Thursday 1 May 2014

UFUMBUZI WA KISAIKOLOJIA WA TATIZO LA UGUMBA.



Ni ukweli usiopingika kuwa ndoa
nyingi zimepoteza furaha kutokana na
watoto kukoseka miongoni mwa
wanandoa. Wanawake na wanaume
wamejikuta wakiangukia katika
mikono ya matapeli wanaojiita
waganga na kufanyiwa mambo mengi
ya ajabu, ikiwa ni pamoja na  kufanya
mapenzi na mizuka au na watu ambao
hawakuwatarajia ili tu waweze kupata
watoto.

Hakuna ubaya wa kutafuta tiba ya
ugonjwa endapo upo, lakini kutafuta
tiba ya ugonjwa ambao haupo ni
kuchosha mwili na matokeo yake huwa
ni mabaya zaidi. Uchunguzi uliohusisha
matatibu kutoka hospitali na vituo vingi
vya afya unaonesha kuwa wagumba
wengi wanaosaka tiba hospitalini
wamebainika kutokuwa na matatizo ya
kibaiolojia.
Ninaposema kibaiolojia nina
maana kwamba wanandoa wengi
wagumba wamekutwa wakiwa na uhai
katika viungo vyao vya uzazi.
Katika ulimwengu wa leo idadi ya watu
wanaokosa watoto bila kuwa na
sababu ya msingi inatajwa kuwa ni
kubwa na kila siku wasichana na
wavulana wanaingia katika chumba
hiki cha huzuni isiyojulikana chanzo
chake. Kukosa uzazi bila sababu ni
tatizo ambalo limekuwa likizisumbua
akili za wahitaji watoto wengi na
mwisho kuwagotesha katika mawazo
ya kurogwa na sababu kubwa ikiwa ni
kutojulikana kwa chanzo cha wazi cha
kutokuzaa kwao.

Ukweli pekee ambao nimekusudia
kuuzungumza leo kuhusiana na
wasiokuwa na matatizo ya uzazi
kutokuzaa ni ule ambao
umeshawekewa misingi na watafiti
walioandika taarifa yao katika jarida la
Minerva Ginecologica la nchini Italia
kwamba uchovu unaoletwa na mawazo
ndiyo unaochangia kwa kiasi kikubwa
watu wasipate watoto licha ya kwamba
kibaiolojia hawana matatizo.

Tafiti za hivi karibuni zimebaini kuwa,
wanawake wengi wenye viungo
salama lakini hawazai, wana kiasi
kikubwa cha homoni ya Cortisol
inayoletwa na uchovu. Kwa mujibu wa
utafiti huo aina hii ya homoni ndiyo
inayosimamisha mchakato wa
uzalishaji mayai kwa wanawake
wakimbia riadha. Hivyo basi uwiano
huu wa kasoro za ukuzaji mayai kati ya
wakimbia riadha na wanawake
wagumba unaweka usawa baina ya
uchovu mkubwa wa mazoezi ya viungo
na ule uchovu unaotokana na msongo
wa mawazo ya ugumba.

Uchovu wa kihisia huweza kumfanya
mwanaume au mwanake asiweze
kuzaa kabisa katika maisha yake. Hii ina
maana kuwa watu wanaotingwa zaidi
na mawazo ya kukosa fedha, migogoro
katika ndoa zao na kujaribu mara
kadhaa kupata watoto bila mafanikio
wana uwezekano mkubwa wa
kutokuzaa hata kama maumbile yao
yataonekana kitabibu hayana kasoro.
Imebainika kuwa watu wengi
hujisogeza wenyewe katika nguvu ya
kukosa mtoto kutokana na ukubwa wa
kiu yao ya kupata mtoto, huku
wakilazimisha kimawazo mchakato wa
kubeba au kubebesha mimba kwa
wakati ulipangwa na malengo yao.

Mkazo huu wa mawazo huwakumba
hasa wanandoa na wapenzi ambao
wanatamaa ya kupita kiasi ya kupata
mtoto katika uhusiano wao. Hawa
hujiweka katika uzalishaji mkubwa wa
homoni ya Cortisol ambayo huchipuka
kwa kasi kutokana na msukumo wa kiu
kubwa na ya haraka ya kukumbatia
mwana.

Kutokana na ukubwa wa tatizo hili la
msongo wa mawazo, imebainika kuwa
wagumba wengi wasiokuwa na kasoro
katika viungo vya uzazi wanaweza
kupona au kupata watoto bila hata
kupewa tiba ya miti shamba au
vidonge.
Tiba yake kubwa
iliyobainishwa ni kupatiwa nasaha
zitakazowaondolea mawazo tasa,
wasiwasi na kutojiamini.
Ukweli wa tiba hii ya ushauri
imethibitishwa hivi karibuni na kituo
kimoja nchini Marekani
kinachojishughulisha na utafiti wa
kuzalisha watoto, ambapo majibu yake
yalichapishwa katika majarida na
mitandao mbalimbali.
Kwa mujibu wa
taarifa ya kituo hicho asilimia 75 ya
wanawake waliokosa watoto ambao
walifika kituoni hapo na kupewa
ushauri walifanikiwa kuzaa baada tu ya
kuhudhuria kliniki na kupewa ushauri
uliowatoa katika msongo wa mawazo.
Nasaha ambazo zimekuwa zikitolewa
na wataalamu hao si ngumu, bali ni zile
zilizojaa maneno yenye kugeuza fikra
hasi zenye kuondoa kiu kali ya kupata
watoto kwa utashi na nyakati
zilizopangwa na wahusika.
 Pia
wagumba hufundishwa namna ya
kuepuka migogoro ya kimapenzi na
kutoumizwa kupita kiasi na kejeli za
watu kuhusiana na kutozaa kwao,
huku wakijengewa imani kuwa kuzaa
ni suala linalowezekana kwao, hivyo
kuwafanya watupilie mbali hofu na
mawazo kuwa wao ni wagumba.

Lakini pamoja na nchi zilizoendelea
kuwa na vituo vya kutolea nasaha kwa
waathirika, bado wanasaikolojia
wanakiri kwamba mtu mwenyewe
anaweza kujiepusha na uchovu
unaoletwa na mawazo kwa kurahisisha
tatizo lake kutoka kutowezekana na
kuwa linawezekana kutatuliwa.
Akili ya
mtu ndiyo inayopima na kuongoza
utambubuzi wa ukubwa wa tatizo na si
kwamba kuna matatizo makubwa na
madogo kama watu wanavyofikiria.
Kwa maana hiyo ili mtu ambaye
amejiwekea ukuta wa kutozaa kwa
msongo wa mawazo yake kama
nilivyosema aweze kuzaa lazima
aondoe mawazo ya kwamba yeye ni
mtu asiye zaa,  kwani hakuna mtu wala
vipimo vilivyompa majibu ya kwamba ni
mgumba. Jambo jingine la kufanya ni
kupuuza maneno ya kukatisha tamaa
toka kwa watu wengine.
Hii ina maana
kuwa lawama zozote toka kwa mume/
mke au wanafamili zinazohukumu kosa
la mtu kutokuza lazima zipuuzwe na
zisipewe nafasi ya kutia simanzi
moyoni.
Sambamba na hilo kuna suala la
wanawake kuzingatia kalenda zao kwa
kujichunguza na kubaini muda
muafaka wa kukutana kimwili na
mwanaume ili kupata matokeo mazuri
ya utungishaji mimba.
Kwa mantiki hii
kuna wanandoa wengi wameshindwa
kupata mtoto kwa kutozingatia siku
zenye uwezekano wa kupata mimba
ambazi ni siku ya 11 hadi ya 16 tangu
siku ya kumaliza hedhi.
Lakini kwa kuwa kuna suala la utumiaji
wa dawa za uzazi wa mpango ni budi
wahusiaka kusimamisha matumizi yake
pindi mtoto anapohitajika ndani ya
ndoa. Hata hivyo kuna umuhimu wa
kutumia mitindo ya kuvuta kizazi
nyakati za kufanya mapenzi, ili kuzipa
msukumo wa haraka mbegu kunasa
kwenye mfuko wa uzazi.

Sambamba na hilo wanaume
wanatakiwa kuepuka ufanyaji holela
wa mapezni ili kuzifanya mbegu
zikomae na wakati wa tendo kuvuta
hisia kali ili kuongeza msukumo wa
manii kutoka kwenye uume kwenda
kwenye uke. Na jambo la mwisho
katika mchakato wa kupata mtoto ni
lishe bora miongoni mwa wanandoa.

Lazima miili iwe na nguvu za kutosha
kusimamia uzalishaji wa mbegu bora.
Inashauriwa wanaume waepukane na
uvaaji wa nguo za ndani za kubana
ambazo zinatajwa kuongeza joto
kwenye kiwanda cha kuzalisha mbengu
na hivyo kuzidhoofisha.

1 comments:

  1. Kutana na dr mitishamba kanyas anatibu ugumba uzazi nguvu za kiume kukuza uume na kunenepesha uume kukuza hips shape na makalio kwa mvunge. .anatibu matatizo ya hedhi. .pumu ..figo..kisukari. .ini..uti sugu..mpigie dr kupitia 0744903557 tanga..pia anatibu uchawi zindiko. .

    ReplyDelete