Tuesday 6 May 2014

UHUSIANO WA MAGONJWA SUGU NA TATIZO LA KUTOPATA UJAUZITO!



MAGONJWA sugu yapo mengi sana na yamegawanyika katika makundi mawili yaani yale ya kuambukiza na yasiyoambukiza.
Magonjwa haya yapo mengi kama tulivyoona lakini siyo yote yana athari za moja kwa moja katika mfumo wa uzazi.
Hapa tutaona magonjwa mawili tu ambayo huchangia kuleta athari katika mfumo wa uzazi ingawa yapo mengi.

Upungufu wa damu (Anaemia)                        

Upungufu wa damu ambao watu wengi huwapata ni ule unaotokana na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Takwimu za kimataifa zinaonyesha zaidi asilimia 50 ya wanawake duniani wana tatizo hili.
Ingawa pia kuna upungufu mwingine wa damu uitwao ‘Pernicious Anemia’ ambao huambatana na upungufu wa vitamin ya Folic Acid. Ukiwa na upungufu wa madini ya chuma kwa ujumla ni vigumu kupata ujauzito kwa 

sababu mwili unakuwa unahangaikia matokeo mengine ya mwili.
Ukiwa na upungufu wa madini ya chuma,  kiwango cha hewa ya Oksijeni katika chembe hai za mwilini hupungua kutokana na chembe hai nyekundu kupungua. Mwili huchukua muda mrefu kufidia hali hiyo.

Chanzo cha tatizo

Mwanamke mwenye tatizo la upungufu au ukosefu wa madini ya chuma ni vigumu kupata ujauzito, upungufu huu si tu hupatikana kwa kuugua, bali hata ulaji wa baadhi ya vyakula huathiri.

Kama unataka kushika mimba bila tatizo pia angalia utaratibu wako wa mlo. Vipo vyakula ambavyo huzuia ufyonzaji wa madini ya chuma. Unaweza kuwa na bidiii ya kula vyakula bora lakini isiwe na tija kwako.

Vyakula vyenye kiwango kizuri 
cha madini ya chuma ni nyama aina zote, maini, dagaa na maharage, kwa hiyo vyakula vinavyozuia ufyonzaji wa madini ya chuma tumboni ni kama vile chai ya rangi, kahawa, unywaji wa maziwa 

kwa wingi au mtindi, ukosefu wa vitamin B
ulaji wa vyakula vyenye asili ya ngano na matumizi ya dawa za kuondoa tindikali au Acid tumboni, na wakati mwingine hutumika kutibu kiungulia.

Vyakula hivi siyo kwamba havitakiwi bali visiliwe wakati wa mlo kamili yaani pamoja na mlo kamili au mara tu baada ya mlo kamili, bali unaweza kuvitumia masaa matatu baada ya mlo kamili.

Hata mama mjamzito pia anatakiwa afuate utaratibu huu ili kuepuka tatizo hili la upungufu wa damu.
Wanawake wengine ambao wapo katika hatari ya kupatwa na tatizo hili ni wale wenye matatizo ya muda mrefu katika tumbo la chakula na wanaotumia zaidi mboga za majani, kamwe hawali nyama.


Dalili za ugonjwa
Mtu mwenye tatizo la upungufu wa madini ya chuma mwilini hupata upungufu wa damu ambao huambatana na hali ya kushindwa kupumua vizuri, kizunguzungu, moyo kwenda mbio, kuwa mchovu na dhaifu, kukosa hamu ya kula, ngozi kupauka, kutokana na damu nyingi wakati wa hedhi.


Ugonjwa wa kisukari 
Katika hili pia hakuna uhusiano wa moja kwa moja lakini kiwango cha sukari kikizidi mwilini huathiri upevushaji. Hali kadhalika hata kwa mwanamke anayetumia dawa ya Insulin huweza kupata tatizo hili la kutopevusha mayai na vilevile huweza kuharibikiwa na mimba.


Kisukari 
hutokea baada ya kongosho kushindwa kuzalisha kichocheo cha Insulin ambacho husaidia seli au chembe hai kuyeyusha sukari kwa ajili ya nishati mwilini.
Unaweza kuwa na tatizo la kisukari lakini usijue kutokana na dalili zake za awali kutokuwa wazi.

Ila mgonjwa wa kisukari huhisi kuchoka mara kwa mara, macho kutoona vizuri, kupata haja ndogo mara kwa mara, kupata fangasi mdomoni, mdomo kuwa mkavu daima na kiu ya maji mara kwa mara.

Kwa hiyo katika ugonjwa huu, chembe hai muhimu mwilini hushindwa kushirikiana na homoni ya Insulin.
Watu walio katika hatari ya kupatwa na ugonjwa huu ni wale wenye maumbo makubwa au wanene kupita kiasi.

0 comments:

Post a Comment