Monday, 30 June 2014

TAMBUA JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA





1. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.

2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia. 

3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation. Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive.

4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito.

5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.

6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu 'enjoyable' na sio tendo 'mechanical' kwa ajili ya kutafuta mtoto. Plan a romantic evening or try something different to spice things up. How you are feeling sexually may increase your chances of getting pregnancy. For women a better orgasm may help pull the sperms into the uterus and for men a better orgasm may increase their sperm count.

7.Kufanya mapenzi katika mtindo (style) ambayo itafanya mbegu za kiume zikae kwa muda mrefu ukeni na hivyo nyingi kupanda kuingia kwenye kizazi na kwenda kurutubisha yai. 'missionary position' ni nzuri zaidi, ambapo mwanaume anakuwa juu, epuka positions za mwanamke kuwa juu kwani hufanya mbegu zimwagike kwa gravity. Jaribu pia kuweka mto chini ya kiuno ili kukiinua na kufanya mbegu ziingie ndani kwa urahisi zaidi.

Kumbuka kuna asilimia 10 - 25 ya couples ambazo zina matatizo ya infertility lakini vipimo havionyeshi tatizo, inaweza kuwa namna ya kufanya mapenzi ndio ikawa shida, jaribu njia hizo 7 juu.

Kama hizi njia hazijakusaidia basi utakuwa na matatizo na unaweza kumuona daktari kwa msaada wa vipimo na matibabu.

Natumaini uzi huu unaweza kuwa msaada kwa watafutao watoto.

NAMNA YA KUDHIBITI MAUMIVU YA VIUNGO KIASILI ZAIDI



KATIKA  makala yaliyopita nilipokea simu nyingi kutoka kwa wazee, wakilalamika na kuomba msaada wa tiba ya kupambana na tatizo la kuumwa viungo vya mwili. Lakini katika siku za hivi karibuni, siyo wazee tu, bali hata vijana pia wanasumbuliwa na maumivu ya viungo.
Wazee:
Kundi hili linajumuisha watu wa kuanzia umri wa miaka 45 na kuendelea. Idadi kubwa ya wenye matatizo ya maumivu ya viungo, huwa wamepoteza ile nyama ya plastiki kama tuliyozoea kuitafuna juu ya mfupa wa paja la kuku ambayo hukaa katika maungio ya mifupa ya binadamu kama sponji linalo kinga mifupa kugusana na kusagika, hasa sehemu za mgongo, kiuno, magoti na vifundo. Kitaalamu nyama hii hujulikana kama ‘cartilage’.

Wajawazito na wenye vitambi    
Binadamu anapoumbwa hupewa mifupa kama fremu ya kumbeba kwa uzito uliokadiriwa kulingana na urefu wake na si vinginevyo. Tumewashuhudia akina mama wajawazito wakitembea kwa shida na hata kuanguka wakati mwingine kutokana na mifupa yao kushindwa kuubeba mzigo wa mtoto tumboni ambaye ni kama dharura kwa wakati huo.


Vivyo hivyo wenye vitambi nao hulalamika sana kuwa wanaumia sehemu za miguu, mgongo, nyayo na kiuno. Kitendo cha kuubadili mwili na kuwa na muonekano wa ‘V’, yaani juu kukubwa chini kudogo, huifanya mifupa kushindwa kuubeba uzito wako na kukufanya usikie maumivu sehemu hizo tajwa.
Maumivu haya pia huweza kuwakuta watu wengine bila kujali umri, wakiwemo wagonjwa mahututi, waliopatwa na ajali, n.k. Hata hivyo, wengi hupatwa na matatizo ya viungo kutokana na mwili kukosa lishe inayotakiwa kuufanya mwili ujiendeshe wenyewe.

Tiba asilia za maumivu haya
Tiba za maumivu haya zipo nyingi, lakini leo nitazitaja tatu:
Mdalasini: Chemsha mdalasini na maji glasi nane kisha yaache yapoe, kunywa kidogokidogo kwa kutwa moja. Rudia zoezi hilo kwa siku 10 mpaka 15 na ndani ya muda huo utabaini mabadiliko mazuri, utatakiwa kufanya hivyo kila mara unapohisi maumivu.

Muarobaini: Chuma na twanga majani ya muarobaini na uyakamue upate juisi yake robo ya glasi moja. Changanya juisi hiyo na maji ya kunywa glasi 7, kunywa kidogo kidogo mpaka yaishe kwa kutwa moja, kwa muda wa siku 10 mpaka 15.
EsteoEze Gold: Hii ni tibalishe maalumu ya vidonge (food supplement) ambayo ina ‘Glucosamine Sulphate’ na ‘Chondroitin Sulphate’ ambayo ukiitumia kwa mwezi mmoja kama ilivyo dozi yake, unaweza kupata nafuu ya muda mrefu. ‘Glucosamine’ imethibitishwa na matabibu duniani kote kuwa husaidia kujaza mapengo katika mifupa na ‘Chondroitin’ hufanya ripea katika maungio yaliyosagika, kuzuia maumivu na uvimbe.


Miongoni mwa virutubisho vingine vilivyomo kwenye tibalishe hii ni pamoja na vitamin C na Manganese kwa wingi ili kurahisiha uponyaji na kumfanya mgonjwa ajisikie nafuu kwa muda mfupi sana. Kwa maoni na ushauri usisite kuwasilina nasi kwa namba iliyopo hapo juu.

Sunday, 29 June 2014

STAFELI: LINA UWEZO WA AJABU WA KUTIBU MAGONJWA HATARI


MAPEMA wiki iliyopita, ilitawala habari ya tunda la stafeli kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa hatari, ukiwemo ugonjwa wa saratani. Hata hivyo, utafiti wa kwanza kuonesha uwezo wa stafeli kutibu saratani, uligundulika tangu miaka ya sabini, lakini ulifanywa siri hadi hivi karibuni ulipowekwa bayana tena.
Hivi sasa wakereketwa wa tiba mbadala na dunia kwa ujumla, wanafahamu kuwa stafeli lina virutubisho vyenye uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa ya saratani kushinda hata dawa za kisasa. Tunda hili linapatikana nchini kwa wingi, mjini na vijijini. Kwa lugha za kigeni linajulikana pia kama Soursop au Graviola.

VIRUTUBISHO VILIVYOMO
Kwa mujibu wa tafiti za kisayansi, stafeli limesheheni idadi kubwa ya virutubisho ambavyo ni: Amino Acid, Acetogenins, Vitamin C, Iron, Riboflavin, Phosphorus, Thiamine, Calcium, Carbohydrates, Niacin na Fibers na vingine vingi.

SARATANI NA STAFELI
Ingawa suala la stafeli peke yake kutibu saratani lina mjadala, lakini hakuna shaka kabisa kuwa lina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana au kupunguza makali ya saratani. Ukweli uliogundulika hivi karibuni, umewapa 

wagonjwa wa saratani njia nyingine mbadala ambayo haikuwepo hapo awali. Kwani hivi sasa wanaweza kulitumia stafeli kama dawa ya kupunguza makali au kuwapa kinga dhidi ya saratani na wanaweza pia kuitumia pamoja na matibabu wanayopewa ya mionzi na kupata ahueni kubwa.
USHAHIDI WA KIMAABARA
Zaidi ya majaribio 20 ya kimaabara yaliyofanywa kuhusu uwezo wa stafeli, yamebaini haya yafuatayo:


Stafeli huua chembechembe za saratani (cancerous cells) aina 12, ikiwemo saratani ya matiti, mapafu, kongosho, kibofu na tumbo.
Stafeli lina mchanganyiko wenye uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa seli za saratani mara 10,000 zaidi ya dawa ya ‘Adriamycin’ ambayo ndiyo hutumika kutibu aina mbalimbali ya saratani.


Mchanganyiko wa virutubisho vya ‘Annonaceous’ ‘Acetogenins’ vilivyomo kwenye stafeli huua seli (cells) zilizoathirika tu na saratani, tofauti na dawa za kisasa ambazo zenyewe huua seli zilizoathirika na hata zisizoathirika.


Stafeli hudhibiti ukuaji wa seli za saratani bila kusababisha madhara mengine kama ilivyo kwa dawa za kisasa, ambazo wakati mgonjwa anapozitumia, iwe zile za njia ya mionzi, sindano au vidonge, huwa zina athari mbaya kwa mtumiaji na wakati mwingine huweza kumsababishia matatizo mengine ya kiafya.
UMUHIMU WA STAFELI KWA WANAOTUMIA TIBA YA KISASA
Mgonjwa wa saratani anayetumia tiba ya hospitali anashauriwa pia kula sana stafeli kwani lenyewe husaidia kupunguza makali ya dawa anazotumia.




KWA mfano baadhi ya dawa za hospitali huathiri njia ya chakula na kumsababishia mgonjwa ukosefu wa choo kwa muda mrefu, lakini stafeli likitumika hurekebisha hali hiyo na kumsaidia mgonjwa kupata choo kama kawaida.
Vilevile, baadhi ya dawa za hospitali za saratani hudhoofisha kinga ya mwili, lakini virutubisho vilivyomo kwenye stafeli, hasa vitamin C, huzifanya kinga kuwa imara na hivyo kuziimarisha hivyo kumuepusha mtu kupatwa na maambukizi mengine, kama ya njia ya mkojo, mafua na kikohozi cha mara kwa mara.

FAIDA ZINGINE ZA STAFELI NI KAMA ZIFUATAVYO:
Hutoa nafuu ya kipanda uso.
Kirutubisho aina ya Riboflavin kilichomo kwenye stafeli, husadia kutoa nafuu kwa ugonjwa wa kichwa cha kipanda usoni.

HUZUIA UGONJWA WA ANEMIA
Madini ya chuma (iron) yaliyomo kwenye stafeli, hufaa sana katika kuzuia ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia).

HUTIBU MAGONJWA YA INI
Juisi ya stafeli inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu matatizo ya kwenye ini na uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.

HUIMARISHA MIFUPA
Stafeli ni chanzo kizuri pia cha madini ya kopa (copper) na kashiamu (calcium), virutubisho ambavyo huwa muhimu kwa ukuaji wa mifupa mwilini.
Matatizo mengine yanayoweza kudhibitiwa na stafeli ni pamoja na kuumwa miguu, maumivu kwenye ‘joints’, mwili kukosa nguvu na matatizo mengine ya viungo.

MAJANI, MIZIZI, MAGAMBA NAYO NI DAWA
Mbali ya tunda lenyewe kuwa na faida lukuki kama zilivyoanishwa hapo juu, vilivyomo vingine kwenye mti huo kama vile mizizi, majani na magamba yake ni dawa ya magonjwa mbalimbali:
Unywaji wa maji yaliyotengenezwa kutokana na majani ya mstafeli hutibu magonjwa ya ngozi, chunusi na uvimbe wa mwili.
Maji ya majani ya mstafeli pia hutibu ugonjwa wa kuhara, kukohoa, kuvimba miguu, mapunye kichwani. Aidha, maji ya majani ya mstafeli yamethibitika kushusha kiwango cha sukari mwilini.

TAHADHARI
Inaelezwa kwamba stafeli linaweza kuwa siyo salama kwa wajawazito, wagonjwa wa presha ya kupanda au kushuka (hypotension or hypertension), hivyo wanashauriwa kabla ya kula, wapate ushauri wa daktari kwanza.

USHAURI
Kwa asili yake, stafeli lina kiasi kingi cha virutubisho vinavyoua bakteria, hivyo ulaji wa muda mrefu wa tunda hili kunaweza kuua bakteria wote tumboni hata wale wazuri, hivyo iwapo utalila tunda hili kwa zaidi siku 30 mfululizo, unashauriwa pia kuongezea na dawa za kulainisha njia ya chakula.

JINSI YA KULITUMIA STAFELI
Stafeli linaweza kuliwa katika aina tofauti. Kama unataka kupata faida zake zote, unaweza kulila lililoiva kama lilivyo au unaweza kutengeneza juisi yake. Unywaji wa maji yatokanayo na majani, mizizi au magamba yake, unaweza kunywa kama chai au kinywaji kingine cha kawaida.

TIBA YA MARADHI YA KUHARISHA



MARADHI YA KUHARISHA:
MARADHI ya kuharisha ni maradhi ambayo mgonjwa hupata haja kubwa mara kwa mara na haja kubwa huwa laini na wakati mwingine huambatana na gesi au maumivu. 
SABABU ZAKE: 
(1) Kula chakula kichafu. 
2) Kula chakula kilichoingia viini vya maradhi.

TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua kijiko kimoja cha Maua ya babu naji (chamomile) ukoroge ndani ya kikombe cha chai na maji ya moto. Yakishapoa unywe bila ya kuongeza sukari.Fanya hivyo kutwa mara tatu. Ndani ya babunaji mna virutubisho vyenye uwezo wa kusitisha kuharisha.
Kanuni ya pili: Chukua anisuni (aniseed) kijiko kimoja kidogo uweke ndani ya kikombe kimoja cha chai cha maji ya moto yaliyochemka kisha ukoroge. Wacha dawa ikae ndani ya maji dakika tano kisha uchuje halafu uongeze asali kijiko kimoja. unywa kikombe kimoja kutwa mara mbili. Zaidi ya hayo, tukuweke wazi tu kuwa, dawa hii pia huvipa nguvu jamii ya viungo vya kulia chakula.
Kanuni ya tatu: Chukua majani ya nanaa (Mint)na utayarishe dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu anisuni.
Kanuni ya nne: Chukua zaatar na uandae dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu majani ya nanaa na anisuni
Kanuni ya tano: Changanya kijiko kimoja cha mafuta ya habat soda ndani ya glasi moja ya maziwa ya mtindi unywe glasi moja kutwa mara mbili.

TATIZO LA UUME KUSINYAA




TATIZO LA UUME KUSINYAA

Mwanaume anayepatwa na tatizo hili anapokuja kujigundua huona kama mabadiliko makubwa yaliyotokea ghafla katika viungo vyake vya siri. Mwanamke mwenye tatizo hili pia naye huona kama tatizo geni linaloanza ghafla. 

Kwa kawaida hali hii hutokea katika umri mkubwa kwa mwanaume na mwanamke yaani kuanzia umri wa miaka hamsini lakini ikitokea katika umri chini ya miaka hamsini basi ni tatizo. Wapo vijana wenye matatizo haya ambayo vyanzo vyake tutakuja kuviona katika safu hii.

CHANZO CHA TATIZO
Hali ya kusinyaa kwa viungo vya uzazi kwa mwanamke na mwanaume hutokana na kuwepo kwa msukumo hafifu wa damu sehemu hiyo, maambukizi sehemu za siri ambayo huwa ya muda mrefu hasa kaswende, hitilafu katika misuli ya uke na sehemu za siri za mwanaume inayoathiriwa na kaswende virusi vya HIV, ugonjwa wa kifua kikuu na hata baadhi ya magonjwa sugu ya ngozi. Matatizo mengine yanayochangia hali hii ni ugonjwa wa kisukari.

Matatizo katika mishipa ya damu vilevile huweza kusababishwa na magonjwa ya moyo au mishipa ya damu inayosambaa sehemu hizo. Misuli inaposinyaa kwa mwanamke nayo huweza kusababishwa na magonjwa kama tulivyoona, uke unasinyaa pia huweza kusababishwa na uzazi wa mara kwa mara na karibu kufanya ngono mara kwa mara na wanaume tofauti na hitilafu katika mfumo wa homoni. 

Mwanamke anapata tatizo hili la kusinyaa uke endapo pia homoni au kichocheo cha Estrogen' kitakuwa kimepungua mwilini na kufanya mafuta yapungue ukeni. Kwa upande wa mwanaume homoni inayopungua kwa mwanaume ni Testosterone.

DALILI ZA TATIZO
Mwanaume mwenye tatizo hili hasa kijana, ingawa kwa wazee ni hali ya kawaida, kijana huanza kuona mfuko wa pumbu hulegea na kushuka sana, usinyaa na kujikunja kunja, kokwa huinekana ndogo na mishipa mikubwa ya damu huanza kujitokeza na mishipa mbegu toka katika kende huonekana wazi. Uume huwa kama wa mtoto mdogo na mishipa ya damu huchomoza wazi. Nguvu za kiume hupungua sana na endapo ukiweza tendo la ndoa la kwanza unawahi kumaliza na kushindwa kabisa kupata tendo la pili.

Mara kwa mara maandalizi kabla ya tendo la ndoa kwa mwanaume mwenye tatizo hili ni kuchezea sana uume kwa kuurusharusha au kuupiga piga kidogo kidogo ili kuamsha au kuhamasisha msukumo wa damu. Baada ya hapo uume huanza kusimama taratibu na endapo utasimama basi inabidi uwahi tendo na kama utachelewa, basi uume utalala na kushindwa tena kufanya tendo kwa siku hiyo. 

Mwanamke yeye daima huwa mkavu na wakati wa tendo hapati hisia zozote hadi tendo linapokwisha na kama mwanaume hana tatizo lolote na mwenye nguvu za kutosha basi mwanamke atapata michubuko na maumivu na kuhisi karaha ya tendo na hawezi kufika kileleni.

UCHUNGUZI
Tatizo hili kama tulivyoona husababishwa na magonjwa mbalimbali, pia yapo matatizo na magonjwa mengine yanyochangia hali hii, magonjwa kama kisukari, endapo ugonjwa utakuwa wa muda mrefu unaweza kuathiri hali hii. 

Tabia ya kujichua kwa mwanaume na mwanamke pia huweza kuathiri au kusababisha tatizo hili kama mtu atakuwa amejichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani msukumo wa damu sehemu za viungo vya uzazi utakuwa umeathiriwa.

Viungo vya uzazi vinaweza kupooza kutokana na hitilafu katika mishipa ya fahamu. Mishipa ya fahamu inapoathirika viungo hupooza (paralysis of genitalia) na mwanaume kushindwa kabisa kufanya tendo la ndoa na ukeni hakuna kabisa mawasiliano yanayoleta msisimko.

Vipimo vya damu na mkojo na vingine ambavyo daktari ataona vinafaa vitafanyika.

MATIBABU NA USHAURI
Tiba hutolewa kadiri daktari atakavyoona inafaa. Matibabu hutolewa katika kliniki za matatizo au magonjwa ya kinamama ambapo na kina baba hutibiwa matatizo haya. 

Baada ya uchunguzi tiba itatolea kuona kama hitilafu ni maambukizo au katika mfumo wa homoni. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba zaidi.

TIBA YA MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):




MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):
Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na
hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa. Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.
SABABU ZA MARADHI HUSIKA: (1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. (2) Maradhi ndani ya utumbo mpana. (3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano. (4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. (5) Kutokunywa maji ya kutosha. (6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. (7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo. 


TIBA: Kanuni ya kwanza:
Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.
Kanuni ya pili: Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asalirobo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.
Kanuni ya tatu: Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili. 
Kanuni ya nne: Kunywa kwa wingi maji ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.
Kanuni ya tano: Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini. 


MARADHI YANAYOMSIBU BINAADAMU NA TIBA YAKE: MARADHI YA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA (NAUSEA)




Maradhi ya KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Hali ya kujisikia kuwa unataka kutapika lakini hutapiki inaitwa kichefuchefu (Nausea). Hali hii ni kawaida sana hasa wakati unaposafiri kwa chombo kama meli au ndege, hali ya
ujauzito,kupata harufu mbaya, kuona au kuhisi kinyaa baada ya kuona kitu au chakula Fulani kibaya chenye ladha na harufu mbaya, wengine hupata kichefuchefu akimuona mtu mwengine akitapika. Hali ya kichefuchefu humsababishia mtu kuweza kutapika wakati mwingine.
TIBA: Chukua kijiko kimoja kidogo cha unga wa pilipili manga ukoroge ndani ya glasi moja ya maji halafu ukamulie ndani yake ndimu nusu. Kunywa glasi moja kutwa mara tatu.


MARADHI YANAYOMSIBU BINAADAMU NA TIBA YAKE: KUTIBU MARADHI YA GESI TUMBONI (COLIC)



GESI TUMBONI (COLIC): I
kiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya
kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.
TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.


MATIBABU YA MARADHI YA BAWASIRI




Kutibu Maradhi ya BAWASIRI (MGORO): 
Haya ni maradhi ambayo humsibu mgonjwa sehemu ya haja kubwa ambayo humsababisha kupata maumivu. 
DALILI ZAKE
(1) Kupata choo kigumu. 
(2) Kutokwa damu sehemu ya haja kubwa baada ya kujisaidia. 
(3) Muwasho au maumivu na joto kali sehemu ya bawasiri. 
(4) Kupata maumivu wakati unapokaa. 
(5) Vidonda au kutokwa nje na kijinyama sehemu ya kutokea haja kubwa.
 (6) Upungufu wa nguvu za kiume.



TIBA: Jambo la kwanza kabla ya tiba mgonjwa aweze kutibiwa maradhi ya kutopata choo vizuri ikiwa anayo kwa sababu huzidisha maradhi haya. Pia epuka kula Nyama hasa ya ngombe, Pilipili na vitu vikali. Halkadhalika usinywe maziwa kwa wingi.
Kanuni ya kwanza: Kunywa juisi ya tikiti maji asubuhi kabla ya chakula na usiku kabla ya kulala.Dawa hii hutibu na kuondoa maumivu ya bawasiri.

Kanuni ya pili: Chukua asali nusu lita , unga wa kamun aswad vijiko vitatu vikubwa,unga wa Habat soda vijiko vitatu vikubwa na unga wa kamun abyadh vijiko viwili vikubwa. Vitu vyote hivi vichanganye pamoja kwa kuvikoroga kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu kisha ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje halafu unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Ikiwa ni bawasiri ya kutoka nje au yenye vidonda, paka mafuta ya nyonyo au mafuta ya lozi.


MARADHI YANAYOMSIBU BINAADAMU NA TIBA YAKE: MARADHI YA VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS)





Maradhi ya VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS): Haya ni maradhi ambayo hufanya vidonda upande wa ndani ya ukuta wa tumbo. Kuna Duodenal ulcer na Gastric ulcer.
DALILI: (1) Kupata maumivu makali chini ya kifua kwa

upande wa ndani. (2) Kuchoka bila sababu. (3) Kuumwa kwa mgongo au kiuno. (4) Kupungua kwa nguvu za kiume. (5) Kuwa na kichefuchefu baadhi ya wakati. (6) Kuwa na kiungulia . (7) Tumbo kujaa gesi. (8) Tumbo kuwaka moto. (9) Kukosa choo na wakati mwingine kupata choo kigumu kama cha mbuzi. (10) Kukosa hamu ya kula. (11) Kutapika damu au wakati mwingine kutapika nyongo. (12) Maumivu makali baada ya kula vitu vikali au chakula cha moto.



TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua asali robo lita uchanganye na unga wa arki susi vijiko vinne vikubwa kisha ukoroge kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu.
Kanuni ya pili: Chukua viazi vya mviringo (vya chipsi) kama vitatu halafu uvikoshe na kuvimenya. Baada ya kuvimenya upate juisi yake kwa kuvisaga kwenye blenda. Kunywa vijiko vitatu vikubwa vya chakula kutwa mara mbili. 
Kanuni ya tatu: Chukua lozi gramu 30 halafu usage iwe unga.
Changanya lozi hii yote ndani ya kikombe kidogo cha maziwa ya moto kisha uongeze asali vijiko viwili vikubwa. Kunywa kikombe kimoja robo saa kabla ya kula chakula cha asubuhi. Fanya hivyo kwa muda wa mwezi na utapata shifaa.


MARADHI YANAYOMSIBU BINAADAMU NA TIBA YAKE: MATIBABU YA MATATIZO YA HEDHI



MATATIZO YA HEDHI: Matatizo ya Hedhi
Matatizo ya Hedhi yanawagusa moja kwa moja wanawake, tena yako katika aina na namna tofauti; hata hivyo nayo yana tiba yake inayolingana na aina ya tatizo husika.

TIBA YA HEDHI ILIYOFUNGA (AMENERRHOEA): Kanuni ya kwanza: Tafuna ufuta kiasi cha kijiko kimoja kila siku mara tatu. Fanya hivyo hadi upate hedhi. Ni bora zaidi kula ufuta kabla ya zile siku ambazo hedhi hutoka na uendelee wakati inapotoka hedhi. Dawa hii ni hatari kwa mwanamke mja mzito, hivyo atahadhari nayo,na tangu hapoyeye haimuhusu. Kanuni ya pili: Chukua Harmal gramu 50, uchemshe ndani ya
maji lita moja. Ikishapoa uichuje. Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara mbili kwa muda wa siku tatu.

TIBA YA HEDHI ISIYOTOKA VIZURI: Chukua Jirjir (rocket) kijiko kimoja ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje.Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara tatu.

TIBA YA HEDHI INAYOTOKA KWA WINGI ZAIDI YA ADA: Kanuni ya kwanza: Chukua kijiko kimoja cha maua ya Babunaji (Chamomile) ukoroge ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto. Yakishapoa, unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu kabla ya kula.
Kanuni ya pili: Chukua zaatar kijiko kimoja kikubwa cha chakula ukoroge ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto. Kunywa kikombe cha chai kutwa mara tatu.
TIBA YA MAUMIVU YA HEDHI YANAYOTOKA KIDOGOKIDOGO (DYSMENORRHOEA): Kanuni ya kwanza: Chukua nanaa na utayarishe mfano wa chai Kunywa kikombe kimoja cha chai kutwa mara tatu
Kanuni ya pili: Chukua mvuje wa kidonge (kidonge kimoja ) na unga wa pilipili manga gramu 50. Weka dawa hizi mbili ndani ya glasi moja ya maji kisha uifunike na uiache ilowane. Bila ya kuchuja kunywa kijiko kimoja kikubwa kutwa mara moja .Rudia tena kunywa siku ya pili ikiwa hujapata mabadiliko.Dawa hii huzibua hedhi iliyoganda au kufunga.
TIBA YA HEDHI INAYOCHELEWA KUTOKA KWA SIKU ZAKE AU KUTOKA KABLA YA SIKU ZAKE KUFIKA: Hapa maana yake ni kuwa baina ya hedhi mbili huenda yakakaribiana sana au kuachana sana kinyume na ada. Yaani siku za tarehe zake haziendi sawa Chukua bakdonise (parsley) gramu 50 kisha uweke ndani ya maji lita moja, ichemshe kwa muda wa dakika tano na ikishapoa uchuje. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili.

MWANAMUME KUWAHI KUMALIZA ANAPOFANYA TENDO LA KUJAMIANA..................!!!!!




Kutoka mbegu za kiume muda mfupi baada ya kumwingilia mwanamke huitwapremature ejaculation. Huu ni udhaifu wa kawaida kwa wanaume walio wengi kwa ujumla wake, ikiwa ni pamoja na vijana. Mtaalamu Ira Sharlip anasema katika utafiti wake kuwa, ni kiasi cha asilimia 20 hadi 30 ya wanaume wa rika zote ambao wana matatizo haya.

Njia za kitabibu za kuweza kumtambua mtu mwenye udhaifu huu inaitwa Intravaginalejaculatory latency time (IELT). Hata hivyo, mtaalamu Ira Sharlip anaongeza kwa kusema kwamba, utaratibu huu hausaidii sana kumjua mtu mwenyepremature ejaculation. Kuna wanaume ambao wanamaliza katika dakika moja tu baada ya kumwingilia mwanamke na wao hudai kwamba, hawana matatizo.

Na halafu upande mwingine, kuna wanaume ambao wanaweza kuchukua dakika 20 bila kutoa mbegu baada ya kumwingilia mwanamke. Hawa nao ni wagonjwa, kwani muda huo ni mkubwa kuliko wastani. Kwa maana nyingine ni kwamba, maana ya nenopremature, zaidi zaidi liko katika mtazamo wa mhusika mwenyewe. Inategemea na mtu mwenyewe anavyotosheka kimapenzi na uwezo wake wa kujidhibiti muda wa kumaliza unapokuwa umewadia.

Utafiti wa mwaka 2010 katika jarida la Journal of Sexual Medicine uliona kwamba, kipimo kizuri cha premature ejaculation ni dakika 5.4. Yaani mtu akitoa mbegu baada ya dakika pungufu ya hizo, tangu amwingilie mwanamke basi ana ugonjwa huu wapremature ejaculation.

Lakini Ian Kerner anasema kipimo ni dakika mbili. Yaani mwanaume akimaliza haja yake kabla ya dakika mbili, basi ana ugonjwa huo. Anaongeza kwamba, watu wengi anaokabiliana nao ni wale ambao wanatumia muda mfupi chini ya dakika mbili kumaliza haja zao. Wengine hutumia sekunde 30 tu!

Pia hata sababu za nje zinaweza kuchangia kumfanya mwanaume akawa na tatizo hili. Mtu mwenye mawazo mengi ni rahisi kukumbwa na tatizo hili. Mtu mwenye mawazo mengi anamaliza haraka mara baada ya kumwingilia mwanamke, kwa mujibu wa mtaalamu Kerner.

Lakini kumaliza kwa namna hii pia kuna uzuri wake kwamba, tumejaza dunia kwa kuwa na watu wengi. Kama watu wangekuwa wanachukua saa nzima kumaliza baada ya kumwingilia mwanamke, dunia ingekuwa na uadimu wa watu!

Washauri nasaha wanaojihusisha na ushauri wa kimapenzi na matibabu wanatoa tiba mbalimbali kwa ajili ya watu wenye wasiwasi; wasiwasi ambao huwafanya wawe wanamaliza haraka sana baada ya kumwingilia mwanamke.

Kuna dawa ambayo mgonjwa akipewa zinamsaidia kurefusha muda wa kuendelea na tendo, baada ya kumwingilia mwanamke. Dawa hizo ni kama zile za kupooza msongo wa mawazo. Pia kuna mazoezi ambayo yanashauriwa kufanywa. Mazoezi haya humsaidia mtu kujenga upya mkabala wa namna anavyochukulia tendo.

Kwa wale wakazi wa Dar wanaweza kutembelea ofisi zetu za Faji zilizoko Tabata Kimanga ambapo tunatoa tiba ya tatizo hili pamoja na matatizo mengine yanayohitaji ushauri wa kisaikolojia na yale ya tiba yatilifu (Tiba mbadala).

Lakini pia njia iliyo rahisi zaidi ili kutokuwa mwepesi wa kumaliza haraka ni kujizoeza kuacha kulifikiria tendo hilo la ngono unapokaribia kufikia kileleni (kwa kufanya pole pole zaidi au kufikiria mambo mengine ya nje kama ya mpira, mfano Yanga na Simba au Manchester na Chelsea). Jenga mazoea kufanya namna hiyo. Ukizoea itakuwa ni kama kitu cha kawaida kwa kujikaza kisabuni na kuhakikisha unamsubiri mwenzio ili mwende pamoja kileleni.

Kila kitu ni kujifunza. Ukijizoeza kujikakamua bila kumaliza hata katika hali ya ham ya juu kwa kumsubiri mpenzi wako, tatizo la premature ejaculation litakuwa limethibitiwa. Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu Prosterman

Saturday, 28 June 2014

SIRI YA KUONDOA MARADHI YA KOLESTRO MWILINI




KWA kuzingatia kwamba wenye lehemu nyingi mwilini (Bad High Cholestol) huwa katika hatari zaidi ya kupatwa na magonjwa ya moyo, ikiwemo kupooza (stroke), suala la kuhakikisha mwili wako unakuwa na kiwango cha mafuta kinachotakiwa ni la lazima.
Siri ya kujiepusha na magonjwa hayo iko kwenye chakula, hususan mboga na matunda, ambayo nimeyaorodhesha katika makala haya ya leo, kama ifuatavyo:

CHAI YA KIJANI (GREEN TEA)
Ingawa hata chai nyeusi nayo inavyo virutubisho vyenye uwezo wa kupunguza kolestro mwilini, lakini chai ya kijani ndiyo yenye nguvu zaidi. Chai ya kijani huwa haipitii mchakato wa moto ambao hupunguza nguvu nyingi za virutubisho kama ilivyo kwa chai nyeusi.

Kwa mujibu wa watafiti, kwa kuwa chai ya kijani haipitii mchakato wa moto, hubaki na kiwango kingi cha kirutubisho chenye uwezo wa kushusha lehemu mwilini, kirutubisho hicho kinajulikana kama Catechins.
MAHARAGE (Beans)
Utashangaa lakini ndiyo ukweli wenyewe! Maharage haya haya ambayo baadhi huwa hawapendi kabisa kuyala na hata wanapoyala huonekana kama ni kwa sababu ya shida.

Aina zote za maharage zimeonekana kuwa na kiwango kingi cha kamba lishe (fibre) ambayo husaidia kuondoa kolestro na sumu zingine mwilini wakati wa kwenda haja kubwa. Hivyo maharage nayo ni sehemu ya chakula muhimu kwa moyo wa binadamu.

KARANGA (Nuts)
Kama ulikuwa siyo mpenzi sana wa kula karanga, korosho na jamii nyingine za karanga, basi unatakiwa kujiangalia upya, kwani vitafunwa hivi vina virutubisho vya kutosha vya kuzuia na kuondoa mafuta mabaya mwilini. Kiasi cha kiganja kimoja cha karanga kwa siku kinatosha, hasa karanga mbichi.

PARACHICHI (Avacado)
Ingawa kwa kawaida yanaonekana kama yana mafuta, lakini maparachichi yana kirutubisho aina ya Oleic Acid, ambacho siyo tu huondoa mafuta mabaya mwilini (LDL), bali huyaboresha mafuta mazuri yanayotakiwa mwilini.

Si hayo tu, maparachichi yana kamba lishe za kutosha ambazo husaidia usagaji wa chakula na uimarishaji wa kiwango cha kolestro mwilini.

PEASI (Pears)
Kama msemo maarufu wa Kiingereza usemao, An Apple a Day, keeps the doctor away (Epo moja kwa siku, humuweka daktari mbali), kwa peasi ni zaidi ya epo. Mapeasi yana uwezo mkubwa sana wa kushusha kolestro mwilini kushinda hata epo. Ili kupata faida zake zote, inashauriwa kulila peasi pamoja na maganda yake.

Halikadhalika matunda mengine kama vile machungwa, ndizi mbivu na nyanya za mboga, vina uwezo mkubwa wa kushusha na kuondoa mafuta mabaya (bad cholestrol) mwilini ambayo ndiyo huwa chanzo cha matatizo makubwa ya moyo na kiharusi.

Kama unajali afya yako, hakikisha unakula matunda hayo kila siku au kila msimu ili kujilinda dhidi ya magonjwa ya moyo na athari zake. Kwa lolote, usisite kuwasiliana nasi kwa namba zilizopo hapo juu.

MADHARA YA UNENE KWA WAJAWAZITO NA WATOTO




Unapaswa kujua kuwa, wanawake wenye uzito wa kupitiliza (obese women) wakiwa wajawazito wanakabiliwa na hatari ya kupata madhara makubwa.

Madhara hayo ni kama haya yafuatayo, kupata ugonjwa wa kisukari cha ujauzito ambacho ni hatari kwa maisha yake.


Mjamzito pia anaweza kupata matatizo ya shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba ambacho ni hatari sana kama kinamtokea wakati wa kujifungua. Vilevile wajawazito wanene kupindukia wanaweza kupata tatizo la kujifungua kwa njia ya upasuaji kitabibu huitwa Caesarean section.

Lakini pia mjamzito mnene kupindukia anaweza kupatwa na tatizo la mtoto aliye tumboni kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito, kitaalamu huitwa Fetal distress. 

Matatizo ya unene kwa watoto
Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), inatahadharisha juu ya unene wa kupindukia kwa watoto. Wamesema kwamba watajaribu kupunguza kutumiwa vyakula holela (junk food) kwa kupiga marufuku matangazo ya vyakula hivyo katika vyombo vya habari na kwa kutumia mabango mitaani na mawaziri wa afya wa nchi mbalimbali wamepewa angalizo hilo.

Viwanda vya vyakula na vinywaji vimetakiwa kuongeza udhibiti wa aina zote za mauzo ya vyakula kwa watoto na wauzaji vyakula vya watoto wadogo pia wametakiwa kuacha kuzalisha na kuuza vyakula ambavyo si vizuri kwa afya ya watoto.

WHO imesema kwamba, unene wa kupindukia kwa watoto unaongezeka duniani kote. Shirika hilo limeshauri kwamba, wazazi wanapasa kupunguza muda wa watoto wao kutazama televisheni.
Limeshauri pia watoto kubanwa kutumia vyakula holela na vinywaji vyenye sukari nyingi mashuleni na sehemu za michezo ya watoto, hili walimu wanapaswa kulizingatia. 
USHAURI
Watoto waepuke kula vyakula vyenye sukari nyingi na vyenye mafuta mengi na ni vema kwa wajawazito kufanya mazoezi na kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi.