Thursday, 11 December 2014

KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME NA MATIBABU YAKE PART-2




MATIBABU UPASUAJI NA BAADHI YA MATIBABU YA DAWA

Matatizo yanayosababishwa na matibabu ya dawa na upasuaji, ni kwamba, neva na mishipa ya damu inayohusika na usimamaji wa uume zinaweza kudhuriwa na aina ya matibabu ya dawa kama vile kutumia mionzi kuua seli za kansa; na upasuaji wa kibofu, utumbo mkubwa, kende au rektamu.


Kwa mfano, kama wanaume wanye saratani ya tezidume (prostate gland) na kibofu wanaelekea sana kukosa nguvu za kiume kwa sababu neva na tishu zingine zinazozunguka uvimbe mara nyingi hutakiwa kuondolewa pamoja na uvimbe.


Upasuaji katika fupanyonga, upasuaji au mionzi kwenye tezidume, kibofu cha mkojo, rektamu au utumbo mpana unaweza kusababisha kudhurika kwa neva katika eneo linalozungukwa. Madhara yanaweza kuingiliana na vichocheo ambavyo lazima vipite baina ya ubongo na viungo vya kujamiiana kuruhusu kusimama uume na kumwaga kwa shahawa.


Pindi madaktari wanapokata nyama katika tezidume, kibofu, au utumbo mpana, wakati mwingine hutenganisha neva zilizoungana na eneo la uume. Hapo upungufu wa nguvu za kiume hauepukiki.


Baadhi ya dawa zinaweza pia kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. Moja ya dawa kama hizo ni lithium, ambayo imeundwa kutokana na kemikali iitwayo lithium salts. Lithium hupewa watu ambao huugua aina ya baadhi ya magonjwa ya akili ambayo huwafanya kugeukageuka kitabia. Wakati mwingine hujisikia furaha na rafiki, kisha huwa na hasira na chuki sana. Lithium husaidia kupunguza idadi ya ugeugeu na pia hushusha kiwango cha nitric oxide ndani ya damu za corpora cavernosa.


POMBE

Pombe huathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu kwa wakati mmoja.

Pombe hutia ganzi (hali ya kutokuwa na hisia) na pia vilevile hutia ganzi fahamu na hivyo kusababisha msisimko dhaifu sana katika viungo vinavyohusika na tendo la ndoa.


Pombe huua seli za uzazi na hupunguza shahawa. Pia, huvuruga muungano baina ya ubongo na uume kwa kukata mawasiliano kisaikolojia na hivyo kushindwa kuwa katika hali ya kuwa na hamu ya tendo la ndoa na hivyo kutosimamisha uume; na pia pombe huzuia uundwaji wa homoni ya kiume, androgen.


Pombe hupunguza uwezo wa mwili kufanya kazi. Na pia hupunguza kiwango cha kufikiri vema na kufanya maamuzi mazuri.


MADAWA YA KULEVYA


Kama unatumia madawa ya kulevya, afya yako iko katika hatari kubwa sana ikiwa ni pamoja na kuishiwa nguvu za kiume. Amphetamines, kokeini, heroini, bangi, mirungi, gundi n.k. ni madawa ya kulevya ambayo yana madhara makubwa katika afya ya binadamu.


Bangi:
Bangi hudhuru shahawa (mbegu za kime). Wanaume wenye kuvuta bangi, wana kiwango kidogo cha maji ya shahawa kuliko wasiovuta.


Bangi husababisha shahawa kuogelea haraka sana na kuungua kabla ya kufikia yai. Ina kemikali ambazo huathiri mwili.


Bangi huvuruga programu ya kurithisha tabia na maumbile na hivyo kuleta mabadiliko ya urithi yasiyotakiwa.


Na mara nyingi, wanaume wanaovuta bangi, utungaji wa mimba kwao huwa tatizo.


Matatizo mengine ni kuchanganyikiwa na kufanya maamuzi mabaya, wasiwasi na hofu. Kupoteza kumbukumbu hasa za matukio ya muda mfupi. Kupungua kwa mwili kuweza kufanya kazi yake.


Mirungi/miraa:
Aina ya tindikali ni sumu na inaathiri maini.
Inaathiri nguvu za kiume na inaweza kusababisha uhanithi.
Kufunga choo na kukosa hamu ya kula.
Uvimbe katika utupu wa nyuma na ngiri inaweza kutokea.


Gundi:
Kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Kukosa oksijeni kwenye damu.
Kuharibika kwa ubongo.
Kuchanganyikiwa na kufanya maamuzi mabaya.


SIDE EFFECTS ZA DAWA ZA KEMIKALI

Madhara au athari (side effect) ya dawa za kemikali au dawa za hospilini, imekuwa ni tatizo na gumzo kubwa katika jamii yetu ya leo duniani kote. Ni moja ya sababu za kushindwa katika mchakato wa maendeleo ya dawa na kujiondoa kwa dawa baada ya kufika sokoni.


Athari ni matatizo ambayo hutokea pindi matibabu yanapokwenda kinyume na kinachotakiwa. Kwa mfano, kutoka damu/bawasiri ni athari iliyosababishwa kutokana na kwenda kinyume na kinachotakiwa.


Kwa mfano, athari maarufu ya matibabu ya saratani, ni uchovu, kichefu chefu, kutapika, kupungua kwa chembe hai za damu, kupoteza nywele, vidonda vya mdomoni ni miongani mwa athari ambayo hutokea.
Watengenezaji wa dawa wanatakiwa kuorodhesha athari zote za bidhaa zao.


Athari huweza kutofautiana kwa kila mtu kutegemeana na hali ya ugonjwa wake, umri, uzito, jinsia, na afya kwa ujumla. Athari inaweza kutokea wakati wa kuanza dawa, kupunguza au kuongeza dozi, au wakati wa kumaliza dawa. Pindi athari inapokuwa kubwa, dozi inaweza kubadilishwa, au dawa nyingine. Mtindo wa maisha na mfumo wa lishe husaidia kupunguza athari.


Dawa zinazoathiri mfumo wa neva, mzunguko wa damu na homoni lazima pia zinaathiri nguvu za kiume.


Kuna zaidi ya dawa 200 ambazo husababisha tatizo la kuishiwa nguvu za kiume. Licha ya kuwa dawa hutibu maradhi, katika kufanya hivyo, huathiri homoni, neva, mzunguko wa damu, matokeo yake hupunguza nguvu za kiume.


Baadhi ya dawa hupunguza ashki, kiwango cha utendaji wa tendo la ndoa, na pia hupunguza raha katika tendo la ndoa.


Dawa nyingi hasa za shinikizo la damu la kupanda, dawa za kukojoza kukosa usingizi, madawa ya ugonjwa wa kukakamaa (kutetemeka), tibakemikali na dawa za homoni, dawa za kupunguza maumivu:
Madawa mengine ambayo yanaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na madawa ya burudani na madawa ya kulevya kama vile: Alcohol (dawa inayotokana na sukari au vitu vyenye sukari vinapochacha, pombe, spiriti n.k). Amphetamines (amfetamini: aina ya dawa ya kulevya) Barbiturates (aina ya dawa ya usingizi), Cocaine (kokeini: aina ya dawa ya kulevya, Bangi, Heroin (heroini: dawa ya usingizi/kulevya itokanayo na afyuni), Nicotine (nikotini: sumu iliyo katika tumbaku), Opiates (Dawa za kutia usingizi);


Dawa zingine ni za vidonda vya tumbo na zile zinazotumika kupambana na mzio (allergy) na dawamfadhaiko za kutibu mfadhaiko zinaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.


Hata hivyo, kinachosababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa mwanamme huyu siyo kile kinachosababisha upungufu kwa mwanamme mwingine. Kama unadhani dawa unazotumia zinaweza kuwa na madhara katika tendo la ndoa, jaribu kupata ushauri wa daktari.
Pia, usiache kutumia dawa ghafla bila kupata ushauri wa daktari wako, kwa sababu baadhi ya dawa zitaweza kuweka uhai wako hatarini kama hazitaachwa kwa utaratibu mzuri.


BAISKELI

Wanaume wengi hufurahia kuendesha baiskeli na pia ni kama mazoezi. Kuendesha baiskeli ni zoezi ambalo pia humsaidia mtu kuweka uzito wa wastani.


Lakini pia, kuna tatizo ambalo linaweza kuletwa na uendeshaji wa baiskeli, “Upungufu wa nguvu za kiume.”


Tafiti za hivi karibuni, zinaonyesha kwamba, kuendesha baiskeli kwa muda mrefu ni jambo linaloweza kusababisha kuishiwa nguvu za kiume.


Wanaume ambao hukimbia maelfu ya maili kwa kunyonga baiskeli hudhuru korodani na mifuko ya korodani hizo; na hivyo kupunguza uwezo wa kumzalisha mwanamke au kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.


Viti vya baiskeli husugua neva. Hali hii huzuia damu kwenda kwenye uume na hivyo kusababisha tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.


Pindi unapoendesha baiskeli, tumia kiti chenye nafasi ili neva zinaoenda kwenye uume zisisuguliwe, na pia mara kwa mara pumzika kuendesha.


Hata hivyo, tatizo la kuisha nguvu za kiume kutokana na uendeshaji baiskeli linaweza kuisha kama mtu ataacha kuendesha baiskeli.


MATATIZO YA HOMONI

Kutolingana au kupungua kwa homoni ni sehemu ya sababu za matatizo ya kuishiwa nguvu za kiume. Tatizo hutokana na kama vile kutokuwa na testestorone* za kutosha, homoni dundumio, prolactin huweza kuathiri mwili kuitikia msisimko wa mapenzi. [Testestorone* ni homoni ya kiume ambayo hutengenezwa kwenye korodani, kazi yake ni kuleta hamu ya tendo la ndoa na kusaidia uume kusimama].


Tatizo hili linaweza kuwa ni matokeo ya uvimbe na teziubongo (pituitary gland), maradhi ya figo, maradhi ya ini na matibabu ya saratani ya tezidume.


Kama mgonjwa atahitaji matibabu yetu, tunaweza kumshauri kama anahitaji vipimo vya kuangalia homoni zako pale tutakapoona kuna umuhimu baada ya kufanya mahojiano naye kwa kina.


MARADHI YA ZINAA


Maradhi ya zinaa ni magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya vitendo vya kujamiiana. Kuna zaidi ya magonjwa 25 ya zinaa. Magonjwa mengi ya zinaa husambaa wakati wa kujamiiana (katika uke au sehemu ya utupu wa nyuma), lakini aina nyingine za kukutana kimapenzi kama kwa kutumia midomo (oral sex) zinaweza kusambaza magonjwa.


Magonjwa mengine ya zinaa yanaweza kusambazwa kwa njia nyingine zaidi ya kujamiiana. Magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na virusi kama UKIMWI yanaweza kuambukizwa kwa kukutana na damu iliyoathirika.


Wakati dalili zinapoanza kujitokeza wanaume husikia maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa usaha katika uume. Wanawake wanaweza kutokwa damu nje ya kipindi chao, maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa usaha katika uke, au maumivu chini ya kitovu.


Magonjwa ya zinaa kama yataachwa bila kutibiwa, yanaweza kusababisha maumivu makali, na kupunguza nguvu za kiume kwa wanaume pia na madhara mengine mengi. Pia huweza kumuondolea mwanamke uwezo wa kupata mtoto na hata mwanamme vilevile.


Magonjwa ya zinaa huambukizwa na bakteria wadogo wadogo, virusi, vijidudu vya maradhi, kuvu na protozoa wakaao katika sehemu vuguvugu na zenye unyevunyevu katika mwili kama vile sehemu za siri, mdomoni na kooni.


UMRI

Kadri umri unavyokuwa mkubwa ndio uwezo wa nguvu za kiume unavyozidi kupungua. Baadhi ya watu huanza kuona tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40 na kuendelea na hasa kama maisha yao hayakuwa na mazoezi ya mwili, na lishe yao ilikuwa duni.


Wanaume huwa na nguvu vizuri tu hadi wanapofika miaka 30, na baada ya hapo, baadhi yao huanza kuwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.


Hata hivyo, kuwa na umri mkubwa, haimaanishi kuwa ni wakati wa kutofurahia tendo la ndoa, licha ya kuwa wanaume wengi karibu asilimia 70 kuanzia umri wa miaka 65, uwezo na kiwango cha utendaji hushuka chini.


Ingawa wanaume wenye umri wa kati na wazee, ndiyo mara nyingi wenye matatizo ya nguvu za kiume kuliko vijana. Lakini, bado wazee wengi wanaona kuishiwa nguvu ni sehemu ya umri wao. Wengine wanaona aibu na wengine wamekata tama kutafuta ushauri na matibabu.


Kuishiwa nguvu za kiume ni tatizo ambalo linaweza kumkumba mtu yeyote. Na ajabu siku hizi, mambo yamekuwa kinyume sana tofauti na zamani ambapo zamani wazee ndiyo waliokuwa wakipatwa na tatizo hili sana.


Lakini, siku hizi vijana wanaonekana kukabiliwa na tatizo hili sana kuliko wazee! Mfumo mbaya wa maisha umechangia jambo hili sana. Watu wanakula hawajui wanakula nini, almuradi “kinaingia” tumboni!


Sababu za kupungua nguvu za kiume kutokana na umri:


Sababu za kupungua nguvu za kiume kutona na umri ni nyingi, zifuatazo ni baadhi yake na ambazo pia ndio zinazochangia kwa sehemu kubwa:


Kupungua kwa mtiririko wa damu: Uume husimama kama mtu anakuwa na mtiririko wa damu mzuri katika eneo la uume.


Kuanzia miaka ya 70 na kuendelea, tatizo la kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida sana. Kwa watu wengi katika umri huu, tatizo ni kutokana na kuta za mishipa ya ateri kuwa minene na hivyo mishipa ya damu inayobeba damu kwenda kwenye uume kuwa midogo sana ambapo hupunguza mtiririko wa damu.


Kupungua kwa kiwango cha testosteroni: Kiwango cha testosteroni na baadhi ya homoni za kiume huanza kushuka baada ya kufika umri wa kati, kushuka kwa homoni ya testostoroni ni sababu mojawapo kubwa ya kupungua nguvu za kiume.


Kupungua kwa kiwango cha Nitric Oxide: Nitric Oxide ni kemikali iliyohifadhika katika kuta za mishipa ya damu ambazo husambaza damu kwenda kwenye uume. Ni muhimu sana kwa usimamaji barabara wa uume. Kazi ya nitric oxide ni kuisaidia mishipa ya damu kutanuka kiasi cha kuchukua mbubujiko wa damu uliongezeka.


Pindi mwanamme anaposisimkwa pigo linalopita katika nyuzi za neva kutoka katika ubongo na neva hufyatua ufungukaji wa nitric oxide. Kufunguliwa kwa nitric oxide husisimua kimeng’enya ambacho huzalisha kipeleka habari kinachoitwa guanosine monophosphate (cGMP). cGMP husababisha misuli laini ya seli kutanuka ikiruhusu damu kuingia ndani ya tishu za sponji za uume. Hii ina maana kama hauna nitric oxide ya kutosha, hautakuwa na uwezo wa kusimamisha uume.


Uzalishaji wa nitric oxide hupungua kutokana na umri, na hii husababisha kupungua nguvu za kiume kwa wanaume.


Matokeo ya kutokuwa na nitric oxide ya kutosha, ni uume kusimama kwa udhaifu sana (laini laini) ambao hautakudumisha muda mrefu kwa ajili ya kufurahia tendo la ndoa. Nitric oxide ni muhimu sana kwa sababu hutanua mishipa ya damu. Pindi mishipa yako ya damu inapotanuka kutokana na nitric oxide, damu nyingi inaweza kuingia katika misuli na tishu laini katika uume wako.


Hata hivyo unaweza kusaidia uzalishaji wa nitric oxide kwa kutumia dawa asilia. Tunazo dawa asilia ambazo zina uwezo wa kuzalisha nitric oxide.


KUENDESHA MALORI YA BEHEWA

Idadi kubwa ya watafiti wa matatizo ya kuishiwa nguvu za kiume wanasema kwamba, kwa kukaa muda mrefu katika gari inaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. Hadi leo, bado hakuna ushahidi wa kisayansi wa kuishiwa nguvu za kiume kutokana na sababu hii.


Lakini, wanasayansi wengi wanaonyesha muungano kuthibitisha nadharia kwamba, uendeshaji wa gari kwa muda mrefu sana husababisha nguvu za kiume kupungua.


MARADHI YA FIGO

Maradhi ya figo yanaweza kusababisha mabadiliko ya kikemia kutokea ndani ya mwili wako ambayo huathiri homoni, mzunguko wa damu, ufanyaji kazi wa neva, na kiwango cha nishati.

Mara kwa mara mabadiliko hayo hushusha hamu ya tendo la ndoa au uwezo wa kufanya tendo la ndoa.


Madawa yanayotumika kutibu maradhi ya figo pia yanaweza kusababisha kuishiwa nguvu za kiume. Asilimia kubwa sana ya wenye maradhi ya figo, wana tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.


UPASUAJI


Sababu za kimwili zinazosababisha upungufu wa nguvu za kiume siyo maradhi peke yake yanayosababisha matatizo. Kuna sababu zingine ikiwa ni pamoja na upasuaji unaofanywa kwa ajili ya kutibu maradhi kama vile saratani ya kende.


Saratani ya kende peke yake tu haisababishi ukosefu wa nguvu za kiume, bali matibabu (ya mionzi ya upasuaji wa kuondoa saratani) inaweza kusababisha kuishiwa nguvu za kiume.


Matibabu ya saratani ya kende na kansa ya kibofu mara nyingi huhitaji uondoshaji wa neva na tishu kwenye eneo lililoathiriwa; ambapo huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.


Baadhi ya upasuaji huweza kuleta matatizo ya muda mfupi (miezi 6-18) na mingine inaweza kuleta madhara ya kudumu kwenye neva na tishu kwenye uume na inahitaji matibabu ili uume uweze kusimama.


MAJERAHA

Vyumba viwili kama sponji: ‘corpus covernosum’ hujaa damu kutoka kwenye mpwito neva zilizotumwa kutoka kwenye ubongo wakati wa msisimko wa mapenzi. Matokeo yake uume husimama.


Kama neva za kwenye uume zitadhuriwa, kuishiwa nguvu za kiume hutokea. Hii inaweza kutokea kupitia kibofu cha mkojo au upasuaji wa tezi dume, au inaweza kutokea kama nyonga, uti wa mgongo, uume au kende imejeruhika.


Majeraha yanayosababishwa na ajali, hasa ajali zinazotokana na baiskeli, michezo ya maji, upandaji farasi zinaweza kusababisha kuishiwa nguvu za kiume.


Waathirika wa majeraha katika uti wa mgongo huishiwa nguvu za kiume kwa sababu kuna madhara ya neva katika sehemu iliyoumia.


Majeraha kwenye fupanyonga, kibofu, uti wa mgongo na uume huhitaji upasuaji, pia husababisha kupungua nguvu za kiume.


VIDONDA VYA TUMBO


Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo.


Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo.


Vidonda vya tumbo vinaweza pia kuenea na kuathiri pia viungo vya jirani kama vile ini au kongosho (pancrease), na hivyo kusababisha matatizo ya nguvu za kiume.

MSONGO WA MAWAZO

Msongo wa mawazo ya kifamilia, matatizo ya mahusiano ya ndoa yanaweza kuleta madhara makubwa katika utendaji wako wa tendo la ndoa. Msongo hautaweza kukuruhusu kukuangazia kwenye tendo la ndoa pindi unapokuwa na mke wako.


Hofu, wasiwasi ni tatizo kubwa sana linalosababisha upungufu wa nguvu za kiume. Wanaume wengi hushindwa kutafuta tiba na badala yake huzidi kujiumiza kisaikolojia kwa kujisikia unyonge.


Ubongo hutoa kemikali zinazojulikana kama neurotransmitters ambazo hubinya misuli laini za uume na mishipa yake ya ateri. Mbinyo huu hupunguza mtririko wa damu kuingia katika uume na huongeza mtiririko wa damu kutoka nje ya uume. Hata msongo wa kawaida unaweza kuongeza utoaji wa kemikali za ubongo ambazo hudhuru nguvu za kiume.


Mwanamme ana jukumu la kuufunza mwili wake uwe katika mtindo autakao. Unapoufunza mwili wako kuamka asubuhi huzoea na ndivyo itakavyokuwa, utakapoufunza mwili wake kufanya mazoezi ndivyo itakavyokuwa, na utakapoufunza mwili wako.


Ili uume usimame, lazima mwili ujisikie vizuri na uchochewe. Mchakato huu huanzia katika ubongo, hivyo kama una matatizo ya kisaikolojia utauathiri utendaji wa ubongo wako, na hivyo, kuishiwa nguvu za kiume hutokea.


• Mwanaume anaweza kushindwa kurudia ‘raundi’ ya pili kwa sababu ya kutopewa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa mke wake. Mwanamke anatakiwa atoe msaada mkubwa, siyo kusema tu, “Sijatosheka!”


• Kufanya mapenzi na mke wako katika mazingira yale yale ya kila siku inaweza kukufanya ujione una tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.


• Kufikiria mapenzi na huku kuna mtu anakufanya ujisikie hofu.


• Kama kuna matatizo katika uhusiano wenu wa ndoa, kama vile kuwa na malumbano, kutopendana tena, au talaka iko mbele yenu.


• Kama unajisikia msongo sana kutokana na kupoteza kazi yako, pesa au mabadiliko makubwa katika maisha yako kama vile kifo cha mtu wako wa karibu.


• Kama huna uhakika wewe ni wa jinsia gani (ingawa ni mwanaume unaweza kujisikia kama mwanamke).


Kuishiwa nguvu za kiume kutokana na matatizo ya kisaikolojia mara kwa mara ni ya muda. Huendelea kuwepo kama kipengele cha kisaikolojia bado kipo. Kama utahisi kuwa hili ndilo tatizo, unaweza kujaribu kutazama kama upungufu wa nguvu za kiume uko ndani ya akili yako.


Ondoa fikra zenye kukinaisha na tengeneza mazingira masafi wakati wa tendo la ndoa. Mwili uko tayari kutii mafunzo na kubadilisha tabia zake kulingana na utashi wa mhusika.


Tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kutokana na matatizo ya kisaikolojia linaweza kuwa la muda mfupi au la muda mrefu. Hata hivyo, kwa yote mawili tiba SAHIHI inahitajika.


Kama jambo hili litatokea mara kwa mara, wewe pamoja na mke wako mnaweza mkakosa hamu ya mapenzi kabisa. Jambo hili litaongeza msongo mwingine wa mawazo katika maisha yako. Usipongalia, msongo utakuwa unazalisha msongo mwingine.


Kuudhibiti msongo wa mawazo ni pamoja na kufuata utaratibu wa mlo bora, na kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na kuweka muda kupumzika peke yako bila kuingiliwaingiliwa.


NGIRI

Ngiri ni sehemu ya viungo kuingia sehemu nyingine kwa sababu ya kulegea.
Kama mtu atahisi uvimbe katika tumbo, hiyo inaweza kuwa ngiri. Uvimbe unaweza kuwa laini, mdogo na usio na maumivu, au unaweza kuleta maumivu kidogo na kuvimba. Uvimbe unaweza kurudishwa ndani.


Viliomo ndani ya uvimbe vinaweza kuwa ni utumbo au tishu za mafuta. Mara nyingi ngiri hutokea katika maeneo ambapo ukuta wa tumbo ni dhaifu au mwembamba, ama kwa sababu eneo hilo tayari ni dhaifu au kutokana na muingiliano uliotokea siku za nyuma kama vile michakato ya upasuaji.


Mamilioni ya watu, hasa wanaume, wana ngiri ya tumboni.

Hali zinazoongeza msukumo wa uwazi wa tumbo pia zinaweza kusababisha ngiri au kuzidisha madhara kwenye ngiri iliyopo. Baadhi ya mifano inaweza kuwa ni unene mkubwa, kujikaza sana wakati wa kukojoa, maradhi sugu ya mapafu, na pia, majimaji katika uwazi wa tumbo.


Na pia kama misuli imedhoofishwa kutokana na lishe duni, sigara, na kazi za kutumia nguvu sana kupita kiasi ngiri inaweza kujitokeza. Ngiri hupunguza nguvu za kiume, hasa ngiri ya kinenani ambayo ni mzingo wa utumbo kutokezea moja kwa moja ndani ya eneo la kinena kupitia eneo dhaifu la ukuta wa tumbo.


KOMPYUTA & TV

Kuna ushahidi wa kisayansi kwamba, kuziweka korodani katika joto hupunguza kiwango cha shahawa. Kuweka kompyuta (laptop) kwenye mapaja huweza kumuondolea mwanamme uwezo wa kutunga mimba kwa sababu ya joto linalotolewa na kompyuta.


Sababu kwa nini korodani ziko nje ya mwili ni kwamba zinahitaji kuwa chini kidogo ya joto la mwili.


Pia, TV au kioo cha kompyuta hutoa mionzi ya sumaku umeme. Haishauriwi kuwa karibu sana na TV au kioo cha kompyuta (monitor). Wanawake wajawazito hawashauriwi kabisa kutazama TV.


Mionzi ni zaidi ya vile unavyofikiria. Unaweza kuipata mionzi hii kutoka katika vyanzo vingi kama vile mwanga wa jua, cheche za mnunurisho zinazotokana na mlipuko wa bomu la nyuklia, na katika vifaa vyako vya mawasiliano.


Simu yako ya mkononi unayotumia, kompyuta, TV, redio za FM, satelaiti za upelelezi, rada, ipods na vifaa vyote vya mawasiliano vina madhara makubwa.


Wanasayansi wamegundua kwamba, mionzi kutoka katika vifaa hivi huleta madhara kwenye ubongo wako, mwili na akili. Matumizi ya laptop/kompyuta zilizounganishwa na internet kwa wireless na zikawa karibu na viungo vya uzazi hupunguza ubora wa shahawa na hivyo kusababisha ugumba kwa wanaume, huathiri utendaji wa tendo la ndoa, na hivyo kupunguza nguvu za kiume. Pia husababisha saratani na kuleta mabadiliko katika DNA.


Unaweza kujiona wa kisasa zaidi kuwa na vifaa vya mawasiliano, lakini unaweza usijue madhara yake.


SIMU ZA MKONONI

Kuna tafiti nyingi ambazo zinaonyesha simu zina madhara. Madai kwamba simu za mkononi zinaweza kusababisha saratani ni maarufu sana, na ni madai ambayo yana ushahidi wa kisayansi.


Kuna nadharia kwamba antenna ambayo hupokea mawimbi ya sumaku umeme (EMWs : Electromagnetic Waves) hutoa mawimbi ya sumaku umeme yale yale na kuingia kwenye ubongo wa mtu anayetumia simu.


Kuna baadhi ya simu zina hatari zaidi kuliko zingine. Pia, kuna vipengele vingine kama umbali wa simu kwenye ubongo. Matatizo mengine ambayo simu za mkononi zinaweza kusababisha ni ugonjwa wa damu (leukemia), licha ya kuwa bado hakuna ushahidi wa kisayansi.


Chukulia mfano, simu yako ina FM Radio, upigaji picha, video, kamera, mtandao wa kimawasiliano wa kompyuta (internet), barua pepe (e-mail), maonyesho ya TV ya moja kwa moja na zaidi. Hizi kompyuta zilizo kwenye simu yako hufanya kazi katika kanuni ile ile kama kompyuta zingine.


Simu huleta madhara mengi yakiwemo saratani. Simu hudhuru kumbukumbu.

Katika tafiti za hivi karibuni, simu za mkononi pia zimeonyesha dalili kuwa zinaweza kudhuru afya ya shahawa, na hivyo hata kuathiri utungaji wa mimba. Kuna tafiti zilizofanywa kwa panya na kuonyesha kwamba mionzi ya simu inaweza kusababisha matatizo ya shahawa.


Tafiti zinaonyesha pia simu hudhuru uwezo wa nguvu za kiume.

Simu huweza kusababisha kichaa, mfadhaiko na maradhi ya neva ambayo hayana tiba ya aina yoyote ya dawa. Hii ndiyo sababu baadhi ya nchi zimepiga marufuku matumizi ya simu kwa watoto wadogo.


Kama utatumia simu yako kulingana na maelekezo ya watengenezaji utapunguza kiwango cha madhara katika afya yako.


MARADHI YA MGONGO/KIUNO

Mwili ni umbile tata sana uliounganishwa kwa vitu vingi ambavyo hufanya kazi kwa pamoja au kushindwa kufanya kazi vizuri pindi kitu kimoja kinapodhurika.


Uti wa mgongo umezungukwa na ‘pingili’ za mifupa zinazoitwa pingili za uti wa mgongo (vertebra). Mifupa hii huunda uti wa mgongo.


Uti wa mgongo ni mkusanyo wa neva ambazo hubeba mpwito neva kwenda kwenye ubongo na kutoka kwenye ubongo kwenda kwenye viungo vingine vya mwili.


Uti wa mgongo una takribani inchi 18 kwa urefu na hutanuka kutoka katika sehemu ya awali ya ubongo kuelekea chini katikati ya mgongo karibu na kiuno.


Neva ambazo zimo ndani ya uti wa mgongo ni upper motor neurons (UMNs) na kazi zao ni kubeba ujumbe kutoka katika ubongo na kupeleka kwenye neva za uti wa mgongo.


Neva za uti wa mgongo ambazo hutanuka, kusambaa kutoka katika uti wa mgongo kwenda kwenye viungo vingine vya mwili huitwa lower motor neurons (LMNs). Hizi neva za uti wa mgongo hutoka na kuingia katika kila usawa wa pingili za uti wa mgongo na maeneo maalumu ya mwili.


Licha ya kwamba maumivu ya mgongo yako kwa wanaume na wanawake, lakini wanaume ndiyo wanaoenekana kuwa na matatizo ya maumivu ya mgongo hasa kiunoni sana. Wanawake wengi wanaonekana kulalamika zaidi maumivu ya mgongo katikati.


Majeraha ya uti wa mgongo ni kudhurika kwa uti wa mgongo ambao matokeo yake ni kupotea kwa kazi kama ujongeaji na hisia (feeling).


Sababu nyingi za kudhurika uti wa mgongo ni mshtuko, ajali, kupigwa risasi, kuanguka n.k. au maradhi. Hata hivyo, uti wa mgongo hauhitaji kudhurika sana ili kuacha kufanya kazi.


Kushindwa kusimama kwa uume, mara nyingi husababishwa na kuharibiwa kwa mzunguko wa damu, au kupelekwa polepole au kuzuiwa kabisa.


Matatizo ya mgongo yanaweza kusababisha kuishiwa nguvu za kiume. Hii ni kwa sababu neva au vena hubanwa na hivyo kusababisha kupungua kwa damu inayokwenda katika eneo la nyonga.

Wanaume wengi ambao hupata ajali katika gari au majeraha kazini na majeraha hayo yakadhuru mgongo au sehemu za nyonga hujikuta wakiishiwa nguvu za kiume.

Katika kutibu tatizo la kuishiwa nguvu za kiume, kutibu mgongo ni jambo muhimu sana.

Licha ya kwamba maumivu ya mgongo yanaweza kuwapata watu wa rika zote, hata hivyo zaidi huwapata watu wazima, na hasa wanawake. Kama maumivu ya mgongo au kiuno yataambatana na dalili zifuatazo, basi yakupasa upate matibabu 

haraka na mapema: Kupungua uzito, kupanda joto la mwili, maumivu ambayo hayatoweki hata ukipumzika, maumivu ambayo yanakwenda mpaka chini ya miguu/magoti, kushindwa kujizuia haja ndogo au haja kubwa, kukojoa kwa shida, kuhisi ganzi sehemu ya viungo vya uzazi au sehemu ya haja kubwa, n.k.

MARADHI YA KUPINDA UUME

Moja ya matatizo ya kimwili ambalo linaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume ni maradhi ya mpindiko wa uume.

Maradhi haya mara nyingi hutokea baina ya umri wa miaka 45 na 60. Wastani ni umri wa miaka 50, lakini hata hivyo yanaweza kutokea kwa mtu mwenye umri wowote. Dalili za ugonjwa huu ni maumivu, uvimbe katika uume, mpinduko wa uume wakati wa kusimama.

Baadhi ya wanaume wana uume ambao husimama moja kwa moja. Ni hali ya kawaida kwa uume uliosimama kuwa na mpinduko mdogo. Mpinduko unaweza kuwa juu au chini, au kushoto au kulia. Mpinduko wa 30º ni wa kawaida, matibabu hayahitajiki labda kama pembe ni zaidi ya 45º.

Uume uliopinduka mara nyingi haumletei mwanamme tatizo lolote anapokuwa anafanya tendo la ndoa. Hata hivyo, ikiwa mpinduko wa uume utabadilika, hii inaweza kusababishwa na ugonjwa uitwao Peyronie.


Mwanamme anapokuwa na maradhi haya uume wake unaposimama huwa na mpinduko sana; na huweza kusimama kwa maumivu na kusababisha kupungua nguvu za kiume.

LISHE MBOVU

Misingi ya kula na kunywa ni kuwezesha mwili kufanya kazi katika hali ya kawaida.

Lishe mbovu ni sababu za kupungua nguvu za kiume. Kila mtu lazima ale mlo wenye matunda na mboga za majani, nafaka zisizokobolewa na za nyuzinyuzi na mafuta kidogo.
Kila mmoja ni dakari katika mwili wake. Vyakula vyetu vinatakiwa viwe dawa zetu siyo sumu.
Mlo bora huufanya mwili kuwa na afya nzuri na viungo vinavyohusika na tendo la ndoa.


Kula matunda mengi na mboga za majani, punguza nyama.

MTINDO MBAYA WA MAISHA

Maradhi si chochote zaidi ya mwili kuitikia kwa kitu ambacho tulichokifanya kibaya.

Siku hizi watu wanaishi katika mazingira ya kisasa sana. Lakini, kwa ujumla ni mazingira hatarishi sana juu ya afya zao.

Kwa nini “ugonjwa” wakati mwingine hushindwa kutibika? Kuna vipingamizi na vizuizi. Kushindwa kutazama vipingamizi vya matibabu, ni kipengele kikuu cha kutopona. Kupona siyo kazi rahisi. Matatizo hutoka katika vipengele vingi ambavyo unakuwa huvijui kabisa.


Kuishiwa nguvu hutokea sana kwa wanaume walevi na madawa ya kulevya, watu wanene zaidi (ambao wana mafuta ambayo hayafai kiafya) na watu wazee.


Wataalamu asilia wa elimusiha husema kwamba, sababu moja ya magonjwa yote ni kujaa sumu katika seli za tishu za mwili, mikondo ya damu na majimaji yaliyoletwa kwa kuisha kabisa kwa baki ya nishati ya neva kupitia mtindo mbaya wa maisha. Hali hii mtu kujitia sumu mwenyewe huelezewa kama kusumu damu (taxemia).


Hatua ya kwanza ya mtu yeyote katika programu yake ya kusafisha mwili ni kusafisha na kufungua viungo vinavyohusika na uondoaji taka mwilini.


Ini dhaifu na lililozongwa, kibofu cha mkojo, matumbo au figo zinaweza kusababisha matatizo mengi sugu ya kiafya kwa kusababisha sumu na uchafu uliooza kusharabiwa (kufyonzwa) katika mifumo mingine ya mwili. Kadiri muda unavyokwenda, hii itaathiri utendaji wa kazi wa kila seli na kiungo katika mwili; kwa sababu huingiza sumu katika damu, mifumo ya upumuaji, mfumo wa neva na ubongo, huku ikizuia moyo, mifumo ya mirija ya damu, na mapafu.


Kwa muda mrefu sababu kuu ya ugonjwa na maradhi ni kuendelea uchafu huu wa sumu kutunzwa na kusharabiwa tena.


Leo, mazingira yetu yamejaa sumu na vyakula tunavyokula, hata hewa tunayovuta na maji tunayokunywa vimesheni kemikali na kuingia katika mfumo wa mwili.


Ingawa kuondosha sumu huanza na mlo, programu za kuondoa sumu mwilini uimarishaji wa viungo vya lishe kwa ajili ya ini, mapafu, figo matumbo na damu ni muhimu. Kwa nini viungo hivi ni muhimu?


Ndivyo viungo vinavyohusika na uondoaji sumu za kemikali na sumu za mwili. Ini hutenda kazi kama chujio ya kuondoa vitu vilivyoingia na uchafu katika damu. Figo huchuja uchafu kutoka ndani ya damu na kuufanya kuwa mkojo, wakati mapafu huondoa gesi iliyokuwa mvuke pindi tunapopumua.


Kubadilisha tabia na mtindo wa maisha ni tiba ya kwanza katika kutatua tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.

Dumisha afya yako kwa ujumla, kwa sababu matatizo mengi ya kuishiwa nguvu za kiume ni kutokana na kupungua kwa mtiririko kutokana na kuzibwa kwa ateri, ni muhimu kudumisha mtindo mzuri hasa zaidi kuepuka mtindo ambao huongeza hatari ya kuongezeka kwa maradhi ya moyo.

KUTOFANYA MAZOEZI

Kwa kutembea, damu inayobeba oksijeni, virutubisho n.k, itabubujika katika sehemu mbalimbali za mwili ikiwa ni pamoja na kwenye uume wako.

Kutofanya mazoezi kama vile kukaa tu kila siku inaweza kusababisha kufunga choo, kuishiwa nguvu za kiume n.k.

Fanya mazoezi ya viungo walau mara 4-5 kwa wiki. Mazoezi huboeresha mzunguko wa damu na huongeza testosteroni na kukua kwa kiwango cha homoni, vyote hivyo huongeza nguvu za kiume.

Mazoezi ni muhimu sana. Tafiti moja ilionyesha kwamba wanaume wenye umri mkubwa ambao hukimbia maili 40 kwa wiki waliongeza viwango vyao vya testosterone kwa asilimia 25 kulinganishwa na wanaume ambao hawafanyi vizuri.

KUTOPATA USINGIZI WA KUTOSHA

Mwili wako unahitaji usingizi wa kutosha. Ukosefu wa usingizi ni moja ya chanzo cha kupata tatizo la kuishiwa nguvu za kiume. Jaribu kupata walau saa 7-9 za usingizi usiku ili kuongeza kiwango chako cha nguvu za kiume.

KUFANYA KAZI KUPITA KIASI

Siku hizi kulingana na hekaheka za maisha, watu wengi wamejikuta wakifanya kazi kupita kiasi, na hivyo kujidhuru kiafya ikiwa ni pamoja na kuishiwa nguvu za kiume. Kiasi ndiyo njia ya sawa. Jaribu kupumzika, sehemu nzuri zenye hewa nzuri na miti ya ukijani huleta afya nzuri na kuboresha mfumo wa neva.

MATIBABU

Ukiwa na Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume unaweza kunitafuta mimi nitaweza kukusaidia kunipata mimi bonyeza hapa. Mawasiliano

0 comments:

Post a Comment