Saturday 27 September 2014

WANAWAKE WANAVYO-SHAMBULIWA NA U.T.I - 2


Leo tunaendelea kueleza dalili za UTI na tiba yake pia tutatoa ushauri.
DALILI
Unaweza kugundua kuwa una UTI kwa kuona dalili zifuatazo. Kujisikia maumivu au mkojo unachoma wakati wa kukojoa, kujisikia kukojoakojoa mara kwa mara na ukienda haja ndogo mkojo hautoki au unatoka kidogo sana.
Dalili nyingine ni mkojo kuwa na rangi ya mawingu au mweusi na kuwa unatoa harufu mbaya, kujisikia maumivu chini ya kitovu au maumivu yanayozunguka kiuno.
Wakati mwingine UTI huleta homa kali na mgonjwa kutetemeka na akipima anakutwa hana malaria. Muathirika huchoka na kujisikia kichefuchefu na kutapika.
TIBA NA USHAURI
Matibabu yake hufanyika hospitalini na daktari na siyo katika duka la dawa, hivyo ni vema kuwaona wataalamu hao wa tiba ambao watatoa dawa za antibayotiki zinazoua bakteri, ugonjwa ukiwa ‘umekomaa’ mwilini hali ambayo kitaalam kuitwa kidney infection au pyelonephritis.
Kuna wengine wana UTI lakini pia wana fangasi, hivyo tiba maalum ya kuua fangasi (specific antifungal or antiparasitic medications) itahitajika kwa mgonjwa huyo.      
Wagonjwa wa kisukari na wajawazito ni vizuri wakapima UTI mara kwa mara kwani wanaweza kuwa na ugonjwa huo na wasijielewe ikiwa hawatapimwa maabara.
Mtu  mwenye dalili hizo hapo juu aende hospitali na kumuona daktari ambaye atampima  mkojo ili aweze kujua aina ya bakteria waliomshambulia na akigundua atampa dawa stahiki.

0 comments:

Post a Comment