FAIDA NA MATUMIZI YA MISK:
Hali yake ina ujoto na uyabisi katika daraja la pili. Ina ladha na harufu tofauti na mafuta mengine mazuri. Inatokana na mnyama anaeitwa kwa kiarabu AL GHAZALI. Namna ya kutofautisha Misk halisi na feki ni kwa kuonja ladha yake na kunusa harufu yake. Pia njia nyingine ni kwa kusomea aya za Ruqya kwenye misk halisi halafu ajipake mwenye matatizo ya majini, italeta athari na kama ni misk feki haiwezi kuleta athari. Vile vile misk feki haiwezi kutibu maradhi ya kimwili kama vile maradhi ya ngozi.
MATUMIZI YA MISK KATIKA TIBA:
1) UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU: Kuna tiba iitwayo kitaalamu Aromatherapy. Maana yake ni kupata dawa kwa njia ya kunusa au kupata harufu yake kama vile kufukiza udi, misk huchangamsha ubongo na kuipa nguvu mishipa ya fahamu. Utakuwa unanusa misk mara kwa mara au upate mvuke wake. Kwa kupata mvuke wake chukua bakuli halafu uweke ndani yake maji ya moto yaliyochemka halafu uweke ndani yake matone kadhaa ya misk. Sogeza bakuli karibu ya usoni mwako ili upate kuvuta mvuke wake. Hali kama hii, mvuke wa misk utakuingia kupitia puani au mdomoni. Tiba hii inaitwa Aromatherapy. Ni nzuri kwa watu wenye kifafa, dege dege, kuumwa na kichwa, kizunguzungu, kutopata usingizi na kuondosha kichefuchefu. Pia huongeza kumbu kumbu.
2) RHEUMATISM: Ni dawa ya kuondosha maumivu ya miguu, ganzi na viungo. Ule ujoto wa misk huondosha maumivu ya mishipa, viungo, miguu, mgongo na kiuno.
3) MZUNGUKO WA DAMU: Husaidia mzunguko wa damu na kuondosha presha.
4)Kwa mwanamke inazidisha hisia na hamu ya tendo la ndoa.
5) HUONDOSHA HARUFU MBAYA: Kwa kuondosha harufu mbaya makwapani au miguuni, jipake misk.
6) FANGASI SEHEMU ZA SIRI: Huondosha sehemu za siri mwashowasho, mapele na harufu mbaya.
MATUMIZI YA MISK KWA KUMDHOOFISHA AU KUMFUKUZA JINI WA MAHABA:
Kwanza kabisa misk isomewe aya za Ruqya, kisha mgonjwa mwenyewe ajipake kila siku asubuhi na jioni viungo 32 vya mwili wake.
-Tundu mbili za pua.
-Tundu mbili za masikio.
-Kope mbili za macho.
-Mdomoni kama vile mfano wa lipstiki.
-Chuchu mbili (mwanamke anaenyonyesha asipake)
-Sehemu za siri mbele na nyuma.
-Kitovuni.
-Mbele mwa kucha zote za vidole 20 vya mikono na miguu.
TAHADHARI:
Ikiwa misk ni feki faida zote hapo juu za tiba haziwezi kupatikana.
naweza ipataje hii mafuta ya miski?
ReplyDeleteKuna uhusiano kati ya majini na mafuta? Au hayo mafuta yana majini pia
ReplyDeleteNaomba nisaidiwe namna ya kuya
ReplyDeletepata Hayo mafuta ya miski