Friday, 4 July 2014

UVIMBE WA TEZI DUME ( PROSTATE ENLARGEMENT)





Tezi dume ni tezi ambayo ipo chini ya kipofu cha mkojo. Tezi hii  hutoa majimaji ambayo hutoa chakula na kulinda mbegu za kiume. Tezi hii hupatikana kw wanaume pekee. Mrija wa mkojo( urethra) hupita katikati ya tezi hii. Tezi huu huongeza ukubwa taratibu kadri mwanaume anapokuwa. Kwa kawaida ina uzito  wa gram 11.

Tezi hii inaweza kupata magonjwa mengi kama vilivyo viungo vingime vya mwili. Katika makala haya tutazungumzia uvimbe wa tezi dume usiokuwa saratani (benign prostate hypertrophy.
Tezi dume hupanuka zaidi mwanaume anapofikisha miaka 50.  8 kati ya 10 ya wanaume walio na miaka 70 wana uvimbe.

Dalili
Kwa sababu mrija wa mkojo unapita kwenye tezi dume,  hivyo mrija unaweza kuminywa na kusababisha mkojo  kuziba. Hizi huleta dalili pingamizi(obstructive symptoms). dalili hizi ni 
-mkondo hafifu (poor stream)- mtiririko wa mkojo ni dhaifu na huchukua muda kumaliza kukojoa.
-kusitasita(hestitancy)- mkojo unachelewa kutoka unapokwenda choo.
-kuchuruzka(dribbling) -mkojo unapoeleka ukingoni  huanza kuchuruzika na kutoka matonetone.
mkojo kutoisha- baada ya kukojoa unahisi kama bado kuna mkojo kwenye kipofu.
Tatizo hili pia hufanya mtu kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine kwenda haraka chooni pale anapopata haja.
Kwa kawaida dalili hazisumbui sana lakini muda unavyosonga ndivyo tatizo husumbua zaidi. Wakati mwingine tatizo hili husababisha mkojo kujifungia kabisa hivyo kuleta maumivu makali eneo la chini la tumbo. Pia mgonjwa anaweza kupata maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo.

Uchunguzi 
Tatizo hili hubainika kutokana na dalili kama ilivyo eleza hapo juu. daktari hupima ukubwa za tezi hii kwa kupitisha kidole chenye glovu kwenye njia y haja kubwa. Ultrasound pia hutumika katika uchunguzi wa tatizo hili. Daktari anaweza kufanya vipimo vingine ili kuangalia matatizo mengine yanayoambatana na tatizo hili.
Matibabu.
Matibabu hutegemea dalili. Matibabu ya msingi ni upasuaji.

Prostatelead.jpg

0 comments:

Post a Comment