Friday 2 May 2014

MBINU ZA KUKABILIANA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUPIZI HARAKA, NA KUSHINDWA KURUDIA RAUNDI YA PILI -2



Lakini ukweli uko wazi kwamba kukimbilia
kutafuta uwezo wa kufanya mapenzi mara
sita au saba hakumfanyi mwanaume awe
mlinganifu mwenye kusifiwa na
 
wanawake wengi, kwani si wanawake
wote wana uwezo wa kufanya mapezi
kwa raundi hizo na si wote wanapenda
kutumia takika 30 kucheza mpira wa
 
kikubwa, wengine hukinai mapema na
huona kero kuwa na wanaume
ving’ang’anizi wenye sifa za kuganda
wanapopewa.

Kwa kufahamu haya utagundua kuwa
kukimbilia kutafuta tiba ya kumudu
kwenda mara saba ni jitihada mfu kabisa
zisizohitajika katika maisha ya mwanaume
 
hasa ukizingatia kwamba wenye uwezo
wa kufanya mapenzi mara nyingi
hawakuzaliwa hivyo, bali walijizoeza
kupitia mazingira ya malezi na makuzi yao.
 
Maana hawezi kuwa mzoefu wa raundi
mvulana aliyelelewa katika mafundisho ya
kukatazwa ngono na kulindwa hadi
akakakua.

Kadhalika hawi hodari wa kimapenzi
msichana aliyefundishwa kujitunza, yote
yatakayofuata kwa mvulana au msichana
humea baada ya kupandwa na tabia
chipukizi za ukubwani. Kwa msingi huo
mwanaume anajukumu la kuutengeneza
 
mwili wake uwe katika staili aitakayo.
Ndiyo maana kuna wengine hawamudu
kulala bila kufanya ngono, hii ikiwa na
maana kuwa wamejizoeza tu, si kwamba
wameumbwa na nguvu hizo.
 
Labda ili kufikia kilele cha somo hili ni
vema tukalejea matatizo matatu niliyosema
hapo juu ili tujue ni jinsi gani tunaweza
kuepukana nayo bila hata kumeza vidonge
na tukawa wanaume wa mbegu kama
wengi wenu mjuavyo.

Kwa kuanza tuzungumzie Kukosa
msisimko. Hapa tunatakiwa kuajitambua
sisi wenyewe kwanza, tukijua historia na
mazingira yetu ya kimapenzi.
Kwa wanaume ambao wamebanwa sana
 
kikazi na hufanya mapenzi mara moja
moja, hukabiliwa na tatizo la kukosa
msisimko kwa sababu miili yao imezoea.
Sasa ili kuifanya ichangamke lazima
waanze kuirejesha kwa kufanya mapenzi
 
mara kwa mara na kwa raundi chache.
Kisha wanatakiwa kufanya mazoezi na
kula vyakula, vinywaji vyenye nguvu ili
kujipa nguvu.

Pia kama mwanaume ameishi na
mwanawake kwa muda mrefu na
amekuwa na desturi ya kufanya mepenzi
mara kwa mara katika mazingira yale yale
anaweza kukumbwa na kasoro hiyo. Hivyo
anashauriwa kubadili mazingira ya
kufanyia mapenzi, kupeana mahaba
 
mapya, kuamsha mapenzi kwa kujaliana,
pia kuondoa fikra zote zenye kukinaisha
ikiwa sambamba na kuzingatia usafi wa
mwili. Yakifanyika hayo mwili utaitikia
taarifa ya akili na nguvu zitapatikana.
 
Kwa wanaoshindwa kurudia tendo
wanatakiwa kufuata kanuni hizo hapo juu.
Jambo kubwa ni suala la kuuzoeza mwili.
Usiulazimishe kuanza mara moja kwenda
 
mara nyingi wakati mapenzi yako
yamekuwa ya kuiba mpaka baba alale na
wakati mwingine muda wako wa kutoka
 
kazini umebana na hivyo kukufanya ufanye
mapenzi ya chap chap kila siku. Ukiwa mtu
wa namna hii haiwezi ikatoke siku moja
ghafla tu ukafanya mpenzi mara tatu bila
kuchoka.

Pia inawezekana mwanaume akashindwa
kurudia tendo si kwa sababu hana nguvu
bali hapewi ushirikiano wa kutosha toka
kwa mpenzi wake. Hivyo wakati wa
kutafuta uwezo wa kwenda raundi nyingi
ni vema usaidizi wa mwanamke
 
ukatolewa, isitokee kupokea lawama tu za
“huwezi, sijatosheka” kwani hizo ndizo
zinazowafanya wanaume washindwe
kabisa kwa hofu kuwa wanaaibika.
 
Mawazo ya kuaibika yanapopewa
kipaumbele huufanya uume kuzidi
kusinyaa, kwa maana hiyo ni vema
kuyatupilia mbali na kuacha kujihukumu.

Pia kuna hitilafu ya wakati wa
kuridhishana, inaweza kutokea
mwanamke akawa kamaliza raundi yake
ya kwanza, wakati anaingia msisimko wa
pili mwanaume anafika kileleni,
 
kinachotokea ni mwanamke kumlazimisha
mwanaume arudie tendo kwa muda mfupi
tangu amalize, jambo ambalo ni vigumu.
Sasa ikitokea mwanaume kachezewa na
 
hana msisimko anapata hofu kuwa
haweze, ikijengeka hivyo hata iweje jambo
halitawezekana tena. Hivyo ni bora
kupeana muda wa kupumzika kabla ya
hatua ya pili ya mchezo.

Pale inapotokea hamasa ya kurudia haipo
fikra za mwanaume zisipewe nafasi ya
kushindwa kwani nyakati, mchoko,
makujukumu, hofu za maisha na mambo
kama hayo yanapokuja katika siku ya
kustarehe ni wazi kuwa kiwango cha
ufanyaji mapenzi kitakuwa chini na hali hii
 
huwatokea wanaume wote, hata walio
hodari wa kwenda raundi kumi kwa siku.
Sambamba na hilo wanawake
wanashauriwa kutoonesha kujali pindi
inapotokea hali hiyo, badala yake
wawaambie wenzao kuwa siku hiyo
 
inatosha hata kama hawajatosheka, lengo
ni kuondoa hofu ambayo ndiyo msingi wa
wanaume kuishiwa uwezo wa kufanya
mapenzi. Hata hivyo maudhi, kufanya
mapenzi na usiyempenda, msongo wa
mawazo na kutokuaminiana huchangia
kupoteza msisimko wa kuwa ‘kidume’.
 
Ushauri wangu ni kwamba chochote
ambacho unataka mwili wako ukifanye
lazima uuzoeze. Ukizoea kuamka saa 12
asubuhi mwili utatii kanuni hiyo. Na
ukizoea kufanya mapenzi kila siku mara
mbili au tatu hali itakuwa hivyo.
Mwisho
katika sura hii ni vema wanaume na
wanawake wakajifahamu kuwa uwezo wa
kufanya mapenzi unapungua kufuatana na
umri isitokee mtu akakosa raha kisa
hawezi kwenda mara nyingi kama zamani
wakati anajua kabisa umri wake umekuwa
mkubwa.

Jamani kutafuta nguvu za ujana zirudie
uzeeni ni kujipa taabu ya bure. Ukiona
umeingia kwenye utu uzima na mwili
wako unaishiwa uwezo, kubaliana na hali.
Lakini jambo la kushangaza siku hizi hata
vikongwe wanapanga foleni kwa
 
waganga kutafuta tiba ya kufanya mapenzi
mara tatu kwa siku! Mapenzi yanataka
uwezo wa akili na mwili tusishindane na
uwezo asili tutapoteza muda na pesa bure.
Tatizo la mwisho ambalo nalo linatajwa
kuwasumbua zaidi wanaume ni maumbile
madogo ya uume.
Wanaume wengi
wamekuwa wakilalamika kuwa maumbile
yao yanawazuia kuwapa dozi wapenzi
wao. Lakini kama nilivyosema huko nyuma
kwamba mapenzi hayana kanuni kwamba
lazima mtu awe hivi ili amtosheleze
mwenzake. Kinacholeta raha katika
 
mapenzi ni hisia, hii ikiwa na maana
kwamba mwanaume au mwanamke
anaweza kufurahia mapenzi kwa
kutomasana na kuhamasishana kwa
viungo vingine vya mwili na kujikuta
wameridhika hata bila ya kuingiliana.

Kwa maana hiyo wale ambao
wanamaumbile madogo wanaweza
kutafuta wanawake ambao nao
wanamaumbile ya aina yao. Baadhi ya
watalaam wanasema kwamba kwa
 
kawaida umbile la nyeti za mtu linakwenda
sambamba na urefu wa mwili wake. Kwa
maana hiyo wanawake wafupi, ingawa si
wote wanatajwa kuwa na nyeti zenye
ukomo mfupi zaidi ya warefu na
wembamba wa umbo.

Mbali na chaguo la mtu mwenye kuendena
naye umbo, wanaume wenye kasoro hii
wanatakiwa kujifunza sana michezo ya
kimapenzi ambayo itawasaidia
kuwafikisha kileleni wapenzi wao. Ni
muhimu kwao kutumia sanaa na mitindo
inayopunguza umbali na ukomo wa nyeti
za kike.

 
Mwisho ni misingi ya tiba hii:
MOJA ni kuepuka hofu. Ikitokea siku moja
umeshindwa katika tendo haina maana
una kasoro, bali ni hali ya kawaida, hivyo
usiingize huzuni na hofu utakuza tatizo.
Hivyo kwa wale wenye tatizo hili
wapunguze wasiwasi na wajiamini kuwa
hawana tatizo.
 
PILI, nguvu za kiume zinahitaji mwili
wenye nguvu, hivyo ni busara kula lishe
bora na kufanya mazoezi yasiyokuwa
makali sana.
 
TATU, kumfundisha mwanamke namna ya
kukusisimua.
 
NNE, kuepuka mawazo ya kuhuzunisha
wakati wa tendo.
 
TANO, kupata muda wa kupumzisha mwili.
 
SITA, kuepukana na pupa, tumia muda
usiopungua takika 20 kufanya romance.
 
SABA, kujiamini.


0 comments:

Post a Comment