Saturday 3 May 2014

UJUE UGONJWA WA DENGUE





SIKU chache zilizopita Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii nchini ilitoa taarifa
kuhusu kuwapo ugonjwa wa homa ya
dengue.

Hadi asubuhi ya Jumanne iliyopita
mpaka sasa wagonjwa wapatao 37
walikuwapo nchini Tanzania
walioripotiwa kuwa na ugonjwa huo
unaosababishwa na kirusi kiitwacho
dengue. Kirusi hicho kinaenezwa na
mbu aina ya aedes (adesi), jamii ya mbu
huyu ndiye pia hueneza ugonjwa wa
homa ya manjano.

Asili ya jina Dengue Kwa mujibu wa
taarifa rasmi kutoka kwenye mitandao,
jina ‘dengue’ halijafahamika rasmi
limepatikanaje, ila watafiti wanabainisha
kuwa limetokana na moja ya neno la

lahaja za Kiswahili liitwalo Ka-dinga
pepo, linaloelezea ugonjwa
unaosababishwa na pepo mbaya.
Neno dinga ni la Kiswahili ambalo asili
yake inatoka Hispania na hutamkwa

‘dengue’, ambalo linamaanisha maumivu
ya mtu anayeumwa na mifupa na kupata
homa kali. Hata hivyo, jina dengue
lilianza kutumika rasmi kwa ugonjwa
huo tangu 1828 hadi leo.

Wakati ugonjwa huo ukiripotiwa nchini,
taarifa za afya duniani zinasema kuwa
kila mwaka katika nchi mbalimbali
duniani watu wanaokadiriwa kufika
milioni 100 wanaugua ugonjwa huo na
hatari ya ugonjwa huo iko kwenye nchi
zenye hali ya hewa ya kitropiki.
Sababu za ugonjwa huu
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya na
taarifa mbalimbali za afya, ugonjwa huo
unaenezwa na mbu huyo (aedes) jike
ambaye huwa na virusi vya ugonjwa
huo na huvieneza kwa binadamu kwa
kumuuma.
Dalili za ugonjwa huo
Dalili za ugonjwa huu kwa mujibu wa
wa watalaamu wa afya ni
pamoja na
· homa ya ghafla,
· mwili kuchoka,
· kuumwa na viungo,
· kuvimba
tezi na kupatwa na harara.
· Lakini dalili kubwa ya ugonjwa huo ni mtu kuwa na
homa kali,
· harara na kuumwa kichwa na
kwamba dalili hizo huanza kujitokeza
kati siku ya tatu hadi ya 14,
· tangu kuumwa na mbu huyo.

Hata hivyo, anasema kawaida dalili hizo
hujitokeza kuanzia siku ya nne hadi ya
saba na kwamba wakati mwingine dalili
za ugonjwa huo huweza kufanana
kabisa na dalili za ugonjwa wa malaria,
hivyo wananchi wanashauriwa
kuchukua tahadhari kwa kwenda vituo
vya afya kufanya uchunguzi.
Pia Wananchi wenye
dalili hizo wakienda hospitali kufanyiwa
uchunguzi wa vipimo kama vya malaria,
majibu huwa hasi, hivyo mgonjwa

hudhani labda ni uchovu tu, lakini
huenda hizo ni dalili za ugonjwa wa
dengue.
Ugonjwa huo umethibitishwa
baada ya sampuli zilizochukuliwa kutoka
kwa wagonjwa waliohisiwa kuwa na
ugonjwa huo kepelekwa kwenye
maabara.

Sampuli hizo zilipelekwa kwenye
maabara ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dar es
Salaam na kuthibitisha kuwa na virusi
vya dengue Juni 9, mwaka 2010. Hata
hivyo, hadi sasa idadi ya wagonjwa
ambao wameripotiwa kuwa na dalili za
ugonjwa huu ni 37, na hakuna
mgonjwa aliyepoteza maisha.

Kati ya wagonjwa hao wagonjwa 24,
wamethibitishwa kuwa na virusi vya
dengue, watatu kati yao ni Watanzania
na wengine ni raia kutoka nje.
Aina za ugonjwa huo
zipo aina au hatua
kuu tatu za ugonjwa huo.
Aina ya
kwanza ni homa inayotokana na
ugonjwa huo, inayoambatana na dalili
tatu kubwa ambazo ni
· homa kali ya
ghafla,
· mwili kuwa na harara na
· kuumwa kichwa.

Aina ya pili inajulikana kitaalamu kama;
Dengue Hemorrhagic Fever .
Hiyo ni aina
ya homa ambayo huwa imeambatana na
dalili za magonjwa ya kutokwa na damu
kwenye fizi au puani na pia kutokwa na
damu chini ya ngozi.
Ikiwa mgonjwa huyo ataumia
sehemu yoyote ni rahisi kwake kupoteza
damu nyingi kupitia kwenye michubuko.
Aina ya tatu ya ugonjwa huo huitwa
Dengue Shock Syndrome ambapo
mgonjwa hupata homa inayoambatana
na kupoteza damu nyingi ambayo
hupelekea kupata mshtuko na mgonjwa
anaweza kupoteza fahamu.
Aina ya pili na tatu
ya ugonjwa huo ndizo zenye dalili
mbaya ambazo zinaweza kuhatarisha
maisha ya mgonjwa na hatimaye
kusababisha kifo na kwamba kwa hapa
nchini hadi sasa wagonjwa
waliogundulika wote wana dalili ya
kwanza ya ugonjwa huo.
Maeneo ya maambukizi
Mbu Aedes hupendelea kuzaliana
kwenye maji yaliyotuama karibu na
makazi ya watu au hata ndani ya
nyumba. Inasadikiwa kuwa viwavi wa
mbu hawa huweza kuishi katika
mazingara ya ndani ya nyumba mpaka
mbu kamili akomae na kuanza
kusambaza ugonjwa huo kwa
binadamu kwa njia ya kuuma na
kunyonya damu.
Mbu huyu mwenye kawaida ya kuwa na
mistari myeupe na myeusi mara nyingi
huuma nyakati za machweo, mawio na
hata mchana, hasa kunapokuwa na
mawingu.

Hata hivyo, Ugonjwa wa Dengue
hauambukizwi kutoka binadamu mmoja
kwenda mwingine,
bali huambukizwa
kwa kuumwa na mbu huyo.
Je,ugonjwa huu unatibika?
Homa ya
Dengue haina tiba bado, bali mgonjwa
hutibiwa dalili alizonazo kwa haraka,
Iwe kuhara,
· maumivu ya kichwa au
maumivu ya viungo.
· Dalili nyingine ni
pamoja na homa,
kupungukiwa maji au

damu na kwamba hadi sasa hakuna pia
chanjo kama kinga kwa binadamu.
Jinsi ya kujikinga ya ugonjwa huo
Pamoja
na kwamba hakuna chanjo wala tiba
maalumu ya ugonjwa huo, lakini
wananchi wanaweza kujikinga wasipate
ugonjwa huo kwa kuangamiza mazalia
ya mbu. Wananchi wanashauriwa kuwa
ni vyema wakafukia madimbwi ya maji
yaliyotuama au kunyunyuzia dawa ya
kuua vimelea vya mbu kwenye
madimbwi hayo.

Kadhalika kuondoa vitu vyote
vinavyoweza kuweka mazalia ya mbu
kama vile vifuu vya nazi makopo na
mrundikano wa taka. Aidha wananchi
wanashauriwa kuwa maeneo yao ya
makazi yawe safi na kwamba kama
kuna majani ni vyema wakafyeka
vichaka vilivyo karibu na makazi na
kufunika mashimo ya maji taka kwa
mifuniko imara.
Pia kutumia dawa ya kufukuza mbu
“mosquito repellants”, kuvaa nguo
ndefu wakati ukiwa nje kwenye

mazingira ya mbu, kutumia chandarua
vilivyowekwa dawa na pia kuweka wavu
wa kuzuia mbu kwenye milango na
madirisha ya nyumba.
Hata hivyo,

Wizara ya Afya imeshachukua
hatua kwa kutoa taarifa za kuwepo na
ugonjwa huo kwenye mikoa mbalimbali
nchini ikiwemo Dar es Salaam na
Zanzibar.

“Wananchi wachukue tahadhari kwani
ugonjwa huu unaweza kusambaa mikoa
mingi ya nchi, kwa kuwa kuna
muingiliano mkubwa wa watu
wanaongia jijini Dar es Salaam na
kutoka,”
wizara inaendelea
kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa
ugonjwa huu katika Mkoa wa Dar es
Salaam na Zanzibar na kutoa mafunzo
kwa watumishi wa afya ili kutambua na
kutibu ugonjwa huo kwa wananchi
wanaojitokeza kuwa na maambukizi ya
ugonjwa huo.
Aidha wizara imeendelea
kuimarisha utambuzi wa ugonjwa
katika maabara ya NIMR na pia
imepatiwa msaada na vitendanishi
(Primers na Probes) ili kuweza
kuthibitisha ugonjwa huu kwa
wagonjwa wenye dalili hizo.
Kwingineko duniani
Nchini Kenya ugonjwa huo pia
umeripotiwa kutokea ambapo zaidi ya
watu wanane wamelazwa kwenye
hospitali moja jijini Mombasa wakiwa na
dalili za homa ya dengue. Vyombo vya
habari nchini humo vimeripoti.
Shirika la Afya la Umoja wa
Mataifa (WHO) homa ya dengue
inasababishwa na mbu wa kike, Aedes
mosquito ambapo mgonjwa anaonesha
kati ya dalili nne zifuatazo.
Historia ya dengue
Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya
Duniani (WHO) ugonjwa huo
uligunduliwa kwa mara ya kwanza
nchini China kipindi za miaka (265- 420
AD), ambapo ugonjwa huo ulihusishwa
na kuambukizwa na mdudu anayeruka.

Hata hivyo, ugonjwa huo uliendelea
kusambaa duniani kote na barani Afrika
iliingia karne ya 15 hadi 19 na mwaka
1779 hadi 1780 ugonjwa huo
ulisambaa barani Asia, Afrika na Amerika
ya Kaskazini na hivi leo nchi na mabara
mengi ugonjwa huo umeingia na kuleta
athari kwa wagonjwa

0 comments:

Post a Comment