Saturday, 3 May 2014

VIJUE VIKWAZO KATIKA UZAZI WA MPANGO VINAVYO IKABILI JAMII-2

“Hayakuwa mapenzi
yangu kabisa kutumia vidonge lakini kwa
sababu ya kukosa mtaalamu wa kuniwekea
vijiti, nikalazimika kutumia,” anasema Binti huyo.


Binti huyu anakosa mtaalamu wa kumweka
vijiti, hali ikoje mikoani, wilayani na vijijini
ambako hakuna wahudumu wa kutosha?
 
Jibu ni kwamba wanawake wengi hawana
uamuzi wa kuchagua njia za kupanga uzazi,
wanapewa huduma zilizopo au vinginevyo
wapate mimba ambazo hawajapanga.


Mama mmoja nae niliongea nae katika kliniki moja,
nilipomhojiwa ni njia gani anatumia
katika kupanga uzazi, anasema alijaribu
 
kutumia kitanzi, lakini siku alipokwenda
kliniki akaambiwa muuguzi wa kuweka
kitanzi amehamishwa.


Kutokana na pilikapilika zake za ujasiriamali,
akarudi nyumbani bila kupata huduma, na
haukupita muda kwa sababu hakujua vizuri
njia ya kufuata kalenda, akadaka mimba,
 
akajifungua mtoto wa tano, jambo ambalo
linampa wakati mgumu kulea kutokana na
kipato chake duni cha kuuza vitumbua.


Serikali ifanye kila
linaloweza kuhakikisha kila zahanati, kituo
cha afya na hospitali wanakuwa na
wataalamu wa masuala ya uzazi wa
mpango.


Mama mmoja alipata
tatizo kubwa kutokana na mumewe
kutotaka kusikia kabisa habari ya mpango
wa uzazi, hivyo akawa akidunga sindano
kwa siri.
 
Siku moja alipoenda hospitalini, akakosa
sindano, akaambiwa zipo tu kondomu,
jambo hilo likawa gumu kwake kwani
 
mumewe asingemwelewa kumwambia
watumie kondomu. Hivyo akarudi
 
amejiinamia kwamba atakwenda kupata
mimba ambayo hakupanga apate wakati
huo, na kweli ikawa hivyo na sasa analea
moto ambaye hakumpangilia.


Kutokana na wanaume wengi kuwa
wapinzani wa mpango wa uzazi, wakati
 
umefika kuhimiza kampeni ya kuwapa elimu
na umuhimu wa uzazi wa mpango katika
kulea familia.

Mama huyu ni mmoja wa
wanawake wengi, ambao wanaficha kadi
zao hospitalini ili wanaume wao wasijue
 
kuwa wanafuata mpango wa uzazi, na
wengine wanasahau tarehe na kujishtukia
wamepata mimba zisizotarajiwa.


Wanaume wanatakiwa kubadili mtazamo
hasi na kuwasindikiza wanawake zao
kwenda nao kliniki kujifunza elimu ya uzazi
wa mpango.

Utoaji mimba kiholela
umekithiri kutokana na wanawake wengi
kupata mimba wasizotarajia, ambazo
 
zinachangiwa na uhaba wa wahudumu na ukosefu wa elimu ya uzazi,
uhaba wa huduma za uzazi wa mpango na
ugumu wa wapenzi wao wa kiume.


Idadi ya wanawake
wanaofika mahospitalini hapo baada ya kutoa
mimba kienyeji ni kubwa, jambo ambalo
linachangia wengine kupoteza maisha.


Kama elimu na matumizi ya vidhibiti
mimba ingefuatwa, utaoji mimba nao
ungepungua ama kuisha kabisa.

uhaba wa watalaamu wa huduma za
mpango wa uzazi katika maeneo ya vijijini
unachangia kwa kiasi kikubwa mimba
 
zisizotarajiwa. Upatikanaji wa huduma za
uzazi wa mpango katika maeneo
wanayoishi ni shida, wakati mwingine
 
wanatakiwa kufuata umbali wa kilometa
kadhaa kwenda wilayani au mahali pengine,
kufuata huduma hizo.
 
Kutokana na uhaba wa wataalamu wa
huduma za uzazi, kumeibua mimba za
utotoni na matatizo mengine katika jamii
 
yakiwamo ya kuongezeka watoto wa
mitaani, yatima na wanaoishi katika
mazingira magumu ambao wazazi wao
wanawatelekeza baada ya kuwazaa.


Vifo vya watoto na wanawake wajawazito,
vimekuwa havipungui kwa kasi inayotakiwa
kutokana na wanawake wengi kuishia
kuharibu mimba hizo na wakati mwingine
wao wenyewe kufa.


Elimu ya uzazi wa
mpango kwa kila Mtanzania ni muhimu
kwani itasaidia kujua umuhimu wa
wanawake kupanga aina ya uzazi na idadi
na watoto anaotaka.

0 comments:

Post a Comment