrefu. Huchukua asilimia mbili ya saratani zote za kibofu cha mkojo.

DALILI
Dalili za kwanza za mgonjwa kuwa na tatizo katika kibofu cha mkojo  ni kwenda haja ndogo mara kwa mara, hasa usiku na mara nyingine mtu huweza kujikojolea.
Pia mkojo hutoka kidogokidogo ama kwa kukatika katika na wakati mwingine mwanamume hupata maumivu wakati wa kukojoa na hata kutoka damu.
Maumivu huenea kwenye sehemu za mgongo, kiuno na sehemu za juu ya mapaja na kupunguza uwezo wa tendo la ndoa au kupata maumivu wakati wa kufikia kilele.
Matatizo mengine ni kupata maambukizi ya magonjwa kwenye kibofu, njia ya mkojo na figo na mkojo hubaki kwenye damu na kuwa sumu. Utafiti waonesha kuwa asilimia 25 ya wanaume wenye umri wa miaka 30 na kuendelea wana chembechembe za ‘prostate cancer’.
‘Prostate cancer’ ndio aina kuu ya saratani inayowashambulia sana wanaume japokuwa inaweza kutibika mgonjwa akiwahi hospitali.
Matibabu na ushauri
Matibabu ya saratani hii hutegemea uchunguzi. Inashauriwa kutibu ugonjwa wa kichocho mapema na kukwepa vihatarishi vya kupata ugonjwa huu.Ulaji wa matunda, mboga za majani na unywaji maji ya kutosha angalau lita moja kwa siku unaweza kupunguza tatizo la saratani ya kibofu. Inashauriwa watu waepuke matumizi ya tumbaku.

Thursday, 28 August 2014

MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO KWA WANAWAKE/WANAUME



LEO tuangalie tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo (Urinary disorders) kwa wanawake na wanaume.
Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalamu huitwa simple cystitis au Bladder infection na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa pylonephritis au kidney infection.
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia coli. Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa.
Lakini watu wengine wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi japokuwa kuna visababishi vingine vichache.Bakteria wa Escherichia coli hawapo peke yao huambatana na waitwao staphylococcus, saprophyti cus, pseudom onas, enterobacter n.k.
Maambukizi katika njia ya mkojo  lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo  na si pengine popote. Wapo wanawake wamekuwa wakiniuliza kuhusu tatizo la kutokwa na uchafu ukeni na kudhani ni ugonjwa huu, huo ni ugonjwa tofauti kabisa na huu tunaouchambua leo.
Tunapozungumzia maambukizi katika njia ya mkojo, tuna maana ni kutoka eneo la nje la utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo, kitaalamu huitwa Lower Urinary Tract Infect na ikihusisha eneo la juu ya kibofu jina hubadilika na kuitwa, Upper Urinary Tract Infection.
Mara nyingi maambukizi haya kwa wanawake hutokea wakati wa kujisafisha, kutonawa vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani chafu. Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bakteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bakteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi.
Upungufu wa homoni ya kike iitwayo Oestrogen husababisha bakteria wasababishao maambukizi katika njia ya mkojo kuzaliana kirahisi.Matatizo haya ya maambukizi licha ya kuwapata zaidi wanawake, huwakumba pia watoto wadogo kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vyao vya uzazi, njia ya mkojo na haja kubwa vipo jirani.
Watoto wa kiume ambao hawajatahiriwa nao hupata maambukizi rahisi kutokana na viungo vyao vya uzazi kuwa vifupi na wanaponawa maji yasiyo salama kwa watoto wa kiume huwa rahisi bakteria kubaki katika ngozi inayoning’inia (govi), hivyo kusababisha tatizo hili.
Lakini pia wanaume watu wazima ambao hawajatahiriwa wanaweza kupata maambuzi kutokana na sababu ambazo tumezitaja hapo juu ambapo pia ni rahisi kwao kuambukizwa Ukimwi kama watafanya ngono zembe na ndiyo maana tunasisitiza tohara kwa wanaume.
Maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo zaidi ni bakteria wanaoishi katika mfumo wa haja kubwa kusafiri kwa bahati mbaya  na kujikita katika mfumo wa mkojo. Bakteria wengine waambukizao njia ya mkojo ni wale watokanao na magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia na trimonas na fangasi wanapojamiiana bila kutumia kinga.
Ili kuepuka kupata maambukizi katika njia ya mkojo, mara kwa mara, ni vema kutumia kinga yaani kondomu na kwa mwanamke kila anapomaliza kufanya ngono akojoe ili kuondoa bakteria walioingia au waliokaa katika tundu ya mkojo wakisubiri kuingia.Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu, unywaji wa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na kutokunywa maji ya kutosha huchangia tatizo hili.
Uwepo wa mawe katika figo na mirija ya figo hata ndani ya kibofu pia ni mojawapo ya chanzo cha maambukizi haya katika njia ya mkojo.
Dalili 
Baadhi ya dalili za mtu kuambukizwa bakteria katika njia ya mkojo kubwa ni maumivu wakati wa kukojoa, mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali japokuwa siyo kila mwenye dalili hizo ana maambukizi katika njia ya mkojo au wengine huita UTI yaani urinary tract infection wana ugonjwa huu.
Dalili nyingine za maambukizi ni maumivu,  kutokwa na usaha au majimaji wakati wa kukojoa kabla au baada ya kukojoa kukiambatana na maumivu na kuhisi moto wakati wa kukojoa mkojo.
Baadhi ya wanaume wakati mwingine hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa.
Wengine wenye maambukizi hujikuta wakipata vichomi katika njia ya mkojo, au kuhisi kuwashwa sehemu hiyo, kuumwa kiuno au tumbo na kadhalika.Mgonjwa anaweza pia kukumbwa na homa kali mara kwa mara na mwili kuwa mchovu, kwa watoto hupoteza hamu ya kula na mwili kuonesha kushoka.
Wagonjwa wengine hupata maumivu kwenye kibofu cha mkojo ambapo husikia maumivu  ya chini ya tumbo usawa wa kitovu na huwa hayaishi.Matatizo haya ya mfumo wa mkojo kama tulivyoona huko juu huwapata watu wote wanawake na wanaume. 
Watu wenye  matatizo haya kila wakipima huambiwa wana UTI. Kwa wanaume huhisi hata nguvu za kiume kupungua na wanawake hupoteza hamu ya tendo la ndoa.
WAJAWAZITO
Kwa wajawazito ugonjwa unaweza kuhatarisha maisha yao na mtoto aliye tumboni. Bakteria wanaweza kuingilia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhara mengine kama vile  shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo.
TIBA
Maambukizi katika njia ya mkojo hutibika kwa dawa mbalimbali za kisasa baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa mgonjwa ana maambukizi hayo.Dawa ambazo anaweza kupewa ni kama vile Ciprofloxacin, Fosfomycin, Monurol, Furadantin, Sulfam ethoxazole, co-trimax, ampicillin, gentamicin na kadhalika lakini usitumie dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri wa daktari.
Ushauri
Tunashauri kwa mwanamke kwamba epuka kujisafisha sehemu za siri na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupaka marashi sehemu hizo, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi.
Ujisafishapo baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bakteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo.
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauriana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi.
Kwa mwanaume maambukizi haya huathiri nguvu za kiume na kujipenyeza hadi katika korodani na huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kukufanya uwe mgumba.
Maambukizi ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume (prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bakteria kujenga makazi. Hali hiyo ikitokea mgonjwa lazima akamuone daktari ili awekewe mrija wa kutolea mkojo.