Wednesday 30 April 2014

FAIDA ZA GILIGILIANI KAMA KIUNGO, DAWA NA UREMBO.




Giligiliani  Mboga.

Giligiliani ni kiungo cha kawaida sana,wengi tunakitumia jikoni 

kwenye mapishi mbalimbali,Kinaharufu nzuri na ladha ya uchachu 

kwa mbali.Majani na mbegu za giligiliani vyote hutumika kama 

viungo jikoni.


Giligiliani inawingi wa Vitamini A, B6, C,B12,pia ina wingi wa madini 

chuma(iron),Calcium na Magnesium

Giligiliani inasifika kwakua dawa na kinga ya magonjwa 

mengi.Historia inaonyesha kwamba Kiungo hiki kilitumika kama 

dawa tangu enzi za kale nchini Egypt.Hata hivyo,tafiti za kisayansi 

za karne hii ya 21 zinathibitisha taarifa hizi



Giligiliani  Mbegu


Ni vyema kujua kwamba tunaposema chakula Fulani ni dawa,basi 

maana yake ni kwamba chakula hicho 


kinavirutubisho Fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa 

Fulani au laa kuupa mwili uwezo wa 


kukabiliana na kujikinga na ugonjwa Fulani na si vinginevyo.


Hizi ni baadhi ya faida za giligiliani katika afya :



1.     Inawezesha usagaji mzuri wa chakula mwilini,hutuliza 

tumbo na huondoa gesi kwenye 

 
utumbo mwembamba  ambayo mara nyingi husababishwa na 

vyakula tunavyokula hivyo 

hupunguza 


utoaji  gesi chafu (kunyampa) kwa kiasi kikubwa sana


2.   Inazuia magojwa ya tumbo yasabaishwayo na bacteria 

aina ya Salmonella.moja ya magonjwa haya ni kuumwa 

tumbo na kuhara.


3.  Inazuia Ugonjwa wa (UTI.) Yaani Urinary tract infection


4.  Inazui kutapika na hali ya kuvurugika tumbo


5.  Inaondoa gesi tumboni


6.  Inashusha sukari kwenye damu.(lower blood sugar)


7.  Inapunguza  cholesterol mbaya mwilin



8.   Chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zinazoitajika mwilini ili 

kuwezesha usagaji mzuri wa chakula (Dietary fiber)


9.   Inawafaa sana wanawake ambao hupata hedhi nzito



10.Inaondoa maumivu,muwasho,na uvumbe(antinflammatory)


11. Huondoa chunusi na madoa kwenye ngozi


Unaweza kuandaa giligiliani katika njia mbalimbali ili 

kuitumia kama dawa

 

Kuondoa hedhi nzito.chemsha kijiko 1 cha chai cha mbegu za 

giligiliani na maji vikombe 


viwili.Chuja kisha ongeza sukari kidogo.Kunywa ikiwa 

yamoto au Maji ya vuguvugu

 

Kuondoa maumivu (Inflamation) chemsha kijiko kimoja cha 

chai cha mbegu za giligiliani 


zilizosagwa  na maji kikombe kimoja.Chuja kisha kunywa 

ikiwa vuguvugu



Kushusha sukari na kushusha cholesterol.Kunywa chai ya 

giligiliani (mbegu) mara kwa mara,pia 


tumia mbegu na majani ya giligiliani kwa wingi kwenye 

chakula.


Ili kuondoa chunusi na madoa meusi.Twanga au sigina 

majani ya giligiliani,chuja au kamua ili 


kupata maji yake.Pima vijiko vinne vya maji ya giligiliani 

kisha changanya na kijiko 1 cha chakula 


cha manjano(Binzari manjano).pakaa kwenye ngozi ,acha 

ikauke kisha osha au nawa na maji 


vuguvugu.Onyo:usisugue ngozi


Kutibu kuhara damu (dysentery).Changanya vijiko 2 vya 


chai vya maji ya giligiliani na kikombe 


kimoja cha maziwa fresh ambayo hayajatolewa krim


Chai ya giligiliani (mbegu) husaidia kuondoa au kutuliza 

asidi tumboni 


Matumizi ya mara kwa mara ya vyakula ambavyo ni tiba 

huupa mwili nafasi nzuri ya kuvuna 


virutubisho na kupata tiba ya magonjwa mbalimbali.


Ni vyema kujua kwamba asilimia kubwa ya vyakula na viungo 

tulivyonavyo majumbani ni tiba ya 

magonjwa mbalimbali.Madawa na Tiba nyingi za kisasa pia 

hutokana na mimea,virutubisho 

huvunwa kutoka kwenye mimea na vyakula na kuchanganywa 

na Kemikali ili kutoa vidonge na 

madawa ya magonjwA mbalimbali.



1 comments:

  1. Am Lisa by name, i was diagnosed with Herpes for 3years ago i lived in pain with the knowledge that i wasn't going to ever be well again i contacted so many herbal doctors on this issue and wasted a large sum of money but my. condition never got better i was determined to get my life back so one day i saw mr Brown post on how Dr Aba saved him from the VIRUS with herbal medicine i contacted Dr Aba on his email address dr.abaherbalhome@gmail.com we spoke on the issue i told him all that i went through and he told me not to worry that everything will be fine again so he prepared the medicine and send it to me through courier service and told me how to use it,after 14days of usage I went to see the doctor for test ,then the result was negative,am the happiest woman on earth now. this testimony is real.thanks to Dr Aba God bless you. you can also reach him on his whatsApp number +2348107155060   

    ReplyDelete