Monday 24 November 2014

UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU



Kuna magonjwa mengine yakikupata hujui hata namna ya kujitibu. Lakini kwa kutumia vyakula na matunda unaweza ukashangaa namna ambavyo unaweza kuliondoa tatizo ambalo pengine ulidhani halina tiba.
Katika makala haya ya leo, nakuletea uwezo wa ajabu unaopatikana kwenye juisi ya kitunguu maji (Onion) kama tiba. Kuna maradhi mengi yanayoweza kutibika kirahisi kabisa kwa kunywa juisi ya kitunguu, vilevile kuna maradhi mengi unaweza kujikinga nayo kwa kunywa juisi hii.
Yapo magonjwa mengi yanayoweza kutibiwa kwa juisi ya kitunguu, lakini katika mfululizo wa makala haya ya leo, nawaletea machache yafuatayo:
TATIZO LA KUTOKA DAMU
Kuna ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa, tatizo ambalo huwapata watu wengi hasa wale ambao huwa na matatizo ya kukosa choo kwa muda mrefu kutokana na ulaji mbovu walionao. Lakini pia tatizo hili huweza kuwapata pia hata wale wanaokula vyakula sahihi lakini hukaa muda mwingi bila kufanya mazoezi.
Kwa kitaalamu ugonjwa huu hujulikana pia kama ‘Hemorrhoids’. Wako ambao husikia maumivu makali na wako ambao hawasikii maumivu ingawa hutokwa na damu.
Kwa utafiti na ushuhuda mbalimbali uliokwisha tolewa juu ya tatizo hili, mtu unaweza kupona kabisa tatizo hili iwapo utaliwahi, kwa kunywa juisi ya kitunguu kwa utaratibu maalum.
JINSI YA KUANDAA
Awali ya yote, hakikisha unapata kitunguu halisi kilichotokana na kilimo cha kawaida kabisa (Organic Faming). Natoa tahadhari hii kwa sababu siku hizi kuna vitunguu kutoka China, ambavyo ni vikubwa na vyeupe kuliko kawaida. Hivi ni feki, havina virutubisho asilia.
Chukua kitunguu kimoja, ondoa maganda ya juu kama unavyofanya wakati wa kuandaa kwenye mboga. Kama una ‘blender’ au ‘Juicer’, katakata na weka kwenye kifaa chako, weka maji robo kikombe na saga ili kupata juisi. Kama huna vifaa hivyo, usikonde, chukua kinu, changanya maji kidogo na twanga hadi kupata juisi.
Bila shaka juisi yako itakuwa ni mchanganyiko wa maji maji na vipande vya vitunguu vilivyosagika, usichuje bali kunywa hivyo hivyo kiasi cha glasi moja. Hakikisha unatengeneza juisi na kuinywa wakati huohuo, haitakiwi kuwekwa kwa muda mrefu kwani itapoteza ubora.
Inashauriwa kunywa juisi hiyo asubuhi kabla hujala kitu chochote na baada ya kunywa, unaruhusiwa kula mlo wako baada ya saa moja mpaka saa mbili. Kama huna nafasi ya kunywa wakati wa asubuhi, unaweza kutengeneza juisi hiyo usiku na kuinywa kabla ya kupanda kitandani kulala.

0 comments:

Post a Comment