Monday 19 January 2015

UGONJWA WA MAFINDOFINDO (TONSILS)



Tonsil husababishwa na sababu nyingi tu . Pia husababishwa na upungufu wa white blood Cells katika mwili ambazo cells hizi ndio hupigana na vidudu vyote venye kuleta maradhi ndani ya mwili sasa vinaposhindwa kufanya kazi lymph zinavimba na husababisha Tonsils.


Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili, wapo ambao wanapata tonsils kwa kunywa maji ya baridi ambayo maji ya baridi huwa ni moja katika chanzo cha kupata tonsils, mavumbi huchangia vile vile pilipili na vitu vikali kama vile embe mbichi limau pia huwa ni sababu kuu ya kupata tonsil.



Wakati unapokuwa na tonsils muhimu zaidi kuacha maji ya baridi na vitu vyote vikali, zaidi utumie maji ya moto 



Dawa za tonsils ni : kama ni mtumiaji wa dawa za chemicals basi epincilin inasaidia sana kuondosha tonsils.

Dawa nyengine ambayo mimi binafsi naipendelea hii zaidi kwani inafanya kazi mara moja : Kamua ndimu moja katika glass yako kisha tia maji ya Uvuguvugu (warm water) na baadae tia vijiko vinne vidogo vya asali na kijiko robo cha chumvi kuroga uzuri na unywe pole pole



Au Dawa hii Jaribu pia Dawa ya TONSILS ni kusukutuwa maji yaliokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala Tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto.



Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia.



Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako.



Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya kazi na mdomo uko wazi basi pia unaweza kuumwa na Tonsils.



Vile vile kutoka nje kwenye joto kisha ukaingia pahala baridi huwa inasababisha Tonsils na maradhi mengine kama flu na kuumwa na kichwa..n.k 





6 comments:

  1. Asanteni sanatorium kwq msaada wenu

    ReplyDelete
  2. Asante sana, ni njia gani sahihi ya asili ya kuongeza white blood?

    ReplyDelete
  3. hii nakubaliana nayo 100% mi nimuanga wa hili tatizo na limeanza baada ya uck kuwa naamka kugeuza barafu (ice candy) uck nimekuwa nikiongea sana na kula tangawizi na miogo full chachandu na chill ndo kwanza nazidi kuuumwa kila siku ngoja nizingatie masharti naimani itanisaidia.

    ReplyDelete
  4. Nashukuru sana kwa kujifunza dawa hii ya tonsils

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. Hilo swala la tangawizi nakubaliana nalo 100%.maana mm nakunywa sana chai ya aina hiyo na tatizo ndio linazidi..

    ReplyDelete