Thursday 1 May 2014

MWANAMKE HUPEVUKA KIAKILI MAPEMA KULIKO MWANAUME




Ukuaji wa ubongo wa mtoto wa kiume na
wa kike ni tofauti sana. Msichana akili yake
huanza kukua kumzidi wa mvulana ndani ya
miezi mitatu ya mwanzo tangu kuzaliwa.
Katika uchunguzi wa wazazi watagundua
kwamba pindi wanapolea mtoto wa kike
husogea haraka zaidi kuliko wakati wa
kulea mtoto wa kiume," anasema Tuzie.
Licha  ya watoto wengi wa kike shuleni
kutofanya vizuri katika baadhi ya masomo
kama watoto wa kiume, wanasayansi
wanasema mtoto wa kike hupata uelewa
zaidi mapema kuliko wa kiume.

Imekuwa ni dhana ya muda mrefu
miongoni mwa wanajamii katika Afrika
kuwa   msichana hawezi kuolewa na
mwanamume waliyelingana umri kwa kuwa
ni vigumu kuelewana na kuheshimiana.
Dhana hiyo inajikita katika kuchambua
tofauti ya ufahamu kati ya mwanamke na
mwanamume wenye umri sawa. Mwanamke
huwa na akili iliyokomaa zaidi kuliko
mwanamume wa umri huo huo. Utafiti
mpya umeipa uzito nadharia yao, baada ya
kugundua kuwa ubongo wa msichana
hukomaa haraka kuliko wa mvulana.

 
 Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle
wamasema hii inaweza kusaidia kuelezea
sababu za wasichana wadogo kuonekana
kukua kwa kasi zaidi, kuliko wenzao wa
kiume wenye umri sawa.

Wanasayansi walitumia kipimo  maalumu
kwa ajili ya kuchunguza ubongo kwa watu
121 waliokuwa na umri kuanzia miaka
minne hadi 40. Matokeo ya utafiti huu
yalionyesha kwamba mchakato wa kubalehe
huanza  kati  ya miaka 10 kwa msichana,
huku mvulana huchukua muda mrefu
kuanzia miaka 11 mpaka 20.

Dk.  Marcus Kaiser, ambaye nbi mtafiti,
anasema: "Hii ni sehemu ya mchakato wa
kawaida wa kujifunza ubongo kwa jumla.
 "Kwa kawaida hata katika utambuzi,
imeonekana kwamba msichana ana uwezo
wa kushika mambo mengi zaidi kuliko
mvulana, ndiyo maana katika nchi za Afrika
mtoto wa kike anapika, anajaribu kutekeleza
majukumu ya nyumbani kama mama yake,
bado shuleni atafanya vizuri, lakini si kwa
mvulana. Akishazongwa na mambo mengi
hupunguza morali shuleni."

Dk. Kaiser anafafanua kuwa hatua za ukuaji
wa mtoto wa kike ni za haraka
ukilinganisha na wa kiume. Hii inatokana na
mfumo wa kike. Binti hukua haraka
kutokana na homoni zake mwilini na pia
akishabalehe ndipo anakuwa na uelewa
mpana kutokana na via vyake vya mwili
kumruhusu kubeba ujauzito."
Wataalamu nchini
Tuzie Edwin, ambaye ni msemaji wa Afya ya
Mama na Mtoto kutoka Kituo cha Huduma ya
Ushauri Nasaha, Lishe na Afya
(COUNSENUTH), anasema mtoto wa kike
huanza kupevuka kiakili ndani ya miezi
mitatu baada ya kuzaliwa.

"Ukuaji wa ubongo wa mtoto wa kiume na
wa kike ni tofauti sana. Akili ya Msichana
huanza kukua kumzidi wa mvulana ndani ya
miezi mitatu ya mwanzo tangu kuzaliwa.
Katika uchunguzi wa wazazi watagundua
kwamba wakati wanapomlea mtoto wa
kike, huongea haraka zaidi kuliko wakati wa
kulea mtoto wa kiume," anasema Tuzie na
kuongeza:

"Msichana hutambaa na kutembea haraka
zaidi ukilinganisha na mvulana, hata katika
kuongea. Pia huwa na uelewa mpana wa
mazingira, anakuwa mwepesi kuanza
kutumia choo mapema na ana
kumbukumbu kwamba hivi sasa anahitaji
kujisaidia na pia huanza kujitegemea ndani
ya miaka miwili ikilinganisha na wa kiume,"
anasema Edwin.

Anasema msichana huwa mwepesi katika
kuwasiliana na pia huweza kuanza
kushirikishwa katika baadhi ya mambo,
kama kutumwa dukani mapema zaidi
ukilinganisha na mvulana.
"Msichana pia anawahi kupevuka
ukilinganisha na mvulana, lakini
akishabalehe tu ubongo wake hukomaa
haraka na hapo ndipo maumbile yake
yanapoanza kujitengeneza mapema kwa
ajili ya mwili kujitayarisha kubeba ujauzito
wakati wowote. Hata hivyo akili yake hukua
kwa nafasi kubwa kipindi hiki, ukilinganisha
na mwanamume ambaye ni hadi miaka 10
baadaye," anasema Edwin.

Mkurugenzi  wa Idara ya Sayansi katika
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dk.
Elifatio Towo anasema mtoto yeyote ana
uwezo wa kukua kwa haraka zaidi,
kutokana na namna mzazi anavyomlisha na
haina tofauti na jinsi yake.

"Ikumbukwe kwamba mtoto yeyote
anaweza kukua kwa haraka zaidi ikiwa
mzazi atampa lishe bora na matunzo mazuri.
Kunyonyesha ndiyo sababu pekee
inayowafanya watoto akili zao zikue kwa
haraka zaidi. Lakini ikumbukwe kwamba
watoto wa kike huwa na busara zaidi katika
baadhi ya mambo na katika kufanya uamuzi
ikilinganishwa na wa kiume," anasema na
kuongeza:

"Huyu anaweza kufikiria makubwa zaidi ya
umri alionao, lakini mara nyingi inatokana
na maumbile kwamba yeye  ni mwanamke
hivyo kupevuka na anakuwa tayari kubeba
ujauzito, mwili wake unajitengeneza
wenyewe," anasema Dk. Towo.

Wasemavyo wazazi

Maimuna Jitegemee, mama  mwenye watoto
watatu, anasema "Binti yangu niliweza
kumwachia nyumba akiwa na umri wa
miaka 13 tu, niliweza kusafiri na kurudi.
Hata hivyo hali imekuwa tofauti kwa mtoto
wangu wa kiume, kwani licha ya kwamba
dada yake yupo chuoni hivi sasa, siwezi
kumwachia nyumba japokuwa ana umri wa
miaka 15."

0 comments:

Post a Comment