Saturday, 4 October 2014

KABICHI:KINGA KUBWA DHIDI YA MARADHI YA SARATANI (CANCER)


Ugonjwa wa saratani (cancer) ni miongoni mwa magonjwa hatari yanayosumbua watu duniani hivi sasa, Tanzania ikiwemo. 

Wagonjwa wanaongezeka kila kukicha katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, ambayo ni maalum kwa ugonjwa huu.

Katika makala ya leo, tutajifunza faida za kabichi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, licha ya kuchukuliwa kama ni mboga ya kimaskini na ambayo huliwa kwa shida zaidi kuliko kimanufaa ya kiafya. 

Ingawa inaonekana kuwa kabichi ni miongoni mwa mboga za majani zinazolimwa kwa wingi na kusambazwa kwenye masoko mengi nchini, hasa katika miji mikubwa, lakini ni watu wachache sana wanaopenda kula mboga hii.

Katika miji mikubwa, kabichi inatumika zadi kwa walaji wa chips. Hata hivyo hawaitumia ipasavyo kwa sababu huwa inapikwa na kukaangwa kwa mafuta kwa muda mrefu na hivyo kupoteza baadhi ya virutubisho vyake muhimu.

 KINGA DHIDI YA SARATANI
Miongoni mwa faida nyingi zinazopatikana kwa kula kabichi (nyeupe na nyekundu), inayoongoza ni ile ya kutoa kinga dhidi ya ugonjwa hatari wa saratani. 

Inaelezwa kuwa zaidi ya tafiti 475 zimefanyika kuhusu virutubisho vinavyopatikana kwenye kabichi na kuthibitisha kuwa vina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani na wakati mwingine kutibu.

Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee katika kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za virutubisho; 
Antioxidant’, ‘Anti-inflammatory’ na ‘Glucosinolates,’ ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa nyemelezi kadhaa ambayo husababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.

Kwa kuzingatia madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatia upatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuzia ulaji wake. Laiti kama watu wote tungejua sawasawa faida za kabichi, bila shaka mboga hii ingekuwa ghali kuliko hata samaki.

AHUENI YA VIDONDA VYA TUMBO
Mbali ya kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani, juisi ya kabichi inaelezwa kuwa na faida nyingi tumboni, hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo (peptic ulcers). Ikitumika mara kwa mara huwa kama tiba kwao. Hali kadhalika mfumo wa usagaji chakula tumboni, huwa imara.

HUIMARISHA MFUMO WA MOYO
Utafiti mwingine uliofanyika kuhusu kabichi umeonesha kuwa mboga hii huimarisha mfumo mzima wa moyo kwa kudhibiti utengenezwaji wa lehemu (cholesterol) mbaya mwilini ambayo inapozidi mwilini, husababisha matatizo ya moyo.

VITAMINI ZINAZOPATIKANA KWENYE KABICHI
Ndani ya kabichi, kuna kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin, hususan Vitamin K, Vitamin B1, Vitamin B2, Vitamin A na Vitamin C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha kambalishe (fiber) Manganizi (Manganese), Potashiamu (Potassium) na Fatty-3 acids. Vyote hivi ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.

Ili kupata faida za kabichi na kujenga kinga imara dhidi ya magonjwa ya saratani, weka mazoea ya kula kabichi mara kwa mara, angalau mara tatu kwa wiki, kwa namna ambayo utaona mwenyewe inafaa, iwe kama mboga au kachumbari.

Wednesday, 1 October 2014

UKIMWI, UGONJWA UNAOKWENDA SAMBAMBA NA UGONJWA WA KIFUA KIKUU.



Mchoro unaoonyesha mapafu ya mwanadamu yaliyoathiriwa na maradhi ya Kifua Kikuu. Picha kwa hisani ya Shutterstock. 

Kwa Ufupi
Ni marafiki ambao hawachezi mbali na ndiyo maana siku hizi wagonjwa wengi wanagundulika kuwa nao pamoja.

Asilimia kubwa ya watu wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu (TB) duniani wamekuwa wakigundulika pia kuwa na Virusi Vya Ukimwi(VVU).

Hii ni kwa sababu mtu mwenye VVU, huwa na kinga dhaifu jambo ambalo husababisha vimelea vya TB navyo kupata nafasi ya kuushambulia mwili.

Hivyo, mtu mwenye VVU ana uwezekano mkubwa wa kupata TB hai mara 29.6 ukilinganisha na yule asiye na VVU. Kwa mwaka 2012, walikuwepo wagonjwa milioni 1.1 wenye VVU na TB kati yao, karibu asilimia 75 ni watu wanaotoka katika nchi zinazoendelea hasa kusini mwa Jangwa la Sahara .

Pale inapotokea mtu ana maambukizi ya VVU , kinga ya mwili nayo hutetereka na kushuka na hivyo mwili nao hukosa kinga na ugonjwa wa TB hujitokeza.

Ugonjwa wa TB ndio unaongoza kuwaua wagonjwa wa VVU, hesabu ikiwa kwa kila vifo 5, mmoja hufariki kwa TB.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2012, watu 320,000 walikufa kwa VVU uliombatana na TB, ingawa duniani vifo hivyo ni sawa kwa wake kwa waume, ingawa kwa Afrika vifo ni zaidi kwa wanawake kuliko wanaume.

Kwa upande wa Tanzania, watu 120,191 wanakisiwa kupata kifua kikuu kila mwaka, hii ni kutokana na taarifa ya Shirika la Misaada la Marekani (USAID) mwaka 2007.

Kati ya watu hao (120,191), 56,233 ni wale waliogundulika kuwa na ugonjwa huu kupitia makohozi, yaani vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kifua kikuu ni 32,000 kila mwaka nchini Tanzania.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha kuwa Tanzania ni ya 15 kati ya nchi 22 ambazo zimeathiriwa sana na ugonjwa huu.

Kati ya asilimia 50 ya wagonjwa wa kifua kikuu waliopimwa virusi vya Ukimwi mwaka 2007.

Inakadiriwa kuwa Ukimwi huathiri asilimia 47 ya wagonjwa wote wa kifua kikuu. Ugonjwa sugu wa kifua kikuu (Multi-Drug Resistant Tuberculosis) huathiri watu 1,300 nchini Tanzania kulingana na taarifa ya mwaka 2007.

Wengi wa wagonjwa wa VVU wanakumbana na udharura unaotishia maisha yao hii ni kutokana na kuwapo kwa TB sugu na ile isiyotibika hata kwa dawa mchanganyiko.Kutokana na hilo, ndipo urafiki wa VVU na TB unapotokea na kushirikiana kuushambulia mwili na kama hatua za haraka zisipochukuliwa basi mtu huweza kudhoofu haraka na kupoteza maisha. Takwimu zaidi zinaonyesha kuwa mwaka 2011 wagonjwa 


wa Ukimwi na TB walipoteza maisha kwa magonjwa hayo mawili.

WHO katika mikakati ya kidunia imeweka mikakati ya kusambaza huduma za afya za tb kila mahali kwa ajili ya huduma za matibabu, ushauri na upimaji, na tayari kuna wagonjwa wa TB ambao tayari huduma hizi zimewafikia wagonjwa na kati ya hao wengine wanatumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARVs).

Dalili za TB

Kukohoa kwa zaidi ya wiki mbili, upungufu wa uzito wa mwili wa zaidi ya asilimia 10 ya uzito wa mwili, kupumua kwa shida, maumivu ya kifua, kukohoa damu, homa kali na kutokwa na jasho hasa nyakati za usiku, mwili kuwa mchovu, kuvimba tezi za shingo na kwapani na kuumwa kichwa

Jinsi ya kukabiliana na TB kwa wenye VVU

Jambo la msingi na muhimu ni kuwahi kufika katika huduma za afya mapema uwepo wa VVU na TB mwilini, hatari huwa zaidi kwani mwili hudhoofu na kufariki haraka ukilinganisha na yule mwenye TB bila VVU.

Zingatia matibabu pale unapoanza kutumia dawa za TB na ARVs hakikisha unatumia dawa kama ulivyoelekezwa na wataalamu wa afya, kumbuka usugu wa dawa na kushindwa kwa dawa hizi ni hatari zaidi katika kupambana na TB na VVU. Usiache kutumia dawa za TB ili kuepuka kupata TB sugu na ile isiyotibika kwa dawa mchanganyiko.

Hakikisha pale unapoona unakohoa zaidi ya wiki mbili unafika katika huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Funika mdomo na pua kwa kitambaa pale unapokohoa au kupiga chafya hii inasaidia kuzuia kuenea maambukizi.

Kuepuka mikusanyiko au mrundikano wa watu kama vile kwenye mabweni, kambi za jeshi, baa na kadhalika.

Kuishi kwenye nyumba ambayo ina mfumo mzuri wa kuingiza na kutoa hewa yaani iwe na madirisha makubwa na ya kutosha.

Pia, kuishi katika mienendo bora inayozingatia afya, kula mlo kamili, kunywa maji mengi angalau lita 1.5 kwa siku na mazoezi mepesi kama kutembea kwa dakika 15 kwa siku yanachangia kuujenga mwili na kuwa wenye afya njema. Pata mapumziko ya kutosha angalau lala masaa sita kwa siku, epuka matumizi ya ulevi wa pombe. chanzo.Ukimwi; ugonjwa unaokwenda sambamba na kifua kikuu 


Tuesday, 30 September 2014

5 Veggies That Are Disease Fighters



Certain fruits, vegetables, herbs, and spices have healing properties. Nourishing your body with good nutrition helps lead to optimal performance, if you have a disease process going on proper nutrition is even more important. Adding these 5 vegetables to your regular meal plans can help make you your healthy best!
1- Onions
onion
Onions are loaded with Vitamin C and folate and have a peptide that can help fight osteoporosis, the peptide helps minimize calcium loss.
2- Sweet Potatoes
Sweet potatoes are a good source of fiber and iron, and also have Vitamins A,C, and manganese. They build energy and help with your digestive system.
3- Spinach
Spinach is high in iron and chlorophyll and is laden with vitamins and minerals your body needs every day. Scientists also believe it can help prevent heart disease, colon cancer, osteoporosis, and arthritis.
4- Eggplants
Eggplant can help reduce your risk of stroke and dementia, as it is full of nutrients that are good for your heart. It’s also a superfood that helps protect your body from damage caused by free radicals.
5- Bell Peppers
peppers4
Bell peppers are a great source of lycopene and folic acid, and come in a rainbow of pretty colors to dress up your food. Researchers believe they can reduce cancers of the colon, pancreas, lungs, and bladder.

CURE HEADACHES AND MIGRAINE WITHOUT PILLS




Have you been attacked by an annoying migraine? In today’s lifestyle, it is really common, more common than it should be. Stress, rushing here and there, and many other factors affect our neurological system and entire health.
There is a better solution for this continuous headache than pills, since they just ease the momentary pain, instead of treating the real problem.
There are many natural cures for headaches, but the following juices will provide relied on cures for your chronic headaches and migraine:
1. GRAPE JUICE: Grape juices act as an effective home remedy for migraine headaches but the juice that is used for the cure is the juice of the red grapes. All you have to do is add this juice to your daily use without adding any sweetener or sugar.
2. CARROT JUICE: Carrot juice is rich in vitamin A. Vitamin A is an essential element that creates healthy tissues and is perfect for helping with your vision. It also contains other important minerals like potassium which is known to keep the cells in the body well-hydrated.
3. ORANGE JUICE: orange juice can get rid of toxins in the body that cause headaches and it will reduce the risk of heart disease and stroke.

For headaches there are plenty variety of natural remedies for you to choose:
• You can try a double espresso with a splash of lemon, a miraculous remedy for milder headaches since caffeine blocks pain transfer.
• With headaches, soaking your feet in hot water also helps. A hot bath redirects your blood to your feet, so it relieves the pressure in your veins. With very severe headaches, you should add to hot water some powdered mustard.
• Aromatherapy: The three main essential oils that help to relieve headaches are Roman Chamomile, Clary Sage and Lavender.
• Apply an ice pack to the painful area of your head. Try placing it on your forehead, temples, or the back of your neck. Ice is known to be one of the best anti-inflammatories.
• Yoga and aerobic exercise help decrease stress and loosen muscles to alleviate tensionheadaches.
migraine triggers

UGONJWA WA ZINAA WA TRICHOMONIASIS








Leo pia tutaendelea kuyajadili magonjwa ya zinaa ambapo tutazungumzia ugonjwa wa Trichomaniasis, ambao huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume. I.


Ugonjwa wa Trichomoniasis ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya jamii ya protozoan vinavyojulikana kama Trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitisha mkojo unaojulikana kama urethra na tupu ya mwanamke. Trichomoniasis pia hujulikana kwa majina mengine kama Trichomonas vaginitis au Trich.

Trichomoniasis huathiri watu milioni 170 kwa mwaka duniani kote ambako nchini Marekani pekee watu milioni 8 huambukizwa ugonjwa huo. Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume labda kutokana na wanaume kutoonyesha dalili zozote wakati wa maambukizi au kutokana na majimaji ya kwenye tezi dume kuwa na madini ya zinc ambayo huathiri vimelea hivi vya Trichomonas vaginalis vinavyosababisha ugonjwa huo. 

Trichomoniasis hupatikana kwa njia ya kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathirika ugonjwa huo. Wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huu, na ili kuufahamu vyema ni bora kwanza tuelezee nini hutokea wakati wa maambukizi au Pathofiziolojia ya ugonjwa huo.
Umbile la vimelea vya Trichomonas vaginalis ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe kwa upana, ingawa wakati mwingine ukubwa unaweza kutofautiana kulingana na mazingira. Kuwepo kwa umbile kama mikono 

kwa nje kwenye kimelea hicho inayojulikana kama flagellum, husaidia vimelea hivi kuingia kwenye tishu za mrija wa kupitisha mkojo pamoja na tupu ya mwanamke na hivyo kuharibu seli aina ya epithelium na kusababisha vidonda 

katika tishu hizo. Hii ndiyo sababu, watu wanaopata ugonjwa huu huwa kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Ukimwi (HIV) na magonjwa mengineyo ya zinaa. Je, wagonjwa huwa na dalili zipi?
Dalili za Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4 hadi ya 28 baada ya mtu kupata maambukizi ya ugonjwa huu. Kwa wanawake, Trichomoniasis huathiri shingo ya kizazi (cervix), mrija wa mkojo, tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo na tezi zinazojulikana kama Bartholin glands na Skene glands. Kwa wanaume 

vimelea hivi vya Trichomonas vaginalis hupatikana katika sehemu za siri za mwanamume, sehemu ya nje ya mrija wa kupitisha mkojo (anterior urethra), kwenye tezi dume, kwenye mirija ya kuhifadhi na kutoa mbegu za kiume (epididymis) na hata kwenye mbegu zenyewe. Dalili kwa wanawake zinaweza kuwa: 1) Uchafu unaotoka kwenye tupu ya mwanamke ambao huwa wa rangi mchanganyiko ya njano na kijani, au rangi ya kama kijivu na huwa mzito sana. 2) Maumivu wakati wa kujamiana. 3) Kutoka harufu kwenye tupu ya mwanamke. 4) Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo. 5) Shingo ya kizazi kuwa nyekundu hali ambayo hugundulika wakati daktari anamfanyia mgonjwa uchunguzi. 6) Kuwasha sehemu za siri, ambako huwatokea baadhi ya wanawake na sio wote. 7) Maumivu chini ya kitovu ambayo pia huwapata baadhi ya wanawake.
Ingawa wanawake ndio huonyesha dalili na viashiria vya ugonjwa huu, lakini mara nyingine wanaweza kuwa na vimelea hivi hata kwa muda wa miaka kadhaa hata kama vipimo vya uchunguzi havitaonyesha kama wameathirika na vimelea vya ugonjwa huo.


Wanaume huwa hawaonyeshi dalili zozote lakini baadhi huonyesha dalili ambazo ni za kuwasha ndani ya uume, kutokwa na uchafu au majimaji kwenye uume na kuwashwa au kuhisi kichomi baada ya kujisaidia haja ndogo au baada ya kutoa mbegu za kiume. Baada ya mtu kuhisi dalili hizo anashauriwa kwenda hospitalini au katika vituo vya afya ili kufanyiwa uchunguzi na vipimo. Trichomoniasis hugundulika kwa kutumia kipimo cha hadubini ambapo 

daktari humfanyia mgonjwa uchunguzi kwa kuingiza kifaa maalum katika tupu ya mwanamke na kuchukua kipimo kwa kutumia pamba maalum. Hatua ambazo hufanywa kitaalamu na bila kusababisha maumivu kwa mgonjwa na kisha kupelekwa maabarani ili kuangalia kama kuna vimelea vya Trichomonas vaginalis. Kwa kufanya uchunguzi huu, daktari pia anaweza kuangalia kama kuta za ndani za tupu ya mwanamke au shingo ya kizazi zimeathirika 

kwa kuwa na vidonda ambavyo ni vyekundu. Kwa mwanamume, daktari huchukua kipimo cha uchafu unaotoka kwenye uume au hupangusa sehemu za siri za mwanaume kwa wale ambao hawatoi uchafu au majimaji yoyote kwa kutumia pamba na kupeleka maabara kuyafanyia uchunguzi. Pia kipimo kilichochukuliwa na daktari kinaweza kuoteshwa kwenye maabara (culture) na kuangalia kama kuna uoto wa vimelea vya Trichomonas vaginalis baada 

ya siku tatu. Daktari pia anaweza kuangalia kiwango cha tindikali (PH) kwenye tupu ya mwanamke kwa kutumia karatasi maalum ya kipimo hiki ijulikanayo kama PH paper, ambapo kiwango kitakuwa alkaline kama ameathiriwa yaani PH zaidi ya 5. Kwa kawaida PH ya tupu ya mwanamke inakuwa ni ya tindikali (acidic) ya kuanzia PH 3.8 mpaka 4.5, na magonjwa yanayobadilisha PH hii ni pamoja na Trichomoniasis, na Bacteria Vaginosis. Mabadiliko ya hali hiyo humfanya mwanamke kuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi tofauti.

Kipimo kingine ni cha damu ili kuchunguza Prostate Specific Antigen (PSA). PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume. Uzalishaji wake huongezeka wakati seli za tezi dume zinapokua kuelekea kuwa kensa hali inayojulikana kitaalamu kama BPH, au wakati tezi dume inapopata maaambukizo (prostitis), na katika saratani ya tezi dume. Kipimo hiki kinapaswa kufanywa kwa wanaume wanaopata ugonjwa wa Trichomianisis mara kwa mara au wale wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea na ambao wamepata ugonjwa huu, na wanapaswa wafanyiwe kipimo hiki angalau mara moja kwa mwaka. Kipimo kingine ni cha Pap smear ambapo 

chembechembe au seli za shingo ya kizazi huchukuliwa na kuchunguzwa kwa kutumia hadubini. Kipimo hiki pia hutumiwa katika uchunguzi wa wanawake ili kujua kama wamepata saratani ya shingo ya kizazi au la. Wanawake wenye zaidi ya miaka 18 au wale wenye upungufu wa kinga mwilini wanashauriwa kufanya kipimo hiki pia angalau mara moja kwa mwaka ili wajue afya zao. Pia waliothirika na Trichomaniasis wanapaswa kufanyiwa kipimo cha kuangalia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, kipimo cha mkojo na kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu, chembechembe tofauti za damu na chembechembe bapa (platelets).


Tunasonga mbele tukiendelea kujadili ugonjwa wa zinaa wa Trichomoniasis kwa kuelezea tiba ya ugonjwa huo. Tiba ya Trichomaniasis ni kutumia dawa aina ya metronidazole au flagyl. Kwa wanawake wajawazito, dawa hii haitumiki kwa wale wenye ujauzito wa chini ya miezi mitatu au kwa wale ambao wananyonyesha. Ni vizuri kumuona daktari kabla ya kutumia dawa hii. Wale walioathirika na ugonjwa huu wa zinaa, wanashauriwa kupata tiba pamoja 

na wenza wao. Madhara ya dawa ya metronidazole ni pamoja na mzio au mcharuko mwili kwa maana ya allergic reaction, kichefuchefu, kukauka midomo, kuharisha, kuhisi ladha kama ya chuma mdomoni na kushuka kiwango cha chembechembe nyeupe za damu (leukopenia) ambazo hutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na hivyo upungufu wake kumfanya mtu awe katika hatari ya kupata maambukizi tofauti tofauti. Msishituke wapenzi wasikilizaji, hali hizo za allergic kwa dawa hutokea mara nyingi iwapo masharti ya dawa hayakufutwa vyema au mtu anapokunywa dozi

ya dawa zaidi ya alivyoelekezwa na daktari. Ni muhimu kufahamu kuwa, unapohisi hali kama hizo katika matibabu yoyote inakupasa kuacha kutumia dawa zilizokudhuru na kumuona daktari haraka. Baada ya kujua matibabu, yafuatayo ni madhara ya ugonjwa wa zinaa wa Trichomoniasis. Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kama tulivyosema huko nyuma. Pia Trichomaniasis husababisha mwanamke kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo. Ugonjwa huu vilevile huwaongezea wanawake hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi na kwa wanaume huwaongezea hatari ya kupata saratani ya tezi dume

USAFI WA KINYWA NA UTUNZAJI WA MENO





leo tutazungumzia usafi wa kinywa na umuhumu wake na jinsi utunzaji wa sehemu hiyo ya mwili unavyoathiri afya ya mtu kwa ujumla. Karibuni.

Afya ya kinywa ina umuhimu mkubwa zaidi ya unavyoweza kufikiria na kwa ujumla inaweza kutoa ufahamu kuhusiana na jinsi afya yako ya mwili ilivyo. Kuelezewa uhusiano uliopo kati ya afya ya kinywa na afya ya mwili mzima kunasaidia kufahamu umuhimu wa kutunza kinywa na hasa meno na fizi. Kama zilizo sehemu nyingine za mwili, kinywa nacho kimejaa bakteria ambao wengi wao hawana madhara. Kwa kawaida mfumo wa kulinda mwili na utunzaji mzuri wa kinywa kama vile kupiga mswaki na kutumia uzi kuondoa uchafu katika meno kunaweza kudhibiti bakteria walioko kinywani wabakie katika hali ya kawaida na kutodhuru kinywa. Lakini bila kutunza vyema kinywa, bakteria hao wanaweza kusababisha maambukizo na kusababisha meno kuoza na maradhi ya fizi.

Afya ya kinywa inajumuisha siha na namna ya utunzaji wa sehemu zote za mdomo hasa meno na fizi. Mbali na kinywa kutuwezesha ipasavyo kula, kuzungumza na hata kuwa na muonekano mzuri wa uso, meno na fizi zinapaswa zisiwe zimedhurika na kuwa na matatizo kama vile meno kuoza, magonjwa ya fizi, kung'oka meno na mdomo kunuka. Kuoza meno na meno kuwa na matundu ni matatizo ya kinywa yanayoshuhudiwa sana miongoni mwa watu. Sababu zinazoweza kuzuia matatizo hayo ya meno ni kudumisha usafi wa kinywa, kupata fluoride ya kutosha na kutokula kwa wingi vyakula vinavyoweza kudhuru meno na kusababisha matundu.


Afya ya meno na kinywa kwa ujumla inahusiana na afya ya mwili mzima kwa njia tofauti. Kwanza kabisa uwezo wa kutafuna chakula na kukimeza ni muhimu ili mwili uweze kupata virutubisho muhimu vya kujenga mwili. Halikahalika kuwa na kinywa chenye matatizo kunaweza kuathiri namna mtu anavyozungumza na hata kujiamini kwake. Matatizo ya meno yanaweza kumsababishia mtu gharama kubwa ya matibabu na ukarabati wa meno.


Sababu zinazoweza kuathiri afya ya kinywa

Uimara wa meno na fizi unatofautiana kati ya mtu na mtu, na umbo la taya, mdomo, meno na hata kiasi cha mate. Hayo yote ni mambo muhimu yanayoweza kuainisha kwa nini baadhi ya watu meno yao yanaoza zaidi kuliko wengine. Baadhi ya meno yanaweza kuwa na vishimo na nyufa zinazoweza kuruhusu bakteri na tindikali kupenya kwa urahisi na baadhi ya wakati umbo la taya huweza kuzuia meno yasisafishike vizuri na

kuondoa vyema uchafu kinywani. Kiwango na namna mate yalivyo pia huweza kuathiri uozaji wa meno. Kwa mfano matundu na nyufa huwa haziko sana katika meno ya mbele ambako kuna mate mengi ikilinganishwa na meno ya nyuma. Bakteria wote walioko kinywani wanaweza kubadilisha wanga kuwa tindikali lakini aina ya streptococci na

Lactobacili wana uwezo mkubwa wa kutengeneza tindikali. Kuwepo kinywani vijidudu vya aina hii huongeza uwezekano wa meno kuoza. Baadhi ya watu wana kiasi kikubwa cha bakteria wanaosababisha meno kuoza kuliko watu wengine na hii ni kutokana na kuzembea katika kutunza na kuimarishwa usafi wa kinywa.


Wataalamu wanatwambia kuwa, usafi wa kinywa na matumizi ya dawa za meno zenye fluoride hupunguza kasi ya meno kuoza. Usafi wa meno ni pamoja na kupiga mswaki kila siku kwa kutumia dawa za meno zenye flouride, kutumia uzi wa meno kusafisha eneo lililo kati ya meno, kuchokonea meno kwa kijiti ili kundoa mabaki ya chakula na kufanyiwa uchunguzi wa meno mara kwa mara. Flouride huzuia kupungua madini katika molekuli za meno, kuongeza madini hayo kwenye meno na kuimarisha meno ili yasiathiriwe na tindikali. Matumizi ya fluoride kwa kiwango

kinachotakiwa huzuia na kudhibiti matundu kwenye meno. Flouride inaweza kupatikana kutoka katika maji ya kunywa na baadhi ya vinywaji vilivyoongezwa mada hiyo. Pia mada hiyo hutiwa katika dawa za mswaki, geli na dawa za kusafishia kinywa. Katika baadhi ya nchi mada ya fluoride huongezwa hata katika chumvi na maziwa. Kiwango cha flouride katika maji ya kunywa na vyakula kinapaswa kuzingatiwa kwa mujibu wa mahitaji ya mwili. Suala hili ni muhimu kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 6 ambao meno yao bado yanakua. Kutumiwa sana au kwa kiwango kikubwa mada hiyo husababisha matatizo katika enamel au mfupa wa jino hali inayojulikana kinaalamu kama kama fluorosis.


Vyakula na athari yake katika kuoza meno

Ijapokuwa katika nchi nyingi kuoza meno kumekuwa kukiambatanishwa na matumizi ya fluoride na utunzaji wa kinywa, aina ya vyakula anavyokula mtu pia ni jambo muhimu linalochangia meno kuoza. Jinsi chakula chenyewe kilivyo kwa mfano kama kinanata na kung'ang'ania kwenye meno pia husababisha meno kuoza. Vyakula

vinavyong'ang'ania kwenye meno kama vile bisikuti na crips huongeza uwezekano wa kuoza meno kwani hubakia juu ya meno kwa muda mrefu zaidi kuliko vyakula vingine. Pia vyakula vyenye sukari zinazoyeyuka kwa haraka husafishwa kwa wepesi kinywani na mate, na kila vyakula vyenye wanga vinavyokaa muda mrefu kinywani na kuzunguka meno, ndivyo bakteria wanavyopata fursa zaidi ya kutengeneza tindikali na kuondoa madini katika meno. Kila tunapokula vyakula vyenye wanga, bakteria walioko kwenye kinywa huanza kutengeneza asidi suala linalopelekea meno kuoza. Mwenendo huu huendelea hadi baada ya dakika 10 hadi 20 baada ya kula au kunywa. Katika kipindi tusichokula au kunywa mate huzimua tindikali na kusaidia kurejesha madini katika meno. Iwapo

vyakula au vinywaji vitaliwa mara kwa mara na kinywa kisipate muda wa kurejesha madini kwenye meno, hapo ndipo meno huanza kuoza. Kwa ajili hiyo tunashauriwa kutokula na kunywa wakati wote na pia kupunguza kula vyakula vyenye wanga na sukari kwa uchache tusile vyakula hivyo zaidi ya mara 6 kwa siku. Pia tunashauriwa kuhakikisha kuwa tunapiga mswaki meno kwa kutumia dawa za meno zenye fluoride, kwa uchache mara mbili kwa siku.


Mmomonyoko wa meno

Mmomonyoko wa meno ni kuharibika tishu ngumu ya juu ya meno kutokana na acidi bila kuathiriwa na bakteria wanaosababisha meno kuoza. Kuna vyakula na vinywaji vingi vyenye tindikali katika lishe zetu na kuna uwezekano suala hilo likatuathiri. Kwa mfano kupendelea sana kula vyakula au kunywa vinywaji vyenye tindikali husababisha mmomonyoko wa meno. Tatizo hilo lisiposhughulikiwa huweza kuathiri ufanisi wa kinywa na hutofautiana baina ya

watu. Ili kuepukana na tatizo hilo tunashauriwa kujiepusha kupenda sana kunywa vinywaji au kula vyakula vyenye acidi na kupiga mswaki kwa uchache mara mbili kwa siku kwa kutumia dawa ya mswaki yenye fluoride. Pia tunashauriwa kutopiga mswaki mara tu baada ya kunywa au kula chakula chenye acidi kwani kufanya hivyo huweza kuyafanya meno yaharibike kutokana na kusugua meno wakati tindikali ikiwemo kinywani. Pia ni bora tujizoeshe kutafuna chingamu au ubani mara tu baada ya kula vyakula vyenye acidi ili kufanya mate yatengenezwe ambayo husaidia kuondoa acidi mdomoni.

MARADHI YA FIZI NA MENO




Aina za maradhi ya fizi na dalili zake

Kupiga mswaki na kutunza meno sio suala gumu na iwapo tutapiga mswaki ipaswavyo pamoja na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno, tunaweza kuzua maradhi ya fizi na pia meno kuoza. Maradhi ya fizi husababishwa na utando kwenye meno unaotengenezwa na bakteria, ute na chembechembe nyinginezo zinazoganda kwenye meno. 

Kwa mujibu wa Taasisi ya Meno ya Marekani (ADA) iwapo utando katika meno hautaondolewa huwa mgumu na kuwa ugwagwa wa meno au tarter inayotumiwa na bakteria. Mchanganyiko wa utando na ugwagwa katika meno husababisha uvimbe kwenye fizi hali inayojulikana kitaalamu kama gingivitis. Ukoga wa meno au ugwagwa 

unaweza kundolewe na daktari wa meno au dentist.Maradhi ya fizi yana awamu tatu. Awamu ya kwanza kama tulivyosema ni gingivitis, ambapo fizi huwa nyukundu, huvimba na hutokwa na damu kwa urahisi. Iwapo hali hiyo itagundulika mapema inaweza kutatuliwa kwa kupiga mswaki vizuri na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno.Awamu ya pili ya ugonjwa wa fizi ni hali ijulikanayo kama Periodontitis ambapo uvimbe hutokea kuzunguka 

jino. Awamu hii ni iliyoendelea zaidi ya ugonjwa wa fizi inayotokea wakati sumu ya bakteria katika utando inapoharibu fizi zilizoshikilia jino. Suala hilo husababisha fizi ziachane na jino na kutengeneza mada haribifu. Baadhi ya wakati mfupa ulioliwa kuzunguka jino unaweza kuonekana. Matibabu ya maradhi haya ya fizi ni muhimu sana ili kuzuia mmomonyoko wa mfupa na kung'oka meno.Awamu ya tatu ya maradhi ya fizi ni periodontitis iliyoendelea. Katika steji hii uharibifu wa fizi huwa mkubwa zaidi kuliko kabla na mfupa wa jino hulika. Pia meno huweza kung'oka na baadhi ya wakati huhitaji kung'olewa iwapo matibabu hayatosaidia.

Dalili za maradhi ya fizi

Hapa linajitokeza swali kwamba ni zipi dalili zinazojitokeza wakati mtu anapokuwa na ugonjwa wa fizi ulioendelea? Dalili za advanced periodontitis ni kuwa na harufu mbaya ya mdomo ambayo haiishi. Fizi kuvimba, kuwa nyekundu na laini. Dalili nyingine ni fizi kusogea mbali na meno, kuhisi maumivu wakati wa kutafuna na kupoteza hisia katika meno.

Sababu za maradhi ya fizi

Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu awe katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya fizi. Miongoni mwa sababu hizo ni kuvuta sigara au kutafuna tumbaku. Mbali ya kuwa uvutaji sigara unaathiri mwili wa binadamu kwa njia tofauti, moja ya athari za ufutaji sigara hudhihirika katika kinywa cha mtu. Kwa kuwa moshi wa sigara 

hupita kwenye meno na fizi, kinywa cha mvuta sigara huwa kituo cha nicotine ambayo huharibu muonekano wa meno kwa kuyabadilisha rangi na kuacha harufu mbaya kinywani. Si hayo tu bali uvutaji sigara pia huathiri tishu za fizi na kupunguza mtiririko wa damu katika fizi, na kuleta uharibifu unaosababisha fizi zisogee mbali na 

meno.Wataalamu wanatuarifu kuwa, asilimia 75 ya watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fizi ni watu wazima huku wale wanaovuta sigara wakiwa kwenye hatari ya kusumbuliwa na ugonjwa huo mara 7 zaidi ikilinganishwa na watu wasiovuta sigara.Sababu nyingine inayochangia katika kupata ugonjwa wa fizi ni mabadiliko ya homoni kwa wasichana na wanawake. Wanawake wako katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya kinywa na meno kuliko wanaume kutokana na mabadiliko ya homoni yanayosababishwa na maumbile yao. Sio tu mabadiliko ya homoni 

kwa wanawake na watoto huathiri mtiririko wa damu katika tishu za fizi, bali pia huchangia katika suala zima la kupatikana ugando kwenye meno au plague unaosababisha meno kuoza. Mabadiliko ya homoni huwafanya wanawake wawe kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa fizi wanapokuwa katika hali tofauti kwenye maisha yao ambazo ni wakati wa kubalehe, wakati wa hedhi, wanapotumia vidonge vya kuzuia mimba, wanapokuwa 

wajawazito na wakati wanapoacha kupata hedhi yaani menopause. Hayo yote husababishwa na mabadiliko yanayoshuhudiwa katika homoni za estrogen na progesterone kwenye vipindi hivyo. Kwa sababu hiyo tunaweza kusema kuwa, watoto wa kike, wasichana na wanawake kwa ujumla wanapaswa kuzingatia zaidi usafi na utunzaji 

wa fizi na meno ili kuepusha uharibifu wa meno unaowapata zaidi kutokana na jinsia yao kuliko wanaume.Sababu nyingine inayoweza kumfanya mtu apatwe na maradhi ya fizi ni ugonjwa wa kisukari. Madaktari wanatuambia kuwa, watu walio na ugonjwa wa kisukari ambao hawadhibiti vyema ugonjwa huo, wako katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya meno na maambukizi katika fizi. Hii ni kwa sababu ugonjwa wa kisukari hupunguza mtiririko wa 

damu kwenye fizi na pia kiwango cha juu cha sukari kwenye damu husababisha kinywa kiwe kikavu na kuzidisha ugonjwa wa fizi. Upungufu wa mate mdomoni huongeza bakteria wanaoharibu meno na kuleta utando. Iwapo mtu mwenye kisukari atadhibiti ipasavyo kiwango cha sukari kwenye damu, hatari ya kupata matatizo ya meno hupungua.

Namna ya kuzuia maradhi ya fizi

Suala muhimu zaidi linaloweza kuzuia mtu asipatwe na maradhi ya fizi na kuoza meno ni kupiga mswaki na kutumia nyuzi kuondosha uchafu katikati ya meno kwa uchache mara moja kila siku. Suala hilo linaweza kuzuia maradhi ya fizi, meno kutoboka na kung'oka. Licha ya kusafisha meno kila siku, jambo jingine muhimu ni kufanyiwa uchunguzi na daktari wa meno kwa uchache mara moja kwa mwaka. Hii ni kwa sababu hata kama tunajitahidi kwa kiasi gani kupiga mswaki, lakini mgando na ugwagwa hujitokeza na kusababisha matatizo katika fizi.


Je, ni Namna gani tupige mswaki kwa njia iliyo sahihi?
Kwanza kabisa tunashauriwa kupiga mswaki asubuhi na kabla ya kwenda kulala. Ikiwezekana piga mswaki baada ya kula chakula. Kama hauwezi, piga mswaki baada ya kula vyakula vya sukari. Tunapaswa kutumia mswaki laiini na wa wasitani, kwani mswaki mkubwa hautafika kwenye meno ya nyuma ilhali ule ulio mdogo utakufanya utumie 

wakati mwingi sana katika kusugua meno. Ikiwa unahitaji usaidizi katika kuchagua mswaki, pata ushauri kutoka kwa daktari wako wa meno. Tumia dawa ya meno iliyo na floraidi. Watoto wanapaswa kutumia kiasi kidogo cha dawa ya meno na watu wazima watie dawa ya meno kulingana na urefu wa nywele za mswaki.Wataalamu 

wanatushauri kubadilisha mswaki pindi ule tunaotumia unapochoka, kila baada ya miezi mitatu au minne. Pia tunashauri kuwa ni vizuri kubadilisha mswaki mpya kila baada ya kupata mafua, uvimbe katika koo na magonjwa mengineyo kama hayo.

Kumbuka kusugua pande zote za meno kwa njia ifuatayo:
Sugua meno yako polepole bila kutumia nguvu kutoka sehemu ya nyuma hadi mbele. Sugua karibu na ufizi kwa mwendo wa mviringo, ili mswaki ufike sehemu ambapo meno na ufizi zinakutanika mahali ambako chembechembe za chakula hujificha.Sugua sehemu zote za meno, sehemu ya nje, sehemu ya kutafunia chakula na 

sehemu ya ndani ya meno.Tumia sehemu ya juu ya mswaki kusafisha sehemu ya ndani ya meno ya juu, kwa mwendo wa juu na chini.Sugua ulimi wako kwa upole ili kuondoa vijidudu au viini vinavyosababisha harufu mbaya.Sukutua na hifadhi mswaki wako sehemu nzuri na salama kwa matumizi ya baadaye.

Monday, 29 September 2014

MARADHI YA KIPANDAUSO (MIGRAINE) CHANZO DALILI TIBA NA JINSI YA KUJIKINGA





Kuumwa na kichwa kumegawanyika sehemu kuu nyingi sana japo kuwa 1% yake ni ashirio la matatizo ya kiafya ambayo yame-advance. Kama vile concussion of brain,meningitis,encephaliti, na stroke. Kuumwa na kichwa pia inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate.

Sehemu ambazo huuma ni kama ifuatavyo:

- Mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa.
- Baadhi ya neva za fahamu zilizoko usoni

Misuli ya kichwani
Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwana chini ya ubongo kuna mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishu za ubongo kwa zenyewe haziumi kwani hazina mifumo ya fahamu ambayo inahisia.
Mambo haya 12 nayo yanahusika sana.

1:Nervous tension headaches;
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia vitamin b2 na c , ounguza au acha matumizi ya sukari,kahawa,chakula chenye kukusababishia mzio,misongo ya mawazo na ufanye mazoezi yakutosha.

2: Cluster headaches;
Kichwa kuuma haswa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protein ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.

3: Hangover headaches;
Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali haswa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kichogoni au shingoni,kunywa maji mengi na juice ya matunda freshi na uache pombe.

4: Exertion headaches;
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na haswa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili na usifanye mazoezi.

5: Caffein headaches;
Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokodogo mpaka utakapo acha kabisa.

6: Sinus headaches;
Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa zingine hii utkana na maambukizi.

7: Bilious headaches;
Kichwa na macho huuma haswa kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji yakutosha na kasha fanya enema.

8: Hunger headaches;
Maumivu ya kichwa ambaya husababishwa na kutokula kwa muda. Kula chochote ilimradi kiwe ni protein au carbohydrates .

9: Eyes ram headaches
Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo saa zingine inaweza kuwa sababu. lakini chanzo chake haswa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuana mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.

10: Menstrual headaches;
Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya.

11: Arthritis headaches;
Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa zingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu haswa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo.

12: Hypertension headaches;
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na halii itaisha bila shaka.

Kabla ya kukupa dawa na ushauri wangu nina maswali nikuulize unijibu.

Je unapata Usingizi wa kutosha? Unalala usiku masaa mangapi? Je, unakunywa maji ya kutosha? Una miaka mingapi? Unapata haja kubwa ya kutosha? Nenda pia kapime macho yako na ukapime tena kwenye mishipa yako ya fahamu huenda una matatizo. Na kitu kingine unakuwa upo juani uwe unavaa kichwani kofia.



TIBA MBADALA YA KIPANDA USO:



Grape Juice Juisi ya Zabibu Dawa ya Ugonjwa wa Kipanda uso Migraine Kunywa kutwa mara 3 kwa muda wa siku 3 au siku 7utapona.

Sunday, 28 September 2014

MBINU ZA KUWA MTU MAARUFU KATIKA JAMII-3



Kwa muda wa wiki mbili tangu tumenza kujifunza somo hili, nimepokea ujumbe wa watu wengi sana wakikiri kwamba mada imewasaidia kujitambua na sasa wanaelewa jinsi ya kuishi na watu na kuwa maarufu kwenye jamii zao. Leo tunaendelea kuangalia vipengele vingine vinavyozungumzia sheria ya kuwa mtu maarufu na mwenye mamlaka kwa watu.
MWANGAMIZE KABISA ADUI YAKO
VIONGOZI wote maarufu tangu Musa wamefahamu kwamba adui anayeogopewa ni lazima aangamizwe kabisa. 
(Wakati fulani wamelitambua hilo kwa matatizo.)  Iwapo ukuni mmoja ukiachwa unawaka, hata kama una moto mdogo kiasi gani, hatimaye moto utalipuka.  Mambo mengi hupotea kwa kufanywa nusu nusu badala ya kuyamaliza kabisa: Kumwacha adui yako akinusurika kunaweza kuleta kisasi kitatachokugharimu maisha.
KUTOONEKANA SANA KUNAONGEZA HESHIMA
Kuonekana mno kunapunguza thamani ya mtu: Unapoonekana sana na kusikika kila mara, ndivyo unavyozidi kuonekana mtu wa kawaida. 
Ikiwa umejijenga katika kundi fulani, jiondoe kwa muda, jambo ambalo litakufanya uzungumziwe zaidi na kupendwa zaidi.  Jifunze ni wakati gani wa kujitokeza hadharani.  Unapoadimika ndivyo unavyokuwa na thamani mbele za watu.
WAFANYE WENGINE WAISHI KATIKA WOGA
Binadamu ni viumbe wanaopenda kufahamu mambo ya wengine.  Wakikufahamu kwa undani wanaweza kukutawala.  Wachanganye: uwe mtu usiyetabirika.  Tabia isiyofahamika itawafanya washindwe kukuzoea na hivyo kujenga hofu kwako: “Mmmm…huwa hatabiriki unaweza kusema hatajali akaja kukuadhibu.”
USITAKE KUJITENGA KWANI NI HATARI
Dunia ni ya hatari na maadui wako kila mahali, kila mtu anabidi kujilinda. Kujitenga kunaonekana kuwa ndiyo njia salama zaidi. 
Lakini kujitenga kunakuweka katika hatari zaidi kuliko kukulinda.  Kunakunyima fursa ya kupata habari muhimu.  Ni vyema kuchanganyika na watu na kupata marafiki.  Uhusiano na watu wengine ni kinga ya maadui zako.
MFAHAMU MTU UNAYESHUGHULIKA NAYE
Kuna watu wa aina nyingi duniani, na huwezi kudhani kwamba kila mmoja atakabiliana nawe katika namna ile ile.  Walaghai na kuwachanganya baadhi ya watu ili ikitokea uadui au hali ya kutotaka kukuunga mkono wao kwa wao waanze kupingana. Ni muhimu kuwafahamu walio karibu nawe.

USITAKE KUJIUNGA NA UPANDE WOWOTE
Mpumbavu huharakisha kujiunga na upande fulani.  Usitaka kujiunga na upande wowote au suala fulani bali tumikia nafsi yako.  Ukiendelea kuwa mtu huru, utakuwa ni bwana wa watu wengine, ukiwagonganisha watu na kuwafanya wafuate utashi wako. Kama uko mtaani usikubali kuwa mwanachama wa makundi hasimu.

JIFANYE MNYONGE: UBADILI UNYONGE WAKO KUWA NGUVU
Ukiwa mnyonge, kamwe usijaribu kupigana; badala yake jifanye umesalimu amri.  Kusalimu amri kunakupa muda wa kujipanga upya, muda wa kumchanganya na kumkasirisha adui yako, muda wa kusubiri hadi nguvu zake ziishe.   
Usitake kumpa heshima ya kupigana halafu akakushinda .  Wewe salimu amri tu. Ukifanya hivyo utamuudhi na kumfanya achanganyikiwe.   Lichukulie suala la kusalimu amri kama chombo cha kukupatia nguvu.
IMARISHA NGUVU ZAKO
Imarisha nguvu na juhudi zako kwa kuhakikisha ziko katika hali ya juu.  Siku zote nguvu zinazokwenda sehemu moja hushinda zaidi ya zile zinazogawanywa mara nyingi. Kwenye harakati zako za kutafuta umaarufu na kuwashusha maadui zako hakikisha unachagua upande mmoja wa kuelekeza mashambulizi, usikubali kupigana kote kote. Utaelemewa.
JIFUNZE KUBEMBELEZA KATIKA MAMBO YENYE MANUFAA 
Mtu anayejua kubembeleza hufanikiwa katika dunia hii ambayo inategemea nguvu na umahiri wa kisiasa.  Mtu anayebembeleza na kujikomba kwa wakuu wake, hufanikiwa kupata nguvu na ustawi.
UWE MTU SAFI KATIKA JAMII
Lazima uwe mfano wa ustaarabu na ufanisi.  Hakikisha mikono yako haichafuliwi na  makosa na vitendo viovu.  Endesha maisha ya uadilifu ambayo yatawafanya watu wengine waonekane si waadilifu.
EPUKA KUSEMA UKWELI
Ukweli kila mara hukwepwa kwani ni mbaya na unaudhi.  Usikimbilie kusema ukweli labda kama uko tayari kupambana na hasira na maudhi yanayotokana na kufanya hivyo. Maisha ni magumu kiasi kwamba watu wanaoweza kuanzisha uwongo hupendwa na watu wengi.  Kila mtu huwaendea.  Kuna nguvu kubwa kwa kutumia uwongo kwa watu.