Showing posts with label MAGONJWA YA MOYO. Show all posts
Showing posts with label MAGONJWA YA MOYO. Show all posts

Tuesday, 15 May 2018

UGONJWA WA PRESHA KUTOKANA NA UMRI WAKO.(BLOOD PRESSURE CHART BY AGE)





Presha ya kawaida isiwe zaidi ya 140/90mmlHg. 
Presha ikiwa haitibiwi huharibu mishipa ya damu katika macho, misuli ya moyo kuwa minene , kusababisha mshutuko wa moyo (heart attack), mshipa ya damu safi kuwa migumu, figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure) na kiharusi (stroke). 
Presha kwa mwanamke mjamzito inaweza kusababisha kifafa cha mimba na kufanya hata kiumbe kufa tumboni. Hivyo ni muhimu kuchunguza presha ya wanawake wote wajawazito.

Visababishi vya presha kuwa juu 


Chumvi nyingi
Unene uliozidi
Umri mkubwa au uzee
Figo ikiwa haifanyi kazi
Historia ya ugonjwa wapresha kwenye familia
Ugonjwa wa kisukari
Dalili ya mtu mwenye ugonjwa wa presha
Mara nyingi presha haina dalili hadi ilete madhara na hivyo huitwa( silent killer ) muuaji wa kimyakimya 


kichwa kuuma
kizunguzungu
kubanwa na pumzi
kutokuona vizuri
kichevuchevu

Vitu vinavyo changia hali presha kuwa mbaya zaidi ni


Kula chumvi nyingi
Unene uliozidi
Kutofanya mazoezi mara kwa mara
Kunywa pombe nyingi
Uvutaji wa sigara
Tiba ya ugonjwa wa presha


Mojawapo ya tiba ya presha ni kuacha vyakula vyenye chumvi kabisa kama itatumika iweke kidogo ya ladha wakati chukula kipo jikoni.
Pia mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito ni muhimu kwa tiba ya ugonjwa wa presha. Jitahidi kutenga mda wa mazoezi angalau dakika 30-60 mara tatu kwa wiki.
Epuka vyakula vyenye mafuta na lehemu maana vinaganda kwenye mishipa ya damu na kusababisha presha.
Daktari atakapo baini kuwa presha yako ipo juu, kulingana na aina na kiwango cha presha atakushauri kuhusiana na vyakula na jinsi ya kubadili mwenendo wa maisha au atakuanzishia dawa mara moja. Ni muhimu uelewe kuwa utakao anzishiwa dawa hutakiwi kuziacha maisha yako yote vinginevyo hali ya presha itarudi kama mwanzo.

Monday, 3 November 2014

UGONJWA WA TUNDU KATIKA MOYO KWA WATOTO


Leo tutazungumzia ugonjwa unaojulikana kama tundu katika kuta za ventrikali za moyo au kwa kitaalamu Ventricular Septal Defect (VSD).
Tatizo hili hutokea mara nyingi ambapo watoto 2-6 kati ya 1,000 uzaliwa nalo.
Tundu katika kuta za chini za moyo au VSD ni pale panapokuwepo na uwazi katika sehemu ya kuta ya septum inayotenganisha chemba za ventrikali zilizo chini ya moyo.
Moyo unapoanza kuumbika huanza kama bomba lililo wazi na kuendelea kujigawa katika sehemu mbalimbali na kuunda kuta.
Iwapo kitendo hicho hakitatekelezwa ipasavyo, hutokea uwazi katika kuta ya septum kwenye chemba za chini.
Kuwepo tundu hilo huruhusu damu yenye oksijeni kupita kutoka chemba ya kushoto ya chini ya moyo na kuingia katika chemba ya kulia ya chini ya moyo, badala ya kuingia kwenye mshipa wa aorta na kuelekea nje ya moyo kama inavyotakiwa.
Tundu la VSD linaweza kuwa dogo, la kati au kubwa. Tundu dogo katika kuta za chini za moyo huruhusu damu ndogo tu kutoka upande mmoja wa moyo kwenda wa pili hivyo haliathiri utendaji wa kawaida wa moyo na kwa kawaida huwa halihitaji matibabu maalumu.
Matundu ya aina hiyo huziba yenyewe wakati moyo unapoendelea kukua kipindi cha utotoni. Matundu yenye ukubwa wa kati na kubwa katika kuta za chini za moyo huruhusu kiwango kikubwa zaidi cha damu kupenya toka upande mmoja wa moyo kwenda mwingine, na mara nyingi huhitaji matibabu maalumu.
Watoto wenye tundu dogo katika moyo, huweza kukua bila matatizo yoyote, wakati wale wenye tundu kubwa huanza kuonyesha dalili mapema.
Vifuatavyo ni vihatarishi ambavyo vinaweza kusababisha mtoto kuzaliwa na tundu katika kuta za chini za moyo. Mama kuwa na maambukizi ya Rubella katika kipindi cha ujauzito au kuwa na ugonjwa wa kisukari cha wakati wa ujauzito ambao haujadhibitiwa na kuwa mnywaji wa pombe au mtumiaji wa madawa ya kulevya.
Mjamzito akitumia bila ushauri wa daktari baadhi ya dawa za hospitali katika kipindi cha ujauzito pia huweza kusababisha mtoto azaliwe na tundu katika kuta za chini za moyo.
DALILI
Iwapo tundu ni dogo huwa halina dalili yoyote na pale mtoto anapoendelea kukua tundu hilo hujifunga lenyewe. Lakini tundu likiwa kubwa, japokuwa mtoto anayezaliwa huwa haonyeshi dalili yoyote katika kipindi  hicho lakini baadaye huwa na dalili zifuatazo.
Rangi ya ngozi yake, midomo na kucha hubadilika na kuwa ya bluu, kunyonya au kula huwa kwa shida sana, ukuaji na kupumua kwa shida, kuchoka haraka, kujaa miguu na kuvimba tumbo, kuwa na mapigo ya moyo ya haraka.
Mtoto mwenye tatizo hili anapopimwa na daktari kwa kifaa, huweza kusikia ishara ya ongezeko la sauti ya ziada ya mapigo ya moyo wa mtoto hali ambayo kitaalamu huitwa holosystolic murmur.

UGONJWA WA TUNDU KATIKA MOYO KWA WATOTO-2



MADHARA YA TUNDU KATIKA MOYO
Madhara ambayo yanaweza kusababishwa na tundu katika kuta za chini za moyo ni Eisenmenger syndrome, hali ambayo hutokea pia pale mtu anapokuwa na tundu katika kuta za juu za moyo.
Tatizo hili hutokea wakati mtiririko wa damu unapoongezeka kutoka kushoto kwenda kulia kupitia tundu katika kuta za moyo, suala ambalo huongeza mtiririko wa damu katika mishipa ya mapafu na kusababisha shinikizo la damu katika mapafu.
Hali hii husababisha ongezeko la shinikizo la damu katika upande wa kulia wa moyo na kubadilika kwa shanti kutoka kulia kwenda kushoto.
Matokeo yake ni kuwa damu isiyo na oksijeni iliyotakiwa kwenda kwenye mapafu kwa ajili ya kusafishwa huchanganyika na damu yenye oksijeni iliyoko upande wa kushoto na kusambaa mwilini.
Madhara mengine ya tundu la VSD ni kupata ugonjwa wa kiharusi, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri pia maambukizi katika kuta za ndani za moyo (endocarditis) ugonjwa ambao tutauelezea katika matoleo yajayo.
Akinamama waliozaliwa na tatizo hili, ambao wametibiwa na hawakupata madhara wanaweza kushika mimba na kupitisha kipindi cha ujauzito bila matatizo yoyote.
Isipokuwa wale ambao hawakutibiwa au ambao tayari wameshapata madhara, hushauriwa kutoshika ujauzito kwa sababu ya hatari zinazoweza kutokea katika kipindi cha ujauzito.
Vilevile kwa akinamama waliozaliwa na tatizo hili, uwezekano wa watoto wao kuzaliwa na tatizo hili huwa mkubwa.
TIBA
Inafaa kujua kuwa, karibu nusu ya wagonjwa wenye tatizo hili huwa hawahitaji matibabu ya aina yoyote ile kwa kuwa tatizo hili hujirekebisha katika miaka ya mwanzo ya maisha yao.
Hata hivyo, kwa wale ambao watahitaji matibabu, hutibiwa kwa dawa au upasuaji kwa kutegemea ukubwa wa tatizo lenyewe.
Dawa zinazotumika kutibu ugonjwa huu ni zile ambazo hupunguza kasi ya moyo, huongeza nguvu ya mapigo ya moyo na zile ambazo hupunguza maji mwilini au diuretics.
Utaratibu wa kuziba tundu umegawanyika katika sehemu mbili na hufanyika iwapo tundu ni kubwa sana, au halikujirekebisha lenyewe wakati mtoto alipokuwa anakua na pale ikiwa dawa alizopewa mgonjwa hazikusaidia.
Pale inapohitajika upasuaji, mgonjwa hufanyiwa oparesheni ambapo kifua hufunguliwa ili kuziba tundu la VSD.
Matibabu mengine ni kupitisha mrija katika mshipa wa damu hadi katika sehemu ya tatizo kwenye moyo na kuliziba kwa kutumia kifaa maalumu. Kwa njia hii, huwa hakuna haja ya kufanya upasuaji wa kufungua kifua cha mgonjwa.
MWISHO

MAAJABU YATOKANAYO NA MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU MWILINI



Maajabu ya Mfumo wa Mzunguko wa Damu
WAZIA nyumba yenye mfumo tata wa mabomba kiasi cha kwamba kioevu kinachopitia humo kinaweza kusafirisha chakula, maji, oksijeni, na uchafu kwa njia salama. Isitoshe, mabomba hayo yanaweza kujirekebisha ili kumudu mahitaji mbalimbali nyumbani. Huo ungekuwa uhandisi bora kama nini!
Lakini, “mabomba” ya mwili wako hufanya mengi zaidi. Mbali na kudumisha halijoto ya mwili wako, husafirisha pia homoni nyingi sana, au chembe zinazosafirisha kemikali, na kingamwili dhidi ya maradhi. Mfumo wote ni laini na hunyumbulika pia, na hivyo huweza kustahimili mshtuko na kunyumbulika na viungo vya mwili. Mfumo huo haungeweza kubuniwa na mhandisi yeyote mwanadamu, lakini ndivyo alivyofanya Muumba alipoumba vena, ateri, na kapilari za mwili wa mwanadamu.

Sehemu za Msingi za Mfumo Huo
Kwa kweli mfumo wa mzunguko wa damu wa mwanadamu ni mifumo miwili inayofanya kazi pamoja.
  • Mmoja ni mfumo wa mishipa ya damu ya moyo, ambao umejumuisha  

    moyo, damu, na mishipa yote ya damu.
  • Mwingine ni mfumo wa limfu—mfumo wa mishipa inayosafirisha maji ya ziada, yanayoitwa limfu, kutoka kwa tishu za mwili na kuyarejesha kwenye damu. Mishipa ya damu ya mtu mzima mmoja tu ikiweza kuunganishwa kwa mstari ulionyooka, inaweza kufikia umbali wa kilometa 100,000 na hivyo kuizunguka dunia mara mbili na nusu! Mfumo huu wenye kuenea sana husafirisha damu ya uhai, inayofanyiza asilimia 8 hivi ya uzito wa mwili, hadi kwenye mabilioni ya chembe.
Bila shaka, moyo ndio chanzo cha nishati inayoendesha mfumo wa mishipa ya damu ya moyo. Unalingana na ngumi yako, nao husukuma angalau lita 9,500 za damu kila siku katika mwili wako wote—kwa ujumla ni kama kuinua uzani wa tani moja kwa kimo cha meta kumi kila muda wa saa 24!

Kuuchunguza Mfumo wa Mishipa ya Damu ya Moyo
Damu huzungukaje? Acheni tuanze na damu isiyo na oksijeni inayoingia katika moyo kupitia vena mbili kubwa—vena kubwa (ya juu) na vena kubwa (ya chini). (Ona picha.) Vena hizo hupeleka damu kwenye chumba cha kwanza cha moyo, chumba cha juu cha kulia (rightatrium). Chumba cha juu cha kulia husukuma damu kwenye chumba chenye misuli zaidi, chumba cha chini cha kulia (right ventricle.) Kutoka humo damu huenda mapafuni kupitia shina la mapafu na ateri mbili za mapafu—ateri pekee zinazosafirisha damu isiyo na oksijeni. Kwa kawaida damu hiyo husafirishwa na vena.

Mapafu huondoa kaboni dioksidi na kutia oksijeni katika damu hiyo. Kisha damu hutiririka kwenye chumba cha juu cha kushoto cha moyo (left atrium) kupitia vena nne za mapafu—vena pekee zinazosafirisha damu iliyokolea oksijeni. Chumba cha juu cha kushoto huelekeza damu hiyo katika chumba cha moyo chenye msukumo wenye nguvu zaidi, chumba cha chini cha kushoto (left ventricle), humo damu iliyokolea oksijeni husambazwa mwilini kupitia aorta (ateri kubwa). 

Vyumba viwili vya juu vya moyo hufumbuka pamoja kisha vyumba vya chini hufumbuka, utendaji huo wa pamoja hutokeza pigo la moyo. Vali nne za moyo huruhusu damu kusonga mbele moyoni bila kurejea nyuma.

Chumba cha chini cha kushoto chenye misuli zaidi huwa na msukumo unaozidi ule wa chumba cha chini cha kulia kwa mara sita, kwa sababu chumba cha chini cha kushoto husukuma damu katika mwili mzima. Msukumo huo ungeweza kwa urahisi kusababisha uvimbe (kuvimba au kupanuka kwa kuta za ateri) au hata kiharusi hatari ubongoni endapo hakungekuwa na utaratibu bora wa kupunguza msukumo huo wenye nguvu.

Ateri Zenye Kunyumbulika
Ateri kubwa zaidi mwilini mwako, aorta, na matawi yake makuu huitwa “ateri zenye kunyumbulika.” Sehemu yake ya ndani ni kubwa, ikiruhusu damu itiririke kwa urahisi. Zina kuta nene pia, zenye misuli zinazofunikwa na matabaka ya elastin, protini inayoshabihi mpira. Chumba cha chini cha kushoto 

kinaposukuma damu kwenye ateri hizo, zinapanuka au kuvimba, kisha hupunguza msukumo huo wenye nguvu sana na kusukuma damu hadi kwenye ateri, ateri zenye misuli au ateri zinazosambaza damu, ambazo pia zina kuta zenyeelastin. Msukumo wa damu huimarishwa na umbo hilo la ajabu kabla ya kufika katika kapilari (mishipa midogo) laini.*

Ateri zinazosambaza damu zina kipenyo cha kati ya sentimeta 1 hadi milimeta 0.3 hivi. Mishipa hiyo ya damu huelekeza mtiririko wa damu kwa kutunuka au kunywea kama zinavyoongozwa na nyuzinyuzi za pekee za neva, jambo hilo hufanya mfumo wa mzunguko wa damu utende kwa bidii sana. Mathalani, kunapotokea zahama au hatari, vipima-msukumo katika kuta za ateri huonya 

ubongo, kisha ubongo huwasilisha ujumbe kwa ateri zifaazo ili kupunguza mtiririko wa damu kwenye sehemu zisizo muhimu sana kama vile ngozi na kuielekeza kwenye viungo muhimu. Gazeti la New Scientist lasema hivi: “Ateri zako zaweza ‘kuhisi’ mtiririko wa damu, na kuitikia.” Je, si ajabu kwamba ateri zimetajwa kuwa “mabomba yenye akili”?

Kabla ya damu kutoka kwenye ateri ndogo zaidi—arterioles—msukumo wake huwa umeimarika kufikia milimeta 35 hivi za hidrajiri. Msukumo taratibu na imara, ni muhimu wakati huo kwa sababu ateri hizo ndogo sana huungana na mishipa midogo zaidi ya damu, kapilari.

Msururu wa Chembe Nyekundu
Zikiwa na kipenyo cha mikrometa nane hadi kumi, kapilari huwa nyembamba sana kiasi cha kwamba chembe nyekundu za damu hupenya kwa msururu. Japo kuta za kapilari huwa na tabaka moja tu ya chembe, huwa zinapitisha virutubishi (vinavyobebwa na plasma au umajimaji wa damu) na oksijeni 

(inayosafirishwa na chembe nyekundu) kwenye tishu zilizo karibu. Wakati huohuo, kaboni dioksidi na uchafu mwingine hutoka kwenye tishu na kukusanywa na kapilari ili ziondolewe mwilini. Kapilari zaweza pia kuelekeza mtiririko wa damu ikitegemea mahitaji ya tishu iliyo karibu, kupitia kwa msuli mdogo wenye umbo la kitanzi unaoitwa sphincter.

Kutoka kwa Vena Ndogo Kupitia kwa Vena Kubwa Hadi Moyoni
Damu inapotoka kwenye kapilari, huingia kwenye vena ndogo sana zinazoitwa venules. Vena hizo ndogo zenye kipenyo cha kati ya mikrometa 8 na 100, huungana kufanyiza vena ambazo hurejesha 

damu moyoni. Msukumo wa damu huwa umepungua sana inapofika kwenye vena, hivyo basi kuta za vena huwa nyembamba sana kuliko kuta za ateri. Pia zina kiasi kidogo chaelastin. Hata hivyo, sehemu yake ya ndani ni kubwa zaidi, hivyo hubeba asilimia 65 ya damu yote mwilini mwako.
Ili kushinda hali hiyo ya kupungua kwa msukumo wa damu, vena hurejesha damu moyoni kwa njia ya kustaajabisha sana. Kwanza, zina vali maalum zinazoshabihi vikombe ambazo huzuia damu 

kutiririka kutoka moyoni kwa sababu ya nguvu za uvutano. Pili, zinatumia misuli ya kiwiliwili cha mwili wako. Vipi? Misuli yako inaponyooka, tuseme katika miguu unapotembea, inabana vena zilizo karibu. Mbano huo husukuma damu kupitia vali zinazofunguka upande mmoja kuelekea kwenye moyo. Hatimaye, msukumo katika tumbo na katika kifua, unaosababishwa na kupumua, husaidia vena kusukuma damu kwenye chumba cha juu cha kulia cha moyo.

Mfumo wa mishipa ya damu ya moyo hufanya kazi kwa njia bora sana hivi kwamba hata mtu anapopumzika, unarejesha moyoni takriban lita 5 za damu kila dakika! Kutembea huzidisha kiasi hicho kufikia takriban lita 8, na mwanariadha mkakamavu aweza kuwa na lita 35 za damu zikibubujika kwenye moyo wake kila dakika—kiasi kinachozidi mara saba kile kiasi cha damu inayorejea moyoni mtu anapopumzika!

Nyakati nyingine vali za vena zinaweza kuvuja kwa sababu ya kasoro zilizorithiwa au kwa sababu mtu amenenepa kupita kiasi, au ni mja mzito, au mtu anaposimama kwa muda mrefu zaidi. Vali hizo zinapoziba, damu hufanyiza madonge chini yake, hilo huvimbisha vena na kusababisha ugonjwa wa kuvimba vena. Vivyo hivyo, kukaza misuli wakati wa kujifungua mtoto au wakati wa kwenda haja kubwa msalani, hubana sana tumbo, na hivyo damu hushindwa kurejea toka kwenye vena za mkundu na utumbo mpana. Hilo laweza kuvimbisha vena na kusababisha ugonjwa wa puru.

Mfumo wa Limfu
Kapilari hupeleka virutubishi kwenye tishu na kuondoa uchafu, lakini hukusanya maji machache sana kuliko yale ambayo zinasambaza. Protini muhimu za damu huvuja kwenye tishu. Ndiyo sababu mwili unahitaji mfumo wa limfu. Unakusanya maji yote ya ziada, yanayoitwa limfu, na kuyarejesha kwenye damu kupitia kwa vena kubwa iliyo chini ya shingo na nyingine iliyo kifuani.

Kama ilivyo na ateri na vena, kuna mishipa mbalimbali ya limfu. Mishipa midogo sana, inayoitwa kapilari za limfu, hufanyiza matabaka ya kapilari za damu. Mishipa hiyo midogo sana yenye kupenyeka kwa urahisi, hufyonza maji ya ziada na kuyapeleka kwenye mishipa mikubwa zaidi inayokusanya limfu na kuisafirisha kwenye mashina ya limfu. Mashina hayo huungana na kufanyiza vifereji vya limfu, vinavyopeleka limfu kwenye vena.

Limfu hutiririka upande mmoja tu—kuelekea kwenye moyo. Kwa hiyo, mishipa ya limfu haifanyizi mzunguko kama mfumo wa mishipa ya damu ya moyo. Utendaji dhaifu wa misuli ya mishipa ya limfu, pamoja na mpigo wa ateri zilizo ujiranini na kusogea kwa viungo, husaidia kusukuma maji ya limfu kupitia mfumo huo. Mishipa ya limfu inapoziba popote husababisha mrundamano wa maji kwenye sehemu iliyoathiriwa, hilo hutokeza uvimbe unaoitwa chovya.

Viini vya maradhi vyaweza pia kupitia kwenye mishipa ya limfu na kuingia mwilini. Kwa hiyo, Muumba wetu aliumba mfumo wa limfu ukiwa na kinga thabiti, viungo vya limfoidi: mafundo ya limfu—yaliyosambaa katika mishipa ambayo yanakusanya limfu—wengu, matezi ya dundumio, mafindifindo, kidole-tumbo, na folikali za limfoidi (Peyer’s patches), katika utumbo mwembamba. Viungo hivyo 

husaidia kutengeneza na kuhifadhi chembe za limfu ambazo ni chembe muhimu za mfumo wa kinga. Kwa hiyo, mfumo wa limfu wenye afya huchangia mwili wenye afya.

Hapa ndipo uchunguzi wetu wa mfumo wa mzunguko wa damu unapofikia tamati. Lakini, hata uchunguzi huu mfupi umefunua maajabu ya uhandisi yaliyo tata na bora zaidi. Isitoshe, mfumo huo hufanya kazi zake nyingi kimyakimya, bila wewe kujua—ila unapougua. Kwa hiyotunza mfumo wako wa mzunguko wa damu, nao utakutunza.



Mfumo wa Mishipa ya Damu ya Moyo
                                Damu iliyokolea oksijeni
             →   MAPAFU   →
MOYO                              MOYO
Chumba cha Chini Kulia           Chumba cha Chini Kushoto
   ↑                                 ↓
VENA                            ARTERI
   ↑                                 ↓
VENA NDOGO                       ATERI NDOGO
          ←   KAPILARI   ←
Damu isiyo na oksijeni
       Damu isiyo na oksijeni
    Kutoka mwilini                Kutoka mwilini
VENA KUBWA YA JUU         VENA KUBWA YA CHINI
        ↓                        ↓
              CHUMBA CHA JUU KULIA
                    ↓
             CHUMBA CHA CHINI KULIA
                   vali
                    ↓
                Hadi mapafuni
              ATERI YA MAPAFU
            Damu iliyokolea oksijeni
                Kutoka mapafuni
                    ↓
            CHUMBA CHA JUU KUSHOTO
                   vali
                    ↓
           CHUMBA  CHA CHINI  KUSHOTO
                    ↓
                  AORTA
                    ↓
                 Hadi mwilini

* Moyo ndio chanzo cha nishati inayoendesha mfumo wa mishipa ya damu ya moyo. Unalingana na ngumi yako, nao husukuma angalau lita 9,500 za damu kila siku katika mwili wako wote—kwa ujumla ni kama kuinua uzani wa tani moja kwa kimo cha meta kumi kila muda wa saa 24!

Thursday, 9 October 2014

NJIA 4 ASILIA ZA KUDHIBITI PRESHA YA KUPANDA (HIGH BLOOD PRESSURE)



LICHA ya kusababisha vifo vingi duniani ikiwemo Tanzania, shinikizo la damu (High Blood Pressure), inaelezwa na wataalamu kuwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari ya moyo, kiharusi na figo. Hata hivyo ugonjwa huu unaweza kuzuilika na kutibika kwa njia asilia, mbali na matibabu ya kawaida.
POTASIAMU MWILINI
Ulaji wa mboga na matunda yenye kiwango kingi cha Potasiamu (Potassium) ni sehemu muhimu sana katika mikakati na mipango anayoweza kuwa nayo mtu ya kudhibiti au kushusha kiwango cha shinikizo la damu alichonacho, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Profesa wa Tiba za Kinga, Dk. Linda Van Horn wa Chuo Cha Tiba cha Feiberb.
Profesa huyo anasema kuwa ulaji wa Potasiamu kati ya miligramu 2000  na 4000 kwa siku kutasaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu kwa kiasi kikubwa. Vyakula vinavyoaminika kuwa na kiwango kingi cha Potasiamu ni viazi vitamu, maharagwe, nyanya, juisi ya machungwa pamoja na karanga na korosho.
KUWA MAKINI NA CHUMVI
Baadhi ya makundi ya watu yanayougua ugonjwa wa shinikizo la damu, ulaji wa chumvi kiasi chochote huwa na athari mbaya kwao, hasa wale wenye historia ya kifamilia ya kuugua ugonjwa huu.
Kwa kuwa siyo rahisi mtu mwenye shinikizo la damu kujitambua kama chumvi ina muathiri zaidi, inashauriwa kila mtu kupunguza matumizi ya chumvi katika vyakula vya kila siku.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya lishe ya moyo na mapafu, Dk. Eva anasema kuwa kiwango cha chumvi cha wastani anachotakiwa kutumia mtu kwa siku kisizidi miligramu 1,500. Kipimo hicho ni zaidi kidogo ya kijiko kimoja cha chai ambacho huwa na miligramu 1200. Kwa maana nyingine, matumizi ya mtu kwa siku nzima katika milo yote hayatakiwi kuzidi kijiko kimoja na nusu cha chai.
ULAJI WA CHOKOLETI
Aina nyingi za chokoleti (Chocolate) zina aina ya kirutubisho (flavanols) kinacholainisha mishipa ya damu na kuwezesha damu kutembea vizuri mwilini. Katika utafiti mmoja, asilimia 18 ya wagonjwa wa presha waliokula chokoleti walionesha kupata ahueni kwa presha kushuka. Kiasi cha chokoleti moja kinatosha kwa siku, muhimu iwe inayotengenezwa kutokana na Cocoa.
TATIZO LA KUKOROMA USIKU
Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Alabama nchini Marekani, watu wengi wenye tatizo la kukoroma usiku, wana homoni ijulikanyo kama ‘aldosterone’ ambayo huongeza shinikizo la damu na inakadiriwa kuwa nusu ya watu wote wenye tatizo la kukoroma wana presha.
Mbali ya kukoroma kama dalili moja wapo ya kuwa na presha kwa baadhi ya watu, kusikia uchovu sana na kizunguzungu asubuhi nako ni dalili moja wapo, hivyo inashauriwa kumuona daktari akushauri kuondoa tatizo la kukoroma ili kujiepusha na matatizo yatokanayo na shinikizo la damu.
Kama hujui hali yako kuhusu  presha, ni vyema ukamuone daktari na kupima sasa.

Tuesday, 7 October 2014

SHAMBULIZI LA MOYO HEART ATTACK


Moja ya magonjwa hatari sana ambayo yanaweza kumpata mtu yoyote ni ugonjwa wa shambulizi la moyo. Huu ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanaume na wanawake.

Kwa kawaida, ugonjwa huu hutokea pale ambapo sehemu ya nyama ya moyo inapoharibika au kufa kutokana na kukosa damu ya kutosha.





Je tatizo hili husababishwa na nini?Husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo (coronary artery blockage) kutokana na mafuta mabaya mwilini (atherosclerotic plaque).

Watu gani wapo katika hatari ya tatizo hili?Watu walio katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu ni pamoja na

  • Wenye umri mkubwa miaka 45 kwa wanaume na 55 kwa wanawake
  • Wavutaji wa sigara
  • Watu wenye mafuta ya lijamu katika damu au wale wenye mafuta mabaya aina ya triglycerides na low density lipoprotein kwa kiwango kikubwa katika damu zao
  • Wenye kisukari
  • Wenye matatizo ya shinikizo la damu
  • Walio na unene kupita kiasi (obesity)
  • Wenye matatizo sugu ya kushindwa kufanya kazi kwa figo zao (chronic renal failure)
  • Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
  • Wanywaji wa pombe kupindukia
  • Watumiaji wa madawa ya kulevya hasa cocaine na methamphetamine
  • Watu wenye msongo wa mawazo (Chronic high stress levels)
  • Upungufu wa vitamin B2, B6, B12 na folic acid

Dalili za shambulizi la moyo
  • Maumivu makali ya ghafla kifuani ambayo husambaa kwenye taya, shingo, bega na mkono wa kushoto
  • Kupumua kwa shida
  • Kutoka jasho kwa wingi sana (diaphoresis)
  • Kuhisi mapigo ya moyo yanapiga haraka (palpitations)
  • Kichefuchefu
  • Kutapika
  • Kuchoka haraka sana
  • Kupoteza fahamu

Shambulizi la moyo limehusishwa na nini?Tafiti mbalimbali zimeusisha mambo yafuatayo na shambulizi la moyo
  • Msongo wa mawazo
  • Maambukizi hasa vichomi vinavyosababishwa na vimelea vya chlamydophila pneumonia.
  • Hutokea zaidi asubuhi hasa saa tatu (saa 3 asubuhi)


Vipimo na uchunguzi
  • ECG - Kipimo hiki huonyesha ni sehemu gani ya moyo iliyoathirika
  • Coronary angiography - Kinasaidia kwa kuangalia wapi ambapo mishipa ya damu imekuwa membamba sana kupita kiasi (narrowing of vessels) au imeziba.
  • Cardiac markers levels
  • X-ray ya kifua (chest X-ray)
  • MPI (Myocardial Perfusion Imaging) - Kipimo hiki hufanywa kwa kutumia mashine maalum ya PET Scan ambapo kinauwezo wa kugundua tatizo la shambulizi la moyo, huchunguza kikamilifu maumivu ya kifua, huangalia mwelekeo wa tiba ya kuzuia damu kuganda, hutoa mwelekeo wa ugonjwa wa shambulizi la moyo kama ni mzuri au mbaya, hutathmini ubora wa tiba ya shambulizi la moyo kabla na baada ya mgonjwa kupata tiba, huweza kutambua hata shambulizi la moyo ambalo si rahisi kugundulika kwa kutumia vipimo vyengine na pia hutathmini ukubwa wa tatizo la shambulizi la moyo. Hata hivyo kwa sasa kipimo hiki hakipatikani nchini kwetu.

Ili kuweza kutambua uwepo wa tatizo hili, mwaka 1979, shirika la Afya Duniani (WHO) liliweka vigezo vya kutambua shambulizi la moyo. Vigezo hivyo ni
  • Historia ya kuwa na maumivu ya kifua zaidi ya dakika 20
  • Mabadiliko katika kipimo cha ECG, na
  • Kupanda na kushuka kwa kipimo kiitwacho kitaalamu cardiac biomarkers hasa creatine kinase - MB na troponin

MatibabuShambulio la moyo ni tatizo linalohitaji matibabu ya dharua. Lisipotibiwa kwa haraka husababisha kifo katika muda mfupi sana tangu mgonjwa apatwe na tatizo. Matibabu ya tatizo hili hujumuisha
  • Kumpa mgonjwa hewa ya oksijeni
  • Mgonjwa hupewa vidonge vya Aspirini ndogo kuzuia damu kuganda (thrombolytic) kwa ajili ya kuyeyusha damu iliyaganda na hivyo kuzibua mirija midogo ya damu katika moyo iliyozibwa na kuganda huku kwa damu.
  • Vile vile mgonjwa hupewa dawa za kuweka chini ya ulimi kiitwacho nitrogylycerin (glyceryl trinitrate) ambazo husaidia kutanua mishipa ya damu (vasodilation)
  • Dawa ya kutuliza maumivu kwa mfano morphine
  • Dawa ya kuyeyusha mafuta katika mishipa ya damu kama vile clopidogrel
  • Kuzibua mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo kwa kutumia - Percutaneous coronary intervention (PCI)
  • Upasuaji (CABG)

Njia za kuzuia shambulizi la moyo
  • Kuacha kuvuta sigara
  • Kufanya mazoezi ya mara kwa mara
  • Kupunguza unywaji wa pombe
  • Kubadilisha aina ya mlo. Kupunguza mafuta katika mlo na chumvi.
  • Kutumia mafuta ya samaki (omega-3 fatty acids)
  • Kuna utafiti unaosema kuwa uchangiaji damu hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo hasa kwa wanaume.

Madhara ya shambulizi la moyo
  • Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
  • Matatizo katika mfumo wa mapigo ya moyo (Atrial fibrillation) ambayo hatimaye hupelekea kifo
  • Shambulizi la moyo kurudia mara ya pili
  • Kifo cha ghafla (sudden death)

Friday, 25 July 2014

MAAJABU YA MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU




Moyo ndio chanzo cha nishati inayoendesha mfumo wa mishipa ya damu ya moyo. Unalingana na ngumi yako, nao husukuma angalau lita 9,500 za damu kila siku katika mwili wako wote—kwa ujumla ni kama kuinua uzani wa tani moja kwa kimo cha meta kumi kila muda wa saa 24!


Maajabu ya Mfumo wa Mzunguko wa Damu
WAZIA nyumba yenye mfumo tata wa mabomba kiasi cha kwamba kioevu kinachopitia humo kinaweza kusafirisha chakula, maji, oksijeni, na uchafu kwa njia salama. Isitoshe, mabomba hayo yanaweza kujirekebisha ili kumudu mahitaji mbalimbali nyumbani. Huo ungekuwa uhandisi bora kama nini!
Lakini, “mabomba” ya mwili wako hufanya mengi zaidi. Mbali na kudumisha halijoto ya mwili wako, husafirisha pia homoni nyingi sana, au chembe zinazosafirisha kemikali, na kingamwili dhidi ya maradhi. Mfumo wote ni laini na hunyumbulika pia, na hivyo huweza kustahimili mshtuko na kunyumbulika na viungo vya mwili. Mfumo huo haungeweza kubuniwa na mhandisi yeyote mwanadamu, lakini ndivyo alivyofanya Muumba alipoumba vena, ateri, na kapilari za mwili wa mwanadamu.
Sehemu za Msingi za Mfumo Huo
Kwa kweli mfumo wa mzunguko wa damu wa mwanadamu ni mifumo miwili inayofanya kazi pamoja.
  • Mmoja ni mfumo wa mishipa ya damu ya moyo, ambao umejumuisha moyo, damu, na mishipa yote ya damu.
  • Mwingine ni mfumo wa limfu—mfumo wa mishipa inayosafirisha maji ya ziada, yanayoitwa limfu, kutoka kwa tishu za mwili na kuyarejesha kwenye damu. Mishipa ya damu ya mtu mzima mmoja tu ikiweza kuunganishwa kwa mstari ulionyooka, inaweza kufikia umbali wa kilometa 100,000 na hivyo kuizunguka dunia mara mbili na nusu! Mfumo huu wenye kuenea sana husafirisha damu ya uhai, inayofanyiza asilimia 8 hivi ya uzito wa mwili, hadi kwenye mabilioni ya chembe.
Bila shaka, moyo ndio chanzo cha nishati inayoendesha mfumo wa mishipa ya damu ya moyo. Unalingana na ngumi yako, nao husukuma angalau lita 9,500 za damu kila siku katika mwili wako wote—kwa ujumla ni kama kuinua uzani wa tani moja kwa kimo cha meta kumi kila muda wa saa 24!
Kuuchunguza Mfumo wa Mishipa ya Damu ya Moyo
Damu huzungukaje? Acheni tuanze na damu isiyo na oksijeni inayoingia katika moyo kupitia vena mbili kubwa—vena kubwa (ya juu) na vena kubwa (ya chini). (Ona picha.) Vena hizo hupeleka damu kwenye chumba cha kwanza cha moyo, chumba cha juu cha kulia (right atrium). Chumba cha juu cha kulia husukuma damu kwenye chumba chenye misuli zaidi, chumba cha chini cha kulia (rightventricle.) Kutoka humo damu huenda mapafuni kupitia shina la mapafu na ateri mbili za mapafu—ateri pekee zinazosafirisha damu isiyo na oksijeni. Kwa kawaida damu hiyo husafirishwa na vena.
Mapafu huondoa kaboni dioksidi na kutia oksijeni katika damu hiyo. Kisha damu hutiririka kwenye chumba cha juu cha kushoto cha moyo (left atrium) kupitia vena nne za mapafu—vena pekee zinazosafirisha damu iliyokolea oksijeni. Chumba cha juu cha kushoto huelekeza damu hiyo katika chumba cha moyo chenye msukumo wenye nguvu zaidi, chumba cha chini cha kushoto (leftventricle), humo damu iliyokolea oksijeni husambazwa mwilini kupitia aorta (ateri kubwa). Vyumba viwili vya juu vya moyo hufumbuka pamoja kisha vyumba vya chini hufumbuka, utendaji huo wa pamoja hutokeza pigo la moyo. Vali nne za moyo huruhusu damu kusonga mbele moyoni bila kurejea nyuma.
Chumba cha chini cha kushoto chenye misuli zaidi huwa na msukumo unaozidi ule wa chumba cha chini cha kulia kwa mara sita, kwa sababu chumba cha chini cha kushoto husukuma damu katika mwili mzima. Msukumo huo ungeweza kwa urahisi kusababisha uvimbe (kuvimba au kupanuka kwa kuta za ateri) au hata kiharusi hatari ubongoni endapo hakungekuwa na utaratibu bora wa kupunguza msukumo huo wenye nguvu.
Ateri Zenye Kunyumbulika
Ateri kubwa zaidi mwilini mwako, aorta, na matawi yake makuu huitwa “ateri zenye kunyumbulika.” Sehemu yake ya ndani ni kubwa, ikiruhusu damu itiririke kwa urahisi. Zina kuta nene pia, zenye misuli zinazofunikwa na matabaka ya elastin, protini inayoshabihi mpira. Chumba cha chini cha kushoto kinaposukuma damu kwenye ateri hizo, zinapanuka au kuvimba, kisha hupunguza msukumo huo wenye nguvu sana na kusukuma damu hadi kwenye ateri, ateri zenye misuli au ateri zinazosambaza damu, ambazo pia zina kuta zenye elastin. Msukumo wa damu huimarishwa na umbo hilo la ajabu kabla ya kufika katika kapilari (mishipa midogo) laini.*
Ateri zinazosambaza damu zina kipenyo cha kati ya sentimeta 1 hadi milimeta 0.3 hivi. Mishipa hiyo ya damu huelekeza mtiririko wa damu kwa kutunuka au kunywea kama zinavyoongozwa na nyuzinyuzi za pekee za neva, jambo hilo hufanya mfumo wa mzunguko wa damu utende kwa bidii sana. Mathalani, kunapotokea zahama au hatari, vipima-msukumo katika kuta za ateri huonya ubongo, kisha ubongo huwasilisha ujumbe kwa ateri zifaazo ili kupunguza mtiririko wa damu kwenye sehemu zisizo muhimu sana kama vile ngozi na kuielekeza kwenye viungo muhimu. Gazeti la New Scientist lasema hivi: “Ateri zako zaweza ‘kuhisi’ mtiririko wa damu, na kuitikia.” Je, si ajabu kwamba ateri zimetajwa kuwa “mabomba yenye akili”?
Kabla ya damu kutoka kwenye ateri ndogo zaidi—arterioles—msukumo wake huwa umeimarika kufikia milimeta 35 hivi za hidrajiri. Msukumo taratibu na imara, ni muhimu wakati huo kwa sababu ateri hizo ndogo sana huungana na mishipa midogo zaidi ya damu, kapilari.
Msururu wa Chembe Nyekundu
Zikiwa na kipenyo cha mikrometa nane hadi kumi, kapilari huwa nyembamba sana kiasi cha kwamba chembe nyekundu za damu hupenya kwa msururu. Japo kuta za kapilari huwa na tabaka moja tu ya chembe, huwa zinapitisha virutubishi (vinavyobebwa na plasma au umajimaji wa damu) na oksijeni (inayosafirishwa na chembe nyekundu) kwenye tishu zilizo karibu. Wakati huohuo, kaboni dioksidi na uchafu mwingine hutoka kwenye tishu na kukusanywa na kapilari ili ziondolewe mwilini. Kapilari zaweza pia kuelekeza mtiririko wa damu ikitegemea mahitaji ya tishu iliyo karibu, kupitia kwa msuli mdogo wenye umbo la kitanzi unaoitwa sphincter.
Kutoka kwa Vena Ndogo Kupitia kwa Vena Kubwa Hadi Moyoni
Damu inapotoka kwenye kapilari, huingia kwenye vena ndogo sana zinazoitwavenules. Vena hizo ndogo zenye kipenyo cha kati ya mikrometa 8 na 100, huungana kufanyiza vena ambazo hurejesha damu moyoni. Msukumo wa damu huwa umepungua sana inapofika kwenye vena, hivyo basi kuta za vena huwa nyembamba sana kuliko kuta za ateri. Pia zina kiasi kidogo cha elastin. Hata hivyo, sehemu yake ya ndani ni kubwa zaidi, hivyo hubeba asilimia 65 ya damu yote mwilini mwako.
Ili kushinda hali hiyo ya kupungua kwa msukumo wa damu, vena hurejesha damu moyoni kwa njia ya kustaajabisha sana. Kwanza, zina vali maalum zinazoshabihi vikombe ambazo huzuia damu kutiririka kutoka moyoni kwa sababu ya nguvu za uvutano. Pili, zinatumia misuli ya kiwiliwili cha mwili wako. Vipi? Misuli yako inaponyooka, tuseme katika miguu unapotembea, inabana vena zilizo karibu. Mbano huo husukuma damu kupitia vali zinazofunguka upande mmoja kuelekea kwenye moyo. Hatimaye, msukumo katika tumbo na katika kifua, unaosababishwa na kupumua, husaidia vena kusukuma damu kwenye chumba cha juu cha kulia cha moyo.
Mfumo wa mishipa ya damu ya moyo hufanya kazi kwa njia bora sana hivi kwamba hata mtu anapopumzika, unarejesha moyoni takriban lita 5 za damu kila dakika! Kutembea huzidisha kiasi hicho kufikia takriban lita 8, na mwanariadha mkakamavu aweza kuwa na lita 35 za damu zikibubujika kwenye moyo wake kila dakika—kiasi kinachozidi mara saba kile kiasi cha damu inayorejea moyoni mtu anapopumzika!
Nyakati nyingine vali za vena zinaweza kuvuja kwa sababu ya kasoro zilizorithiwa au kwa sababu mtu amenenepa kupita kiasi, au ni mja mzito, au mtu anaposimama kwa muda mrefu zaidi. Vali hizo zinapoziba, damu hufanyiza madonge chini yake, hilo huvimbisha vena na kusababisha ugonjwa wa kuvimba vena. Vivyo hivyo, kukaza misuli wakati wa kujifungua mtoto au wakati wa kwenda haja kubwa msalani, hubana sana tumbo, na hivyo damu hushindwa kurejea toka kwenye vena za mkundu na utumbo mpana. Hilo laweza kuvimbisha vena na kusababisha ugonjwa wa puru.
Mfumo wa Limfu
Kapilari hupeleka virutubishi kwenye tishu na kuondoa uchafu, lakini hukusanya maji machache sana kuliko yale ambayo zinasambaza. Protini muhimu za damu huvuja kwenye tishu. Ndiyo sababu mwili unahitaji mfumo wa limfu. Unakusanya maji yote ya ziada, yanayoitwa limfu, na kuyarejesha kwenye damu kupitia kwa vena kubwa iliyo chini ya shingo na nyingine iliyo kifuani.
Kama ilivyo na ateri na vena, kuna mishipa mbalimbali ya limfu. Mishipa midogo sana, inayoitwa kapilari za limfu, hufanyiza matabaka ya kapilari za damu. Mishipa hiyo midogo sana yenye kupenyeka kwa urahisi, hufyonza maji ya ziada na kuyapeleka kwenye mishipa mikubwa zaidi inayokusanya limfu na kuisafirisha kwenye mashina ya limfu. Mashina hayo huungana na kufanyiza vifereji vya limfu, vinavyopeleka limfu kwenye vena.
Limfu hutiririka upande mmoja tu—kuelekea kwenye moyo. Kwa hiyo, mishipa ya limfu haifanyizi mzunguko kama mfumo wa mishipa ya damu ya moyo. Utendaji dhaifu wa misuli ya mishipa ya limfu, pamoja na mpigo wa ateri zilizo ujiranini na kusogea kwa viungo, husaidia kusukuma maji ya limfu kupitia mfumo huo. Mishipa ya limfu inapoziba popote husababisha mrundamano wa maji kwenye sehemu iliyoathiriwa, hilo hutokeza uvimbe unaoitwa chovya.
Viini vya maradhi vyaweza pia kupitia kwenye mishipa ya limfu na kuingia mwilini. Kwa hiyo, Muumba wetu aliumba mfumo wa limfu ukiwa na kinga thabiti, viungo vya limfoidi: mafundo ya limfu—yaliyosambaa katika mishipa ambayo yanakusanya limfu—wengu, matezi ya dundumio, mafindifindo, kidole-tumbo, na folikali za limfoidi (Peyer’s patches), katika utumbo mwembamba. Viungo hivyo husaidia kutengeneza na kuhifadhi chembe za limfu ambazo ni chembe muhimu za mfumo wa kinga. Kwa hiyo, mfumo wa limfu wenye afya huchangia mwili wenye afya.
Hapa ndipo uchunguzi wetu wa mfumo wa mzunguko wa damu unapofikia tamati. Lakini, hata uchunguzi huu mfupi umefunua maajabu ya uhandisi yaliyo tata na bora zaidi. Isitoshe, mfumo huo hufanya kazi zake nyingi kimyakimya, bila wewe kujua—ila unapougua. Kwa hiyo tunza mfumo wako wa mzunguko wa damu, nao utakutunza.


Mfumo wa Mishipa ya Damu ya Moyo
                                Damu iliyokolea oksijeni
             →   MAPAFU   →
MOYO                              MOYO
Chumba cha Chini Kulia           Chumba cha Chini Kushoto
   ↑                                 ↓
VENA                            ARTERI
   ↑                                 ↓
VENA NDOGO                       ATERI NDOGO
          ←   KAPILARI   ←
Damu isiyo na oksijeni
       Damu isiyo na oksijeni
    Kutoka mwilini                Kutoka mwilini
VENA KUBWA YA JUU         VENA KUBWA YA CHINI
        ↓                        ↓
              CHUMBA CHA JUU KULIA
                    ↓
             CHUMBA CHA CHINI KULIA
                   vali
                    ↓
                Hadi mapafuni
              ATERI YA MAPAFU
            Damu iliyokolea oksijeni
                Kutoka mapafuni
                    ↓
            CHUMBA CHA JUU KUSHOTO
                   vali
                    ↓
           CHUMBA  CHA CHINI  KUSHOTO
                    ↓
                  AORTA
                    ↓
                 Hadi mwilini