Utafiti wa watoto 625,000 uliochapishwa kwenye jarida JAMA pediatrics nchini Marekani umebaini kwamba watoto ambao mama zao walitumia madawa ya kuongeza uchungu/kusaidia uzazi wakati wa kujifungua wako hatarini kupata ugonjwa wa upungufu wa akili ambao kwa kitaalamu unajulikana kama Autism.
Utafiti huo uliofanyika kwenye jimbo la Carolina kaskazini umeonyesha kwamba watoto wa kiume13 kwa kila watoto 1,000, na watoto wa kike wanne kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa na wamama wanaotumia madawa ya kuongeza uchungu/kusaidia uzazi wakati wa kujifungua, hupata ugonjwa wa Autism.
Utafiti huo pia umeonyesha kiwango cha kupata Autism (Rate) kwa watoto wa kiume ambao mama zao hutumia dawa hizo za kusaidia uzazi ni kukubwa mara tatu zaidi ya watoto wa kike.
Hata hivyo watafiti wa utafiti huu wamesema kwamba kesi (case) za Autism kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa zinaweza kuepukika iwapo wazazi wao wataacha kutumia madawa ya kuongeza uchungu/kusaidia uzazi. Lakini pia wameonya kwamba kwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha gharama kubwa kwa kuwa madawa hayo husaidia katika uzazi salama ambao huokoa maisha ya mama na mtoto.
Utafiti huo umekosolewa vikali na wanasayansi wengi kwa kuwa madawa ya kuongeza uchungu wakati wa kujifungua yanaokoa maisha ya mama na mtoto na iwapo madawa hayo hayatatumika basi kuna uwezekano wa kumpoteza mama au mtoto au wote wawili na hivyo kuomba tafiti zaidi ziendelee kuchunguza sababu hasa za Autism.
Watoto wenye autism huonesha dalili za kutokuwa na tabia za kujichanganya na watoto wengine, kutokuwa na mawasiliano ya njia za maneno na vitendo, kuwa na tabia zinazojirudiarudia n.k. Autism imekuwa ikiaminika kusababisha na mwingiliano wa kifamilia, matatizo ya kurithi (genetic risks) na matatizo yanayojitokeza kwa mama wakati wa ujauzito au matatizo yanayojitokeza wakati mtoto anapokua.
0 comments:
Post a Comment