Showing posts with label MAGONJWA YA KICHWA. Show all posts
Showing posts with label MAGONJWA YA KICHWA. Show all posts

Tuesday, 20 October 2020

MARADHI YA KICHWA HEADACHES


 



Kuumwa na kichwa kumegawanyika sehemu kuu nyingi sana japo kuwa 1% yake ni ashirio la matatizo ya kiafya ambayo yame-advance. Kama vile concussion of brain,meningitis,encephaliti, na stroke. Kuumwa na kichwa pia inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate.

Sehemu ambazo huuma ni kama ifuatavyo:

- Mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa.
- Baadhi ya neva za fahamu zilizoko usoni

Misuli ya kichwani
Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwana chini ya ubongo kuna mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishu za ubongo kwa zenyewe haziumi kwani hazina mifumo ya fahamu ambayo inahisia.
Mambo haya 12 nayo yanahusika sana.

1: Nervous tension headaches;
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia vitamin b2 na c , ounguza au acha matumizi ya sukari,kahawa,chakula chenye kukusababishia mzio,misongo ya mawazo na ufanye mazoezi yakutosha.

2: Cluster headaches;
Kichwa kuuma haswa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protein ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.

3: Hangover headaches;
Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali haswa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kichogoni au shingoni,kunywa maji mengi na juice ya matunda freshi na uache pombe.

4: Exertion headaches;
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na haswa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili na usifanye mazoezi.

5: Caffein headaches;
Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokodogo mpaka utakapo acha kabisa.

6: Sinus headaches;
Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa zingine hii utkana na maambukizi.

7: Bilious headaches;
Kichwa na macho huuma haswa kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji yakutosha na kasha fanya enema.

8: Hunger headaches;
Maumivu ya kichwa ambaya husababishwa na kutokula kwa muda. Kula chochote ilimradi kiwe ni protein au carbohydrates .

9: Eyes ram headaches
Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo saa zingine inaweza kuwa sababu. lakini chanzo chake haswa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuana mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.

10: Menstrual headaches;
Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya.

11: Arthritis headaches;
Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa zingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu haswa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo.

12: Hypertension headaches;
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na halii itaisha bila shaka.

Kabla ya kukupa dawa na ushauri wangu nina maswali nikuulize unijibu.

Je unapata Usingizi wa kutosha? Unalala usiku masaa mangapi? Je, unakunywa maji ya kutosha? Una miaka mingapi? Unapata haja kubwa ya kutosha? Nenda pia kapime macho yako na ukapime tena kwenye mishipa yako ya fahamu huenda una matatizo. Na kitu kingine unakuwa upo juani uwe unavaa kichwani kofia.

DALILI ZA KIPANDA USO
Kipanda uso (Migraine) ni ugonjwa au maumivu makali ya kichwa anayokuwa nayo mtu baada ya mshipa wa damu (Enlargement of Artery ) kutanuka katika kichwa chake.

Baada ya kutanuka kwa mishipa hii ya damu, pia kuna kemikali ndani ya mwili zinazozalishwa na kuizunguka mishipa hii na kupelekea mtu apate maumivu makali ya kichwa na kutanuka zaidi kwa mishipa.

Maumivu makali ya kichwa hupelekea mfumo wa utendaji kazi wa mwili pia ubadilike, mtu atapatwa na kichefuchefu, kutapika, kuharisha, katika utumbo chakula hakitanyonywa vizuri kiingie mwilini, mtu atashindwa kuona vizuri maeneo yenye mwanga na kutopenda kukaa mazingira yenye sauti au kelele.

Vipo vitu mbalimbali vinavyoweza kuchangia mtu apate tatizo la kipanda uso, vitu hivi haimaanishi kuwa ni lazima kusababishe upate na hata kama haupo katika mazingira ya vitu hivi haimaanishi kuwa huwezi kupata tatizo la kipanda uso, miongoni mwa vitu hivyo ni kama vile: sauti kali au kelele, harufu kali, aleji, mwanga mkali, kuvuta sigara, matatizo ya kukosa usingizi, kukaa bila kula kwa muda mrefu, pombe, kubadilika badilika kwa siku za mwanamke (menstrual cycle fluctuations).

Inawezekana ukawa na tatizo hili la kipanda uso, miongoni mwa vitu vinavyowasaidia watu wenye kipanda uso ni kutumia dawa mbalimbali ukijumuisha dawa za maumivu zenye mchanganyiko na caffeine, pia utumiaji wa chai au kahawa umesaidia baadhi ya watu kuwapa nafuu ya maumivu makali ya kichwa.

Tunaweza kupunguza hatari (risk) ya kupata kipanda uso kwa kubadilisha staili ya maisha yetu ya kila siku, kuepuka vitu vyenye harufu kali, kuepuka utumiaji wa tumbaku (sigara), kupata muda wa kutosha kuupumzisha mwili (kulala), kufanya mazoezi, kutokaa bila kula kwa muda mrefu, kunywa maji ya kutosha.Je, unalo tatizo la kipanda uso (Migraine), dalili zako ni zipi na ni vitu gani ukitumia unapata nafuu?

Wednesday, 26 November 2014

JINSI YA KUBORESHA USINGIZI WAKO





MATATIZO YA KUKOSA USINGIZI yamekuwapo tangu zamani.
Leo mamilioni ya watu hawapati usingizi wa kutosha. Kulingana na mtaalamu wa usingizi kutoka Brazili Rubens Reimão, inakadiriwa kwamba asilimia 35 ya watu ulimwenguni wana ugonjwa wa kukosa usingizi.* Dakt. David Rapoport wa Kituo cha Matatizo ya Usingizi katika Chuo Kikuu cha New York alisema kwamba kukosa usingizi ni “mojawapo ya magonjwa mabaya sana mwanzoni mwa karne ya 21.”


Jambo baya zaidi ni kwamba watu wenye ugonjwa huo hawajui kuwa ni wagonjwa. Kulingana na watafiti wa Chuo Kikuu cha Federal huko São Paulo, Brazili, asilimia 3 tu ya wagonjwa ndio hupimwa ifaavyo. Wengi huona kukosa usingizi kuwa jambo la kawaida na hivyo wao husinzia-sinzia na kusumbuka mchana kutwa.

Inapokuwa Vigumu Kupata Usingizi
Kugeuka-geuka kitandani kwa saa nyingi, ukiwa macho, huku watu wengine wote wakiwa wamelala fofofo ni jambo lisilopendeza kamwe. Hata hivyo, ni kawaida kukosa usingizi mara kwa mara kwa sababu ya mikazo na hekaheka za maisha. Lakini mtu anapokosa usingizi kwa muda mrefu huenda akawa na matatizo ya kihisia-moyo au ya kitiba, na ni muhimu amwone daktari.


Je, una ugonjwa wa kukosa usingizi?
Ikiwa baada ya kujibu maswali hayo, unagundua kwamba una tatizo la kukosa usingizi, usikate tamaa. Kutambua kwamba una tatizo hilo ni hatua muhimu ya kulitatua. Mtaalamu wa neva Mbrazili Geraldo Rizzo, alisema asilimia 90 ya watu wenye ugonjwa huo wanaweza kutibiwa na kupona.
 
Hata hivyo, ili upate matibabu yafaayo, ni muhimu kujua hasa ni nini kinachosababisha ugonjwa huo. Uchunguzi wa kitiba unaoitwa polysomnogramumetumiwa kupima na kutibu magonjwa mengi ya kukosa usingizi.
Mojawapo ya visababishi vya kawaida vya kukosa usingizi kwa muda mrefu miongoni mwa watu wazima ni kukoroma. Iwapo umewahi kulala karibu na mtu anayekoroma, unajua kwamba jambo hilo huudhi sana. Kukoroma kunaonyesha kwamba mtu ana tatizo la kuziba koo, na hivyo mapafu yake hayapati hewa ya kutosha kwa muda fulani.

Hatua za kwanza za kutibu ugonjwa huo zinatia ndani kupunguza uzito, kuepuka pombe, na kutotumia dawa za kulegeza misuli. Wataalamu wa tiba wanaweza pia kudokeza mtu atumie dawa fulani au vifaa vinavyotiwa mdomoni au mashine inayoingiza pumzi mapafuni.*

Hali inapokuwa mbaya zaidi, huenda mgonjwa akahitaji kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha koo, taya, ulimi, au pua ili hewa iingie na kutoka kwa urahisi anapopumua.

Pia watoto wanaweza kupata ugonjwa wa kukosa usingizi. Dalili za kukosa usingizi zaweza kuonekana akiwa shuleni, kwa mfano, kuanguka mitihani, kuudhika upesi, na kukosa utulivu. Huenda ikafikiriwa kimakosa kwamba yeye ni machachari.

Watoto fulani hupambana na usingizi kwa kuimba, kuzungumza, kusikiliza hadithi au kufanya jambo lolote ili wasilale. Huenda wakatumia ujanja huo ili wakae na wazazi wao. Hata hivyo, nyakati nyingine, huenda mtoto akaogopa kulala kwa sababu ya kuota ndoto mbaya zinazosababishwa na sinema zenye kutisha, matangazo yenye jeuri, au ugomvi nyumbani. Wazazi wanaweza kuzuia matatizo hayo kwa kudumisha amani na upendo nyumbani. Bila shaka, matatizo yakizidi wanapaswa kumwona daktari. Ni dhahiri kwamba, watoto wanahitaji usingizi wa kutosha sawa na watu wazima.

Jinsi ya Kupata Usingizi wa Kutosha
Kwa karne nyingi imejulikana kwamba usingizi wa kutosha hauji kimuujiza. Kulala vizuri hutegemea mambo kadhaa mbali na kuepuka wasiwasi na mikazo.
Kupata usingizi wa kutosha usiku ni muhimu maishani. Hutia ndani kufanya mazoezi kwa ukawaida wakati ufaao kila siku. Kufanya mazoezi asubuhi au jioni kwaweza kumsaidia mtu apate usingizi wakati wa kulala. Lakini kufanya mazoezi kabla ya kulala kwaweza kuvuruga usingizi.

Kutazama sinema zenye kusisimua au kusoma vitabu vyenye hadithi motomoto pia kwaweza kutufanya tusilale. Ni heri kusoma kitabu kinacho starehesha, kusikiliza muziki wenye kutuliza au kuoga kwa maji moto.
Wataalamu wanasema kwamba unaweza kuzoeza ubongo wako kutambua wakati wa kulala kwa kujilaza kitandani wakati tu unapotaka kulala. Watu wanaokula, kusoma, kufanya kazi, kutazama televisheni, au kucheza michezo ya video kitandani huenda wasipate usingizi kwa urahisi.

Kuutayarisha mwili kwa ajili ya usingizi pia hutia ndani kuwa mwangalifu kuhusu unachokula na kunywa. Ingawa kunywa pombe kunaweza kumfanya mtu asinzie, kunaweza kuharibu usingizi. Kahawa, chai, koko, chokoleti, na vinywaji vilivyo na kola vyapasa kuepukwa usiku kwa sababu vinausisimua mwili. Kwa upande mwingine, kula maembe, viazi vitamu, ndizi, persimmon, machipukizi ya mitende, wali, machipukizi ya maharagwe, au njugu huchochea homoni iitwayo serotonin na kwaweza kuleta usingizi.

Onyo: Kula chakula kingi usiku sana kunaweza kuharibu usingizi kama tu kulala ukiwa na njaa.

Ni muhimu pia kudumisha hali zinazofaa mahali tunapolala. Hali-joto inayofaa, chumba chenye giza kisicho na kelele, godoro na pilo zenye kustarehesha huchangia usingizi mnono.

Ama kweli, huenda ukashindwa kuamka asubuhi kwa sababu ya starehe hizo zote. Lakini kumbuka kwamba kulala muda mrefu isivyo lazima, hata kwenye mwisho-juma,

kwaweza kuvuruga usingizi wako na kukuzuia kulala siku ifuatayo:
Kwa kweli, hungependa kudhuru kimakusudi kiungo chochote mwilini mwako. Usingizi ni muhimu, ni sehemu ya maisha ambayo haipasi kupuuzwa. Ama kweli, sisi hulala thuluthi moja ya muda wote wa maisha yetu.
Je, unaweza kuboresha usingizi wako? Anza leo!

VISABABISHI VIKUU VYA UGONJWA WA KUKOSA USINGIZI
 KITIBA: ugonjwa wa Alzheimer; kuziba koo; miguu isiyotulia; ugonjwa wa kutetemeka; kuamka-amka usiku kwa sababu ya kushtuka-shtuka; ugonjwa wa pumu; magonjwa ya moyo na tumbo

 KIAKILI: kushuka moyo, wasiwasi, hofu ya ghafula, misukumo ya kupita kiasi, mfadhaiko unaosababishwa na tukio lenye kutisha
 KIMAZINGIRA: mwangaza, kelele, joto, baridi, godoro lisilostarehesha, kulala na mwenzi asiyetulia kitandani.

 SABABU NYINGINEZO: pombe na dawa za kulevya, athari za dawa fulani

KUPIMA MAGONJWA YA KUKOSA USINGIZI
  Polysomnogram ni uchunguzi mbalimbali unaofanywa huku mgonjwa akiwa amelala katika hali za kawaida. Vifuatavyo ni baadhi ya vipimo muhimu katika uchunguzi huo.

 ElectroencephalogramHupima utendaji wa ubongo na hutumiwa kupanga na kupima vipindi mbalimbali vya usingizi.

 ElectrooculogramHurekodi misogeo ya macho wakati yanaposogea haraka-haraka usingizini.

 Electromyogram—Hutumiwa kuchunguza ulegevu wa misuli ya miguu na kidevu wakati macho yanaposogea haraka-haraka usingizini.

 ElectrocardiogramHutumiwa kupima mpigo wa moyo usiku kucha.

 Hali ya kupumua na misogeo ya mwilihewa inayopitia katika pua na mdomo hupimwa pamoja na kusogea kwa tumbo na kifua.

 Kiasi cha oksijeni katika damuhupimwa kwa kifaa kinachoitwa oximeter kinachounganishwa na kidole cha mgonjwa

TATIZO LA UKOSEFU WA USINGIZI NI DALILI YA MARADHI YA ALZHEIMER





Picha ya Kopyuta ikionyesha athari za Alzheimer

Tatizo la kukosa usingizi huenda likawa ishara ya kutambua mapema maradhi ya kupiswa na akili au ''Alzheimer'' kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ambaye ana maumbile yanayofananishwa na binadamu.

Vipande vya protini, kwa lugha ya kitaalamu (plaques) au utando kwenye ubongo yanadhaniwa kuwa sehemu nyeti inayosababisha maradhi haya.

Utafiti uliofanywa na kuchapishwa katika jarida la tafsiri ya matukio ya Sayansi, umeonyesha kuwa punde chembe chembe za utando ule ulipoanza kumea kwenye ubongo wa panya, usingizi ukaanza kuwa tatizo kwa viumbe hao.

Taasisi inayosimamia utafiti wa maradhi hayo, (Alzheimer's Research UK) imehimiza kuwa ikiwa uhusiano huo unaweza kuthibitishwa huenda ikawa muhimu kwa Madaktari.

Utafiti wa kutaka kugundua mapema kama mtu anaelea kukumbwa na maradhi ya Alzheimer inadhaniwa kuwa muhimu katika kutibu maradhi hayo.
Mgonjwa wa kupiswa na akili

Wagonjwa hawaonyeshi dalili kupitia hisia au kumbukumbu zao hadi baada ya mda mrefu wa maradhi kumkumba mgonjwa. Yanapofikia hapa sehemu za ubongo huwa zimeharibika kiasi

kwamba tiba inakua vugumu kupatikana au hata kushindwa kupatikana.
Ndiyo sababu wataalamu wanafanya juhudi za kuanza mapema kugundua kama mtu atapata maradhi haya, miaka kadhaa kabla ya dalili hizo kujitokeza.

Viwango vya protini ijulikanayo kama beta amyloid kimaumbile hupanda na kushuka miongoni mwa binadamu na pia panya katika kipindi cha saa 24. Hata hivyo ni ile protini ambayo husababisha utando usiofutika kwenye ubongo na maradhi ya Alzheimer.

Majaribio yaliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Washington yameonyesha kuwa panya wanaotoka usiku kwa kawaida hulala kwa dakika 40 kwa kila saa mchana. Lakini ubongo ulipoanza kupatwa na uchafu panya hawa wakaanza kusinzia kwa dakika 30 pekee.

Mmojapo wa wataalamu, Prof David Holtzman, alisema: "endapo mapungufu katika usingizi huanza mapema kiasi hiki katika ugonjwa wa Alzheimer, mabadiliko hayo yanaweza kutupa ishara ya wepesi wa kuweza kuyatambua maradhi haya."
Utando kwenye ubongo

"ikiwa matatizo haya ya usingizi yapo, hatuelewi hasa yanachukua mfumo gani, kupungua kwa usingizi kikamilifu au ni tatizo la kushindwa kabisa kulala au ni kitu tofauti kabisa."

Hata hivyo, utafiti unaofanyika kwa kutumia panya mara nyingi hayafai kutumika kwa binadamu kwa sababu nyingi zinzosababisha kutatizika na usingizi.

Dr Marie Janson, kutoka shirika la kujitolea Alzheimer's Research UK, ametaka utafiti zaidi ufanywe kwa kuwapima binadamu kuona kama kuna uhusiano baina ya matatizo ya kukosa usingizi na ugonjwa wa Alzheimer.

Aliongezea kuwa: "tayari umekuepo utafiti unaounganisha mabadiliko katika usingizi huchangia katika matumizi ya ubongo kwa fikra, lakini matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna uwezekano kwamba mapungufu katika usingizi pia inaweza kuwa ishara na onyo la maradhi ya kusahau

Friday, 7 November 2014

VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO



BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.
Hata hivyo, wakati mwingine utendaji kazi wa mwili unaweza kuwa siyo mzuri kutokana na sababu mbalimbali zinazoathiri ubongo, mojawapo ikiwa ni kukosekana kwa lishe bora na staili ya maisha inayotakiwa kuimarisha ufanisi wa ubongo.
Chakula ni moja ya sababu za msingi kabisa za kuimarisha ufanisi wa ubongo na kuzuia magonjwa mengine ya akili. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui wale vyakula gani kwa lengo la kujenga akili na kuimarisha ubongo.
Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:
MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.
PILIPILI KALI
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.
MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.
NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.
BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.
KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.
MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

Sunday, 31 August 2014

FAHAMU AINA KUU ZA KIHARUSI (STROKE) - 3



WIKI mbili katika safu hii tumekuwa tukijadili tatizo la kiharusi (stroke) na kufafanua aina za ugonjwa huu. Endelea kuelimika.
Iwapo mgonjwa ataathirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (brain stem), mgonjwa anaweza kuwa na dalili za kuhisi mabadiliko ya harufu, ladha, kusikia na  kuona, kulegea kwa misuli ya macho (ptosis),  kupungua kwa ufahamu na kulegea kwa misuli ya uso, ulegevu wa ulimi  na atashindwa kuutoa nje au kuusogeza upande.
Pia atakuwa na upungufu wa uwezo wa kumeza, ulegevu wa misuli ya shingo na kushindwa kugeuza shingo upande mmoja, kushindwa kusimama sawasawa na kuona vitu kwa hali ya utofauti, mabadiliko ya upumuaji na kiwango cha moyo kudunda.
Iwapo sehemu mojawapo ya mfumo mkuu wa neva (central nervous system) imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kupoteza ufahamu kwa upande mmoja wa mwili na kulegea kwa misuli ya uso, kuhisi ganzi mwilini, na kupungua kwa ufahamu wa hisia na kutetemeka mwili.
Mgonjwa anaweza kukumbwa na matatizo ya kupoteza fahamu, maumivu makali ya kichwa na kutapika hasa kwa wale wenye kiharusi cha kuvuja damu (hemorrhagic stroke) ambacho husababisha ongezeko la shinikizo na mgandamizo wa ubongo ndani ya fuvu kutokana na kuvuja kwa damu.
TIBA
Mgonjwa kabla ya kutibiwa ni lazima afanyiwe vipimo kama vile cha ECG, ECHOCARDIOGRAM ambacho huwezesha kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (na kama kuna damu iliyoganda kwenye moyo ambayo inaweza kufika kwenye ubongo.
Holter monitor husaidia kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) zinazotokea kwa vipindi na Angiogram huwezesha kugundua matatizo kwenye mishipa ya damu na ni mishipa ipi ya damu iliyoziba.
Vipimo vya damu huwezesha kutambua uwepo wa lijamu mwilini (hypercholesterolemia) na mabadiliko mengine katika damu.
Mgonjwa hutibiwa kwa kutumia dawa za kuyeyusha damu iliyoganda (thrombolytics) au kwa kuondoa damu iliyoganda kwa njia mbalimbali (thrombectomy). Dawa nyingine kama vile Junior Aspirin na Clopidogrel hutolewa kwa ajili ya kuzuia chembe sahani kukusanyika na kuganda.
Matibabu ya kiharusi kinachotokana na damu kuvujia kwenye ubongo (Hemorrhagic stroke)  huhitaji tathmini ya upasuaji wa neva ili kuchunguza na kutibu sababu ya damu kuvuja. Haishauriwi kabisa kumpa mgonjwa wa aina hii ya kiharusi dawa za kuyeyusha damu iliyoganda au za kuzuia kuganda maana huhatarisha maisha ya mgonjwa badala ya kumsaidia. Kwahiyo ni vizuri kwa wataalamu kufanya  uchunguzi wa kutosha ili kuwa na uhakika na tatizo.
Hatari ya ugonjwa huu ni kwamba asilimia 75 ya wanaonusurika kifo huwa walemavu wa akili au kimwili na kusababisha kuathirika kwa ufanyaji kazi wao .
USHAURI
Wagonjwa wanashauriwa kutibu au kuzuia tatizo la shinikizo la damu, kisukari na wanapewa ushauri wa kufanya mazoezi kila siku, kuacha kuvuta au kunywa pombe kupita kiasi, kula chakula kisichokuwa na mafuta mengi na kisicho na chumvi nyingi.
Tumia dawa za kupunguza mafuta mwilini na watu wajiepushe kunenepa kupita kiasi (obesity).