Thursday 1 May 2014

HUU NDIO UGONJWA HATARI WA INI / HEPATITIS B NA CHANJO YAKE



Hepatitis B ni nini?
Ni ungojwa wa ini unaosababishwa na uambukizo wa virusi vya hepatitis         B. Mtu anapopata uambukizo, virusi huvamia ba kuanza kuathiri chembechembe hai za Ini.

Baada ya hapo yafuatayo yanaweza kutokea;
1.    Kupata ugonjwa wa ini wa muda mfupi wa chini ya miezi sita na kasha kupona kabisa (acute hepatitis B) au kupata ugonjwa mkali (fulminant hepatitis) na hatimaye hata kufa
2.   Kuendelea kuwa na virusi mwilini kwa muda mrefu wa zaidi ya miezi sita na hapo baadae kusababisha kusinyaa kwa ini (Liver cirrhosis) au 
saratani ya ini ( liver cancer) na hatimae kifo.
NJIA KUU ZA MAAMBUKIZO YA UGONJWA WA INI/ HEPATITIS B
Virusi vya Hepatitis B huingia mwilini kwa njia ya damu au maji maji mengine ya mwilini kama vile maziwa, mate, maji maji ya mbegu za kiume, maji maji ya ukeni n.k.
NJIA KUU ZA KUENEA KWA UGONJWA HUU NI;
1.    Kugusana ngozi kwa ngozi baina ya mwenye virusi vya Hepatitis B na Asiye navyo kupitia kwenye vipele, vidonda, michumbuko, mikwaruzo n;k (horizontal transmission)
2.   Kutumia sindano na mambomba ambayo hayakutakaswa (drcontaminated) na kuzuzwa ( sterilized) vizuri.
3.   Kujamniiana na mtu mwenye virusi vya Hepatitis B
4.   Kutoka kwa mama mwenye virusi vya Hepatitis B kwenda kwa motto wakati wa kujifungua au wakati wa kumnyonyesha. (mother to child transmission)
5.   Kuongezewa damu yenye virusi vya hepatitis B
DALILI ZA UGONJWA WA INI (HEPATITIS B)
Mara nyingi watu wenye ugonjwa huu hawaonyeshi dalili zozote. Karibu asilimia 90% ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, asilimia 50% ya watoto wenye umri zaidi ya miaka mitano na baadhi ya watu wazima huwa hawaonyeshi dalili zza ugonjwa huu;
Dalili za ugonjwa wa Hepatitis B zinaweza kujitokeza wakati wowote kati ya wiki sita na miezi sita tangu mtu apate ambukizo la virusi, kwa wastani huchukua muda wa miezi mitatu.
DALILI ZA MWANZO.
Wagonjwa huonyesha dalili zifuatazo;
·        Dalili za mafua (flue like illness)
·        Kuumwa kichwa
·        Homa
·        Uchovu
·        Kuishiwa nguvu
·        Kupoteza hamu ya kula
·        Kichefu chefu
·        Kutapika
·        Maumivu ya tumbo na hata kuharisha
DALILI ZA BAADAE.
Baada ya siku tatu hadi nne.
·        Macho na ngozi (hasa  viganja na nyanyo) hubadilika rangi na kuwa njano.
·        Rangi ya mkojo hubadilika na kuwa njano iliyokolea na kinyesi huwa cheupe cheupi.
Kwa Kawaida dalili  hizi hupotea katika muda wa wiki mbili.
·        Asilimia 90% ya wagonjwa watu wazima huweza kupona kabisa katiika muda wa miezi sita tangu wapate uambukizo, na wachache wanaweza kufa katika kipindi Fulani hiki. Asilimia 5% hadi 10 huendelea na uambukizo sugu unaodumu zaidi ya miezi sita ambao baadae huleta matatizo ya kusinyaa kwa ini, saratani ya ini na hatimae kifo.
·        Asilimia 70% hadi 90% ya watoto wagonjwa baada yak upon huendelea kuwa na uambukizo sugu wa Hepatitis B (hepatitis B carriers)
KUTHIBITISHA UGONJWA.
Ugonjwa huthibitishwa kwa kupima damu ya mgonjwa katika maabara, kwa kuangalia vitambulishi vya virusi vya Hepatitis B ( HBsAg, Anti-HBc, HbcAG)
TIBA
UGONJWA HUU HAUNA TIBA.
KINGA DHIDI YA UGONJWA WA HEPATITIS B / UGONJWA WA INI.
CHANJO
Njia muhimu ya kujikinga na ugonjwa huu ni kupata chanjo. Chanjo ya hepatitis B inaweza kuwa peke ya au ikichanganywa na chanjo nyingine. Moja ya chanjo dhidi ya ugonjwa huu ambayo imechanganywa tayari hujulikana kama DPT-HB. Chanjo hii ndiyo ilijumuiashwa katika mpango wa chanjo wa Taifa.
NJIA NYINGINE ZA KUJIKINGA UAMBUKIZO
WA UGONJWA WA HEPATITIS B.

1.    Kuepuka matumizi ya damu isiyopimwa virusi vya Hepatitis B/damu isiyo salama.
2.   Kutotumia mabomba na sindano zisizotakaswa na kuzuzwa(sterilized) vizuri
3.   Kuepuka uasherati
4.   Wafanyakazi wa afya kuwa waangalifu wakati wa kutoa huduma hasa zinazohusiana na damu, sindano, upasuaji, uzalishaji n.k
CHANJO HII YA DPT-HB
Ni mchanganyiko wa chanjo nne zinazomkinga motto asipatwe na magonjwa yafuatayo;
1.    Dondakoo- Diptheria (D)
2.   Kifaduro- Pirtussis (P)
3.   PepoPunda- Tetanus (T)
4.   Ugonjwa wa Ini- Hepatitis B (HB)
WANAOSTAHILI CHANJO YA DPT-HB.

Chanjo ya DPT-HB hutolewa kwa watoto wote walio na umri wa chini ya miaka mitano, hususani kati ya mwezi mmoja na miezi mitatu.
Kiasi cha chanjo kwa kila hudhurio ni 0.5ml, ndani ya msuli wa paja la kushoto na chanjo hii hutolewa mara tatu kwa kila mtoto.

MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA BAADA YA CHANJO YA DPT-HB /Side effects)

Matatizo yanayoweza kujitokeza katika muda wa saa 48 baada ya chanjo ya DPT-HB ni;
·        Sehemu iliyochanjwa inaweza kubadilika rangi kuwa nyekundu, kuvimba au kuuma kidogo.
Ø Homa
Ø Mtoto kulia lia
Ø Mtoto kusinzia sinzia
Matatizo haya mara nyingi hutoweka yenyewe bila kupatiwa tiba na si kupingamizi kwa chanjo.

0 comments:

Post a Comment