Thursday 1 May 2014

SAIKOLOJIA INAVYOTATUA TATIZO LA MWANAUME KUFIKA KILELENI MAPEMA!



Miongoni mwa matatizo makubwa
kabisa yanayowakabili wanaume katika
suala la kujamiiana ni kufika kileleni
mapema. Takwimu zisizo rasmi
zinaonesha kuwa, wanaume saba kati
ya kumi wanakasoro hii.


Malalamiko yanayotolewa na baadhi yao
yanaonesha kwamba, muda wa kumaliza
tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika
tatu kwa tendo la kwanza, huku wengine
wakimaliza hamu katika hatua za awali tu
za hamasa ya kimahaba.

Hata hivyo, kumetolewa maelezo na nafuu
ya ongezeko la muda katika tendo la pili na
kuendelea, ingawa bado suala la
kutangulia kufika kileleni kabla ya
wanawake limekuwa likiwahuzunisha
wanaume wengi.

Ni ukweli usiopingika kuwa, mwanaume
anapowahi kufika kileleni kabla ya
mwenzake humsababishia kero
mwanamke anayeshiriki naye tendo,
kwani humwacha njia panda pasipokuwa
na hitimisho la raha ya kujamiiana.

Hali hii inatokana na maumbile ya uume
wa mwanaume ambao husinyaa mara
baada ya kuhitimisha mbio zake, lakini
kwa mwanamke kuwahi si tatizo, kwani
hakumfanyi ashindwe kumsindikiza
mwenzake hadi kileleni.

Utofauti huu ndiyo unaowafanya
wanaume wahuzunike zaidi
wanapokabiliwa na janga hilo kiasi cha
kufikia hatua ya kwenda kwa waganga/
matabibu ili iwasaidie kuepuka balaa ya
kutoka uwanjani na aibu.

Ingawa kumekuwa na mafanikio katika
tiba za kisayansi, lakini bado wanaume
wameshindwa kupata ukombozi wa
kudumu wa tatizo hili. Wengi wamejikuta
wakijiongezea mzigo wa fikra kwa
kuzitumaini zaidi dawa au kuzitumia na
kupata matokeo mabaya zaidi ya kuishiwa
nguvu kabisa.

Kwa kufahamu mikinzamo iliyopo kati ya
akili na tiba ya nguvu za kiume na
madhara yachipukiayo imebainika kuwa,
mtu anaweza kujitibu tatizo hilo kwa
kutumia kanuni za kisaikolojia na
mafanikio yasiyo na madhara
yakapatikana.

Wataalamu wa kisaikolojia wanatambua
kuwa kanuni ya ufanyaji mapenzi iko zaidi
kwenye ubongo kuliko mwilini.
Kinachotokea hadi mtu akapata msisimko
wa kufanya mapenzi si mwitikio wa mwili,
bali ni utambuzi wa akili juu ya kiwango
cha mapenzi kilichopokelewa kwenye
ubongo unaojihusisha na hisia.

 
 Ushauri wa masuala ya kimaisha na
matatizo yote yanayohuzunisha unatolewa,
Inaelezwa
kuwa, akili ikishiba vigezo na kutuma
taarifa zenye usahihi kwenye mwili viungo
hupokea hisia na kuanza kusumbua. Kwa
msingi huo kama tunataka kufika kileleni
mapema au kuchelewa lazima tucheze
zaidi na akili kuliko mwili.

Katika hali ya kawaida nguvu ya kupenda
inayomwingia mtu huwa kubwa, lakini
suala la kupunguza ukubwa wa hisia
lazima lipewe kipaumbele. Jambo kubwa
linalowasumbua wanaume wengi wenye
tatizo la kufika kileleni mapema ni kuwa na
PUPA ya kufanya mapenzi.

Wengi wao hupokea hisia zilizokuzwa na
kwenda nazo katika ufanyaji wa tendo la
ndoa. Saikolojia inaelekeza kuwa ili
mwanaume achelewe kumaliza, lazima
apunguze mhemko unaotokana na kuona,
kuhisi na kupagawishwa na staili au
chombezo toka kwa mwanamke.

Anachotakiwa kufanya ni kutumia zaidi ya
dakika 20 kufanya maadalizi na mpenzi
wake kabla ya kuanza tendo. Hii itasaidia
kuufanya mhemko wake ushuke na
kumuongezea muda wa kumaliza.

Aidha mbinu ya kuidanganya akili lazima
itumike ili kuzima taarifa za juu za uzuri
wa mwanamke, maumbile na raha ya
starehe isipokelewe kwa nguvu kubwa
mwilini.
 Hii ikiwa na maana kuwa kuna
kipindi inabidi fikra za mwanume
zisihamasike sana kwenye tendo badala
yake iletwe mawazoni hali ya kawaida, si
ile ya kuweweseka na kuhema hema
hovyo.
Yafuatayo ni maelekezo ya msingi
ya kufanya,
ili mtu asifike kileleni mapema:
Mume na mke wanapoingia katika uwanja
wa mapenzi wakae kwanza kwa muda,
huku wakiwa wamejiachia na mavazi
mepesi.
Pili wacheze michezo mingi kwa
muda mrefu bila kuanza kazi yao. Wakiwa
kwenye hamasa hizo wasiwe kimya bali
wazungumze na kuulizana maswali ya
kimahaba.
Baada ya hapo mbinu nyingine ya kuzuia
mbegu za kiume zisitoke ni ile ya kujibana.
Inashauriwa kuwa mwanaume akiona
dalili za awali za kumaliza bila kujali
ametumia muda gani anachotakiwa
kufanya ni kukaza misuli ya miguu na
kuzuia mbegu kwa mtindo atumiao kuzuia
haja ndogo isitoke.

Kujibana huko kunatakiwa kuende
sambamba na kuacha kucheza ‘shoo’.
Pacha na hilo mwanaume anatakiwa
kuidanganya akili kwa kuilazimisha iwaze
jambo jingine hasa la kuhuzunisha ili
kuharibu taarifa za raha zilizotumwa
mwilini zisiendelee kufanyiwa kazi na
hatimaye kumaliza tendo haraka.

 
 Zoezi hili linaweza kuwa gumu katika
hatua za kwanza kutokana na kukosea
muda sahihi wa kujizuia, lakini mhusika
akiendelea kujizoeza atajikuta anaweza na
kupata uwezo wa kufanya mapenzi hata
kwa saa nzima, hivyo kuondokana na
tatizo hilo bila tiba wala madhara.
Tatizo la kuwahi kufika kileleni, mara
nyingi huendana na mambo mengine
ambayo huchagiza wenzi wengi
kusalitiana ama kutengana kabisa.
Wanawake wengi wanagombana na watu
wao kwa sababu kama hizi, hawavutiwi
kuwaona waume wao wakiwahi kufika
kileleni, hivyo kushindwa kuwapa dozi
inayotosheleza.

Wanasikitishwa na hali ya wenzi wao ya
kukosa nguvu za kutosha wakati wa
kufanya tendo la ndoa ama ugoigoi wa
kuchelewa kurudiwa na nguvu za kufanya
kweli.

Aidha, wanakosa amani wanapobaini
kwamba wapenzi wao hawana msisimko
wakati wa kufanya yale ‘mambo yetu’. Hata
hivyo, tunapogeuka kisaikolojia hili si
tatizo kubwa, bali linahitaji kutuliza akili.
Ninaposema kutuliza akili, nakuwa
namaanisha kuwa wengi hawana
magonjwa yanayohitaji dawa, isipokuwa
wanasumbuliwa na matatizo ya
kisaikolojia tu.

Vijana na baadhi ya watu wazima wengine
wanaenda kwa waganga na wakati
mwingine wakijikuta wanajiingiza katika
matumizi ya mitishamba bila kuelewa
kwamba ugonjwa wao haupo kwenye
kasoro za kimaumbile, bali upo akilini.
Hapa nataka tukubaliane kwamba jambo
kubwa linalowasumbua wanaume wengi
wanaodai kuwa hawana nguvu ni ukosefu
wa elimu ya mabadiliko ya kibinadamu na
ufahamu duni wa mbinu za kuwawezesha
kucheza michezo ya kimapenzi kwa
ufanisi.

Mpenzi ni sanaa pana, ina mafunzo mengi
na ili uimudu, unatakiwa ujifunze kila siku
mabadiliko yaliyopo. Sambamba na hilo,
kujua mapito, mazingira, mabadiliko ya
mwili na kuyakubali ni mambo ya msingi.
Pamoja na matatizo haya kuwakera
wanawake kama nilivyotangulia kusema,
huwafanya wanaume kukosa amani. Mara
nyingi wanaopata dosari hizi, hujihisi
wana nuksi.

Hata hivyo, mshangao unaokuja hapa ni
kwamba wanaume hupenda kutafuta
mbinu za kutatua tatizo lao bila
kuwashirikisha wenzi wao, kana kwamba
wao haliwahusu.

Saikolojia inatambua kuwa tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume ni zao la
udhaifu wa mke na mume na sio la
mwanaume peke yake kama watu wengi
wanavyodhani.

Kwa mfano, mwanaume atapata wapi
msisimko wa kimahaba kama mwanamke
hatakuwa mtundu wa kubuni mbinu za
kuufanya mwili uliopoa usisimke?

Atavutiwa nini mwanaume kurudia
awamu ya pili, ikiwa kwenye mzunguko
wa kwanza alikutana na harufu isiyofaa?

Nakshi nakshi humuongezea mwanaume
hamu ya kutaka tena na tena. Huo ndiyo
ukweli!

 
 Napenda niweke ukweli kweupe, mara
nyingi tatizo la msisimko wa kurudia
tendo, husababishwa na mwanamke
mwenyewe. Kwa maana hiyo, ili litatuliwe
ni lazima ziwepo juhudi za pande mbili mme na Mke.

0 comments:

Post a Comment