Giligiliani Mboga. |
Giligiliani ni kiungo cha kawaida sana,wengi tunakitumia jikoni
kwenye mapishi mbalimbali,Kinaharufu nzuri na ladha ya uchachu
kwa mbali.Majani na mbegu za giligiliani vyote hutumika kama
viungo jikoni.
Giligiliani inawingi wa Vitamini A, B6, C,B12,pia ina wingi wa madini
chuma(iron),Calcium na Magnesium
Giligiliani inasifika kwakua dawa na kinga ya magonjwa
mengi.Historia inaonyesha kwamba Kiungo hiki kilitumika kama
dawa tangu enzi za kale nchini Egypt.Hata hivyo,tafiti za kisayansi
za karne hii ya 21 zinathibitisha taarifa hizi
Giligiliani Mbegu |
Ni vyema kujua kwamba tunaposema chakula Fulani ni dawa,basi
maana yake ni kwamba chakula hicho
kinavirutubisho Fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa
Fulani au laa kuupa mwili uwezo wa
kukabiliana na kujikinga na ugonjwa Fulani na si vinginevyo.
Hizi ni baadhi ya faida za giligiliani katika afya :
1. Inawezesha usagaji mzuri wa chakula mwilini,hutuliza
tumbo na huondoa gesi kwenye
utumbo mwembamba ambayo mara nyingi husababishwa na
vyakula tunavyokula hivyo
hupunguza
utoaji gesi chafu (kunyampa) kwa kiasi kikubwa sana
2. Inazuia magojwa ya tumbo yasabaishwayo na bacteria
aina ya Salmonella.moja ya magonjwa haya ni kuumwa
tumbo na kuhara.
3. Inazuia Ugonjwa wa (UTI.) Yaani Urinary tract infection
4. Inazui kutapika na hali ya kuvurugika tumbo
5. Inaondoa gesi tumboni
6. Inashusha sukari kwenye damu.(lower blood sugar)
7. Inapunguza cholesterol mbaya mwilin
8. Chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zinazoitajika mwilini ili
kuwezesha usagaji mzuri wa chakula (Dietary fiber)
9. Inawafaa sana wanawake ambao hupata hedhi nzito
10.Inaondoa maumivu,muwasho,na uvumbe(antinflammatory)
11. Huondoa chunusi na madoa kwenye ngozi
Unaweza kuandaa giligiliani katika njia mbalimbali ili
kuitumia kama dawa
Kuondoa hedhi nzito.chemsha kijiko 1 cha chai cha mbegu za
giligiliani na maji vikombe
viwili.Chuja kisha ongeza sukari kidogo.Kunywa ikiwa
yamoto au Maji ya vuguvugu
Kuondoa maumivu (Inflamation) chemsha kijiko kimoja cha
chai cha mbegu za giligiliani
zilizosagwa na maji kikombe kimoja.Chuja kisha kunywa
ikiwa vuguvugu
Kushusha sukari na kushusha cholesterol.Kunywa chai ya
giligiliani (mbegu) mara kwa mara,pia
tumia mbegu na majani ya giligiliani kwa wingi kwenye
chakula.
Ili kuondoa chunusi na madoa meusi.Twanga au sigina
majani ya giligiliani,chuja au kamua ili
kupata maji yake.Pima vijiko vinne vya maji ya giligiliani
kisha changanya na kijiko 1 cha chakula
cha manjano(Binzari manjano).pakaa kwenye ngozi ,acha
ikauke kisha osha au nawa na maji
vuguvugu.Onyo:usisugue ngozi
Kutibu kuhara damu (dysentery).Changanya vijiko 2 vya
chai vya maji ya giligiliani na kikombe
kimoja cha maziwa fresh ambayo hayajatolewa krim
Chai ya giligiliani (mbegu) husaidia kuondoa au kutuliza
asidi tumboni
Matumizi ya mara kwa mara ya vyakula ambavyo ni tiba
huupa mwili nafasi nzuri ya kuvuna
virutubisho na kupata tiba ya magonjwa mbalimbali.
Ni vyema kujua kwamba asilimia kubwa ya vyakula na viungo
tulivyonavyo majumbani ni tiba ya
magonjwa mbalimbali.Madawa na Tiba nyingi za kisasa pia
hutokana na mimea,virutubisho
huvunwa kutoka kwenye mimea na vyakula na kuchanganywa
na Kemikali ili kutoa vidonge na
madawa ya magonjwA mbalimbali.
Am Lisa by name, i was diagnosed with Herpes for 3years ago i lived in pain with the knowledge that i wasn't going to ever be well again i contacted so many herbal doctors on this issue and wasted a large sum of money but my. condition never got better i was determined to get my life back so one day i saw mr Brown post on how Dr Aba saved him from the VIRUS with herbal medicine i contacted Dr Aba on his email address dr.abaherbalhome@gmail.com we spoke on the issue i told him all that i went through and he told me not to worry that everything will be fine again so he prepared the medicine and send it to me through courier service and told me how to use it,after 14days of usage I went to see the doctor for test ,then the result was negative,am the happiest woman on earth now. this testimony is real.thanks to Dr Aba God bless you. you can also reach him on his whatsApp number +2348107155060
ReplyDelete