Ugonjwa
wa saratani
Saratani
ni ugonjwa unaotokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo wake wa kugawanyika
na hivyo hazipo katika hali yake ya kawaida. Seli huweza kugawanyika bila
mpangilio maalum na kuharibu mkusanyiko wa seli nyingine. Seli za saratani
hutokea sehemu moja ya mwili na zinaweza
kusambaa sehemu nyingine za mwili,
saratani pia husababishwa na hali ya mazingira ya vitu mbalimbali kama vile
ulaji wa vyakula vyenye visabbishi vya saratani (carcinogenic compounds), ulaji
usiofaa, unywaji wa
pombe, uvutaji sigara au minoni hatari, “asbestos” lisasi (lead), uranium na
zebaki.
Zipo
pia baadhi ya saratani zinazosabishwa na virusi kama
hepatitis B
ambayo
huleta saratani ya ini na human papiloma inahusishwa na saratani ya
shingo ya kizazi. Saratani huweza kutokea kwenye sehemu mbalimbali za mwili
kama vile mapafu, matiti ovary, kibofu cha mkojo, shingo ya uzazi, utumbo, koo,
kinywa, tezi dume (prostate), ini na ngozi.
Ulaji
unaofaa na mtindo bora wa maisha ni vigezo muhimu sana katika kuzuia saratani
na pia ni sehemu muhimu ya matibabu na kudumisha maisha bora baada ya kupata
matibabu. Matumizi ya baadhi ya vyakula huweza kuongeza uwezekano wa kupata
saratani. Uzito wa mwili ukiwa mkubwa unaweza pia kuongeza uwezekano wa kupata
baadhi ya saratani Ni muhimu kufuata mtindo bora wa maisha kwani ni bora kuzuia
kuliko kutibu.
Mambo
yanayohusiana na mtindo wa maisha yanayoweza kuchangia katika
kupata saratani.
Tafiti
zinaonesha kwamba saratani za kurithi ni chache sana ila saratani nyingi
hutokana na sababu za kimazingira. Tafiti nyingi zimeonesha kuwa kiasi cha
asilimia 40 hadi 60 za saratani husababishwa na mtindo wa maisha usiofaa hasa
ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi ya mwili. Mtindo wa maisha usiofaa
unajumuisha:
Ulaji
wa vyakula vyenye nishati-lishe kwa wingi ambavyo husababisha unene. Unene
umeonekana kuhusiana na saratani ya mji wa uzazi, matiti, figo, tezi dume,
utumbo mpana na kibofu cha mkojo;
·
Ulaji
wa nyama nyekundu kwa wingi na zile zilizosindikwa vimehusishwa na saratani ya
tezi la kiume, utumbo mpana, mapafu, kinywa na koo;
·
Utumiaji
wa pombe kwa wingi huongeza hatari ya kupata saratani ya mdomo, koo, koromeo,
utumbo mpana, kongosho, ini na matiti;
Ushauri
wa chakula na lishe wa jinsi ya kukabiliana na matatizo ya kiafya
yanayoambatana na kuwa na saratani au tiba yake:
Matatizo
mbalimbali yanaweza kujitokeza kutokana na hatua ya ugonjwa au aina ya matibabu
mgonjwa anayopata, hasa dawa za saratani (chemotherapy) au mionzi. Matatizo
hayo ni kama kukonda, upungufu wa damu, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu,
kutapika, kuhara, kukosa choo, vidonda kinywani, na matatizo ya ngozi.
Kukonda
Wagonjwa
wengi wa saratani wanapungua uzito wakati wa matibabu. Hii inaweza kusababishwa
na madhara ya saratani yenyewe, ongezeko la mahitaji ya virutubishi mwilini,
kukosa hamu ya kula, aina ya matibabu anayopata mgonjwa (dawa, mionzi au upasuaji).
Yafuatayo huweza kusaidia katika kukabiliana na tatizo hili:
·
Kuzingatia
ulaji wa mlo kamili na ulaji wa aina mbalimbali za vyakula;
·
Kuongeza
ulaji wa vyakula vyenye protini kwa wingi yenye asili ya wanyama (isipokuwa
nyama nyekundu) na mimea.
·
Kula
vyakula vilivyo laini vilivyoboreshwa na kuongezewa vyakula vyenye protini na
nishati-lishe kwa wingi.
·
Kula
milo midogo midogo mara kwa mara na kuongeza asusa zenye virutubishi vingi;
·
Kujitahidi
kula wakati una hamu yakula au ukiwa na njaa kali na kula vyakula vile vyenye
virutubishi kwa wingi;
·
Kufanya
mazoezi kabla ya kula (kama vile kutembea) ili kuongeza hamu ya kula na
kusaidia uyeyushwaji wa chakula;
·
Kula
taratibu, usile kwa haraka bali jipe muda wa kutosha wakati wa kula;
·
Kutumia
viungo vyenye harufu unayoipenda
·
Kutumia
vinywaji kati yam lo na mlo na sio wakati wa kula kuepuka tumbo kujaa na hivyo
kushindwa kula chakula cha kutosha; na
·
Kutumia
vinywaji vyenye virutubishi vingi na nishati-lishe.
JINSI
YA KUZUIA AU KUPUNGUZA MAGONJWA SUGU YASIYO YA KUAMBUKIZA
Magonjwa
sugu yasiyo ya kuambukiza yanaweza kuzuiwa au kupunguzwa kwa kufuata mtindo
bora wa maisha. Mtindo bora wa maisha ni muhimu katika
kuendeleza na kudumisha
afya ya mtu na kuzuia maradhi, hususani magonjwa sugu yasiyo ya
kuambukiza.Mtindo bora wa maisha ni ule unaozingatia ulaji unaofaa, kufanya
mazoezi ya mwili, kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku,
kuepuka matumizi ya pombe, na kuepuka msongo wa mawazo.
Ulaji
unaofaa:
Ulaji
unaofaa hutokana na kula chakula chenye mchanganyiko wa angalau chakula kimoja
kutoka katika makundi matano ya vyakula na kupunguza kiasi cha mafuta, chumvi,
na sukari kinachotumika.
Ulaji
unaofaa unatakiwa kuzingatia mahitaji ya mwili kutokana na jinsi, umri,
mzunguko wa maisha (mfano utoto, ujana, uzee), hali ya kifiziolojia (mfano
ujauzito, kunyonyesha), kazi au shughuli na hali ya afya.
Ulaji
unaofaa huchangia katika kudumisha uzito wa mwili unaotakiwa na kupunguza
maradhi, yakiwemo magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.
Mambo
ya kuzingatia ili kufanikisha ulaji unaofaa:
•
Kula mlo kamili mara tatu kwa siku.
•
Kula matunda na mboga mboga kwa wingi kila siku.
•
Kula vyakula venye makapi mlo kwa wingi.
•
Epuka kutumia sukari nyingi.
•
Epuka kula vyakula venye chumvi nyingi.
•
Kunywa maji safi, salama na ya kutosha
•
Kula asusa zilizo bora kilishe.
Kufanya
mazoezi ya mwili :
Ni
muhimu kwa binadamu wote, mtoto au mtu mzima, mnene au mwembamba, mgonjwa au
mwenye afya njema kufanya mazoezi kwani husaidia mifumo mbalimbali ya mwili
kufanya kazi kwa ufanisi. Mazoezi hupunguza uwezekano wa kupata saratani,
ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo, na shinikizo kubwa la damu.
Mazoezi
husaidia pia katika kuzuia ongezeko la uzito wa mwili, kupunguza msongo wa
mawazo, na pia huboresha afya ya akili ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo wa
kufikiri, kuelewa na kukumbuka. Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili angalau
kwa dakika 30 kila siku, yaani mazoezi yanayotumia nguvu kiasi kama kutembea
kwa haraka.
Anza
kwa kutembea kwa muda mfupi, na baadaye unaweza kuongeza muda hadi dakika 60
kila siku, ukishindwa kabisa kufanya kila siku fanya angalau dakika 60 mara
tatu kwa wiki.
kuepuka
matumizi ya pombe:
Pombe
husababisha ongezeko la uzito wa mwili ambalo linahusishwa na magonjwa mengi
sugu yasiyo ya kuambukiza. Tafiti zimethibitisha kwamba pombe inaongeza sana
uwezekano wa kupata saratani hasa ya mdomo, koo, koromeo, matiti, utumbo mpana
na ini.
Tafiti
zimeonyesha kwamba pombe ina madhara mengikiafya, ikiwa ni pamoja na
kusababisha magonjwa, kupunguza uwezekano wa ini kufanya kazi vizuri, na pia
huathiri uwekaji wa virutubishi mwilini.
Endapo
unakunywa pombe kwa mwanaume inashauriwa kunywa vipimo viwili ambavyo ni sawa
na milimita 500 za bia, mvinyo milimita 200, na pombe kali milimita 50 kwa siku
. Kwa mwanamke anashauriwa kunywa nusu ya vipimo vinavyotumika kwa mwanaume.
Kuepuka
matumizi ya sigara na bidhaa nyingine za tumbaku:
Uvutaji
wa sigara, utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake huongeza uwezekano wa kupata
ugonjwa wa moyo, saratani ( hasa za mapafu, kinywa na koo), magunjwa sugu
mengine ya njia ya hewa, shinikizo kubwa la damu na
vidonda vya tumbo hivyo ni
muhimu kuepuka.
Sumu
aina ya nikotini iliyopo katika sigara huharibu ngozi ya ndani hivyo huongeza
uwezekano wa lehemu kujikusanya kwenye sehemu za mishipa ya damu
zilizoathiriwa.
Nikotini
pia huweza kusababisha mishipa ya damu kuziba au kuwa myembamba kuliko kawaida
na hivyo kuzuia damu kupita inavyotakiwa . Matumizi ya sigara pia huweza kuleta
athari kwa wale walio karibu na mvutaji hususani kwa mama mjamzito na mtoto.
Kuepuka
msongo wa mawazo
Msongo
wa mawazo ni hisia ambayo huweza kuamshwa na matukio mbali mbali kama vile
kufiwa na mtu wa karibu, kukabiliwa na tatizo katika( familia,maisha au
shuleni), kuwa na kazi nyingi kwa muda mrefu bila ya kuwa na muda wa kupumzika.
Hisia hizo zinaweza kusababisha hasira, wasiwasi, woga, huzuni, kuchanganyikiwa
na pia kukata tamaa. Msongo wa mawazo ukijitokeza mara kwa mara huweza
kusababisha ulaji usiofaa na mifumo ya mwili kutofanya kazi vizuri
Inashauriwa
kupunguza msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi, kujipa muda wa kupumzika,
kushiriki katika shughuli mbali mbali kama michezo, matamasha, harusi, na pia
kupangilia vizuri jinsi ya kutumia muda wako. Jadili na mtu unayemwmini kuhusu
matatizo yako, cheka au angua kilio, zima simu yako kwa muda katika siku.
HITIMISHO
Watu
wengi tunakumbwa na magonjwa haya kutokana na kuwa na mtindo wa maisha usiofaa,
ni vyema kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kupunguza uwezekano wa kupata
magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.
USHAURI
·
Ni
vyema kushiriki katika michezo, na mazoezi ya viungo.
·
Ni
muhimu kujenga mazoea ya kupima mara kwa mara afya zetu.
·
Tuzingatie
mtindo bora wa maisha ili kuzuia au kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa sugu
yasiyo ya kuambukiza.
0 comments:
Post a Comment