Thursday, 26 June 2014
TIKITI MAJI (WATERMELON) NA FAIDA ZAKE
Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi.
Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.
Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.
Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharibifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.
Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.
Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.
Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.
Kwa kawaida tunda hili huliwa peke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake mpaka mbegu zake, ila ipo siku tutazungumzia kuhusu faida za mbegu zake, In shaa Allah.
Related Posts:
FAIDA ZA KIAFYA ZIPATIKANAZO KWA KULA TUNDA LA NANASI Nanasi NANASI ni tunda lenye ladha nzuri. Mbali na kutumika kama tunda ama juisi yake kutumika kama kinywaji, tunda la … Read More
FAIDA ZA KIAFYA ZIPATIKANAZO KWA KULA TUNDA LA PARACHICHI (AVOCADO) Parachichi Tunda la AVOCADO ama PARACHICHI lina faida nyingi kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni&nb… Read More
FAIDA NYINGI ZIPATIKANAZO KWA AJILI YA KULILA TUNDA LA PAPAI KIAFYA. Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake. Hata hivyo mbali na kuwa na ladha nzuri, tunda l… Read More
FAIDA ZA KIAFYA KWA KULA KAROTI FAIDA ZA KIAFYA ZA KAROTI Watu wengi huitumia karoti kama kiungo ama kikolezeo cha mboga. Mbali na kutumika kama kiungo … Read More
FAIDA ZA KIAFYA ZIPATIKANAZO KWA KULA MATANGO. FAIDA ZA KIAFYA ZA MATANGO. MATANGO yana faida mbalimbali katika afya ya mwili wa mwanadamu. Matango huweza kutengenezwa kama juisi au… Read More
0 comments:
Post a Comment