Saturday 3 May 2014

FAIDA AZIPATAZO MAMA ANAYENYONYESHA MTOTO


Shirika la afya duniani (WHO) linasisitiza mama kumnyonyesha mtoto kwa kipindi cha miezi sita bila kumwanzishia vyakula vingine.
 
WHO inaelekeza kuwa baada ya miezi sita mama anaweza kumwanzishia vyakula vyingine motto wake huku akiendelea kunyonya maziwa ya mama angalau mpaka atakapofikia umri wa miaka miwili au ziadi.
 
Pia, mtoto anyonyeshwe saa moja baada ya kuzaliwa, anyonyweshwe pale anapohitaji mara nyingi kwa kadri anavyohitaji usiku kwa mchana na mama anashauriwa kutotumia chupa kumpatia maziwa mtoto.
 
FAIDA AZIPATAZO MAMA KWA KUMNYONYESHA 
 
MTOTO.
 
Maisha huwa rahisi kwa mama anayenyonyesha kwani akilinganisha na maziwa ya mama ya fomula (yale ya 
 
kutengeneza viwandani), maziwa ya mama hutumia nguvu kidogo au zaidi, hapo baadaye baada ya mama na motto 
 
kutulia na kuzoeana maziwa hutiririka kwa wingi zaidi, huitaji kuwa na kazi ya kusafisha chupa na chuchu yake 
 
kwa mashine maalum za kuchemshia vyombo ili kuua viini vya maradhi, maziwa ya mama hayahitaji kununua, kupima 
 
wala kuchanganya, hayahitaji uamke usiku mwingi na uyapashe, maziwa ya mama hupatikana kwa haraka na kwa muda sahihi pale mtoto anapohitaji.
 
KUNYONYESHA KUONAOKOA FEDHA.
 
Kwa mzazi huhitaji kununua vyombo na maziwa ya fomula,kwa mwaka inakubidi kutumia zaidi y ash milioni 4 ili kugharamia maziwa ya fomula na vyombo, pia 
 
inaonyesha 
 
watoto wanaonyonyeshwa hawapatwi na maradhi mara kwa mara hivyo basi  huokoa pesa nyingi ambazo zingetumika 
 
kwa matibabu.
 
KUNYONYESHA KUNAKUFANYA UJISIKIE MWENYE FURAHA.
 
Kugusana kimwili wakati wa kunyonyeshana na mtoto aliyezaliwa ni uhimu kwani mtoto huwa na usalama zaidi, hupata joto sahihi na kutopata usumbufu wowote, 
 
unapomnyonyesha panakuwa na ukaribu wa kimwili hivyo hufanya uhusiano wako na mtoto kuimarika zaidi hivyo 
 
humpa mtoto faraja na kwako pia.
 
Pia, mtoto huzoea harufu yako na kujiihisi mwenye usalama, hali hii ya mtoto kukutambua hukufanya kujihisi 
 
kupendwa na mtoto wako,
 
Mtindo uliobuniwa uitwao kangaroo ambapo mama humbeba mtoto kwa mfano wa mnyama kangaroo ambavyo mtoto wake, umeokoa maisaha ya watoto waliozaliwa kabla ya 
 
muda na wenye uzito mdogo kwani huwapa joto, kusaidiwa maziwa kutiririka na pia huimarisha uhusiano wa mama na 
 
mtoto.
 
Pia ukaribu wa kugusana kimwili husababishwa mwili kuzalisha zaidi kichocheo (homoni) cha oxtixini, kichocheo hiki kinasaidia maziwa kutiririka na kumpa utulivu mama.
 
KUNYONYESHA KUNAKUEPUSHA NA MARADHI.
 
Tafiti zinaonyesha kuwa kunyonyesha kunappunguza kupata magonjwa ya saratani ya matiti na vifuko vya mayai ya uzazi, kisukari cha aina ya pili na pia huondoa sonono baada ya kujifungua.
 
KUNYONYESHA NI NJIA YA UZAZI WA MPANGO.
 
Kunyonyesha ni moja ya njia ya uzazi wa mpango wa kiasili. Njia hii ya kunyonyesha ina uwezo wa kuzuia mimba kwa asilimia 98 katika miezi sita tangu kujifungua.
 
HUOKOA MUDA WAKO KAZINI.
 
Kunyonyesha kunamwepusha mtoto na maradhi ya mara kwa mara hivyo kunaokoa muda mwingi wa kumuuguza mtoto.
 
FAIDA KWA JAMII.
Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya watoto wangelinyonyeshwa kwa miezi sita bila kupewa vyakula vingine kungeweza kuzuia vifo vya watoto karibu 

1000 na kuokoa vifo hivi, hivyo kunajenga ustawi wa jamii na taifa la kesho.

0 comments:

Post a Comment