Sunday, 20 April 2014

FAIDA YA JUISI YA UKWAJU






Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.

NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU.
  • Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets
  • Andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu   baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni  uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu 
  • Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe  andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe 
  • Weka sukari kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.

FAIDA YA JUISI YA UKWAJU.
  • Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  • Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  • Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  • Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  • Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  • Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  • Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  • Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  • Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  • Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)



Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!




Unatakiwa ujaribu kuweka
ukwaju karibu katika kila mlo
wako kwa kila siku kwasababu
ukwaju una faida nyingi kiafya
ambazo hakika zitakufanya uwe
na afya njema au kukuimarisha
afya yako kiujumla

Watu waishio bara la Asia,
Carribian na America ya kusini
wanajua kuwa kula ukwaju
maana yake ni Afya Njema.


Ukwaju unaoliwaa katika maeneo
haya maeneo hayo una faida
nyingi kwa watu wanaoula.

Kwa hiyo siku nyingine unapoenda
kufanya manunuzi ya vyakula
hakikisha unanunua na ukwaju.
Ukwaju ni zao la rangi ya kahawia
ambalo limefungwa na kasha
gumu. Ndani ya kasha hilo kuna
vifundo vilaini ambavyo ndani
yake kuna mbegu nyeusi.
Vifundo
hivi ndiyo ambavyo watu
wanakula ili kupata virutubisho na
faida za kiafya za ukwaju. Ukwaju
una ladha faluni ya uchachu
ukiwa bado mchanga, lakini kadiri
unavyozidi kukomaa unakuwa na
ladha tamu. Ingawa ukwaju
unakuwa na utamu kadiri
unavyokuwa na kukomaa,
kiujumla ukwaju ni mchachu.

Katika nchi kama Jamaica, Mexico,
Aruba na India, ukwaju
unachanganjwa na sukari na
kuuzwa kama pipi katika mitaa na
madukani. Kula ukwajua au
bidhaa zitokanazo na ukwaju
kuna faida sana. Ukwaju umejaa
Vitamini, fiber, potassium,
magnesium na virutubisho
vingine muhimu kwa afya njema.

Lakini kati ya faida zingine nyingi
za virutubisho na kiafya za
ukwaju, kuna kadhaa ambazo ni
za muhimu zaidi, na ni kama
zifuatazo:
1. Ukwaju chanzo kizuri sana cha
antioxidants ambazo zinasaidia
kupigana na saratani. Ukwaju
una carotenes, Vitamini C,
flavanoids na vitamin B zote.

2. Ukwaju unakuepeusha na
ukosefu wa Vitamini C.

3. Ukwaju unasaidia kupunguza
homa na kukupa ulinzi dhidi ya
mafua.

4. Ukwaju unakusaidia kuyeyusha
chakula tumboni.

5. Ukwaju unakusaidia kutibu
matatizo ya nyongo.

6. Juisi ya ukwaju hutumika kama
kitu cha kustarehesha mwili.
7. Ukwaju unapunguza
cholesterol mwilini.

8. Ukwaju unasaidia kuwa na
moyo wenye afya njema.
9. Ukwaju ukiunywa unasaidia
kupooza koo.

10. Ukwaju ukiupaka kwenye
ngozi unasaidia kutibu uvimbe
Kwa Tanzania ukwaju
unapatikana kwenye masoko
karibu yote. 

Ninakushauri kutengeneza juisi ya
ukwaju nyumbani kwako na weka
sukari kidogo na juisi hiyo iwe
sehemu ya chakula chako. Kama
wewe unapenda kula hotelini au
kwenye vioski basi agizo juisi ya
ukwaju ikusaidi kushushia
chakula. 

Related Posts:

  • FAIDA 10 ZA KULA MATANGO NA MATIKITI MAJI Ulaji wa matango na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji ambayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali amb… Read More
  • FAIDA KUMI ZA KUNYWA MAJI MOTO YENYE LIMAO KILA UNAPOAMKA ASUBUHI 1.Huongeza Kinga yako ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo kama mafua, na kikohozi kutokana na kuwa na vitamin C 2. Husafisha Mfumo wako wa chakula, kuondoa sumu mwilini na kuzuia tumbo kujaa gesi mara kw… Read More
  • FAIDA YA TUNDA LA MKOMAMANGA KITIBA Dr. Clifford B. Majani Mkomamanga (Punica granatum)ni mmea ambao asili yake ni katika nchi za Mashariki ya Kati (Middle East) na umetajwa sana katika vitabu vya kale vya historia ya eneo hilo. Kwa mujibu w… Read More
  • FAIDA ZA KIAFYA ZA MTI WA MWEMBE Mti wa mwembe mbali ya kuzaa tunda la embe ambalo hutumika kama chakula au kinywaji ( juisi ) chenye ladha ninayo vutia, una faida lukuki za kiafya kwa mwili wa mwanadamu. Zifuatazo ni baadhi ya faida za kiafya za mti… Read More
  • TIKITI MAJI (WATERMELON) NA FAIDA ZAKE Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi.Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni m… Read More

2 comments:

  1. Genital herpes is a sexually transmitted disease (STD) caused by the herpes simplex virus type 1 (HSV-1) or type 2 (HSV-2). Herbalist Dr Kham cured me with his two weeks herbs from HSV-1, Hey Friends, I am so glad to write my Review on this article today to tell the world how Dr. Kham cured my herpes virus, I have been detected with HSV-1  Two Years Ago my life has been in complete bizarre and agony, I have used so many drugs that was prescribed to me by several doctors but it didn't cure my herpes virus neither did it reduce the pain until a certain day that I was checking for solution in the internet then I came across Dr. Kham the powerful herbalist that cure numerous individuals STD, Then I contacted his email And I explained everything to him and prepared a cure for me and he ship it to me via a Courier Service and in 7 days I Received it and he gave me the prescriptions on how to take the dosage of the herbal medication that cure my HSV-1 Virus totally after taking the dosage of his herbal medicine for two weeks, So my friends/viewers why wait and suffer when there is someone like Dr. Kham The only caregiver that can cure any diseases & Virus, You can contact him via Email: dr.khamcaregiver@gmail.com  or visit his Website:  herbalistdrkhamcaregiver.simdif.com and for quick response Message him on WhatsApp: wa.me/2348159922297

    ReplyDelete
  2. I am now leaving a healthy life after using the herbal medicine to cure myself from herpes, i am now herpes disease free after the application and usage. You can contact him for your herbal medication from via Email Robinsonbuckler11@gmail com. Thanks and God Bless you for your help, referring people with herpes disease to use this herbal remedy__________________________🌿🌿🌿

    Good for the following

    Shingles,

    Cold sore,

    HPV,

    HSV1&2,

    ReplyDelete