Thursday 1 May 2014

UFUMBUZI WA TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI UNAPOJAMIIANA / PRE MATURE EJACULATION






Mwanaume kuwahi kumaliza
anapofanya tendo la kujamiiana
Kutoka mbegu za kiume muda mfupi
baada ya kumwingilia mwanamke
huitwa premature ejaculation. 

Huu ni
udhaifu wa kawaida kwa wanaume
walio wengi kwa ujumla wake, ikiwa
ni pamoja na vijana. Mtaalamu aitwaye Ira
Sharlip anasema katika utafiti wake
kuwa, ni kiasi cha asilimia 20 hadi 30
ya wanaume wa rika zote ambao
wana matatizo haya.

Njia za kitabibu za kuweza
kumtambua mtu mwenye udhaifu
huu inaitwa Intravaginal ejaculatory
latency time (IELT). Hata hivyo,
mtaalamu Ira Sharlip anaongeza kwa
kusema kwamba, utaratibu huu
hausaidii sana kumjua mtu mwenye
premature ejaculation.
Kuna
wanaume ambao wanamaliza katika
dakika moja tu baada ya kumwingilia
mwanamke na wao hudai kwamba,
hawana matatizo.
Na halafu upande mwingine, kuna
wanaume ambao wanaweza
kuchukua dakika 20 bila kutoa
mbegu baada ya kumwingilia
mwanamke. Hawa nao ni wagonjwa,
kwani muda huo ni mkubwa kuliko
wastani. Kwa maana nyingine ni
kwamba, maana ya neno premature,
zaidi zaidi liko katika mtazamo wa
mhusika mwenyewe. Inategemea na
mtu mwenyewe anavyotosheka
kimapenzi na uwezo wake wa
kujidhibiti muda wa kumaliza
unapokuwa umewadia.

Utafiti wa mwaka 2010 katika jarida
la Journal of Sexual Medicine uliona
kwamba, kipimo kizuri cha
premature ejaculation ni dakika 5.4.
Yaani mtu akitoa mbegu baada ya
dakika pungufu ya hizo, tangu
amwingilie mwanamke basi ana
ugonjwa huu wa premature
ejaculation.

Lakini Ian Kerner anasema kipimo ni
dakika mbili. Yaani mwanaume
akimaliza haja yake kabla ya dakika
mbili, basi ana ugonjwa huo.
Anaongeza kwamba, watu wengi
anaokabiliana nao ni wale ambao
wanatumia muda mfupi chini ya
dakika mbili kumaliza haja zao.

Wengine hutumia sekunde 30 tu!
Pia hata sababu za nje zinaweza
kuchangia kumfanya mwanaume
akawa na tatizo hili. Mtu mwenye
mawazo mengi ni rahisi kukumbwa
na tatizo hili. Mtu mwenye mawazo
mengi anamaliza haraka mara baada
ya kumwingilia mwanamke, kwa
mujibu wa mtaalamu Kerner.

Lakini kumaliza kwa namna hii pia
kuna uzuri wake kwamba, tumejaza
dunia kwa kuwa na watu wengi.
Kama watu wangekuwa
wanachukua saa nzima kumaliza
baada ya kumwingilia mwanamke,
dunia ingekuwa na uadimu wa
watu!

Washauri nasaha wanaojihusisha na
ushauri wa kimapenzi na matibabu
wanatoa tiba mbalimbali kwa ajili ya
watu wenye wasiwasi; wasiwasi
ambao huwafanya wawe
wanamaliza haraka sana baada ya
kumwingilia mwanamke.

Kuna dawa ambayo mgonjwa
akipewa zinamsaidia kurefusha
muda wa kuendelea na tendo, baada
ya kumwingilia mwanamke. Dawa
hizo ni kama zile za kupooza
msongo wa mawazo.
Pia kuna
mazoezi ambayo yanashauriwa
kufanywa. Mazoezi haya humsaidia
mtu kujenga upya mkabala wa
namna anavyochukulia tendo.

Lakini pia njia iliyo rahisi zaidi ili
kutokuwa mwepesi wa kumaliza
haraka ni kujizoeza kuacha kulifikiria
tendo hilo la ngono unapokaribia
kufikia kileleni (kwa kufanya pole
pole zaidi au kufikiria mambo
mengine ya nje kama ya mpira,
mfano Yanga na Simba au
Manchester na Chelsea).
Jenga
mazoea kufanya namna hiyo.
Ukizoea itakuwa ni kama kitu cha
kawaida kwa kujikaza kisabuni na
kuhakikisha unamsubiri mwenzio ili
mwende pamoja kileleni.

Kila kitu ni kujifunza. Ukijizoeza
kujikakamua bila kumaliza hata
katika hali ya hamu ya juu kwa
kumsubiri mpenzi wako, tatizo la
premature ejaculation litakuwa
limethibitiwa.

0 comments:

Post a Comment