Kifafa ni ugonjwa wa ubongo
Ubongo wa binadamu una
mabilioni yz seli za neva zinazoshirikiana na kila mmoja kupitisha chaji ndogo
ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima. Wakati baadhi ya hizi seli zote kwa
ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo
na kusababisha kifafa ama kuzirai.
Kuzirai kwa gafla huathiri
ubongo kufanya kazi. Kunaweza kumsababishia mtu kupata mabadiliko ya gafla
katika fahamu, mwendo ama hisia.
Mshituko wa moyo mmoja
huamanishi ya kwamba mtoto ana kifafa. Kuzirai mara moja kunaweza kutokea Kwa
sababu tofauti kama homa, jeraha la kichwa, kiwango cha chini cha sukari katika
damu na kadhalika.
Kifafa ni jina la kuzirai
kwa ghafla kunapotokea zaidi ya mara moja bila ya sababu ya kutibiwa
inayojulikana.
Dalili na ishara za kifafa
Nitajuaje
ikiwa niimeathiriwa na kifafa?
Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye
huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea
kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali). Hapa, mgonjwa (ambaye
huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika kadhaa. Wakati huu, hawaitikii
jina lao na
hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao
wataona ya kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote
kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika
masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.
Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi
kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu
hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya
mda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu
hiyo ya mwili kwa mda baada ya kuzirai.
Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na
kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala
usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya
kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa zingine wanapoamka
hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo
wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.
Katika aina zingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli
yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu
kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.
Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza
kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na
kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta
ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo
Je kila mtu anayeathiriwa na kifafa anapaswa kupelekwa
hospitalini?
La. Sio kila mtu anayeathirika na kifafa anapaswa kupatiwa
huduma ya matibabu. Mtu mwenye kifafa ambaye yuko chini ya matibabu labda
hahitaji kupelekwa hospitalini mara moja. Kuna visa vingine ambavyo ni muhimu
kumpeleka mtu hospitalini kama dharura.
·
Kuzirai mara ya kwanza. Ikiwa mtu anafahamika ya kwamba huwa
hana kifafa na kishe azirai, mtu huyu anahitaji kumuona dakitari mara moja.
·
Ikiwa kuzirai kumekaa zaidi ya dakika 5, mpeleke mgonjwa
hospitalini.Hili huwa nadra lakini lifanyikapo huwa hatari sana na ni lazima
umkimbize mgonjwa hospitalini hata ikiwa bado yuko katika hali hiyo ili kuokoa
maisha yake.
·
Ikiwa kupumua hakurudii hali ya kawaida baada ya kuzirai.
Ikiwa kuzirai kutaisha na kujirudia tena mara hiyo hiyo Kabla ya
mgonjwa kupata nafuu.
Je,
kuna tiba ya kifafa?
·
Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa
huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu
ya hali zingine kama vile uvimbe kwenye ubongo ,ugonjwa wa figo au
ugonjwa wa ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine
imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa
hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.
·
Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na
kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri
hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa
hazirai kwa mda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai
wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.
Jinsi
nyingine za kudhibiti kifafa Kando na madawa, ni nini
kingine ambacho kinaweza kunisaidia ikiwa niko na kifafa?
·
Imeonekana ya kwamba kuna vitu ambavyo vinaweza
kusababisha mshtuko kwa mtu aliye na kifafa ikiwa hata amedhibitiwa na
matibabu. Kukosa usingizi wa kutosha (mtu mzima anahitaji angalau masaa 8
ilhali mtoto anahitaji angalau masaa 9) kunaweza kusababisha mshtuko wa
kifafa. Mfadhaiko mwingi utokanao na matatizo unaweza pia kusababisha
shambulizi.
·
·
Homa katika watoto imejulikana kuongeza nafasi ya kutokea kwa
mshtuko wa kifafa. Taa zinazomemeteka kama vile kioo cha runinga na mataa ya
disko yanaweza kusababisha mshtuko wa kifafa katika watu wengine. Kupumua kwa
nguvu wakati
unapumzika kumetambuka kusababisha mshtuko. Hutokea mara kwa mara
katika watoto wakati wako kwenye hali ya kuogopesha sana ama hofu kubwa. Ukiwa
unaweza kuepuka haya, unaweza kujisaidia kuepuka kushikwa na mshtuko wa kifafa.
Kwa
nini haupaswi kumwekea mtu kitu mdomoni anaposhikwa na mshtuko wa kifafa?
·
Kwa mda mrefu iliaminika ya kwamba wakati mtu ameshikwa na
kifafa, mgonjwa anaweza kumeza ama hata kunyongwa na ulimi wake na kwa hivyo
kusababisha kifo. Hivi sasa hali imebadilika na inaeleweka ya kwamba hakuna
haja ya kuweka kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na kifafa.
Hili linaweza kusababisha madhara zaidi.
\
·
Wakati wa kifafa kuna mshtuko wa ghafla wa misuli.Mikono, miguu
na sehemu zingine za mwili huwa na mwendo wa kujirudia rudia ambao ni vigumu
kuukabili kwa kutumia nguvu haswa ikiwa mgonjwa ni mkubwa kwa umbo. Kama sehemu
ya tendo la
misuli, mgonjwa husaga meno yake kwa sababu ya tendo la nguuvu
katika taya. Jaribio lolote la kuweka kitu kwenye mdomo linaweza kusababisha
kuvunjika kwa meno ya mgonjwa, kunyongwa na kile kilichowekwa mdomoni ama
mgonjwa kumuuma vibaya mhudumu wake.
Kwa hivyo fahamu: USIWEKE
kitu katika mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na mshtuko wa kifafa.
Kwa
nini wagonjwa wa kifafa hawawezi kugawana madawa yao?
·
Madawa ya kifafa hufanya kazi ya kukomesha shughuli zisizo za
kawaida kwenye ubongo. Kuna aina nyingi za kuzirai katika kifafa na hizi zote
huitikia kwa njia tofauti kwa madawa tofauti. Hii ndio sababu ya kwanza kwa
nini haufai kugawa dawa za kifafa. Dawa ambazo hudhibiti aina moja ya kifafa
zinaweza kukosa athari kwa aina nyingine ya kifafa.
·
Pili, watu tofauti wanahitaji vipimo tofauti vya dawa
iliyotolewa kudhibiti kifafa. Ugonjwa wa kifafa unamaanisha ya kwamba ubongo wa
mtu unaweza kufyatuka kwa njia isiyo ya kawaida.
Watu tofauti hupata kifafa
katika viwango tofauti vya mchangamsho wa ubongo. Watu wengine huchangamshwa
kwa urahisi na kuzirai ilhali wengine hawachangamshwi kwa urahisi. Kipimo cha
dawa kinachotumiwa kumdhibiti mtu ambaye huzirai kwa urahisi ni tofauti na kile
cha yule ambaye hazirai kwa urahisi.
·
Tatu, sio vizuri kugawana madawa ambayo yametolewa kufuatia
maagizo ya dakitari. Maagizo ya dakitari hutoa dawa kwa mtu mmoja kwa kipindi
maalumu cha wakati. Kwa kugawana
madawa, mtu ambaye alipewa maagizo ya dakitari
ataishiwa na dawa kabla ya ahadi ya kuonana na dakitari inayofuatia. Wanweza
kuzirai kwa urahisi kwa sababu hawako kwenye matibabu. Sio salama kwa mtu
mwenye kifafa kugawa dawa zake.
Matatizo
yaweza tokezea wakati wa matibabu?
Je kuna
jambo ambalo linaweza kuenda mrama nikiwa bado kwenye matibabu?
·
Athari ya matibabu ni hisia ya kusinzia na kutokuwa mwepesi
ambako hutoweka baada ya mda. Baadhi ya madawa yanaweza kumfanya mgonjwa
aongeze uzito. Athari mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea ni kwenye ini. Hili ni
jambo la kawaida wakati mgonjwa anatumia madawa kadhaa ili adhibiti kifafa.
·
Unapoanza matibabu, athari yake kwa kifafa huwa siio ya papo kwa
hapo. Inachukua angalau mwezi mmoja kuona athari yoyote ya kudumu na mtu
anahitajiwa kuwa mvumilivu. Katika visa vichache, visa vya kuzirai vinaweza
kuongezeka unapowekwa kwenye matibabu kabla kuzirai hakujapungua.
Ni
kipi kipimo cha dawa za kutibu kifafa?
·
Kipimo cha dawa ni kile ambacho kitatibu kitadhibiti ama
kitatibu hali hii bila ya kusababisha mathara mabaya ya kando. Hii hutofautiana
kutoka kwa matibabu hadi matibabu na hali hadi
hali. Dawa zingine kama Panadol
zina kiwango chake rasmi; watu wazima humeza vidonge 2 kila masaa 6-8. Hali
zingine kama malaria isiyo kali zina kiwango cha dawa kinachopeanwa katika
kiwango cha kipimo cha dawa kama watu wazima humeza vidonge 2 vya
Camoquine mara moja kwa siku 3.
·
Hesabu ya kiwango cha kipimo cha dawa hutegemea uzani wa mgonjwa
ama umri wake. Kila aina ya dawa ina kipimo kwa uzani ama umri wa mgonjwa
uliopeanwa.
·
Katika visa vingine vya kifafa, kiwango cha dawa hakiwezi
kuhesabika kwa urahisi. Matibabu yanayotolewa ili kudhibiti kifafa huathiriwa
kwa urahisi na vipimo vya dawa na hufanya kazi
katika kadiri ndogo. Dawa kidogo
kwenye damu ama dawa nyingi kwenye damu na udhibiti wa kifafa hupotezwa. Kwa
hivyo kila dawa inaweza tu kutumiwa katika kadiri iliyotolewa ya kipimo cha
dawa. Ikiwa kuzirai hakuwezi kudhibitiwa katika kadiri hii,dawa ya pili na saa
zingine dawa ya tatu inaweza kuongezwa. Hii nyongeza ya madawa hujiathiri na
kipimo cha kila dawa kinahitaji kuhesabiwa mara tena ili kila dawa ikuwe katika
kiwango kinachofaa katika damu.
·
Kufanya mambo kuwa magumu zaidi, kutokea kwa kifafa hakuwezi
kutabirika katika watu tofauti. Kuna wale ambao ugonjwa wao wa kifafa unaweza
kudhibitiwa kwa urahisi ilhali
wengine wanahitaji matibabu 2-3 ili
kupunguza visa vya kuzirai bila ya kuvimaliza kabisa. Kwa wagonjwa 2 wenye umri
sawa na uzani sawa, matibabu ya kipekee yanaweza kutolewa katika vipimo tofauti
ili kudhibiti kuzirai kwao.
Ni
kwa mda upi ambao mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia dawa?
·
Mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia madawa aliyopewa
hadi ashauriwe vingine. Kwa kutegemea wingi wa kutokea kwa visa vya kifafa,
wagonjwa wanaweza kutumia dawa kwa maisha yao yote.Katika watoto,hata hivyo
mambo yanabadilika. Kitambo, ilichukuliwa ya kwamba mtoto mwenye
kifafa
angehitajika kutumia madawa kwa miaka mingi ya maisha yake. Lakini hali sio
hivyo tena. Ikiwa mtoto anatumia madawa kwa njia inayofaa na kwa wakati bila ya
kukosa hata kipimo.cha dawa na anabakia bila kifafa kwa angalau miaka 2, basi
dakitari anaweza kufikiria kusimamisha utumizi wa madawa. Ni dakitari pekee
yake anayeweza kutoa ushauri kuhusu kusimamaisha matumizi ya madawa ya kifafa
baada ya kumfuatilia
mgonjwa kwa kipindi fulani cha mda. Ni muhimu maamuzi
haya yafanywe na dakitari, kwa sababu mwanzo utumizi wa madawa umeanza
haufai kukatizwa kwa ghafla. Badala yake dakitari atapunguza kipimo cha dawa
pole pole hadi matumizi ya dawa umesitishwa. Ukisitisha dawa kwa ghafla, kuna
madhara ya kando kama kumwa na tumbo, kutapika na kutomakinika na kuzirai
kunaweza kujirudia.
·
Kwa hivyo, jambo muhimu ni kuzungumza na dakitari wako kuhusu
kusimamisha matibabu. Ikiwa mtoto hajafuzu kwa ajili ya kusitishwa matibabu kwa
sasa, na kisha aendele kutokana na ushauri wa dakitari. Ikiwa mtoto atafuzu,
basi hili linafaa
kufanywa kwa utaratibu. Wakati kipimo cha dawa kinapunguzwa,
ni muhimu kukumbuka ya kwamba mtoto anaweza kushikwa na kifafa. Waweke wakiwa
salama na waangalie kwa karibu hadi dawa zote zimesitishwa kabisa na kila kitu
kiko salama.
Ni
mda gani unaochukuliwa ili kudhibiti kifafa?
·
Wagonjwa tofauti wana aina tofauti za kifafa na aina tofauti za
kifafa hudhibitiwa kwa njia tofauti.Baada ya kubainika kumehakikishwa, mgonjwa
huwekwa kwenye kipimo kimoja cha
dawa hapo mwanzoni.Hushauriwa kurudi baada ya
mwezi ama zaidi dakitari atathmini ikiwa dawa inadhibiti kifafa kwa njia
inayofaa.Ikiwa sivyo, basi kipimo cha dawa huongezwa pole pole.Na ikiwa hii
haina mafanikio, basi dawa ya pili huongezwa na ikiwa inahitajika, dawa ya tatu
itaongezwa.
·
Mda unaochukuliwa kwa ugonjwa wa kifafa kudhibitiwa hutofautiana
kutoka kwa mgonjwa hadi kwa mwingine.Ugonjwa wa kifafa wa mgonjwa mmoja unaweza
kudhibitiwa kwa dawa
moja tu.Katika visa vingine, mgonjwa anaweza kuwa akitumia
madawa 3 na bado anaathirika na kifafa, ingawaje idadi ya kuzirai
kunakosababishwa na kifafa kutapungua ukilinganisha na hapo awali.Wagonjwa
wengine hutibika haraka kuliko wengine na aina zingine za kifafa huwa rahisi
kudhibiti kuliko zingine.
·
Hakuna mbinu iliyobainika katika kudhibiti kifafa.Lengo la matibabu
ni kupunguza idadi ya kuzirai kunakoathiri mgonjwa na ikiwa inawezekana
kusimamisha kuzirai kabisa kwa mda mrefu.
Ni
nani yuko kwenye hatari ya kupata kifafa?
·
Ugonjwa wa kifafa unaweza kuathiri mtu yeyote katika umri
wowote. Madhara ya ubongo ndio hali ya kawaida ambayo inaweza kusababisha
kifafa baadaye. Matatizo wakati wa
kujifungua,homa ya nyonga ya manjano katika
mwezi wa kwanza wa maisha, magonjwa ya utotoni kama homa ya uti wa mgongo ni
sababu za kawaida za kifafa katika watoto. Homa kali pia husababisha kuzirai
kwa watoto wadogo. Katika visa vingine kuzirai huku hufanyika kila wakati kuna
homa. Mtoto ambaye amezirai mara tatu ama zaidi ambako kuna uhusiano na homa
anafaa kuwekwa chini ya matibabu dhidi ya kifafa.
·
Watu wazima ambao huathiriwa na madhara ya ubongo kwa sababu ya
jeraha, ambukizo ama kwa sababu ya ugonjwa mwingine kama maradhi ya ini,
maradhi ya figo wanaweza pia kuathiriwa na ugonjwa wa kifafa.
·
Ni muhimu kukumbuka ya kwamba ugonjwa wa kifafa unaweza
kuwaathiri watu ambao hawana madhara yoyote ya ubongo ama ugonjwa wa hapo
awali. Katika visa vingine hutokea katika familia, lakini wakati mwingi hutokea
bila ya sababu yoyote inayojulikana.
Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa mtu atashikwa na mshtuko wa kifafa?
Wakati
mwingi, huduma ya kwanza ina maana ya kumfanya mtu awe salama wakati mshtuko wa
kifafa unapotokea. Kwa bahati nzuri, mshtuko huwa mfupi na huisha baada ya
dakika kadhaa.
Hatua
ya kwanza katika kujitayarisha kwa ajili ya kifafa ni kufahamu kitu cha kufanya
wakati ugonjwa huu unapotokea. Hii ni muhimu ikiwa unamchunga mgonjwa wa kifafa
lakini pia kwa kila mtu. Ugonjwa wa kifafa unaweza kuanza katika umri wowote na
kila mtu anahitaji kufahamu nini cha kufanya wakati mtu karibu nao anaathiriwa
na kifafa.
Huduma ya Kwanza
·
Kuwa mtulivu na usiogope. Kifafa humuogopesha mtazamaji.
Huchukua dakika chache na kwa kawaida huhitaji matibabu.Kumbuka ya kwamba mtu
aliyeshikwa na kifafa huwa hafamu vitendo vyake na anaweza au asiweze
kukusikia.
·
Walinde dhidi ya majeraha wakati wanaposhikwa na kifafa.Ikiwa
inahitajika mweke chini kwa njia iliyo taratibu.
·
Sogeza vitu vigumu, vitu vyenye ncha kali na vilivyo moto na
linda kichwa na mwili wa mgonjwa dhidi ya jeraha.
·
Usiweke chochote mdomoni ama ujaribu kubanua meno.
·
Mtu hayuko katika hatari ya kumeza ulimi wake
·
Usijaribu kuzuia mwendo wao kwa kutumia nguvu.Hili linaweza
kusababisha majeraha kwa mgonjwa na pia yule anayejaribu kuwasaidia.
·
Popote inapowezekana, jaribu kumlaza mtoto katika sehemu iliyo
laini na wageuze upande mmoja.
·
Weka kitu tambarare na laini chini ya kichwa chake ili
asijiumize.
·
Fungua nguo zilizombana haswa kwenye shingo kama tai, skafu na
kadhalika
·
Usiweke chochote mdomoni.
·
Nakili mda ambao mshtuko umechukua.
·
Jaribu kutazama mwondoko ambao mtu hufanya wakati ameshikwa na
kifafa.
·
Wakati mkutuo unaanza kupungua, hakikisha ya kwamba kupumua
kumerudia hali yake ya kawaida.
·
Baada ya kifafa, mvingirishe mtu ili alalie upande mmoja.Hili
hufanya mate kutoka mdomoni na kuhakikisha ya kwamba hanyongwi. Ikiwa kuna
matapishi, mweke mtu kwa upande mmoja na safisha mdomo wake kwa kidole.
·
Usijaribu kumpatia dawa ama uoevu hadi aamke
·
Waondolee hofu, zungumza nao kwa upole na wasaidie kupata nafuu
pole pole.
·
Usimwache mtu pekee yake hadi apate nafuu.
Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa nadhani nimeathiriwa na kifafa?
·
Ni muhimu kukumbuka ya
kwamba kifafa ni hali ambayo inaweza kudhibitiwa. Sio kitu cha kuona haya. Sio
laana ama ulemavu. Ni hali inayohitaji matibabu na kufuatiliwa kama hali
zingine kama shinikizo la juu la damu, kisukari, pumu na kadhalika
·
Ikiwa unadhani ya kwamba
umeathiriwa na ugonjwa wa kifafa ama ikiwa umewahi kuanguka chini na kuzimia ni
muhimu kutafuta usaidizi wa dakitari aliye karibu. Ikiwa inawezekana andamana
na mtu aliyekuwa nawe wakati ikifanyika ili waeleze kile walichokiona. Hili
litasaidia dakitari kufanya ubainifu sahihi.
Ni sehemu gani ya ubongo huathiriwa na kifafa?
·
Ubongo ni ogani iliyo na
sehemu nyingi (sehemu ya mwili) ambazo hudhibiti mwili wote. Sehemu tofauti za
ubongo hudhibiti sehemu tofauti za mwili na kazi tofauti kwenye mwili. Kuna
sehemu ya ubongo ambayo hudhibiti misuli ya mkono; sehemu tofauti
itadhibiti
kuhisi uchungu wa mkono huo huo na sehemu tofauti ya ubongo itaratibu sauti ya
kupiga mayowe wakati mkono huo unahisi uchungiu ama uko kwenye hatari. Hizi
sehemu zimeunganishwa na seli za ubongo (nyuroni). Muungano huu ndio ule
unaoturuhusu kufanya kazi kama mtu mmoja kwa njia ya kupatana kwa misuli.
·
Kifafa ni shughuli isiyo
ya kawaida kwenye ubongo. Sehemu yoyote ya ubongo inaweza kupatwa na jambo hili
lisilo la kawaida. Kwa sababu sehemu tofauti za ubongo hudhibiti sehemu tofauti
za mwili, hii ndiiyo sababu mtukutiko wa maungo katika kifafa ni
tofauti kutoka
kwa mtu mmoja hadi mwingine ama pia kutoka kwa kuzirai huku na kule. Ikiwa kuna
shughuli isiyo ya kawaida kwenye ubongo katika sehemu ya ubongo inayoathiri
misuli ya mikono na miguu, kutakuweko msukumano mwingi katika hizo sehemu
za mwili.
·
Shughuli hii isiyo ya
kawaida kwenye ubongo inaweza kufanyika tu katika sehemu moja ya ubongo ama
inaweza kusambaa katika
muungano ili kuhusisha ubongo wote.Kuzimia ambako
husababishwa na shughuli ya sehemu moja ya ubongo ndio kule tunakokuita kuzirai
kusio kamili. Kuzirai kunakosababishwa na shughuli ya ubongo wote ndio kule
tunakokuita ugonjwa wa kifafa ulio mbaya ama kuzimia kamili.
·
Kwa jumla tunaweza
kusema ya kwamba ikiwa sehemu ndogo ya ubongo itaathirika basi mtukutiko wa
maungo utakao onekana utakuwa mdogo. Ikiwa sehemu kubwa ya ubongo itaathirika
basi mtukutiko wa maungo utakao onekana utakuwa mkubwa. Kuzirahi kusio kamili
kutaathiri sehemu ndogo ya ubongo kuliko kuzimia kuliko kamili.
0 comments:
Post a Comment