Thursday, 26 June 2014

FAIDA NA MATUMIZI YA MAFUTA YA MISKI





FAIDA NA MATUMIZI YA MISK:
Hali yake ina ujoto na uyabisi katika daraja la pili. Ina ladha na harufu tofauti na mafuta mengine mazuri. Inatokana na mnyama anaeitwa kwa kiarabu AL GHAZALI. Namna ya kutofautisha Misk halisi na feki ni kwa kuonja ladha yake na kunusa harufu yake. Pia njia nyingine ni kwa kusomea aya za Ruqya kwenye misk halisi halafu ajipake mwenye matatizo ya majini, italeta athari na kama ni misk feki haiwezi kuleta athari. Vile vile misk feki haiwezi kutibu maradhi ya kimwili kama vile maradhi ya ngozi.

MATUMIZI YA MISK KATIKA TIBA:
1) UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU: Kuna tiba iitwayo kitaalamu Aromatherapy. Maana yake ni kupata dawa kwa njia ya kunusa au kupata harufu yake kama vile kufukiza udi, misk huchangamsha ubongo na kuipa nguvu mishipa ya fahamu. Utakuwa unanusa misk mara kwa mara au upate mvuke wake. Kwa kupata mvuke wake chukua bakuli halafu uweke ndani yake maji ya moto yaliyochemka halafu uweke ndani yake matone kadhaa ya misk. Sogeza bakuli karibu ya usoni mwako ili upate kuvuta mvuke wake. Hali kama hii, mvuke wa misk utakuingia kupitia puani au mdomoni. Tiba hii inaitwa Aromatherapy. Ni nzuri kwa watu wenye kifafa, dege dege, kuumwa na kichwa, kizunguzungu, kutopata usingizi na kuondosha kichefuchefu. Pia huongeza kumbu kumbu.

2) RHEUMATISM: Ni dawa ya kuondosha maumivu ya miguu, ganzi na viungo. Ule ujoto wa misk huondosha maumivu ya mishipa, viungo, miguu, mgongo na kiuno.

3) MZUNGUKO WA DAMU: Husaidia mzunguko wa damu na kuondosha presha.

4)Kwa mwanamke inazidisha hisia na hamu ya tendo la ndoa. 

5) HUONDOSHA HARUFU MBAYA: Kwa kuondosha harufu mbaya makwapani au miguuni, jipake misk.

6) FANGASI SEHEMU ZA SIRI: Huondosha sehemu za siri mwashowasho, mapele na harufu mbaya.

MATUMIZI YA MISK KWA KUMDHOOFISHA AU KUMFUKUZA JINI WA MAHABA:
Kwanza kabisa misk isomewe aya za Ruqya, kisha mgonjwa mwenyewe ajipake kila siku asubuhi na jioni viungo 32 vya mwili wake.
-Tundu mbili za pua.
-Tundu mbili za masikio.
-Kope mbili za macho.
-Mdomoni kama vile mfano wa lipstiki.
-Chuchu mbili (mwanamke anaenyonyesha asipake)
-Sehemu za siri mbele na nyuma.
-Kitovuni.
-Mbele mwa kucha zote za vidole 20 vya mikono na miguu.

TAHADHARI:
Ikiwa misk ni feki faida zote hapo juu za tiba haziwezi kupatikana.

Related Posts:

  • FAIDA YA UNYWAJI WA KAHAWA Kikombe kimoja cha kahawa kwa siku chapunguza hatari ya ugonjwa wa moyo Mbali na faida kemkem tunazozijua zinazopatikana kwenye kahawa, utafiti mpya umesema kwamba kunywa kikombe kimoja tu cha kahawa kwa siku … Read More
  • FAIDA YA MATUMIZI YA MAFUTA YA ZAITUNI BENEFIT OLIVE OIL Mafuta ya Zaituni Olive OilMafuta ya zaituni yana manufaa mengi katika mwili na maisha ya binadamu kwa ujumla kama ifuatavyo; (1)Mafuta ya zaituni hutibu maumivu ya tumbo kwa kunywa kijiko 1 mara 2 kwa sikukwa muda wa s… Read More
  • FAIDA ZIPATIKANAZO KIAFYA KWA ULAJI WA SAMAKI -Huendesha mfumo wa kinga ya mwili -Huzuia saratani -Hutoa ahueni kwa wenye pumu - Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo -Huongeza nishati ya ubongo -Huyeyusha damu, huifanya kuwa nyepesi - … Read More
  • FAIDA 8 ZA KITUNGUU MAJI KAMA DAWA. Usijali machozi yanayoletwa na  vitunguu maji ni kama karata dume katika kupigana na magonjwa. Ni mmea mahiri katika familia ya lily, vinakupa faida nyingi kiafya pia yaongeza ladha nzuri katika chakula chak… Read More
  • ZIJUWE VYAKULA BORA NA FAIDA ZAKE MWILINI TUNAAMBIWA kuwa kuishi vizuri ni pamoja na kula chakula bora na sahihi. Pia, mtu anayeishi vizuri ni yule ambaye hasumbuliwi na maradhi hatari na njia pekee ya kuulinda mwili dhidi ya maradhi hatari ni kujua ipas… Read More

3 comments:

  1. naweza ipataje hii mafuta ya miski?

    ReplyDelete
  2. Kuna uhusiano kati ya majini na mafuta? Au hayo mafuta yana majini pia

    ReplyDelete
  3. Naomba nisaidiwe namna ya kuya
    pata Hayo mafuta ya miski

    ReplyDelete