Sunday 20 April 2014
DAWA ZA KUJITIBU MARADHI YA SIKIO
i. Nyunyiza juisi ya Kitunguu saumu katika sikio linalouma
ii. Nenda Hospitali ukapigwe bomba ili maji na uchafu upate kutoka
iii. Pasha moto mafuta ya Zaituni (Olive oil) na yasubiri yapowe na ujitie drops mbili hadi 3
iv. Na usafishe masikio yako kila baada ya kutoka kukoga.
KUTOKWA NA USAHA SIKIONI:
Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.
TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA:
Kanuni ya kwanza:
Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio lenye kuuma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.
Kanuni ya pili:
Dondoshea tone moja ya mafuta ya kitunguu saumu ndani ya sikio ambalo linauma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu..
Kanuni ya tatu:
Chukua mafuta ya habat soda na ufanye kama kanuni ya pili.
Kanuni ya nne:
Ikiwa maradhi ya sikio ni kwa ajili ya bacteria, kunywa antibayotiki asilia kama vile juisi ya Aloe vera, kitunguu saumu, n.k
0 comments:
Post a Comment