Thursday, 26 June 2014

FAIDA NA MATUMIZI YA MAFUTA YA MISKI





FAIDA NA MATUMIZI YA MISK:
Hali yake ina ujoto na uyabisi katika daraja la pili. Ina ladha na harufu tofauti na mafuta mengine mazuri. Inatokana na mnyama anaeitwa kwa kiarabu AL GHAZALI. Namna ya kutofautisha Misk halisi na feki ni kwa kuonja ladha yake na kunusa harufu yake. Pia njia nyingine ni kwa kusomea aya za Ruqya kwenye misk halisi halafu ajipake mwenye matatizo ya majini, italeta athari na kama ni misk feki haiwezi kuleta athari. Vile vile misk feki haiwezi kutibu maradhi ya kimwili kama vile maradhi ya ngozi.

MATUMIZI YA MISK KATIKA TIBA:
1) UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU: Kuna tiba iitwayo kitaalamu Aromatherapy. Maana yake ni kupata dawa kwa njia ya kunusa au kupata harufu yake kama vile kufukiza udi, misk huchangamsha ubongo na kuipa nguvu mishipa ya fahamu. Utakuwa unanusa misk mara kwa mara au upate mvuke wake. Kwa kupata mvuke wake chukua bakuli halafu uweke ndani yake maji ya moto yaliyochemka halafu uweke ndani yake matone kadhaa ya misk. Sogeza bakuli karibu ya usoni mwako ili upate kuvuta mvuke wake. Hali kama hii, mvuke wa misk utakuingia kupitia puani au mdomoni. Tiba hii inaitwa Aromatherapy. Ni nzuri kwa watu wenye kifafa, dege dege, kuumwa na kichwa, kizunguzungu, kutopata usingizi na kuondosha kichefuchefu. Pia huongeza kumbu kumbu.

2) RHEUMATISM: Ni dawa ya kuondosha maumivu ya miguu, ganzi na viungo. Ule ujoto wa misk huondosha maumivu ya mishipa, viungo, miguu, mgongo na kiuno.

3) MZUNGUKO WA DAMU: Husaidia mzunguko wa damu na kuondosha presha.

4)Kwa mwanamke inazidisha hisia na hamu ya tendo la ndoa. 

5) HUONDOSHA HARUFU MBAYA: Kwa kuondosha harufu mbaya makwapani au miguuni, jipake misk.

6) FANGASI SEHEMU ZA SIRI: Huondosha sehemu za siri mwashowasho, mapele na harufu mbaya.

MATUMIZI YA MISK KWA KUMDHOOFISHA AU KUMFUKUZA JINI WA MAHABA:
Kwanza kabisa misk isomewe aya za Ruqya, kisha mgonjwa mwenyewe ajipake kila siku asubuhi na jioni viungo 32 vya mwili wake.
-Tundu mbili za pua.
-Tundu mbili za masikio.
-Kope mbili za macho.
-Mdomoni kama vile mfano wa lipstiki.
-Chuchu mbili (mwanamke anaenyonyesha asipake)
-Sehemu za siri mbele na nyuma.
-Kitovuni.
-Mbele mwa kucha zote za vidole 20 vya mikono na miguu.

TAHADHARI:
Ikiwa misk ni feki faida zote hapo juu za tiba haziwezi kupatikana.

Related Posts:

  • KABICHI:KINGA KUBWA DHIDI YA MARADHI YA SARATANI (CANCER) Ugonjwa wa saratani (cancer) ni miongoni mwa magonjwa hatari yanayosumbua watu duniani hivi sasa, Tanzania ikiwemo. Wagonjwa wanaongezeka kila kukicha katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, ambayo ni maa… Read More
  • BAMIA HUWEZA KUSAIDIA WAGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO. Mtandao wa healthandcure.com unawanukuu wataalamu wa afya wakieleza kuwa watu wanaosumbuliwa na maradhi kadha wa kadha ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni a… Read More
  • SOYA: CHAKULA CHENYE KINGA NA TIBA Mpendwa msomaji. Bado tupo katika kudadavua faida za kiafya zitokanazo na chakula. Leo, tutaizungumzia Soya ambayo ni maarufu sana nchini lakini kwa bahati mbaya wengi hawajui kuwa ni chakula chenye tiba ndani yake. Aja… Read More
  • BIZARI: KIUNGO CHA MBOGA CHENYE FAIDA NYINGI Inawezekana katika maisha yako hujawahi kula mboga iliyowekwa kiungo kinachoitwa bizari, kama umewahi, inawezekana pia hujawahi kujua faida zake mwilini.Bizari (Turmeric) ni kiungo cha mboga jamii ya mimea unaochimbwa kam… Read More
  • MAAJABU YA KARANGA MBICHI MAAJABU YA KARANGAWengi wetu huchukulia ulaji wa karanga kamachakula cha kujiburudisha na kisichokuwa naumuhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu.Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuziwaiwapo utajua faida zake kam… Read More

3 comments:

  1. naweza ipataje hii mafuta ya miski?

    ReplyDelete
  2. Kuna uhusiano kati ya majini na mafuta? Au hayo mafuta yana majini pia

    ReplyDelete
  3. Naomba nisaidiwe namna ya kuya
    pata Hayo mafuta ya miski

    ReplyDelete