Tuesday, 17 June 2014

TAMBUA AINA TOFAUTI ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI CHA MWANAMKE





KATIKA makala haya nitachambua  aina tofauti za uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke, dalili zake, vyanzo, athari na jinsi ya kujitibu kiasili na pia jinsi ya kuishi ili kuepuka tatizo hili ambalo mara nyingi husababisha ugumba kama mwanamke hatopata tiba sahihi na kwa wakati mwafaka.
Si jambo  la kushangaza kumsikia mwanamke akisema hajafanikiwa kushika ujauzito katika maisha yake ya ndoa/uhusiano kwa sababu ana uvimbe kwenye kizazi na wakati huohuo ukimuuliza ana uvimbe wa aina gani na upo sehemu gani ya kizazi chake anakujibu hajui.
Aina za vimbe kwenye kizazi cha mwanamke kwa ufupi
- Fibroid. Huu ni uvimbe unaotokea kwenye mji wa mimba ambao kitaalamu unaitwa Uterus. Watu wengine huuita mji wa mimba kwa jina la fuko la uzazi, yaani sehemu ambayo mimba hutunga/hujishikiza na kukua.

- Ovarian Cyst. Huu ni uvimbe ambao hutokea kwenye kifuko cha mayai ya uzazi. Inaweza kuwa kwenye kifuko kimoja au kwenye vifuko vyote viwili.

- Polycystic Ovarian Syndrome (PCOS). Hili ni tatizo la kuwa na vijivimbe vidogovidogo vingi vikiwa vimezunguka vifuko vya mayai ya uzazi. Kwa jina jingine la kitaalamu huitwa Stain livingthal syndrome.

- Salpingitis. Hili ni tatizo la kuvimba kwa mirija ya uzazi au kuvimba kwa kuta za mirija ya uzazi

- Ovaritis. Hii ni tofauti na namba mbili hapo juu. Hili ni tatizo la kuvimba kwa kifiko chote cha mayai ya uzazi. Inaweza kuwa kifuko kimoja au vyote viwili.

Dalili za mwanamke kuwa na aina hii ya uvimbe yaani Fibroid (s).
Kupata hedhi isiyo na kikomo na nzito kupita kiasi ikiambatana na mabonge yanayofanana na maini.

Hali hii husababisha tatizo la upungufu wa damu  (anaemia/low blood count) na hivyo mgonjwa hupatwa na uchovu kupita kiasi, kizunguzungu na maumivu ya kichwa. Mgonjwa mwenye dalili hii anatakiwa kumwona daktari bila kuchelewa.
Maumivu chini ya kitovu kwa katikati Hii ni dalili kwamba uvimbe huu umekuwa mkubwa tayari na mgonjwa hushindwa kulala kifudifudi au kuinama  chini.
Utokwaji wa uchafu ukeni. Mara nyingi uchafu huu unakuwa na rangi ya kahawia/brown na si ile ya kama maziwa mtindi. Uchafu huu mara nyingi unaambatana na harufu kali na mbaya inayoudhi. Uchafu huu huongezeka na pia harufu huongezeka wakati wa kushiriki tendo la ndoa.

Ushauri muhimu
Mwanamke ambaye kafanyiwa vipimo na daktari akajibiwa kwamba ana uvimbe kwenye kizazi ni vizuri adadisi ni aina gani ya uvimbe na upo sehemu ipi kwenye kizazi chake.


0 comments:

Post a Comment