Wednesday, 30 April 2014

TIBA MBADALA YA MARADHI YA MASIKIO

Sikio (Ear) limegawika katika sehemu tatu kuu. Sehemu ya nje ya sikio, sehemu ya kati ya sikio na sehemu ya ndani ya sikio.

 

Kuna aina mbili ya matatizo ya masikio nayo ni:

 

i.              Otitis media : ambayo hutokea katika sehemu ya kati ya sikio na mara nyingi huwatokea watoto wachanga  na watoto wadogo.

 

ii.            Otitis externa: ambayo hutokea katika sehemu ya ndani ya sikio na mara nyingi huwatokea waogeleaji, na  hutokea zaidi wakati wa baridi.

 

Ishara za Matatizo ya masikio kwa Otitis media

i.              Kuumwa na kuchomwa kwa sikio

 

ii.                  Kutokwa na uchafu ndani ya sikio

 

iii.               Kutosikia kwa ghafla

 

iv.                Homa

 

Sababu za Otitis media:

·       Sababu kubwa ya maradhi hayo ni kuziba kwa bomba la sikio(Eustachiantube), kutokana na baridi, allergy pamoja na kuingia takataka. Hii inababisha maji maji ya sikio kujaa maji hayo nayo husababisha uvimbaji wa (ear drum) sikio.

 

Sababu za Otitis externa

·       Hii husababishwa na baketeria au fungi, maji maji yanayoingia ndani ya sikio ndio sababu kuu ya kufanya  bakteria na fungi kuzaana pia Skin allegies husababisha maradhi hayo.

 

Na sababu nyengine ni ulaji mbovu wa chakula pamoja na upungufu wa usafi wa mwili.

 

DAWA ZA KUJITIBU MARADHI YA MASIKIO:

 

i.                    Nyunyiza juisi ya Kitunguu saumu katika sikio linalouma

 

ii.                  Nenda Hospitali ukapigwe bomba ili maji na uchafu upate kutoka

 

iii.               Pasha moto mafuta ya Zaituni (Olive oil) na yasubiri yapowe na ujitie drops mbili hadi 3

 

iv.                Na usafishe masikio yako kila baada ya kutoka kukoga.

 

KUTOKWA NA USAHA SIKIONI:

Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.

 

TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA:


·       Kanuni ya kwanza:

Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio lenye kuuma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.

     Kanuni ya pili

Dondoshea tone moja ya mafuta ya kitunguu saumu ndani ya sikio ambalo linauma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu..

·       Kanuni ya tatu

Chukua mafuta ya habat soda na ufanye kama kanuni ya pili.

 

·       Kanuni ya nne

Ikiwa maradhi ya sikio ni kwa ajili ya bacteria, kunywa antibayotiki asilia kama vile juisi ya Aloe vera, kitunguu saumu, n.k. E.

0 comments:

Post a Comment