MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):
Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na
hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa. Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.
SABABU ZA MARADHI HUSIKA: (1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. (2) Maradhi ndani ya utumbo mpana. (3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano. (4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. (5) Kutokunywa maji ya kutosha. (6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. (7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.
TIBA: Kanuni ya kwanza:
Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.
Kanuni ya pili: Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asalirobo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.
Kanuni ya tatu: Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili.
Kanuni ya nne: Kunywa kwa wingi maji ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.
Kanuni ya tano: Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini.
0 comments:
Post a Comment