Maradhi ya VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS): Haya ni maradhi ambayo hufanya vidonda upande wa ndani ya ukuta wa tumbo. Kuna Duodenal ulcer na Gastric ulcer.
DALILI: (1) Kupata maumivu makali chini ya kifua kwa
upande wa ndani. (2) Kuchoka bila sababu. (3) Kuumwa kwa mgongo au kiuno. (4) Kupungua kwa nguvu za kiume. (5) Kuwa na kichefuchefu baadhi ya wakati. (6) Kuwa na kiungulia . (7) Tumbo kujaa gesi. (8) Tumbo kuwaka moto. (9) Kukosa choo na wakati mwingine kupata choo kigumu kama cha mbuzi. (10) Kukosa hamu ya kula. (11) Kutapika damu au wakati mwingine kutapika nyongo. (12) Maumivu makali baada ya kula vitu vikali au chakula cha moto.
TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua asali robo lita uchanganye na unga wa arki susi vijiko vinne vikubwa kisha ukoroge kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu.
Kanuni ya pili: Chukua viazi vya mviringo (vya chipsi) kama vitatu halafu uvikoshe na kuvimenya. Baada ya kuvimenya upate juisi yake kwa kuvisaga kwenye blenda. Kunywa vijiko vitatu vikubwa vya chakula kutwa mara mbili.
Kanuni ya tatu: Chukua lozi gramu 30 halafu usage iwe unga.
0 comments:
Post a Comment