Thursday 1 May 2014

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI (CERVICAL CANCER)


Saratani ya Shingo ya Kizazi (cervical cancer)yasemekana kuwa yaongoza kwa kusababisha vifo vya  wanawake chini Tanzania

Kati ya wanawake 6,210 waliopata nafasi ya kugundulika kwa ugojwa huu 4,355 wasemekana kufariki dunia.  

(Imaworldhealth, 2010)







Saratani ya shingo ya kizazi ni ugonjwa ambao hutokana na mabadiliko ya mfumo wa  chembe zilizoko  katika shingo ya kizazi, kubadilika zikishamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa kimaumbile na hivyo kupelekea ongezeko la upatikanaji wa saratani.


NINI KISABABISHACHO SARATANI YA SHINGO YA UZAZI ?


Utafiti wa kisayansi umeafiki kwamba 99%  ya saratani za shingo ya uzazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' (HPV).
Virusi hivi vilivyoko katika jamii ya papilloma vina aina zaidi ya 100,ambazo baadhi yake huambukizwa kwa njia ya  kujamiana.




BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA  HATARI  ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?
  • Kushiriki tendo ndoa katika  umri mdogo au chini ya miaka 18
  • Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofauti
  • Utumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system)
  • Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama Ukimwi
  • Uzazi wa mara kwa mara

BAADHI YA DALILI ZA SARATANI YA KIZAZI
  • Kutokwa na majimaji au uchafu wenye harufu kali ukeni.
  • Kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa
  • Maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( pelvic area)
  • Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
  • Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudia
  • Mkojo wenye matone ya damu

PAP TEST (PAPANICOLAOUS TEST)

Pap-Smear ni test ambayo hutumika  kuchunguza  mabadiliko ya chembe zilizopo katika mlango wa kizazi  (cervix) ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo mapema na hivyo kuyakabili mapema, kwani Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema.

Test hii hushauriwa kwa wanamke wa umri wa miaka 21 hadi 65  na chini ya umri wa miaka 21 endapo umeingia katika tendo la ndoa kwa kipindi cha kisichopungua miaka 3.



KUPUNGUZA HATARI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?

  • Pap tests.  Pata test hii mara kwa mara kuanzia mwaka 1 hadi 3,hii itategemea ushauri wa daktari wako,umri na majibu uliyoyapata ili kugundua chembe zisizo sahihi mapema na kuwahisha tiba.

  • Get an HPV vaccine (hii yashauriwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26.

  • Kuwa na mpenzi mmoja. Kitendo cha kuwa na mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magojwa ya zinaa.

  • Tumia kinga (condoms). Hii husaidia kupunguza maambukizi ya magojwa ya  zinaa  

0 comments:

Post a Comment