Saturday, 27 September 2014

MAGONJWA NYEMELEZI KWA WANAWAKE- 6



Ugonjwa huu huanza ghafla na dalili zake ni kama homa kali, kikohozi, maumivu wakati wa kupumua, baridi na kutetemeka.
Ugonjwa wa Ngozi:
Huu husababishwa na vimelea vya Staphylococcus aureus.Vimelea hivi huishi katika mwili wa binadamu (kwenye ngozi ya kichwa na kinena (groins) na kwapani) bila madhara.Pia hupatikana kooni na katika utumbo mpana na mkojo.
Vimelea vya Staphylococcus husambaa kwenda sehemu nyingine ya mwili kutoka kwenye usaha, mgusano na ngozi ya mwenye maradhi, kutumia taulo, matandiko,vifaa vya mtu aliyeathirika n.k
Dalili zake ni pamoja na chunusi, majipu, kubabuka kwa ngozi na magamba magamba katika ngozi.
Yapo pia magonjwa yatokanayo na Protozoa ambayo mojawapo ni Toksoplasmosisi ya Ubongo na hujulikana kama Cerebral toxoplasmosis.
Cerebral toxoplasmosis:
 Ugonjwa hutokana na kuamshwa kwa ugonjwa wa awali kutokana na vimelea vya Toxoplasma gondii.
Kitaalamu kimelea hiki huishi ndani ya seli na huathiri ndege,wanyama na lakini pia na binadamu na ndiyo maana huugua.
Kimelea hiki kinaathiri mfumo mzima wa fahamu,hupatikana kwenye nyama isiyopikwa vizuri na kinyesi cha paka.Huathiri zaidi ubongo na kusababisha maumivu ya kichwa ,kuchanganyikiwa, udhaifu wa viungo, homa, kupoteza fahamu, kupooza na kifafa.
Itaendelea 

0 comments:

Post a Comment