MARADHI YA KUHARISHA:
MARADHI ya kuharisha ni maradhi ambayo mgonjwa hupata haja kubwa mara kwa mara na haja kubwa huwa laini na wakati mwingine huambatana na gesi au maumivu.
SABABU ZAKE:
(1) Kula chakula kichafu.
2) Kula chakula kilichoingia viini vya maradhi.
TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua kijiko kimoja cha Maua ya babu naji (chamomile) ukoroge ndani ya kikombe cha chai na maji ya moto. Yakishapoa unywe bila ya kuongeza sukari.Fanya hivyo kutwa mara tatu. Ndani ya babunaji mna virutubisho vyenye uwezo wa kusitisha kuharisha.
Kanuni ya pili: Chukua anisuni (aniseed) kijiko kimoja kidogo uweke ndani ya kikombe kimoja cha chai cha maji ya moto yaliyochemka kisha ukoroge. Wacha dawa ikae ndani ya maji dakika tano kisha uchuje halafu uongeze asali kijiko kimoja. unywa kikombe kimoja kutwa mara mbili. Zaidi ya hayo, tukuweke wazi tu kuwa, dawa hii pia huvipa nguvu jamii ya viungo vya kulia chakula.
Kanuni ya tatu: Chukua majani ya nanaa (Mint)na utayarishe dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu anisuni.
Kanuni ya nne: Chukua zaatar na uandae dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu majani ya nanaa na anisuni
Kanuni ya tano: Changanya kijiko kimoja cha mafuta ya habat soda ndani ya glasi moja ya maziwa ya mtindi unywe glasi moja kutwa mara mbili.
0 comments:
Post a Comment