Thursday 1 May 2014

TATIZO LA HARUFU MBAYA MDOMO NA JINSI YA KUEPUKANA NALO.


Harufu mbaya  mdomoni inachagizwa na
mambo kadhaa ikiwamo tabia zetu za kila
siku na maradhi ya meno.
Wakati mwingine jambo hili laweza
kukufanya ushindwe kujiamini wakati wa
kuzungumza na watu. Lakini pia laweza
kuwafanya wanaokuzunguka wakushushe
thamani wakidhani wewe ni mchafu...na
kumbe una maradhi.

Tatizo la kunuka mdomo linawapata baadhi
ya watu, ambao hata wakipiga mswaki,
lakini bado  ananuka mdomo hata pale
anapotumia vitu vya kuufanya mdomo
unukie vizuri kama ‘Chewing gum’ pipi
hususan pipi-kifua na hata Big G  bado mtu
mwenye tatizo hilo  ataendelea  kuwa na
harufu mbaya.

Wanasayansi wamekiri kwamba ni vigumu
sana mtu kufahamu kuwa   ana harufu
mbaya kwa sababu ya  mazoea lakini ni
rahisi sana kutambua  harufu kutoka
kwenye kinywa cha mtu mwingine.
Unaweza kutambua kama una harufu
mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu
unayemuamini na pia unaweza kujua
harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya
kiganja na kunusa, wengine hupumua
mbele ya kioo na  kunusa.

Pia unaweza kutumia kijiti cha
kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi
unaweza kutumia vifaa kama ‘Halimeter’,
‘Gas’ ‘Chromatography ‘na ‘BANA Test.

“Magonjwa ya kinywa  yanasababishwa na
mabaki ya chakula kwa kuwa mwili wa
binadamu una vijidudu aina ya bacteria
ambao kwa kitaalamu huitwa ‘normal flora’.
Wadudu hao mara  wanapokula  hutoa
tindikali ambayo husababisha magonjwa ya
fizi na kinywa.

Vitu vyenye sukari ikiwemo sukari ya
kawaida pia huchochea tatizo hili,  lakini
mpangilio wa meno  katika kinywa
huhifadhi mabaki na kuleta harufu mbaya,”
 Anaeleza kuwa tatizo hili pia  huchangiwa
na  vijidudu vya ‘bacteria’  wanaojificha   kati
ya jino na jino na wengine kama ana jino
lililotoboka vijidudu hivi hutumia nafasi ya
kujificha humo.

 Lakini wale ambao wana tabia ya kulala
mdomo wazi, tabaka la juu la ngozi ya
mdomo huoza na kutoa harufu mbaya.
Unywaji Pombe: Unywaji wa pombe
husababisha kiwango cha kabohaidreti
kubaki mdomoni na kuoza hivyo
kusababisha magonjwa ya fizi.

Chanzo  kingine  kikuu  cha  harufu  mbaya
ya  kinywa ni  pale ambapo chakula kingi
kinabaki mdomoni hasa hasa nyama.
Utumiaji  wa  chakula  chochote
kitakachokaa  ndani  ya  mfumo  wa  usagaji
wa  chakula  kwa  muda  mrefu   kitaanza
kuoza, na   siku zote  nyama  inapooza
huanza  kutoa  harufu  mbaya  ( kunuka ).
Kwa  hiyo  hiki  nacho  ni  chanzo  kikubwa
cha  harufu  mbaya  ya  kinywa.
Harufu hii ya mdomo inaanzia kwenye
kinywa na kushuka kwenye mapafu na
kusababisha tatizo hilo kuwa kubwa zaidi.

Nini cha kufanya unapokuwa na tatizo Hili:
Cha kufanya iwapo una tatizo  la kutoa
harufu kwenye kinywa hakikisha  unapiga
mswaki mara baada ya mlo. Ili kuwaondoa
vijidudu vya bacteria wanaotokana na
mabaki ya chakula na pia kama unajino
lililotoboka ni bora kuling’oa au kulitibu kwa
njia ya kusafisha meno na kujaza risasi,

Pia unaweza kutibu kwa njia mbadala kwa
kutumia Ndulele ili kuondoa vijidudu vya
bacteria vinavyotoboa jino wasiambukize
meno mengine. (Ndulele zinafanana na
nyanya chungu lakini haziliwi).
Wale ambao wakipiga
mswaki damu zinatoka kwenye fizi, hiyo ni
dalilia hatari.

Matibabu ya fizi

“Tatizo la Fizi  (Non Communicable disease)
kama yalivyo mafua makali, kifua, koo na
kisukari yanahitaji matibabu ya mara kwa
mara.
 Ni vyema kusafisha meno kwa dawa na
kupata elimu ya jinsi ya kuepukana na tatizo
hili.

Wanawake wanaongoz
Wanawake ndio
waathirika wakubwa wa tatizo la meno
kwani kati ya wagonjwa 10 ambao
amekuwa akipata tiba kwa siku katika hospital ya
Hurbet Kairuki Iliyopo Dar es salaam, saba ni
wanawake huku watoto wadogo wakifuatia
kwa tatizo la kuvunjika meno kutokana na
kula vitu vyenye sukari nyingi.

“Watoto hawanuki mdomo lakini wengi
wanaokuja hapa wametoboka meno na
wengine yamevunjika na hii inasababishwa
na mfumo wa maisha,  wanapewa vyakula
laini hawahitaji kutafuna sana, vyakula vya
makopo, chipsi, na watoto kuanzia umri wa
miaka mitano hadi tisa ndio wanaongoza
kwa tatizo hili,” anasema daktari moja katika
hospitali ya KAIRUKI.

Ushauri aina ya vyakula vya kujiepusha na
magonjwa ya meno, watu
warudi kwenye vyakula vya asili kwani
meno hujisafisha yenyewe.
Kupiga mswaki
Wengi wetu tumezoea kupiga mswaki
asubuhi tu, lakini tunakula vitu vingi kutwa
nzima na kisha kulala na mchanganyiko wa
vyakula hivyo katika ulimi na meno.

 Wataalamu wa afya wanasema, mtu
anatakiwa kupiga mswaki mara tatu kwa
siku  asubuhi anapoamka, baada ya chakula
cha mchana na wakati wa kulala. Akiweza,
apige mswaki kila baada ya mlo.

Magonjwa ya kinywa alisema
kama tatizo linaanzia mdomoni ni vyema
mgonjwa akatumia dawa  maalumu  ya
kusukutua  kinywa  kwa  muda  maalumu
ambayo  itasaidia  kuwaua  bakteria
wanao  sababisha  harufu  mbaya   ya
kinywa.

 Lakini pia nashauri watu kutumia  dawa
maalumu  ambayo  itaenda  kuondoa
uchafu  wote uliooza  na  uliogandamana
tumboni  na kwenye mapafu ambao  ndio
chanzo  cha   kutokwa  na  harufu  mbaya
ya  kinywa.

Tahadhari kwa vitu
vifuatavyo:

Epuka: Kula vyakula kama vitunguu maji,
vitunguu  swaumu, unywaji  wa  pombe,
vyakula  vyenye  protini  nyingi  kama  vile
samaki,  matumizi  ya  sukari, kahawa  na
baadhi  ya  aina  za   dawa  za  mswaki.

“Pombe  hukausha  kinywa,  Kinywa  kikavu
huchochea mazalio  ya  bakteria  wanao
sababisha  harufu  mbaya  ya  kinywa,”

Usivute sigara: “  Kama  kweli  mgonjwa
ana  nia ya   kumaliza  tatizo  la kutokwa  na
harufu  mbaya  ya  kinywa  anapaswa
kuachana  na  uvutaji  wa  sigara kwani
sio  tu unasababisha  harufu  mbaya  ya
kinywa  bali  pia  utakausha  kinywa  chako
na  hivyo  kusababisha  mazalio   ya
bakteria  wasababishao  harufu  mbaya  ya
kinywa.

Unywaji Kahawa: Kahawa  ina  tindikali
ambayo  husababisha  kuzaliwa  kwa
bacteria  wanaosababisha  harufu  mbaya
ya  kinywa.

Zingatia: kunywa  maji  mengi  kila  siku
angalau  lita  tano  kwa  siku, kwani kwa
kufanya hivyo kutakusaidia  kuosha
chembechembe  za  vyakula  ambavyo
vimebaki  mdomoni  na vilevile  usaidia
kuepusha  mdomo kuwa  mkavu.

Pia watu kujenga
utaratibu wa  kuzifanyia uchunguzi afya zao
mara kwa mara sio tu ya kinywa bali ya
mwili mzima kwa ujumla kwani  kuna
baadhi ya watu wananuka mdomo lakini
hawajitambui kama wana hilo tatizo lakini
kwa kufanya hivyo watajitambua na
kushauri angalau mara tatu kwa mwaka
kwa afya ya kinywa na mara moja kwa
mwaka kwa afya ya mwili mzima.

0 comments:

Post a Comment