Sunday, 29 June 2014

MATIBABU YA MARADHI YA BAWASIRI




Kutibu Maradhi ya BAWASIRI (MGORO): 
Haya ni maradhi ambayo humsibu mgonjwa sehemu ya haja kubwa ambayo humsababisha kupata maumivu. 
DALILI ZAKE
(1) Kupata choo kigumu. 
(2) Kutokwa damu sehemu ya haja kubwa baada ya kujisaidia. 
(3) Muwasho au maumivu na joto kali sehemu ya bawasiri. 
(4) Kupata maumivu wakati unapokaa. 
(5) Vidonda au kutokwa nje na kijinyama sehemu ya kutokea haja kubwa.
 (6) Upungufu wa nguvu za kiume.



TIBA: Jambo la kwanza kabla ya tiba mgonjwa aweze kutibiwa maradhi ya kutopata choo vizuri ikiwa anayo kwa sababu huzidisha maradhi haya. Pia epuka kula Nyama hasa ya ngombe, Pilipili na vitu vikali. Halkadhalika usinywe maziwa kwa wingi.
Kanuni ya kwanza: Kunywa juisi ya tikiti maji asubuhi kabla ya chakula na usiku kabla ya kulala.Dawa hii hutibu na kuondoa maumivu ya bawasiri.

Kanuni ya pili: Chukua asali nusu lita , unga wa kamun aswad vijiko vitatu vikubwa,unga wa Habat soda vijiko vitatu vikubwa na unga wa kamun abyadh vijiko viwili vikubwa. Vitu vyote hivi vichanganye pamoja kwa kuvikoroga kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu kisha ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje halafu unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Ikiwa ni bawasiri ya kutoka nje au yenye vidonda, paka mafuta ya nyonyo au mafuta ya lozi.


1 comments:

  1. A.Alkm samahani sana mimi naomba kufahamu Bawasili ni maradhi ama ni ugonjwa na unaweza kutibika kwa siku ngapi na ukifaniwa kupowa kabisa je unatakiwa kuendelea na miko ama kutokutumia vitu ulivyokatazwa kipindi cha ugonjwa ama maradhi haya?

    ReplyDelete