Monday, 30 June 2014

NAMNA YA KUDHIBITI MAUMIVU YA VIUNGO KIASILI ZAIDI



KATIKA  makala yaliyopita nilipokea simu nyingi kutoka kwa wazee, wakilalamika na kuomba msaada wa tiba ya kupambana na tatizo la kuumwa viungo vya mwili. Lakini katika siku za hivi karibuni, siyo wazee tu, bali hata vijana pia wanasumbuliwa na maumivu ya viungo.
Wazee:
Kundi hili linajumuisha watu wa kuanzia umri wa miaka 45 na kuendelea. Idadi kubwa ya wenye matatizo ya maumivu ya viungo, huwa wamepoteza ile nyama ya plastiki kama tuliyozoea kuitafuna juu ya mfupa wa paja la kuku ambayo hukaa katika maungio ya mifupa ya binadamu kama sponji linalo kinga mifupa kugusana na kusagika, hasa sehemu za mgongo, kiuno, magoti na vifundo. Kitaalamu nyama hii hujulikana kama ‘cartilage’.

Wajawazito na wenye vitambi    
Binadamu anapoumbwa hupewa mifupa kama fremu ya kumbeba kwa uzito uliokadiriwa kulingana na urefu wake na si vinginevyo. Tumewashuhudia akina mama wajawazito wakitembea kwa shida na hata kuanguka wakati mwingine kutokana na mifupa yao kushindwa kuubeba mzigo wa mtoto tumboni ambaye ni kama dharura kwa wakati huo.


Vivyo hivyo wenye vitambi nao hulalamika sana kuwa wanaumia sehemu za miguu, mgongo, nyayo na kiuno. Kitendo cha kuubadili mwili na kuwa na muonekano wa ‘V’, yaani juu kukubwa chini kudogo, huifanya mifupa kushindwa kuubeba uzito wako na kukufanya usikie maumivu sehemu hizo tajwa.
Maumivu haya pia huweza kuwakuta watu wengine bila kujali umri, wakiwemo wagonjwa mahututi, waliopatwa na ajali, n.k. Hata hivyo, wengi hupatwa na matatizo ya viungo kutokana na mwili kukosa lishe inayotakiwa kuufanya mwili ujiendeshe wenyewe.

Tiba asilia za maumivu haya
Tiba za maumivu haya zipo nyingi, lakini leo nitazitaja tatu:
Mdalasini: Chemsha mdalasini na maji glasi nane kisha yaache yapoe, kunywa kidogokidogo kwa kutwa moja. Rudia zoezi hilo kwa siku 10 mpaka 15 na ndani ya muda huo utabaini mabadiliko mazuri, utatakiwa kufanya hivyo kila mara unapohisi maumivu.

Muarobaini: Chuma na twanga majani ya muarobaini na uyakamue upate juisi yake robo ya glasi moja. Changanya juisi hiyo na maji ya kunywa glasi 7, kunywa kidogo kidogo mpaka yaishe kwa kutwa moja, kwa muda wa siku 10 mpaka 15.
EsteoEze Gold: Hii ni tibalishe maalumu ya vidonge (food supplement) ambayo ina ‘Glucosamine Sulphate’ na ‘Chondroitin Sulphate’ ambayo ukiitumia kwa mwezi mmoja kama ilivyo dozi yake, unaweza kupata nafuu ya muda mrefu. ‘Glucosamine’ imethibitishwa na matabibu duniani kote kuwa husaidia kujaza mapengo katika mifupa na ‘Chondroitin’ hufanya ripea katika maungio yaliyosagika, kuzuia maumivu na uvimbe.


Miongoni mwa virutubisho vingine vilivyomo kwenye tibalishe hii ni pamoja na vitamin C na Manganese kwa wingi ili kurahisiha uponyaji na kumfanya mgonjwa ajisikie nafuu kwa muda mfupi sana. Kwa maoni na ushauri usisite kuwasilina nasi kwa namba iliyopo hapo juu.

0 comments:

Post a Comment