Thursday, 1 May 2014

MBADALA BORA WA SUKARI :

Xylitol  Sugar

Sukari  ina  tajwa  kuwa  na  madhara  makubwa  kwa  afya  ya  mwanadamu. Watalaamu  wa masuala  ya  afya  wamekuwa  wakiwasisitizia  watu  kupunguza  ama  kuachana  kabisa  na  matumizi  ya  sukari  vinginevyo  wawe  tayari    kwa  madhara  mbalimbali  yatokanayo  na  matumizi  ya  sukari  kama  vile  kupatwa  na  ugonjwa  wa  kisukari nakadhalika.

Hata  hivyo,  kuacha  kabisa  kutumia  sukari, ni  jambo  linalo  onekana  ku wawia vigumu  watu  wengi  sana, kwa  upande  wa  watoto  wadogo  ndio  kabisa, hutakiwi  hata  kufikiria  kuwazuia  waache  kutumia  sukari  kabisa.



Stevia  Sugar

Asali  inatajwa  kuwa  mbadala  wa sukari, lakini  watu wengi  wanalalamika  kuwa   chai  ikiungwa kwa  asali  haiwi  na ladha  nzuri  na  mara  nyingi  humfanya  mtu  ajisikie  kichefu chefu.
Hata  hivyo  wanasayansi  wamegundua  mimea, inayotengeneza sukari    yenye  ladha  nzuri  kuliko  hata  sukari  ya  viwandani.
Mimea  hiyo  ni  Stevia  na  Xyltol.  Mimea   hii  bali  ya  kutengeneza  sukari  asilia  yenye  ladha  sawa  sawa  na  sukari  ya  viwandani, lakini  ina  faida  kubwa  sana  kwa  afya  ya  mwanadamu  kama  vile ; Kupunguza  shinikizo  kubwa  la  damu ,kupunguza  sukari mwilini,  Kutengeneza   virutubisho  vyenye  nguvu  ya  kupambana  na  bacteria  wa  mdomoni,kutengeneza  madini  ya  calcium, kupambana  na  maambukizi  ya  kwenye  sikio  nakadhalika.
Kupata  sukari  iliyo  tengezwa  kwa  Stevia  auu  Xylitol, tembelea  kwenye  supermarkets  mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment