Tuesday 6 May 2014

DHIBITI MAUMIVU YA VIUNGO KIASILI ZAIDI

KATIKA  makala yaliyopita nilipokea simu nyingi kutoka kwa wazee, wakilalamika na kuomba msaada wa tiba ya kupambana na tatizo la kuumwa viungo vya mwili. Lakini katika siku za hivi karibuni, siyo wazee tu, bali hata vijana pia wanasumbuliwa na maumivu ya viungo.
Wazee:
Kundi hili linajumuisha watu wa kuanzia umri wa miaka 45 na kuendelea. Idadi kubwa ya wenye matatizo ya maumivu ya viungo, huwa wamepoteza ile nyama ya plastiki kama tuliyozoea kuitafuna juu ya mfupa wa paja la kuku ambayo hukaa katika maungio ya mifupa ya binadamu kama sponji linalo kinga mifupa kugusana na kusagika, hasa sehemu za mgongo, kiuno, magoti na vifundo. Kitaalamu nyama hii hujulikana kama ‘cartilage’.
Wajawazito na wenye vitambi    
Binadamu anapoumbwa hupewa mifupa kama fremu ya kumbeba kwa uzito uliokadiriwa kulingana na urefu wake na si vinginevyo. Tumewashuhudia akina mama wajawazito wakitembea kwa shida na hata kuanguka wakati mwingine kutokana na mifupa yao kushindwa kuubeba mzigo wa mtoto tumboni ambaye ni kama dharura kwa wakati huo.
Vivyo hivyo wenye vitambi nao hulalamika sana kuwa wanaumia sehemu za miguu, mgongo, nyayo na kiuno. Kitendo cha kuubadili mwili na kuwa na muonekano wa ‘V’, yaani juu kukubwa chini kudogo, huifanya mifupa kushindwa kuubeba uzito wako na kukufanya usikie maumivu sehemu hizo tajwa.
Maumivu haya pia huweza kuwakuta watu wengine bila kujali umri, wakiwemo wagonjwa mahututi, waliopatwa na ajali, n.k. Hata hivyo, wengi hupatwa na matatizo ya viungo kutokana na mwili kukosa lishe inayotakiwa kuufanya mwili ujiendeshe wenyewe.
Tiba asilia za maumivu haya
Tiba za maumivu haya zipo nyingi, lakini leo nitazitaja tatu:
Mdalasini: Chemsha mdalasini na maji glasi nane kisha yaache yapoe, kunywa kidogokidogo kwa kutwa moja. Rudia zoezi hilo kwa siku 10 mpaka 15 na ndani ya muda huo utabaini mabadiliko mazuri, utatakiwa kufanya hivyo kila mara unapohisi maumivu.
Muarobaini: Chuma na twanga majani ya muarobaini na uyakamue upate juisi yake robo ya glasi moja. Changanya juisi hiyo na maji ya kunywa glasi 7, kunywa kidogo kidogo mpaka yaishe kwa kutwa moja, kwa muda wa siku 10 mpaka 15.
EsteoEze Gold: Hii ni tibalishe maalumu ya vidonge (food supplement) ambayo ina ‘Glucosamine Sulphate’ na ‘Chondroitin Sulphate’ ambayo ukiitumia kwa mwezi mmoja kama ilivyo dozi yake, unaweza kupata nafuu ya muda mrefu. ‘Glucosamine’ imethibitishwa na matabibu duniani kote kuwa husaidia kujaza mapengo katika mifupa na ‘Chondroitin’ hufanya ripea katika maungio yaliyosagika, kuzuia maumivu na uvimbe.
Miongoni mwa virutubisho vingine vilivyomo kwenye tibalishe hii ni pamoja na vitamin C na Manganese kwa wingi ili kurahisiha uponyaji na kumfanya mgonjwa ajisikie nafuu kwa muda mfupi sana. Kwa maoni na ushauri usisite kuwasilina nasi kwa namba iliyopo hapo juu.

4 comments:

  1. MPISHI:
    Hutibu Kisukari hivi…

    Wiki ya jana tuliona namna Mpishi alivyo mtu muhimu katika jamii kuliko wafanyakazi wote unaoweza kuwaajiri na hoja kuu ikiwa kwamba Mpishi ndiye anayechanganya kemikali unazokula na kukufanya uwepo, tena katika afya njema. Baunsa, Mwanasheria, Dereva, Mshauri, Daktari na hata Mwalimu na wengineo wote hawana fursa ya kupata ajira kwako endapo mpishi hakutekeleza majukumu yake ipasavyo ili wao wakuone. Unaweza ukamuajiri rasmi mpishi wako, lakini hata kumwajiri kwa masaa ‘Part time’ pia inawezekana na akakupa ushauri mzuri juu ya afya yako na vyakula.
    Mpishi ana nafasi kubwa kuliko daktari katika tiba ya ugonjwa wa kisukari, na dunia nzima inaelewa hivyo. Kisukari, yaani ‘Diabetes Mellitus’ ni maradhi yatokanayo na sukari kuzidi katika mzunguko wa damu mwilini. Hii hutokea iwapo kiungo kiitwacho kongosho hakitazalisha ‘insulin’ au kitazalisha insulin kidogo kwa mahitaji ya sukari kugeuzwa kuwa nishati ‘Calories’ za kumwendesha binadamu. Dalili za maradhi haya huwa hazijifichi: Kiu ya marakwa mara, njaa ya mara kwa mara, Uzito hupotea bila taarifa rasmi, macho huanza kufa taratibu na maambukizi ya mara kwa mara pamoja na homa za kujirudia rudia humkumba mgonjwa kwa kuwa kinga ya mwili nayo pia hushuka.
    Wagonjwa wasiozalisha kabisa insulin hawa huitwa ‘Insulin Dependant’ ambapo mara nyingi hujitokeza toka utotoni kwa kuwa na ulemavu wa aina tofauti katika kongosho. Wagonjwa hawa huhitaji sindano moja au zaidi ya insulin ili kupata mchanganyo sawa na kiwango cha sukari mwilini. ‘Non Insulin Dependant’ hawa ni aina ya pili ya wagonjwa wa kisukari ambao kwa kawaida ni wengi sana na huwatokea wakiwa watu wazima kabisa. Wao, kongosho huzalisha insulin kama kawaida yake ila huwa haitoshelezi mahitaji ya sukari iliyopo mwilini kutokana na sababu tofauti lakini kubwa ikiwa ni unene ambao ni tatizo kwa wengi, msongo wa akili pia husababisha kisukari na hata wazazi wenye kisukari hurithisha watoto kwa 50%.

    Wanawake waliojazia mitaa ya shingo, kifua, mabega na tumbo wapo hatarini au wameshaukwaa ugonjwa huu ukilinganisha na wale walijazia sehemu za makalio na mapajani zaidi. Ila, tafiti za tiba zinatoa uhakika wa tiba kwa lishe kupitia mpishi mbobevu ambaye huponyesha kabisa ugonjwa huu kwa kumpa mgonjwa lishe maalum hasa wagonjwa wa ‘Non Insulin Dependant’ ambao hupona kwa asilimia 58% wengi wao wakiwa ni wazee wa miaka 60 na kuendelea. Mafanikio hupatikana baada ya mpishi kupa mgonjwa vyakula visivyo na kalori nyingi huku akimhimiza mgonjwa kufanya mazoezi na hapo mgonjwa hupoteza 5%-7% ya uzito wake kwa siku. Hii itamsaidia mgonjwa kupona kwa kuwa seli za misuli ya mwili hupata nafasi ya kuidhibiti sukari kikamilifu zaidi.
    Kwa kawaida, wagonjwa wa kisukari, wazee, na watu wanene(Obese) huhitaji kiasi cha kalori 1000 hadi 1600 kwa siku nzima. Mpishi atapunguza kiwango cha kalori 500 kati ya hizo na atafanikiwa kumpunguza uzito mgonjwa kati ya kilo 2 hadi 4 na uhakika upo wazi kweupe. Hata hivyo, mgonjwa atahisi mpishi amebadilisha mapishi kwani vinywaji baridi, vyakula vya mbegu, vyakula vya kukaanga, mafuta, sukari na chumvi bila kusahau ‘chachandu’ yaani achali hubeba kalori nyingi sana hivyo mpishi ataviondoa katika mlo wa mgonjwa. Ila, kukosa mafuta, chumvi na sukari bado sio sababu ya msingi kwa mpishi kukupa vyakula vyenye ladha kwani Mungu ameumba vyakula bila idadi duniani.
    Wiki ijayo, tutaangalia pia ni namna gani mpishi anavyoweza kupambana na homa hivyo usikose nakala yako ya UWAZI jumanne. Sote tumeona namna mpishi alivyo bora kuliko mtu yeyote unayeweza kumwajiri. Ukiwa na swali, hoja, maoni au ukahitaji ushauri wa kina basi tupigie na utembelee mtandao wetu hapo juu.
    Joh Haule
    0768 215 956

    ReplyDelete
  2. MPISHI:
    Mtu muhimu sana…

    Katika makosa makubwa yanayotugharimu mno ni kutoutambua umuhimu wa mpishi. Wengi wetu tumeajiri wanasheria na tumewasikia wakituambia “usishughulikie suala lolote la kisheria bila kunitaarifu”. Tumeajiri madereva, Washauri, Watunza Fedha na idadi ndefu tu bila kikomo lakini tumeshindwa kujua kuwa Mpishi ndiye anayepaswa kuajiriwa kabla ya wote kwa kuwa uhai wako upo mikononi mwake. Kivipi?
    Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa mpishi ni mkemia anaye andaa chakula alacho binadamu. Ofisi yake huitwa Jiko. Jiko si kitu cha kubezwa kwani hata mtaalamu wa tiba wa kale Duniani alipoulizwa jiko ni nini alijibu “Kitchen is a Natural Pharmacy” akimaanisha jiko ni duka la dawa muhimu za binadamu. Wataalamu wa afya wa leo wanaweka bayana kabisa kuwa “Jiko ni maabara inayotengeneza kemikali alazo binadamu, zenye uwezo wa kumstawisha, kumdhoofisha na hata kumuua binadamu huyo.” Isikutishe, Hiyo ni maana halisi aliyotoa Mkongwe Hippocrates kwa kifupi.
    Hapo utagundua kuwa hata kama unaishi na mkeo bado wewe na mkeo mna sababu za msingi kabisa za kumhitaji mpishi awaelekeze cha kufanya au awapikie kabisa kwani hata mkeo si mtaalam wa jiko hivyo ni mtego wa vifo tu (Death Trap) kumtegemea alete vyakula safi na salama kwa walaji mezani bila kuwa na sayansi ya vyakula anavyopika.
    Nitatoa mfano mmoja: Kuna vyakula vya aina nyingi na kwa ajili ya matumizi tofauti pia. Vipo vyakula vya majira tofauti pia kama ilivyo hivi sasa ni kipupwe na hali ni baridi kiasi tumeshuhudia wengi wakishindwa kuhimili baridi na kujikuta mahospitalini na wengine wamefariki dunia pia. Hii hutokea sana kipupwe kinapowadia lakini kutopata mlo sahihi huchangia kwa kiasi kikubwa sana. Wakati mtaalamu wa mavazi akimvesha sweta mgonjwa wake, mpishi hodari humpikia vyakula vya kipupwe vinavyotia nguvu na joto mwilini yaani nafaka, mafuta, na vinywaji vya moto pia. Kwa watoto ni vizuri kipindi hiki cha baridi wakapewa vyakula vya nafaka na mafuta kwa wingi asubuhi kabla hawajatoka maana itawasaidia kuishinda baridi na utawaona wakifurahi mchana kutwa.
    Hata majira nayo huleta vyakula kwa msimu pia. Angalia viazi vitamu, mahindi mabichi, kabichi, mapeasi na apple ni vyakula vinavyotia joto mwilini na Mola wetu akaona ni vema vipatikane majira haya. Majira ya joto wote tunajua kuwa kuna matunda yenye maji na vyakula vyenye maji kwa wingi ili kuturudishia maji yenye virutubisho, madini na vitamin yanayo kaushwa na joto tunalopambana nalo.
    Kipupwe hiki, ni vema wazee wasitumie mafuta. Kwa kuwa wao si watu wanaokua tena basi mafuta hukosa kazi na baadaye husababisha maradhi kwao. Ambao wanapata kinywaji kidogo sio mbaya wakajitia joto kwa matone kadhaa ya pombe kali au bia mbili tatu pia inakubalika kiafya kwa wazee. Kula kabla ya kunywa maji si jambo jema pia. Hivyo hakikisha unapata vinywaji vya moto wakati wa baridi ili angalau upate mkojo glasi 8 hadi 10 ili kujihakikishia afya njema.
    Hizo ni shughuli za mpishi. Unaweza ukamuajiri rasmi au ukampa ajira ya masaa (Part Time) ili akupe dondoo za jikoni kwa usalama wa familia au jamii yako kwa ujumla. Wiki ijayo, tutaangalia Mpishi anavyoweza kuokoa maisha ya wagonjwa kwa kuchagua vyakula vyenye tiba kwao. Ukiwa na maswali, hoja, maoni au ungependa ushauri kwa kina basi usisite kutupigia na kututembelea katika tovuti na simu hapo juu.

    John Haule
    0768 215 956






    ReplyDelete
  3. MPISHI:
    Huikabili homa hivi…

    Wiki iliyopita tuliona jinsi mpishi anavyoweza kuukabili ugonjwa wa kisukari kwa uhakika kabisa. Mpishi bado ana nafasi kubwa sana ya kuokoa maisha ya walaji wake tena katika hali ya hatari ya kufa kwa maradhi yasiyoeleweka kama homa. Kila mtu anaijua kwa uhakika sana homa. Hakuna hata mmoja wetu ambaye hawahi kuugua homa kote ulimwenguni na kibaya zaidi homa hutukumba zaidi watu tulioko kusini mwa jangwa la sahara na hushambulia zaidi akina mama na watoto wenye umri chini ya miaka 15 Watanzania tukiwemo kundini.
    Nikushangaze msomaji wangu kuwa homa sio ugonjwa! Ndio, homa ni maumivu tu au ‘shabiki’ wa maradhi mengine yanayotukumba binadamu. Kwa kawaida mwili ukikutana na shambulio lolote liwe la bacteria, virusi au hata kisaikolojia basi joto litapanda na mtu atajisikia maumivu na hali hiyo ndio kitaalamu inaitwa ‘Homa’

    Ukiwa na homa, protini na virutubisho vingi sana hupotea mwilini huku hamu ya kula nayo hukata na kupotea kabisa. Hii humfanya mgonjwa kupoteza uzito na ikimlaza kwa muda mrefu hupooza na baadaye anaweza akapoteza maisha asipotibiwa. Hali hii hutokana na kupoteza vitamins B complex na vitamin C kwa wingi sana kupitia mkojo wa njano ambao wote tukiugua hukojoa hivyo.
    Mgonjwa anapofikia hatua hii, Mpishi husaidia kuokoa maisha yake kwa kumpa vyakula vyenye protini kwa wingi japo mgonjwa husumbua kidogo kutokana na homa kumpotezea hamu ya kula ila kama atakuwa anatapika pia basi kazi itakuwa ngumu sana na mpishi anaweza akaagiza mgonjwa apewe ‘vitamins supplements’ za vidonge ili kujazia mlo wake kwa usahihi na haraka apone. Bado Mpishi atatakiwa ahakikishe mdomo wa mgonjwa ni safi muda wote maana homa huzalisha taka mdomoni na kumfanya mgonjwa akate hamu ya kula pia. Mpishi anaweza akampa kachumbari mara kwa mara na akaona maajabu!
    Homa huwa za muda mfupi, zipo za muda mrefu na zipo homa za kujirudia mara kwa mara pia. Kwa homa za muda mfupi kama vile malaria, typhoid, kuharisha n.k. Mpishi atampikia mgonjwa wake vyakula vya kimiminika tu kwa siku mbili mfululizo ili kwenda sambamba na upotevu wa maji mwilini na pia mgonjwa ataweza kula kwa urahisi. Juisi, maziwa, uji, supu, mtori n.k. vitamfaa sana mgonjwa na endapo atakojoa mkojo kiasi cha lita mbili ni dalili wazi kuwa anapona.

    Kwa homa za muda mrefu zinazojishabikia katika maradhi kama vile kifua kikuu, ukimwi, majeraha ya upasuaji, saratani, na hata ajali pia Mpishi atahakikisha mgonjwa anapata vyakula laini na kidogokidogo walau milo mitano kwa siku ili mgonjwa aweze kwenda sambasamba na uharibifu unaosababishwa na homa. Msisitizo upo katika vyakula vyenye maji zaidi kwa sababu homa hupoteza maji mengi kupitia jasho la stress, mkojo, kutapika nap engine hata kuharisha pia. Hivyo Mpishi humpa mgonjwa vimiminika kwa wastani wa lita 2 hadi 3 katika mfumo wa lishe ili arudishe madini, vitamin na virutubisho vingine pia na uhakika wa mgonjwa kupona ni mkubwa na uhakika.
    Nadhani tumeelewa vizuri namna anavyoweza kuikabili homa. Bado mpishi ana uwezo wa kuyakabili maradhi kibao! Usikose makala hii kila jumanne kwani bado tunaendelea kukuletea pilikapilika za mpishi jikoni akiwapikia wagonjwa wa maradhi tofauti. Unaweza ukawa na swali, hoja, maoni au ushauri wa kina juu ya Mpishi. Usisite kutupigia na kutembelea tovuti yetu hapo juu.
    John Haule
    0768 215 956

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante ndugu John Haule :Ubarikiwe mbinguni ameen.

      Delete