Wednesday 26 November 2014

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI, INASABABISHWA NA NGONO NA MAMBO MENGINE YA FAHAMU HAPA






UTAFITI mpya wa kitabibu umebaini kuwa
saratani ya shingo ya kizazi, inasababishwa
pamoja na mambo mengine na ngono kama
ilivyo kwa ugonjwa wa Ukimwi, madaktari
bingwa wa magonjwa ya maradhi hayo
wamesema.

Madaktari bingwa wa
uchunguzi wa magonjwa katika Kitengo cha
Patholojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
na Madaktari Bingwa wa
Magonjwa ya Saratani katika Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road.

Madaktari hao wametaja mambo mengine
yanayoweza kusababisha saratani ya shingo
ya kizazi kuwa ni kujiingiza kwenye
mapenzi katika umri mdogo, kuolewa mara
nyingi, kuwa na wapenzi wengi, kusafisha
sehemu za siri kwa bidhaa zenye kemikali
na kuzaa mara nyingi.

Katika kiwango cha kimataifa, wastani wa
mwanamke kuzaa bila kuwa katika hatari ya
kupata ugonjwa wa saratani, ni watoto
wanne.

Madaktari hao walisema saratani ya
shingo ya
kizazi inatokana na aina 40 ya virusi, aina
mbili ikiwa ni virusi vinavyosambaa kwa njia
ya ngono
 “Human papilloma virus (HPV)
Squamos cell carcinoma kirusi namba 16 na
Adenocarcinoma namba 18, ni kati ya virusi
40 vinavyosababisha saratani ya kizazi na
vyenyewe vinachangia tatizo hilo kwa
asilimia 70.”
Wanasema saratani ya uzazi ndiyo inayoongoza
ikilinganishwa na nyingine nchini na
asilimia 80 ya wagonjwa, wameambukizwa
kwa ngono.
“Saratani hiyo husambaa kwa ngono kutoka
mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine.
Mwanamke mwenye saratani ya kizazi
akifanya ngono, mwanamume huchukua
virusi na kumwambukiza mwingine
atakayefanya naye ngono,” alisema na
kuongeza:

“Wagonjwa wengi na wale ambao tayari
wana maambukizi, wamekuwa wakikutwa
na virusi hawa wa aina mbili ambao
wamekuwa wakienezwa zaidi kwa njia ya
zinaa. Inawezekana mwanamume akawa
ametoa kirusi kwa mwanamke mmoja
kwenda kwa mwingine.”

“Hata hivyo, kuna wanaume ambao tayari
wameshakuwa na maambukizi ya HPV
wanatembea na virusi, hawa tunawaita
(high risk sexual male patner) wanaume
hawa utakuta kila akioa mke anakufa kwa
saratani ya shingo ya uzazi, lakini kamwe
virusi hao hawawezi kumwathiri yeye.”

Kuanza ngono mapema nako
kunachangia kwa kiasi kikubwa
maambukizi ya saratani hiyo, kwani binti
anakuwa katika hatari zaidi ya kupata
maambukizi mapema na hivyo kuweza
kumwathiri mapema zaidi, tofauti na yule
aliyeanza baadaye.

“Idadi kubwa ya wanawake wamekutwa na
saratani mapema sana, ukilinganisha na
umri wao, lakini wengi wao wamekuwa
wakikutwa na ugonjwa huu kuanzia umri
wa miaka 35 kwenda juu. Hii inamaanisha
kuwa walipata maambukizi hayo
walipokuwa na miaka 20-25.”

Licha ya hivyo
mgonjwa anaweza asitambue tatizo hilo
mpaka miaka 10 hadi 15 baadaye ambapo
tatizo linajitokeza hadharani.
“Unapopata maambukizi ya HPV
inakuchukua muda mpaka kujulikana, kwa
kawaida mwanamke anaishi miaka 10 hadi
15 na baadaye anagundulika na tatizo hili,
lakini itategemea na kushuka kwa kinga
zake.

Kama ikitokea hapo katikati ukajitokeza
ugonjwa mwingine kama HIV basi saratani
nayo itajitokeza.”
Utafiti walioufanywa Septemba
2011 kuhusu tatizo la HIV na saratani ya
shingo ya uzazi unaonyesha kuwa idadi
kubwa ya wanawake waliokuwa na
maambukizi ya HIV na CD4 ziliposhuka tu,
saratani ya kizazi nayo iliibuka, hiyo
inamaanisha kuwa tatizo hilo ni kubwa
tofauti na linavyodhaniwa.
Kwa upande wake virusi
vya HPV huambukizwa kwa mwanamke
moja hadi mwingine, pale mwanamume
anapofanya tendo hilo na mwanamke
mwenye maambukizi na kwenda kufanya
tendo hilo na mwanamke mwingine.
Kinga
Madaktari hao wameeleza kinga ya maradhi
hayo kuwa ni pamoja na matumizi ya
kondomu na uaminifu wa wapenzi katika
uhusiano wao.

Ninatoa wito kwa
Watanzania na jamii kiujumla
kujijengea tabia ya kupima
mara kwa mara ili kubaini maambukizi
mapema.
Ongezeko la watu wanaougua
saratani ya shingo ya uzazi imetokana na
ongezeko kubwa la watu, ikiwa ni pamoja
na tabia ya kuchangia ngono kwa wapenzi.

Alisema chanjo ya saratani ya shingo ya
uzazi inayotarajiwa kuanza kutolewa kwa
mabinti wa miaka tisa mpaka 12 baadaye,
 Ni moja ya juhudi ya Serikali
katika kupambana na ugonjwa huo.

0 comments:

Post a Comment