Friday 2 May 2014

MBINU ZA KUKABILIANA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUPIZI HARAKA, NA KUSHINDWA KURUDIA RAUNDI YA PILI



Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za
kiume tunakuwa katika uwanja mpana
zaidi wa tafakari za kibaiolojia na
kisaikolojia walizonazo wanaume.
Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo
sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi
mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili
linavyowasumbua wanaume wengi
duniani.

Sehemu kubwa ya malalamiko ya
wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi
maeneo matatu ambayo ni KUKOSA
MSISIMKO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO NA
KUKOSA KABISA NGUVU, huku kufika kileleni
mapema kukihusishwa pia kama pacha wa
janga hili ambalo linawasumbua zaidi
wanaume, ingawa na wanawake
wanakabiliwa na sehemu ndogo ya tatizo
hili.




Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni

uliowahusisha wanaume wanaofika kliniki
au kupata tiba za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume umeonesha kuwa, sio
wanaume wengi wenye sababu za kibaiolojia zinazowafanya wakose nguvu za kiume, isipokuwa wengi wao huwa na  matatizo ya kisaikolojia zaidi ambayo wahusika wanaweza kujiponya nayo bila hata kutumia vidonge wala dawa za mitishamba.


Ingawa Matabibu wanataja magonjwa ya
moyo, kisukari, shinikizo la damu,
magonjwa ya zinaa, unene wa kupita kiasi,
umri mkubwa kuwa ndiyo chanzo cha
wanaume kupungukiwa na nguvu za
kiume, lakini imebainika kuwa idadi
kubwa ya wanaume wanaofika hospitalini
kutafuta nguvu za kiume hawana
magonjwa hayo
Huu ni ushahidi kuwa wanaokabiliwa na
janga hili wamebeba tatizo la upungufu
wa nguvu za kiume kimawazo zaidi kuliko
hali halisi.

Ukweli wa mambo ulioibuliwa na
wanasaikolojia umebaini kuwa, wale wote
wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana
nguvu iwe ya kufika kileleni mapema,
kutokuwa na msisimko na kushindwa
kurudia tendo wamekosa maarifa tu ya
kufahamu na hawaijui miili yao na
kwamba wanaishi kwa kusikia zaidi ya
kujitambua.

Katika hali ya kawaida kila mwanadamu
ameumbwa kwa njinsi yake na inapotokea
kushabihiana basi ni bahati, lakini mara
nyingi usawa hupatikana kwa mmoja
kujifunza au kusaidiwa kufikia kiwango
cha mtu anayemuhitaji kuwa nae katika
maisha hasa ya kimapenzi. Jambo hili
wataalamu wanasema kuwa miili iko tayari
kutii mafunzo na kubadilisha tabia zake
kulingana na utashi wa mhusika.

Tatizo kubwa lililopo kwa wapenzi wengi
wanaolalamikia upungufu wa nguvu ni
kwamba maisha yao wanayachezea
kwenye viwanja vya wenzao wanaokutana
nao katika vijiwe na sehemu za kazi.
Usikivu wa mazungumzo toka kwa
wanaume wengine wenye uwezo wa
kwenda mara nne hadi saba katika tendo
au wanatumia dakika arobaini kufika
kileleni umewafanya wanaume wengi
kujihisi tu kuwa wao wanakasoro eti kwa
kuwa huishia mara mbili au moja katika
kufanya tendo.

Dhana ya kujiona ni mwenye kasoro
inapojengeka akilini mwa mwanaume,
huchipua hofu na hatimaye kumfanya
ashindwe kabisa kusisimka anapofikiria au
kukutana na mwanamke. Matokeo ya
hangaiko la akili hushusha uwezo wa
mwili na kumuongoza mtu kwenye
kuwaza ugonjwa kisha kukimbilia hospitali
au kwa waganga kutafuta tiba ya
ugongwa ambao kimsingi hanao.

0 comments:

Post a Comment